Housegirl: Ushauri

Fanya kutoka nao dina(mkiwa wote watatu), unafanya utambulisho, halafu unajifanya kama unapigiwa simu ya ghafla mara unaongea, unawaacha wawili kwa 30min, ukirudi utapata majibu kwa jinsi watakavyokuwa wanabehave, me najua mtu wa drs la saba anaweza kuelimishwa na kubadilika haraka zaidi, na hawezi kuchange ghafla kama wa mjini( waliokwenda shule).

Good advice Von Mo
 
(Natamani ningepewa mi hio kazi ya kuwasakizia watu)...

Mi kweli hazi ya kusakizia siiwezi, natamani nikupe wewe hiyo kazi ila kama we ni HE, mmmmhhh, naogopa usijefanya mapinduzi bure
 
Utampona huyo housegirl...
Mapepe huenda na mapepe mwenzie
huyo ndugu yako hajatulia ndo maana ali opoa mdada wa mjini

haikuwa bahati mbaya.....ndege wanao fanana huruka pamoja..

sasa wewe utamponza tu huyo housegirl....wakati labda atampata mcha mungu mwenzie..

My boy sio mapepe hata kidogo, I raised him so namjua vizuri. Naweza kusema kuwa na yule mdada ilikuwa bahati mbaya tu na isitoshe dogo alipagawishwa na yule mama sukari (si unajua mimama sukari hupenda watoto wadogo)
 
Ndugu usijaribu kabisa kulazimisha ubavu ambao siyo mahali pake,hilo zigo la lawama cjui utalibebea wapi, yalishatukuta kwetu mambo km hayo yana athari kubwa ktk maisha ya mtu usipime,wacha dogo aone kile kimfaacho na acha hg aende kule kny ubavu wake uliosahihi,km ni mapenzi ya Mungu itatokea tu wala haihitajiki jitihada yako hata kidogo.Tafadhali tafadhal achana na hiyo biashara kabisa!! Kazi yako iwe ni kushauri tu na si kumuamlia dogo.

Asante kwa ushauri wako
 
Yaani wala usilogwe kumtafutia kijana wako aliyesoma mchumba eti Housegirl
Yaani Housegirl huwa hawabadiliki na kuwa na mawazo ya kutafuta au kuendeleza mali na familia itakuwa umemharibu kwa kazi na kufokewa mara kwa mara na kichwani mwake kutakuwa na ratiba aamke alifajiri saa 11.00 adeki awachemshie majimoto ya kuoga hata na mumewe, achemshe Chai, apeleke watoto shule, akanunue mboga sokoni apike
Yaani acha kabisa mm yamenikuta na ninayaona utabeba lawama kibao
JF ni darasa amini usithubutu kumtafutia mchumba bado utawamiliki mpaka kufa kwao na lazima mtagombana tu.

Nakubaliana na wewe kuwa kumtaftia kijana mchumba/mke kunaweza sababisha lawama ila hilo la housegirl kutokubadilika na kuwa na mwazo ya maendeleo nakataa, hii ni tabia ya mtu tu, mbona Joyce Kiria alikuwa house girl?
 
Unachokipenda wewe siyo atakachokipenda mwengine....
Siri kubwa ya ndoa ni kuwa inatoka kwa MUNGU na wala sio kwa matakwa au matamanio ya mtu fulani...
Yes House maid ni mzuri kitabia na muonekano but yet that aint a credit...
Kinachokusumbua ni kuwa umeshampenda huyo binti na ukasahau kuwa ni moyo wako ndio uliomfagilia na si wa mwanao...
 
mwenzangu wacha kijana achague mwenyewe usitake lawama, yalishanikuta nilimpa mke mtoto wa mama yangu mkubwa
anavyo mfanyamkewe utadhani mtumwa na akimwambia kwanini anasema kwani mie ndio nimekutaka si hao mashawishi ndio
wameniletea kituko wewe,hapa najuuuuta lakini ndio wameshaa zaa watoto 4...
 
Habari zenu wana MMU,

Ninaomba mnishauri juu ya hili.

Nina mtoto wa dadayangu (mvulana). Kukweli nampenda sana kama mwanangu, kwanza kalizaliwa mimi nikiwa chekechea, nilimlea and honestly I love him very much. Alibahatika kupata kazi serikalini mwaka juzi, na baada ya miezi 6 alintambulisha mpenzi wake. Kiukweli sikufurahishwa na huyo mchumba kwani kwanza alimzidi 2 years, halafu mdada ameanza kazi 2004, yani anaujua mji ile mbaya. Isitoshe hata marafiki zake pia watata, ni wale masista duu wa bongo movie wenye skendo daily.

Baada ya kutambulishwa sikutoa comment yeyote ila after a week nkamtafta dogo nikamwambia awe makini sana mana wasichana wengi hapa town huwa sio wakweli, so amchunguze uyo binti kabla hajachukua uamuzi wowote ikiwa ni pamoja na kucheki afya zao. Dogo kiaina hakupenda ushauri wangu, ila kwa kila ndugu aliyemtambulisha uyo dada aliambiwa the same thing. Ni miaka 2 imepita sasa, dogo katuambia kuwa kaachana nae na kwamba yule dada hajatulia na hamfai.

Sasa, mimi nina a very beautiful, honest, smart, hardworking,God fearing and humble housegirl na ninatamani huyu my son amuoe. Je, nitumie njia gani ili hawa watu wapendane na hata waoane jamani/ Kiukweli the girl is good jamani, nimeishi nae for 2 years na kweli kama mzazi natamani iwe hivi ( NACHUKULIA ULE MSEMO USEMAO KIZURI KULA NA NDUGUYO). Tatizo moja tu, ameishia darasa la saba sasa sijui kama dogo atamkataa.

Nipeni mawazo wandugu.

kakuruhusu nani kumchagulia mwanao mchumba wa kuoa? Huoni kuwa unamkosea kwa njia moja ama nyingine? Nafikiri wewe kaa kushoto, ana akili timamu, ana mapenzi yake, ana mapigo yake. Pia two years inakupa uhakika gani kwamba huyo HG wako ni mzuri wa kuolewa na mwanao?

Kuna vitu vingine huna authority ya kufanya hivyo. Mwache ikifika siku ataoa tu kwa kuchagua mwenyewe.
 
Habari zenu wana MMU,

Ninaomba mnishauri juu ya hili.

Nina mtoto wa dadayangu (mvulana). Kukweli nampenda sana kama mwanangu, kwanza kalizaliwa mimi nikiwa chekechea, nilimlea and honestly I love him very much. Alibahatika kupata kazi serikalini mwaka juzi, na baada ya miezi 6 alintambulisha mpenzi wake. Kiukweli sikufurahishwa na huyo mchumba kwani kwanza alimzidi 2 years, halafu mdada ameanza kazi 2004, yani anaujua mji ile mbaya. Isitoshe hata marafiki zake pia watata, ni wale masista duu wa bongo movie wenye skendo daily.

Baada ya kutambulishwa sikutoa comment yeyote ila after a week nkamtafta dogo nikamwambia awe makini sana mana wasichana wengi hapa town huwa sio wakweli, so amchunguze uyo binti kabla hajachukua uamuzi wowote ikiwa ni pamoja na kucheki afya zao. Dogo kiaina hakupenda ushauri wangu, ila kwa kila ndugu aliyemtambulisha uyo dada aliambiwa the same thing. Ni miaka 2 imepita sasa, dogo katuambia kuwa kaachana nae na kwamba yule dada hajatulia na hamfai.

Sasa, mimi nina a very beautiful, honest, smart, hardworking,God fearing and humble housegirl na ninatamani huyu my son amuoe. Je, nitumie njia gani ili hawa watu wapendane na hata waoane jamani/ Kiukweli the girl is good jamani, nimeishi nae for 2 years na kweli kama mzazi natamani iwe hivi ( NACHUKULIA ULE MSEMO USEMAO KIZURI KULA NA NDUGUYO). Tatizo moja tu, ameishia darasa la saba sasa sijui kama dogo atamkataa.

Nipeni mawazo wandugu.

Wadada wa kisasa mnamomonyoa maadili ya kiafrika mwache atafute kitu roho inapenda
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom