How Air Tanzania Should be Restructured


For more information unaweza kunipata katika pundamilia@rocketmail.com
---------------------------------------------------------------------
 
Last edited:
Hapana mkuu wangu haikuhusiana na ATCL kusimamishwa hata kidogo.. Kama ingewezekana basi Precision wanakwenda Mwanza angenambia wanaweza kunipa ticket from TO - London - Dar -Mwanza na kurudi - Kweli nataka kusafiri na niliposoma maelezo yako ilikuwa kama umeniamsha!..

Ni mazungumzo ya muda mrefu nimeongea naye na kanambia UPO ushirikiano mkubwa sana baina na mashirika ya ndege na ndio maana unaona connection zinajulikana hata nje..ndege na flight zinapangwa kutokana na abiria wanaotegemewa na kadhalika pia tukumbuke kuwa kila ndege ina nauli zake wakitumia hata fedha local hivyo ni lazima kuwepo na makubaliano kabla hujabeba/ kusubiri ndege au abiria wa mtu..Anyway story ndefu ya nini wakati swala ni ATCL..

Mifano hiyo yote ya ushirikiano kanipa kutokana na maswali yangu.. Mkuu unajua nikisha simama ktk ubishi na hata nimekutumia wewe kumwambia mbona nimeambiwa inawezekana!..jibu la mwisho haiwezekani isipokuwa naweza kwenda hadi Dar na schedule wanayo lakini hawezi kunihakikishia usafiri wa Mwanza kwa sababu hana data zake wala hakuna ushirikiano na shirika la huko bila kulitaja shirika la ATCL ambalo yeye halijui kama lipo wala ni Airline gani zinafanya kazi TZ.
 

Mkandara,

Huenda umeoongea na kanjanja, hebu muulize anatumia mtandao gani wa reservations? Galileo au Amadeus? halafu mueleze akutafutie careers/operators katika route ya DAR-MWZ kama hataona hapo basi umeuliza a wrong person.

Pili, unapokata ticket katika route ya DAR-MWZ fare yake inaonekana katika hiyo reservation system kuwa ni kiasi gani. Abiria abiria anaweza kulipa nauli yake hukohuko alipo kwa kutumia currrency inayotumia kwenye nchi ambayo ni equivalent na ile inayooneshwa katika reservation system. Masuala ya kuconvert hufanyika IATA Clearing House baada career ku-bill aliyepokea pesa.
 
Well, Mkuu alichonambia ni kwamba BA itanifikisha Dar.. Mwanza haiwezekani hana connection na nilipotumia maelezo yako ndipo aliponipa hizo habari za franchise, codeshare partners na Allience kati ya mashirika ya ndege hakugusia kabisa IATA kuhusika na uwezekano wangu kufika Mwanza.
Kama nilikuelewa IATA inahusiana na malipo yaani fedha na ndio maana nikasema hiyo clearance ni sawa na benki sio mpangaji wa ushirikiano wa mashirika ya ndege..
Hata hivyo, nitajaribu na Agencies wengine maanake nilizungumza kwa simu na BA wenyewe...sijui wanatumia mtandao gani lakini ofisi yao iko Airport.
 

Management, Management, Management

Kuna uwezekano mkubwa matatizo ya uongozi yanatokana na schoolarship zetu na utamaduni tuliokuwa nao.

Katika mji ninaoishi kuna jumuia nyingi za kitanzania. Lakini hakuna hata moja naweza kusema iliyokuwa na mafanikio.

Jumuia nyingi zinaanzishwa na sherehe kubwa na zinapotea bila kuelewa zimepotelea wapi. Na baada ya kupita muda fulani wengine watazifufua na kuziacha tena kufa.

Nilihamua kufanyia utafiti wa kufa hizi jumuia. Nilichogundua ni kuwa miundo ya jumuia hizi ni sawa kabisa. Kutakuwepo na Mwenyekiti, Makamu, katibu na kamati zenye wenyeviti na makatibu.

Na miundo hii inafanana kabisa na miundo ya jumuia nilizoziona Tanzania nikiwa shuleni au vyuoni. Ni copycat ya TANU/CCM na jumuia zake. Hakuna innovation yoyote.

Kwa maoni yangu binafsi yanayotokea ATC ni-reflection yetu. Kwa miaka mingi tumefananisha siasa na uongozi. Tumefaninisha usemaji wa maneno mengi na utendaji.

Pale tutakapokubali kuwa management ni art yenye kutumia innovation hatutakwenda mbali. Tutaendelea kufanya kazi kwa utamaduni uliopo sasa.
 

Mkuu Mkandara,

Ninazielewa taratibu zinazotumika katika safari za anga kikamilifu. Ninachangia nikiwa na uzoefu wa kutosha kuweza kuelimishana kupitia katika forum hii. Ninajua siwezi kuwa mchangiaji bora katika masuala yanayohusu utabibu, military nk lakini katika hili ninaweza kuchangia kwa kina.
 
Well, sijasema huna uzoefu, as a fact mimi ndio kabuntas ktk maswala ya ndege na taratibu zake na ndio maana nimeuliza kuhusu usafiri wangu kutoka hapa nilipo kwenda Mwanza baada ya wewe kunambia inawezekana..I had no clue kuwa inawezekana/ haiwezekani zaidi ya experience yangu.
Ushirikiano kati ya mashrika ya ndege upo mkuu usikatae... nachoshindwa kuelewa ni kwa nini kuwepo na Allience, au Partnership kati ya mashirika ikiwa kila ndege inaweza kuchukua abiria wa ndege yoyote maadam ni mwanachama wa IATA..
Pili sidhani kama kuna shrika la Commercial Airline ambalo sii mwanachama wa IATA na likaruhusiwa kufanya kazi, hilo pia ni jipya kwangu..Labda unipe somo wewe kwa nini kuna ushirika wa Allience au Partnership, kisha maelezo ya huyu mama wa BA pia yamechangia kunionyesha kwamba ATCL inaweza kujoin mashirika makubwa ktk kuunda Allience ili kuzidisha ufanisi wa usafiri wa ndege zake na pengine kuongeza soko lake ndani na nje kama mashirika mengineyo i.e Kenya Airways na Ethiopia zinavyofanya..
 

----------------------------------------------------------------
 
Sawa mkuu,
1. This is what I'm talking about! - halafu soma hapa Airline alliance - Wikipedia, the free encyclopedia
Si lazima unapofanya biashara ya usafiri wa anga uwe mwanachama wa IATA. Kuna kundi la wasafirishaji huitwa Non-IATA members ambao hufanya biashara kama kawaida
Unaweza kunipa jina la shirika ambalo ni Commercial Airline na sio mwanachama wa IATA..ni ktk kujifunza tu mkuu usiwe na homa ukafikiria labda nafanya utani..SIJUI..
 

Nyavu hizo hapo chini kavue samaki mwenyewe kwa kadri utakavyoweza, unaweza ku-google utakavyo.

Member airlines and non-IATA carriers worldwide. ... Office addresses of IATA Members (including telephone. and facsimile numbers) and a list of the ...
[media]www.geocities.com/anairline/turist.pdf[/media] - 375k - Cached
 
Pundamilia 07,
Mkuu sasa unafanya utani mbona hiyo link inanipeleka kusiko?..
Anyway tazama ile link niliyokupa utaona kwamba kuna mashirika kama Kenya Airways ina Allience ktk Sky Team wakiwa na mashirika mengine makubwa ambayo hawawezi kabisa kushindana..Pia kuna mashirika kibao kama hilo Adria ktk Star Allience limekuwa likifanya kazi kwa hasara na lina ndege 12 tu lipo pamoja na mashirika makubwa..

Bado hatujazungumzia kabisa partnership ambayo utakuta mashirka haya haya yakirudiana ktk Allience tofauti kwa mfano Air Canada na BA..hizo partnership za nini?..yaani hata sielewi mkuu wangu kama IATA ndio kazi yake kuunganisha connections za ndege zote wanachama.

Mkuu kama ulikuwepo nimechukua muda kusoma mahusiano ya haya mashirika na inanipa picha kabisa kuwa IATA clearing unahusiana zaidi na transaction za malipo within hizi Airline na sio uhusiano kati ya mashirika ktk Usafiri. Na mwisho utaona shirika kama Emirates na Air India hawapo ktk ushirika wa Allience yoyote wakati kuna mashirika madogo sana yamejiunga.
Sasa my conclusion, maadam umekataa kunipa darasa nafikiri kwamba inawezekana kufika Mwanza kwa KLM..Nafanya ku guess tu lakini nadhani inawezekana nikapata ticket ya kwenda Mwanza kwa KLM kwa sababu ya Allience kati yao na Kenya Airways ambayo ina hisa zake Precision Air jambo ambalo halikuwezekana na BA..
Utanisamehe mkuu, kweli nafanya ubishi lakini hii yote inatokana na majibu yako kuwa nje zaidiNa kikubwa zaidi ni imani yangu kwamba ATCL inaweza kabisa kufanya kazi vizuri maadam kuwepo na mikakati madhubuti bila kui underestimate kwa sababu tu ya udhaifu wa viongozi wake wakati Asstes zake tu zinaweza kufikia mabillioni ya fedha ambazo tunaweza kuzipoteza kutokana na uzembe wa kutofikiria mbele..
 


Umegusa penyewe haswaaa!!
Si unajua tena ATCL from ATC which was a parastatal..depending heavily on subvention kutoka serikalini.Si unajua pia kuwa parastatals uedeshajaji wake ulivyokuwa? sidhani kama walikuwa wanaelewa kitu kinachoitwa faida/profit au bottomlines.Kwa vile hakukuwa na drastic changes kiutendaji na hata kwenye mindsets za watendaji basi wanabehave kama kampuni ya umma ambapo wanadhani kazi yao ni kuwepo pale, ku enjoy na si kufanya faida.Ni kama mtoto anayenyonya weeeee na mama akamwendekeza... hataacha ziwa! Its high time serikali wateue watu wenye uwezo wenye track record kiutendaji... wawape mamlaka kamili kiutendaji na kiundeshaji - ili management ichukue hatua watakazoona zinafaa ( be it retrenching staff, ) serikali iwape kianzio na baada ya hapo waendeshe shirika katika namna itakayoleta faida. Kadhalika hao watendaji wawajibishwe pale ambapo hawafanyi faida.
 

---------------------------------------------------
 
Pili, as of today ATCL ni kama haina assets kwani it's technically bankrupty. Kama hawawezi kuwa-bailed out assets zao zitauzwa kufidia madeni
Sawa mkuu nimekusikia...Anyway tuachane na haya hayana mpango mkuu wangu.. ATCL iwezeshwe kujitegemea..
My 2 cent...iwekwe ktk soko letu DSE, hata kama kwa kuanzia share zikiuzwa Tsh500 au 1000 kwa share blaa! blaa! blaa! wawekeshaji wapo I'm sure na zitakuja panda baadaye kwani soko lipo hakuna haja ya kuambiwa zaidi.
Swala la Emerites au Gulf Air ni gumu tu upande wetu sisi kwani nijuavyo mashrika makubwa hupenda kuyameza mashirika madogo ili wapate kushindana sehemu husika..
KLM, Kenya Airways na Precision Air ni tishio kwa mashirika mengine na ili yapate kushindana inabidi nayo yafikirie njia mpya za kutawala soko la East Africa.
Kwa hiyo tunaweza kujenga ushirikiano wa aina fumani na mashirika makubwa ambayo yanaweza sana kutusaidia ktk vifaa na taaluma nyingine zinazoendana na biashara hiyo..Ni imani yangu hili linawezekana.
Pili, kabla ya yote haya serikali imwage stimulus ktk bajeti yake kuokoa shirika..Uuzaji ticket ufanywe na ofisi za mashirika ya Tourism Agents badala ya ofisi za ATCL.
ATCL technically haikuwepo, tuliingia bankrupt toka siku ATC tulipoamua kujiunga na SA.
 

WoS:

Nakumbuka miaka si mingi iliyopita wabunge fulani walitembelea Ethiopia. Baada ya kuona uwanja mzuri, tayari nao wakataka Tanzania iwe na state of the art Airport.

Nadhani na hiki ndio kitu kinachotusumbua. Tukiona mwenzetu kafanya vizuri, hatutaki kuelewa siri ya mafanikio yake bali tunataka kupata vitu vizuri.

Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Addis Ababa umekwenda sambasamba na ukuaji wa shirika lao la ndege.

Kwa mfano wakati Ethiopia hiko kwenye civil war kwa miaka mingi na wakati mwingine vita vilikuwa ndani ya Addis Ababa, Ethiopia Airline iliweza ku-weather matatizo yote. Shughuli zote zilihamishwa nje ya nchi, ndege zikawa zina-operate kutoka Dubai na nyingine Europe.

Sidhani kama Tanzania kuna managers ambao wanaweza kufanya entities wanazoongoza kuwa resilient kiasi hicho.
 

Hivi benki zimewekwa za nini mpaka watu wakopeshane hela zote hizi zikiwa za shirika....nadhani huu ulikuwa ni uchumaji watu walijiandalia wakijua kuwa shirika halina muda mrefu.
 

---------------------------------------------
 
Last edited:

Za10,
Inasikitisha kwelikweli..... mambo ya ad hoc siku zote hayawezi kuleta manufaa wala kuwa sustainable......
unazungumzia miaka ya nyuma... halafu kama ni kuwa na state- of -the -art airport Addis, its a recent development licha ya kwamba ET ina zaidi ya miaka 100 toka iazishwe na bado inadunda.Mimi nimejaribu kuangalia hata viwanja vyetu vya ndege... utaona kabisa hakuna sense of planning for the future..DIA ilivyojengwa in the early 80s ndio imebakia hivyohivyo na inazidi kuminywaminywa kwa kuongezewa ugly structures kila kukicha... vijibadana na vikontena kila mahali...( na wahusika kila leo unawasikia wanasafiri nje ya nchi kwenda kujifunza..sijui wanajifunza nini na wanakuja ku apply vipi!)..

Angalia uwanja wa Zanzibar..hapo tena ni shughuli! Kinachoshangaza ni kwamba pamoja na kusikia kuna mipango ya kuupanua.... kuna watu wanajenga tena si ujenzi mdogo..karibu kabisa na airport...hii maana yake sijui ni nini.... au ndo mbinu za kuja kudai compensation hefty?
Anyway coming back to our national carrier.... may be a divine intervention will salvage the situation.Tusubiri tuone.
 
Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na haya yote; lakini kwanza ningeona serikali iuze hisa za ATCL kwa Watanzania au mashirika ya kitanzania ili iendeshwe kibiashara na umiliki uwe mikononi mwa watu wanaojali faida inayotokana na huduma nzuri.

Naam!

Laiti kama maneno haya yangepewa uzito unaostahili, tungeondoka kwenye huu ujima haraka kuliko njia nyingine yeyote. Kama walivosema wenzangu, tatizo siyo fedha, tatizo ni uendeshaji...

Kuuza hisa kwa Makampuni na Watanzania binafsi kutakaribisha mchakato wa kuondoa udhaifu huo wa uendeshaji, haraka! Na KUPE huyu ataacha kuendelea kutunyonya damu yetu kidogo tuliyobakia nayo. Siyo hivyo tu, muda si mrefu faida itaanza kuonekana, na Hazina kupitia TRA wataanza kujumlisha, siyo kutoa!

Neema kwa Watanzania itaanza kuonekana, badala ya laana!!!!
 
Tatizo la ATCL sio kukosa mtaji na wala sio kukosa wateja, tanzania kuna route ambazo bado zina abiria wengi sana kama wakuwa serious. Kitu cha msingi ni Raisi wetu haachane na wazee wake waliozoea kula pesa za mashirika ya umma.

Anatakiwa kuchagua vijana ambao wana new drive katika operation management, makata amesoma operation mara ya mwisho wakati challenge za operations kwa tanzania zikiwa ni kubeba abiria bila kujari mambo mengine.

Tunatakiwa kuwa na mtu anayejua jinsi ya kubalance costs, time and quality wakati akiacha quality na time videtermine costs. Vinginevyo hilo shirika halitasimama lenyewe hata siku moja maana wanachojua ni kukusanya mapesa wa abiria bila kujari kama ndege itasafiri au haipo na kama haipo abiria anakaa wapi anakuwa compesated vipi kwa muda aliokosa ndege.

Mfano mzuri ni mkurugenzi wa KCB tanzania he is just a young man but doing well in business compared to wazee tuliozoea kuwaona wakiongoza mashirika kumbe ndio wanayamaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…