Housegirl: Ushauri

Vituka

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
2,250
2,000
Habari zenu wana MMU,

Ninaomba mnishauri juu ya hili.

Nina mtoto wa dadayangu (mvulana). Kukweli nampenda sana kama mwanangu, kwanza kalizaliwa mimi nikiwa chekechea, nilimlea and honestly I love him very much. Alibahatika kupata kazi serikalini mwaka juzi, na baada ya miezi 6 alintambulisha mpenzi wake. Kiukweli sikufurahishwa na huyo mchumba kwani kwanza alimzidi 2 years, halafu mdada ameanza kazi 2004, yani anaujua mji ile mbaya. Isitoshe hata marafiki zake pia watata, ni wale masista duu wa bongo movie wenye skendo daily.

Baada ya kutambulishwa sikutoa comment yeyote ila after a week nkamtafta dogo nikamwambia awe makini sana mana wasichana wengi hapa town huwa sio wakweli, so amchunguze uyo binti kabla hajachukua uamuzi wowote ikiwa ni pamoja na kucheki afya zao. Dogo kiaina hakupenda ushauri wangu, ila kwa kila ndugu aliyemtambulisha uyo dada aliambiwa the same thing. Ni miaka 2 imepita sasa, dogo katuambia kuwa kaachana nae na kwamba yule dada hajatulia na hamfai.

Sasa, mimi nina a very beautiful, honest, smart, hardworking,God fearing and humble housegirl na ninatamani huyu my son amuoe. Je, nitumie njia gani ili hawa watu wapendane na hata waoane jamani/ Kiukweli the girl is good jamani, nimeishi nae for 2 years na kweli kama mzazi natamani iwe hivi ( NACHUKULIA ULE MSEMO USEMAO KIZURI KULA NA NDUGUYO). Tatizo moja tu, ameishia darasa la saba sasa sijui kama dogo atamkataa.

Nipeni mawazo wandugu.
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,520
1,225
Mwache mdogo wako achague kitu roho inapenda hata kama alikwishafanya uchaguzi mbaya hapo kabla,unaweza jikuta unaingia kwenye mgogoro ambao utawafanya mgombane kwa jambo ambalo linazuilika,kumbuka ua linapoamua kuchanua halilazimishwi vivo hivyo kwenye mapenzi,kama itatokea wakapendana basi watakuwa pamoja,mambo ya kuchakachuliana wapenzi kwa kisa tu umemuona huyo msaidizi wa kazi anafaa si mazuri maana ndugu yako anafaa afanye chaguo la moyo wake.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Mkuu WALIMWEUSI wewe unaweza kujikuta unaona ana vigezo vyote vinavyofaa ila mwache dogo afanye uchaguzi mwenyewe
Kama unataka amuone huyo dada just mwalike dogo hapo kwako bila hata kumwambia lolote awe anakuja mara kwa mara hapo kwako na kama kweli akivutiwa nae kwa yeye mwenyewe bila wewe kuhusika hapo ni maneno mengine ila usijiingize kabisa kumwambia dogo kuwa aoe huyo house gal wako
Mwache kama kutatokea aina yoyote ya mvutano wakutane wenyewe huko wewe usihusike maana yakija kumharibikia dogo hatasita kukulaumu wewe tena sana
 
Last edited by a moderator:

Von Mo

JF-Expert Member
May 7, 2012
1,820
2,000
Habari zenu wana MMU,

Ninaomba mnishauri juu ya hili.

Nina mtoto wa dadayangu (mvulana). Kukweli nampenda sana kama mwanangu, kwanza kalizaliwa mimi nikiwa chekechea, nilimlea and honestly I love him very much. Alibahatika kupata kazi serikalini mwaka juzi, na baada ya miezi 6 alintambulisha mpenzi wake. Kiukweli sikufurahishwa na huyo mchumba kwani kwanza alimzidi 2 years, halafu mdada ameanza kazi 2004, yani anaujua mji ile mbaya. Isitoshe hata marafiki zake pia watata, ni wale masista duu wa bongo movie wenye skendo daily.

Baada ya kutambulishwa sikutoa comment yeyote ila after a week nkamtafta dogo nikamwambia awe makini sana mana wasichana wengi hapa town huwa sio wakweli, so amchunguze uyo binti kabla hajachukua uamuzi wowote ikiwa ni pamoja na kucheki afya zao. Dogo kiaina hakupenda ushauri wangu, ila kwa kila ndugu aliyemtambulisha uyo dada aliambiwa the same thing. Ni miaka 2 imepita sasa, dogo katuambia kuwa kaachana nae na kwamba yule dada hajatulia na hamfai.

Sasa, mimi nina a very beautiful, honest, smart, hardworking,God fearing and humble housegirl na ninatamani huyu my son amuoe. Je, nitumie njia gani ili hawa watu wapendane na hata waoane jamani/ Kiukweli the girl is good jamani, nimeishi nae for 2 years na kweli kama mzazi natamani iwe hivi ( NACHUKULIA ULE MSEMO USEMAO KIZURI KULA NA NDUGUYO). Tatizo moja tu, ameishia darasa la saba sasa sijui kama dogo atamkataa.

Nipeni mawazo wandugu.

Fanya kutoka nao dina(mkiwa wote watatu), unafanya utambulisho, halafu unajifanya kama unapigiwa simu ya ghafla mara unaongea, unawaacha wawili kwa 30min, ukirudi utapata majibu kwa jinsi watakavyokuwa wanabehave, me najua mtu wa drs la saba anaweza kuelimishwa na kubadilika haraka zaidi, na hawezi kuchange ghafla kama wa mjini( waliokwenda shule).
 
MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,475
2,000
WALIMWEUSI pole kwa hilo ila ningependa ufahamu kuwa huyo house gal wako anaweza kubadilika siku yoyote coz huenda ameficha makucha yake pindi atakapompata huyo kijana wako mambo yakawa opposite na ulivyotarajia.

Pia tambua elimu sio tatizo sana endapo kijana wako amesoma anaweza kumuendeleza mwenziwe ikiwa tu wamesharidhiana.
 
Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Simple. Mtafute dogo, piga nae stori za apa na pale, then chomekea stori kumuhusu huyo hg.. mfagilie kwake ile mbaya. Ikiwezekana chomekea na stor za uongo kuwa alivyomwaminifu anawatoleaga nje wanaume kibao wanaokuja na magari. Mdanganye kuwa hata juzi tu kuna mshefa alikuja akataka kwenda kujitambulisha kwao aoe, lakini binti akasema hataki kwa sababu anataka aolewe na mtu wanaeendana, mpole na atakayemwendeleza kimasomo na kimaisha. Mwambie kuwa ulishawahi kuona wanawake, wasomi na wasio wasomi lakini hujawahi kuona binti kama huyu... Then, muachie hapo, anzisha stori zingine. Chomekea vistori vya jinsi wanawake wa siku hizi wanavyoweza kuharibu maisha ya mtu baada ya kuolewa. Then potezea kama vile haikuwa na muhimu sana... Nenda kwa binti, mdanganye kuwa mwanao anampenda sana lakini anaogopa kumwambia kwa sababu anamuona siriaz... Then fanya kila linalowezekana wakutanishe mara kwa mara kama mara 5 hivi... Then siku moja Nenda nae kwa dogo (kama anakaa peke yake) alafu muache humo kwa kudanganya kuwa utamfuata baadae. Baadae mpigie simu, mwambie kuwa hutaenda tena... aangalie kama ana mda marudishe om. Kama hana bas amtafutie pa kulala aje kesho yake...

(Natamani ningepewa mi hio kazi ya kuwasakizia watu)...
 
Heart

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
2,674
2,000
Wacha achague ile kitu roho yake inapenda...after all yeye ndo ataekwenda kuishi nae sio wewe. Kuna wanaume wanapenda mahusiano yawe na kash kash,wanapenda makanjanja..sasa ukimpelekea mtu amabae yuko doro kama wali wa jana anaweza akaona mizinguo tu....
 
IRINA

Member
Oct 24, 2012
23
0
Simple. Mtafute dogo, piga nae stori za apa na pale, then chomekea stori kumuhusu huyo hg.. mfagilie kwake ile mbaya. Ikiwezekana chomekea na stor za uongo kuwa alivyomwaminifu anawatoleaga nje wanaume kibao wanaokuja na magari. Mdanganye kuwa hata juzi tu kuna mshefa alikuja akataka kwenda kujitambulisha kwao aoe, lakini binti akasema hataki kwa sababu anataka aolewe na mtu wanaeendana, mpole na atakayemwendeleza kimasomo na kimaisha. Mwambie kuwa ulishawahi kuona wanawake, wasomi na wasio wasomi lakini hujawahi kuona binti kama huyu... Then, muachie hapo, anzisha stori zingine. Chomekea vistori vya jinsi wanawake wa siku hizi wanavyoweza kuharibu maisha ya mtu baada ya kuolewa. Then potezea kama vile haikuwa na muhimu sana... Nenda kwa binti, mdanganye kuwa mwanao anampenda sana lakini anaogopa kumwambia kwa sababu anamuona siriaz... Then fanya kila linalowezekana wakutanishe mara kwa mara kama mara 5 hivi... Then siku moja Nenda nae kwa dogo (kama anakaa peke yake) alafu muache humo kwa kudanganya kuwa utamfuata baadae. Baadae mpigie simu, mwambie kuwa hutaenda tena... aangalie kama ana mda marudishe om. Kama hana bas amtafutie pa kulala aje kesho yake...

(Natamani ningepewa mi hio kazi ya kuwasakizia watu)...

Yan wewe ndo unapotea njia kabisa. hamna bana asiwaunganishe in a direct way,tena asisugest chochote ubaya wa mtu na uzuri wa mtu kuukuta sio hapa,binadamu hatutabiriki,kama inawezekana mwalike ajionee mwenyewe,chema chajiuza bwana,unaibua vitu ambavyo vitawakutanisha nae lkn kumwambia direct NO,siadvise
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,216
2,000
Utampona huyo housegirl...
Mapepe huenda na mapepe mwenzie
huyo ndugu yako hajatulia ndo maana ali opoa mdada wa mjini

haikuwa bahati mbaya.....ndege wanao fanana huruka pamoja..

sasa wewe utamponza tu huyo housegirl....wakati labda atampata mcha mungu mwenzie..
 
The Bleiz

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
4,930
2,000
Mwache kwanza aangaike na mashangingi wamuumize kichwa halafu atajua tuu cha kufanya just let him decide his own destiny bhana.
 
everlenk

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
11,627
2,000
Ndugu usijaribu kabisa kulazimisha ubavu ambao siyo mahali pake,hilo zigo la lawama cjui utalibebea wapi, yalishatukuta kwetu mambo km hayo yana athari kubwa ktk maisha ya mtu usipime,wacha dogo aone kile kimfaacho na acha hg aende kule kny ubavu wake uliosahihi,km ni mapenzi ya Mungu itatokea tu wala haihitajiki jitihada yako hata kidogo.Tafadhali tafadhal achana na hiyo biashara kabisa!! Kazi yako iwe ni kushauri tu na si kumuamlia dogo.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
Hahahhaa, una balaa wewe. Na mie nna mlinzi mzuri kweli ngoja nimlengeshee kwa mdada ili asiondoke.
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,010
1,500
isshhh! Uko wapi wewe?

Ukipata dada mzuri, mlengeshe kwa mlinzi ama shamba boy, huwa hawaondoki asilani.

Unaweza wapa kianzio cha maisha tu.

hahaha, chezeiya subbotage. Nawajengea kibanda shamba wananitumikia for life.
Ila mbaya sana setting up people, mmpphhwwee!
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,010
1,500
umeona eeh, wanakuwa watumishi milele

siku ukipita mitumbani, unawachukulia watoto wao mitumba miingi.

hahaha, chezeiya subbotage. Nawajengea kibanda shamba wananitumikia for life.
Ila mbaya sana setting up people, mmpphhwwee!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
umeona eeh, wanakuwa watumishi milele

siku ukipita mitumbani, unawachukulia watoto wao mitumba miingi.
one thing najua nitafanya, watoto wao watapata digrii na watakuwa wajukuu wangu. Aisee, nna wanangu i am very proud of. Mama yao alikuwa maid kwetu, akasomeshwa nursing akaolewa. Wanae wawili wana digrii, na bhange zangu nimewainspire. Nikienda wanakofanyia kazi nadeka na mie, eboo! We are more than family.
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,290
2,000
ngoja nikwambie /nikuulize
1.nani alikuchagulia mwenzi wako wa ndoa!?

2.muache huyo binti achague mume mwenyewe na huyo kijana achague mke mwenyewe!

3.binti anaweza kuwa mzuri kwa tafsiri zako lakini ikawa kinyume na huyo mwanao!na mbaya zaidi anaweza kukubali tu kwa kuwa boss kasema!una hakika na hisia zake?

4.huyo kijana mpaka anadate na mdada wa mujhini ni wazi sio dunia moja na huyo binti!
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,302
2,000
Yaani wala usilogwe kumtafutia kijana wako aliyesoma mchumba eti Housegirl
Yaani Housegirl huwa hawabadiliki na kuwa na mawazo ya kutafuta au kuendeleza mali na familia itakuwa umemharibu kwa kazi na kufokewa mara kwa mara na kichwani mwake kutakuwa na ratiba aamke alifajiri saa 11.00 adeki awachemshie majimoto ya kuoga hata na mumewe, achemshe Chai, apeleke watoto shule, akanunue mboga sokoni apike
Yaani acha kabisa mm yamenikuta na ninayaona utabeba lawama kibao
JF ni darasa amini usithubutu kumtafutia mchumba bado utawamiliki mpaka kufa kwao na lazima mtagombana tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom