How Air Tanzania Should be Restructured

Pundamilia07:

Nadhani posti yangu nilitumia misamiati inasemekana/nilivyosikia. Hivyo sikuwa na authority au sikuweza authenticate kile nilichosema. Nimesema kama rumor.

Zakumi,

Nimekupata mkuu!!
 

Hili nimelieleza kuwa ATC isingeweza kuuza hisa kwa sababu ya sera zilizokuwepo awamu ya kwanza

The bottom line ni kuwa ATCL inahitaji kugeuzwa ili iwe profitable na kuweza kuwavutia wawekezaji wa maana na vilevile iaminike hadi kufikia kukubalika kuwa listed katika soko la hisa ili na akina sisi tununue hisa tufaidike na shirika letu. Viongozi wanaopewa dhamana yakuongoza mashirika yetu halafu wanayapeleka kupata hasara kwa hakika wanawanyima watanzania haki za kuweza kuyamiliki mashirika hayo.
 

Sweetbaby,

Ni kweli hawa waheshimiwa walijikopesha hiyo mikopo kutoka katika fedha za ATCL?

Kama hivyo ndiyo basi Serikali inapaswa kueleza kadhia hii sambamba na wakati huu ambapo kuna matatizo ya kiuendeshaji hapo ATCL. Kutotoa taarifa juu ya jambo hili itakuwa ni makosa makubwa kwa upande wa serikali. Hata kama hizo pesa walizipata kutoka katika financial institution basi taarifa ni lazima iwekwe wazi.

Ikumbukwe kwamba tayari pesa za serikali zimekwisha pelekwa ATCL na huenda nyingine ziko njia kwenda huko, ni vema hili la kujilopesha likawekwa wazi.
 
Pundamilia07,
Mkuu samahani ni wewe ambaye hukunisoma vizuri..maelezo yako hayo hapo juu ndiyo kitu nalichozungumzia muda wote huko nyuma.. Kisha sio sheria za IATA kubadilihana abiria mkuu hata kidogo ni mikataba baina ya mashirika mawili kuhusu usafirishaji wa Abiria. iwe kuna Ubia ama makubaliano ya contracts..Naelewa fika kwamba mashirika yale yote hayafiki tena Tanzania lakini abiria wake wanakuja na mashirika mengine tofauti na wakati wa Nyerere..Lakini mkuu wangu my point is, huwezi kusafirisha abiria wa shirika fulani wakati fedha imelipwa nchi nyingine ni lazima kuna makubaliano kati ya mashirika mawili jinsi ya kugawana mapato ya msafiri mmoja aliyesafiri kwa ndege mbili za mashrika mawili tofauti..Na sio swala Huo ndio Ubia naozungumzia mimi, na sielewi unaposema Emirates wangekwisha nunua hisa ikiwa ATCL sio public sokoni, hizo hisa watazinunua vipi ikiwa hujapeleka mali yetu sokoni? ..
Mkuu Emirates wanahitaji abiria zaidi toka Tanzania ikiwa kuna uwezekano wa kuvunja masoko ya ndege nyingine zilizobakia..tunaweza kuwa regional (Tanzania) partner wa Emirates with our goals being connection Tanzania and the world, na wanaweza tu kukunua hisa pale tutakapo tangaza kuwa Public soko letu DSE..Kitu muhimu kwao ni soko, vitu kama
Ebu wewe nambie mkuu wangu kam Unaishi Mwanza na unaweza kuapata ticket ya kwenda London bila kuja Dar utaacha kusafiri na ATCL toka Mwanza kuja Dar au Kili na kuunganisha na Emirates?.. Je ni Watanzania wangapi watakao penda kufanya hivyo (air of their choice) badala ya kuja Dar kutafuta ticket za BA, KLM au Swiss Air ambazo hatuna mpango wa kubadilishana nao wasafiri kama ulivyozungumzia hapo juu!
Bila shaka mauzo ya ticket za Emirates zitaongezeka..Emirates hawana haja ya kufahamu ATCL ina mtaji kiasi gani isipokuwa tunaweza vipi kuongeza soko lao nchini.. ATCL itakwenda nchi jirani na kuvuta wasafiri wa Emirates nchi za Asia na Ulaya na pengine hata sisi ATCL kuwa na ndege moja kwenda Dubai kila siku..
Ndivyo mashirika yote yanavyoshirikiana mkuu wangu Ubia unakuja tu kwa kutazama thamani ya soko lililopo, vitu kama Load factor, Revenue, seat miles na kadhalika of which I'm pretty sure tupo juu safi, bearing in mind population yetu na matatizo ya Usafiri mwingine nchini.
Again nitarudia kusema tatizo la ATCL ni UONGOZI mbaya nothing to do with shirika ATCL..soko na mali zake zote ziko safi..Kama vile Tanzania yenye Utajiri mkubwa lakini ndio nchi maskini iloshindikana kutokana na Uongozi mbaya... Potential ipo na ndiyo inawasukuma wawekeshaji kumiminika nchini kwa sababu hatuna tena policies za Ujamaa (mkono wa serikali).. Aliyesubiri kuona Tanzania ikiinuka kwanza would be the looser mkuu wangu..Tanzania itainuliwa na wale walio take risk na ndio watakaofaidika na uwekeshaji wao.. Tukisha pata mabawa tu kila kitu kitakuwa ghali na hakuna tena mwalimu..

Sasa ukifikiria njia ya kuondoka Umaskini huu ni kuuza nchi kwanza badala ya ku deal na main problem utakuwa hujafanya kitu zaidi ya kupoteza kila kitu kama tulivyopoteza madini..Watu walinunua share za Barricks mara tu waliposikia wameshinda mikataba fulani ya machimbo.. kabla hata hawajachimba shimo moja mkuu wangu lakini kila siku zinavyokwenda na utajri kuzidi ndivyo share zake zinavyosidi kuwa ghali kwa wananchi..Hivyo swala la ATCL sio swala la Innovation ni swala la kufuata mfumo uliokuwepo sasa hivi duniani.. mashrika yote unayoyaona ya ndege yalitoka mikononi mwa serikali na kuingia ktk soko huria wakati biahsra ya ndege ilikuwa ikitumba..Watabiri wa wall street hutazama mbele na sio kitu ambacho tayari kinazalisha na risk ni ndogo, faida yake huwa ndogo sana..
Swala la uongozi mbaya ndani ya ATCL ni swala ambalo linaweza kabisa kumalizwa within one month of operating. Wakisha ingia wajuzi wa biashara na kuwekesha fedha zao utaona mwenyewe mabadiliko sehemu zote za uzembe..trust me.

Niliyoaandika kuhusu Nyerere ni kwamba hapakuwepo na makubaliano ya namna hii ndio maana mashirka hayo yote yalileta ndege zao. Sasa uliposema kwamba Ubia kati ya KLM na ATC ulitakiwa toka wakati wa mwalimu ndipo niliposema isingewezekana kabisa kwa sababu mbali na siasa zetu mfumo huo haukuwepo kabisa duniani..sijui kama umenielewa hapo..
 
Kwanza, biashara ya ndege siwaachii wazee. Nitawatafuta vijana wa miaka 30 -37 waliowahi kuwa marubani na wenye MBAs au Menejimenti digrii yoyote.

Ningeligawa shirika katika:
i. Uchukuzi mizigo
-ndani ya nchi
-kati ya nchi za Afrika Mashariki
-na nchi za nje
ii. Usafirishaji watu
-ndani ya nchi
-kati ya nchi za Afrika Mashariki
-na nchi za nje

Ningelianza biashara ya ndani na kuhakikisha magazeti, barua, fedha na vifurushi, vyakula, nguo na bidhaa nyingine vinafika katika asilimia 75 ya Tanzania asubuhi saa 12 siku ifuatayo.

Kisha ningelianza kusafirisha mizigo toka na kwenda nchi jirani.

Halafu ningezipa boost EPZ marehemu zilizopo mipakani kwa kuhakikisha kuna dege moja kubwa toka China, Malaysia, Korea, Japan kwenda na kuja Tanzania kila wiki.

Ninaamini mapato kutoka sehemu hizi yatanisaidia kuhakikisha kuwa vijidegee vya Precision sijui Community ninavipa overtime kila siku kwa maana ningelivuta kila Mtanzania mwenye kipato kiwe kidogo namna gani kutamani kusafiri kwa divisheni ya ATC Nafuu Services!

Ningelianzisha divisheni ya helikopta za kivita na kuzigeuza kuwa za usafiri na uchukuzi ambazo Barack Obama atazifuta kazi akiingia Ikulu ya Marekani.
 
Akili,
Kwanza, biashara ya ndege siwaachii wazee. Nitawatafuta vijana wa miaka 30 -37 waliowahi kuwa marubani na wenye MBAs au Menejimenti digrii yoyote
Duh! sasa wewe mkuu wangu umeniacha nje kabisa!.. yaani unafikiria rubani mwenye MBA anaweza kuwa rubani mzuri kuliko yule ambaye hakusomea digriii au sio..
Hivi kweli unaamini kabisa mtu mwenye digrii ya MBA ni dereva mzuri wa gari kuliko yule ambaye hana digrii!.. au una maanisha kitu gani!
 

Haya ya Emirates kuingia ubia na ATCL, ah kwangu mimi sioni uwezekano wa Emirates kufanya hivyo kwa sasa kwani tayari wana-dominate soko na hakuna threat ya aina yeyote.

Tuendelee kukata issue
 
Last edited:
Haya ya Emirates kuingia ubia na ATCL, ah kwangu mimi sioni uwezekano wa Emirates kufanya hivyo kwa sasa kwani tayari wana-dominate soko na hakuna threat ya aina yeyote.

Tuendelee kukata issue

Pundamilia07:

Unasema kuwa sheria za wakati ule zilizuia KLM kuchukua ATC. Naomba unieleze kama Tipper lilikuwa ilikuwa chini ya serikali ya Tanzania au Italy walikuwa na hisa pia. Vilevile naomba data za Tanzania Investment Bank. je serikali ya Tanzania ilikuwa na 100% au Ujerumani ilikuwa na hisa pia?

Kama makampuni hayo yalikuwa hayamilikiwi na serikali kwa 100%. Kwanini sisi tulichukua mzigo wa 100% katika kitu tusicho na expertise nacho?
 

Nadhani iko haja ya kujikumbusha juu ya TIPER na TIB kama ambavyo umeelezea japokuwa si hayo mashirika mawili tu uliyoyataja. Kuna zaidi ya hayo just few to mention NHC, TFC nk.

Tofauti ya ATC na hayo mashirika uliyoyataja ni kwamba yalianzishwa kama sehemu ya msaada baina ya serikali ya Tanzania na nchi husika. Hata serikali ya Uholanzi ilikwishafanya jambo kama hilo pale ilipotoa msaada wa kumalizia Jengo ambalo lingelikuwa ofisi mpya za East African Airways ambalo sasa linaitwa ATC House yalipo makao makuu ya ATCL. Jengo hilo lilimaliziwa na waholanzi na pia ndiyo waliojenga Kilimanjaro Aircraft Maitenance Facility pale KIA.

Kwa case ya ATC shirika hilo lilianzishwa moja kwa moja na serikali na haikuwa ni mradi wa msaada kama ilivyokuwa hayo mashirika mengine uliyoyataja.

Kuhusu swali lako la kwani serikali ilichukua mzigo wa mia kwa mia katika kitu tusicho na expertise nacho, hapo nadhani unakosa kuirejea historia ya kuanzishwa ATC.

ATC ilianzishwa mara tu baada ya iliyokuwa Jumuiya Afrika Mashariki kuvunjika. Tanzania kama ilivyokuwa nchi nyingine za Kenya na Uganda ilikuwa inategemea usafiri wa anga kupitia East African Airways. tanzania kama nchi mshiriki ilikuwa na wataalam wengi tu kuanzia marubani, mafundi (Akina Michael Shirima), watalaam wa uendeshaji, wataalam wa masoko na mauzo, wataalam wa Ground handling & cargo etc etc.
Kwa hiyo serikali ilikuwa na jukumu la kuzikusanya hizo resources ili ziweze kufanya kazi kwa manufaa ya watanzania wote, ndipo Marehemu Jaji Yahya Rubama alipopewa kazi ya kusimamia ATC inazaliwa na kufanya kazi.

haya ni kwa ufupi lakini ATC ina historia ndefu na ya kutukuka kwa upande wa wafanyakazi waliowahi kuwepo hapo na wale waliopo.
 
Pundamilia 07,
Duh, mkuu wangu kazi kweli kweli kukufahamisha nachojaribu kusema..Mkuu navyofahamu mimi IATA clearing House inafanya kazi kama benki vile yaani nyie mna makubaliano yenu kwanza na transaction za kubadilishana malipo wanafanya wao..Lakini sio IATA inayopanga Ubia wa mashirika husika. Ni jukumu lenu kuunda huo ushirikiano, kama vile mimi leo hii bill zangu zinapitia Benki moja kwa moja na pia malipo yangu kupitia benki moja kwa moja lakini sio benki iliyoweka mkataba wangu na kampuni ya simu, cable na hata ajira yangu...

Tukirudi ktk swala la Tipper na mengineyo ninavyofahamu mimi au niseme kuelewa kwangu ni mkataba under contract uliofikiwa baina ya serikali yenu na nchi hizo zilipotupa mikopo ya kuunda miundombinu hiyo. Na serikali za nchi hizo ziliweka mashirika ya kusimamia ujenzi na uendeshaji wa mashirika hayo kama ilivyo TAZARA lakini serikali ya China haina hisa ndani ya shirika hilo..Tulifanya hivyo hata ktk mashamba ya katani, kahawa na kadhalika na nakumbuka mwalimu wakati wa Azimio la Arusha alianza kuwatimua baadhi wazungu tukashika wenyewe wafujaji.. tukaua kilimo na mashirika mengine mengi tu lakini kama hawa jamaa wangekuwa na ubia ndani nina hakika kesi zile zingekwenda UN..kama tulivyopelekwa ktk mkataba wa Citywater..
Kuhusu KLM kuingia Ubia umetumia South Africa nadhani hatuelewani hapa. Nachozungumzia ni wakati wa Nyerere kwanza na pili Emirates wasingeweza kununua share ATC kama South Africa kwa sababu Ubia huo ulikuwa kwa tender na sio soko huru. Hivyo ilitegemnea sisi tutamchagua nani..kama ilivyokuwa Richmond au mashirika mengineyo..

Tunarudi palepale tu kuwa Ushirikiano wetu na Emirates sio lazima wao wanunue share kwetu ila inawezekana kukawepo na partnership kutokana na soko tulilokuwa nalo sisi..Muhimu hapa kwa Emirates ni Umiliki wa chombo hiki na soko letu kwao sio hali ya chombo ATCL kwa sababu hatuwambii wanunue ATCL..
Kivutio kikubwa kinaweza kuwa tukienda public na kuunda upya management yenye mwelekeo..Na zaidi ya hapo Emirates wanaweza sana kutusaidia ktk kupanga malengo mapya, mfumo mpya wa utawala, mafunzo na kadhalika.. haya yote yanawezekana kabisa..
Mkuu wangu hapa kwetu Air Canada ni mbovu kupindukia yaani unachefua roho na Uongozi wake ni mbaya ajabu lakini wanashirikiana na BA vizuri tu.. Kuna wakati shirika lilianza kufirisika, ilibakia kidogo wamuuzie Mchina sijui Mjapan lakini serikali ikaingilia kati wakaweka stimulus ndani kuokoa jahazi, wakabadilisha hata management nzima na mambo kibao wakati huo huo BA haikuwa na tatizo hata moja na walikuwa wakingiza faida..Sikusikia BA wakijiuliza kuingia ubia huo na Air Canada ambayo ilikuwa ktk hali mbaya sana kuongozi na hata service zake ni mbovu hadi leo hii..
 
forget to partner with Emirates

they can codeshare - that means TC will put its code on EK flights in and out of DAR

or Interline - this is the new way. if you interline if other airlines such as BA and EK, you can sell one ticket from TC destination such Mwanza to LHR where TC does not serve

so the flight from MWANZA to LONDON will be on on ticket.

and most important things Emirates will introduce to DAR is daily Boeing 777 - 300 ER which has a capacity of maximum 442 pax effectively from 29 of march where summer timetable starts. Emirates will almost doubled their capacity from their current flight Airbus 330 - 200 which has capacity of 250.

this proved that there is huge opportunity out of DAR.
 

Believe me, kuwa Emirates hawahitaji mshirika katika route ya Dar - Dubai kwani market share yao iko juu. Kinachotakiwa ni kwa ATCL iangalie kutafuta nafasi yake katika route hiyo na jambo hili litahitaji kufanyika utafiti wa hali ya juu na wala si vinginevyo. Moja ya yale ambayo unaweza kuyafanya kama ATCL inataka kwenda Dubai ni lazima 'umpigie magoti' Emirates umwombe unachotaka na hapo unaweza ukashirikiana nae lakini yeye ndiye atakaye command makubaliano. Huo ni ukweli Gulf Air aliyekuwa na nguvu sana alikimbizwa na Emirates, yuko wapi OmanAir?. What Emirates did, alinunua frequent flyers wa Gulf Air na ku-double mileages zao na wengine kuwapa Gold Card, na kuleta equipment ya kisasa kabisa katika soko la Dunia, sasa ikifikia hapo tena unataka nini zaidi ya kukubali atakalosema. Endapo utakubali analotaka Emirates basi ujue pia uwe tayari kukubali hata yale ambayo hayana maslahi kwa taifa na hii ndiyo abia ya mikataba kuna ku-gain na ku-lose ili mkubaliane.
 
Last edited:
Tanzania ianzishe kampuni mpya ambayo haina madeni na inasera mpya. ATC ifungwe na hii itakuwa njia rahisi.
 
Kufa ATC haifi....inasubiriwa kuanza tena kwa nguvu mpya....mapendekezo ya tume yatatoa mwelekeo wa hali ya mbeleni.Hopefully mapendekezo yanayotolewa hapa JF yataonwa na kuchagiza kitakachoamuliwa.
 
Pundamilia07,
Mkuu labda nichukulie kwamba unajua unachokizungumza lakini hadi hapa inaonyesha tunatoka ktk mada na kuanza kuijadili IATA..
Kifupi mkuu, Hivi unaweza kunambia mtu anaweza kukata ticket London BA ambaye ni member wa IATA na kuja hadi Mwanza kwa kuchukua connection Dar na ATCL ambaye pia ni member wa IATA kwa ticket moja alokata London?..kama inawezekana naomba somo na kama Haiwezekani naomba somo pia na hii (hai) ndicho nachozungumzia mimi ili kuiwezesha ATCL.

Swala hapa mkuu wangu ni jinsi gani ATCL should be restructured, bilichotazama mimi ni uwezo wa ATCL kufungua ukurasa mpya wa biashara na mifano yote ya Ubia na ushirikiano kama vile Kenya Airways na Precision..Ni swala la wewe kufikiria kwa nini Precision imeweka ushirikiano na Kenya Airways ikiwa kila member wa IATA anatakiwa kubeba abiria wa mtu mwingine wao watamaliza mahesabu ya malipo!..

Swala la mashamba, mkuu pia nimezungumzia Azimio la Arusha kama chanzo cha mabadiliko nchini haikuwa swala la Utaifishaji.. mfano, mashamba ya sukari Kilombero tuliingia mkataba na serikali ya Kiholanzi kuayendesha mashamba yale lakini hayakuwa yao toka mwanzo..sizungumzii nani aliyenyan'ganywa mashamba hayo kabla serikali haijawaweka Waholanzi..Azimio la Arusha halisisitizi tu Kutaifisha mkuu wangu isipokuwa pia kumwezesha Mtanzania kuendesha uchumi wa nchi yake, hivyo tulipowafukuza Waholanzi kutoka Kilombero halikuwa swlaa la kufaifisha isipokuwa kuwaweka wazalendo wananchi ktk utawasla wa mashamba hayo..hivyo kuuvunja mkataba ambao serikali ilikuwa iki own 100% ya mashamba hayo..

Mwisho swala la Emirates unakosa kitu muhimu sana nachozungumzia hapa..Lee hapo juu kazungumza exacctly nachosema mimi kuwa soko la Abiria Tanzania sio Dar.. wewe unatazama Emirates na Dar hakuna aliyesema tunataka ushirikiano nao kwa ajili ya safari za nje kuja Dar isipokuwa ni sisi tunaweza kuwaletea wasafiri wengi toka mikoani ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya wasafiri wote waendao nchi za nje..Kwa hiyo sisi tunachotazama ni kuijenga ATCL ktk safari za ndani na nchi jirani kwanza.. lakini hatuwezi kufanya hivyo bila kupata mshirika ambaye ana uwezo wa kwenda nchi za nje kwa hiyo tunachotazama sio kutoka Mwanza kuja Dar tu bali msafiri huyo aweze kutoka Mwanza hadi Dubai kwa ticket moja ya ATCL au kutoka Dubai hadi Mwanza kwa ticket moja ya Emirates..Bila shaka navyofahamu mimi hii ndio sababu Precision wameungana na Kenya Airways au Zambia na Swiss Air, nje ya hapo sioni sababu..
 
Kufa ATC haifi....inasubiriwa kuanza tena kwa nguvu mpya....mapendekezo ya tume yatatoa mwelekeo wa hali ya mbeleni.Hopefully mapendekezo yanayotolewa hapa JF yataonwa na kuchagiza kitakachoamuliwa.


WoS:

Kuna jamaa yangu, baba yake alipostaafu kutoka serikani basi akaanzisha biashara zake. Katika biashara yake akaleta mambo yake ya kiserikalini. Akachukua chumba kimoja na kukifanya ofisi. Akaajiri watumishi wa kufanyia kazi na kuwalipa mishahara. Mradi wake ulikuwa ni ng'ombe wa maziwa wawili tu na bustani. Auchukua muda mradi mzima ukawa finito.

Mambo yote ya tume uliyoleta hapa yamefanyika mara nyingi sana katika nchi hile yetu ya mababu. Lakini matokeo ni yaleyale. Ninaweza ku-bet na wewe, katika kipindi cha miaka mitano, shida za ATC zinatakuwa ni zilezile.

Mentality za watendaji wetu ni kama za baba wa jamaa yangu. wanafikiri kuwa kila kitu kikishakuwa katika nafasi yake basi mafanikio yatatelemka kama chakula cha wana waIsrael.

Kama hawatakuwa na model inatakayo-sustain growth na itayo-address kundi la wateja, hakuna kitakachofanyika. Mpaka sasa mashirika ya kiserikali hayajuhi wateja gani wanatakiwa na jinsi gani ya ku-sustain growth. Siku zote wakiona Ethiopia Airline, wanasema na sisi tuanzishe la kwetu.

Katika posti yangu moja nimesema hawa jamaa wanatakiwa kuiga Southwest Airline (period). Na wateja wawe local.
 
Zakumi,
Bahati mbaya sana katika nchi yetu kumekuwa na utamaduni wa diagnosis ya matatizo na hatimaye prescription kutolewa na "tume".Sijaelewa hasa mantiki ya utaratibu huu maana ni wazi kabisa kuwa matatizo ya ATC hayahitaji uvae miwani uyaone na kuyaelewa.Major prob ni management period.Kwanini hawaondolewi mara moja ( board na management) its very hard to comprehend.
Kama ulivyosema vema,uendeshaji wa biashara hii kwa miaka hii unahitaji watu wapya wenye mtizamo mpya wa jinsi ya kufanya mambo.Ukiangalia walioko katika kuendesha ATC ni watu wenye fikra na mtizamo wa 1947! wengi wao hawajawahi kuwa good performers mahali popote.If anything wamewahi kuwaangusha sana watanzania. Itakuwa ngumu.
 

------------------------------------------------------------
 
Kufa ATC haifi....inasubiriwa kuanza tena kwa nguvu mpya....mapendekezo ya tume yatatoa mwelekeo wa hali ya mbeleni.Hopefully mapendekezo yanayotolewa hapa JF yataonwa na kuchagiza kitakachoamuliwa.

Unadhanin watakuja na opendekezo gani jipya litakaloiokoa ATCL? nakuhakikishia hata kama mapendekezo yakiwa mazuri, utekelezaji utakuwa hovyo na matojkeo yake yanaweza kuwa mabaya kuliko tunayoyaona hivi sasa. Hivi ni tatizo gani la ATCL ambalo halijulikani? Kuna haja ya kuunda tume kutafuta ufumbuzi kuhusu katatizo ya ATCL? WIZI MTUPU
 
Pundamilia07,
Mkuu yote sawa...nimepiga simu ofisi ya British Airways hapa wamenambia wana issue ticket ONLY to Dar - Tanzania..siwezi kufikishwa Mwanza kwa sababu hakuna member wa timu yao anayekwenda huko...
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na connection kanambia wanaweza tu kunisafirisha ikiwa kuna mashirika ambayo ni franchise yao, ni codeshare partners wao pia kikubwa zaidi ni member wa network ya ushirikiano (Airlines Allience) ambayo shirika linatakiwa kuwa member au subsidiary wake kunifikisha Mwanza..Sasa sielewi kinachoendelea kama kanifunga kamba sijui lakini majibu yake ndio hayo siwezi kupata ticket moja hadi Mwanza - Tanzania.

Mkuu, hizo hesabu za asilimia 70 ya wasafiri wa ndege kwenda nje unafikira nimetunga!..Hata hivyo haiusiani kabisa na ATCL isipokuwa ni hesabu ambayo nimeipata toka chombo cha serikali hivyo siwezi kuiweka kama unavyodai kwa sababu sikuipata toka site fulani..
Nachokuomba chukulia kuwa ni kweli na jaribu kuangalia jinsi gani ATCL inaweza kufanya kazi zaidi kwa kushirikiana na mashirka kama Emirates kwa sababu nilizoandika mwanzoni..USHIRIKIANO . Iwe kwa kununua hisa, iwe kwa Ubia, iwe kujiunga na Allience yote kwangu ni sawa maadam tunaweza kusafirisha abiria wetu toka Mwanza< Bukoba moja kwa moja kwenda nje with a connection Dar au Kili..

Mkuu wangu Mashrika yote makubwa duniani mbali na ku run international flights yana mashirika madogo yanayo run ndani ya nchi zao iwe Uingereza, France, Japan au America na kuna ushirikiano kmkubwa kati ya shirika mama (International) pamoja na hilo la ndani (Local).. huwezi kuchukua Air Canada kuja Toronto au Vancouver ukaunganisha na shirika lolote la ndani ati maadam kuna ndege inakwenda huko..

Hata hivyo, tumeongea vya kutosha na ushauri wangu kwa serikali yetu ni kuliokoa shirika hili lakini badala ya kuliwekea regulations, wakati umefika sisi tuondoe hizo regulations ambazo hazihusiani kabisa na business Policies zaidi ya kuwepo mkono wa serikali ndani ya Uongozi wa chombo hicho..ATCL iwe huru (public private company) na viongozi wake WAPYA wapewe nguvu ya kuwa Responsible na Accountable..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…