Kitty Galore
JF-Expert Member
- May 24, 2011
- 345
- 100
Aliyekuwa boyfriend kaoa tokea January this year, lakini nimeshindwa kuabsorb hii hali, mbaya zaidi tunaishi mji mmoja so mara nyingi namuona. Wadau kama ilishawahi kukutokea, ulichukua hatua gani kuiona ni ya kawaida. Najua maisha lazima yaendelee lakini duh, roho inauma jamani, the thing is haunting me badly.
Pole sana. Lakini tangu January mpaka sasa ni miezi karibu nane sasa. Unatakiwa kuamini kilichotokea, jishughulishe na pia jichanganye na watu wengine pia. Kama unaweza kuepuka kutembelea sehemu ambazo yeye anatembelea mara kwa mara pia inaweza kukusaidia kumsahau kirahisi. Inawezekana hata namba yake ya simu bado unayo na pengine wakati mwingine huwa unashawishika kuwasiliana naye japo kwa text message. Nakushauri uache hilo na uanze maisha mapya!
Pia epuka sana hali ya upweke.
Kubali matokeo na kuamini kuwa wako wa moyoni anakuja. Kisicho ridhiki hakiliki hivyo riziki yako ipo tu wala hamna aja ya kuumia roho.
Mmekutana nae Januari tu na kishakumwaga na kuoa mwingine,ujue huyo alikuwa hajatulia.Ni ajabu pia na wewe kuwa unammiss mtu uliyekaa nae kwa muda mfupi hivyo,wapo watu wanatoswa after 5 yrs +.Pole.Aliyekuwa boyfriend kaoa tokea January this year, lakini nimeshindwa kuabsorb hii hali, mbaya zaidi tunaishi mji mmoja so mara nyingi namuona. Wadau kama ilishawahi kukutokea, ulichukua hatua gani kuiona ni ya kawaida. Najua maisha lazima yaendelee lakini duh, roho inauma jamani, the thing is haunting me badly.
...bi mdada we ulikosea nn mpaka jamaa akaoa msichana kwingine?...
potezea bana,...utaumia mpaka lini,..anyway ebu tuambie ilikuaje akaoa mtu mwingine wakati wewe unampenda,...au kuna sehemu uliteleza,.....kubali matokeo maisha ndivyo yalivyo....kama vip hama mtaa
Igwe hilo alilolifanya ndio linamfanya aumie zaidi maana she was expecting so much to be married by that guy ila kachemsha mahali mambo yamemgeuka.
Ishatokea na kuifuta huwezi so vumia tafuta wako uendelee na maisha
Pole sana mamiii....! Ninavyoamini mimi ni kwamba kambi zingine zote zinaweza kuvunjwa kwa amani na zikavunjika milele...! Lakini sio kambi ya mapenzi...! Hivyo, inaonekana kambi yenu mliivunja kwa amani mkiamini kuwa inawezekana, na sasa uhalisia unakushinda....! Wahenga walisema usinyee kambi, lakini sio ya mapenzi...! Makosa uliyoyafanya ni haya;Aliyekuwa boyfriend kaoa tokea January this year, lakini nimeshindwa kuabsorb hii hali, mbaya zaidi tunaishi mji mmoja so mara nyingi namuona. Wadau kama ilishawahi kukutokea, ulichukua hatua gani kuiona ni ya kawaida. Najua maisha lazima yaendelee lakini duh, roho inauma jamani, the thing is haunting me badly.
Mmekutana nae Januari tu na kishakumwaga na kuoa mwingine,ujue huyo alikuwa hajatulia.Ni ajabu pia na wewe kuwa unammiss mtu uliyekaa nae kwa muda mfupi hivyo,wapo watu wanatoswa after 5 yrs +.Pole.
mawasilino nilishakata sihitaji tena,namba ya simu ipo kichwani kuifuta sitaweza, maeneo yote tuliyokuwa tunaenda nayaepuka na zaidi anaonekana maeneo hayo na mkewe, hili ndio linalotaka kunitoa roho, kwa kiasi nilichokuwa nampenda naona kama ndio kwanza kaoa jana.