Hotuba za Rais Samia zinaponya bila kutumia dawa

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
478
962
Habarini wakuu,

Kwanza kama kuna watu wanamsaidia kumwandikia hotuba mama basi wanastahili pongezi nyingi sana maaana hotuba ni taamu balaa.

Ni ukweli usiopingika kuwa hotuba za Mama Samia zinatibu harara, chunusi, upele, malaria yani unasikiliza hotuba unasema hapa kweli raisi wa nchi anahutubia yani hakuna kufoka foka hutuba inaingia moyoni kwa faraja teele.

Toka Rais Samia aingie madarakani hotuba zake zina hadhi isiyopimika kwa mizani, yan ile hotuba sku ya kuapishwa, hotuba ya bungeni Tanzania, hotuba ya mei mosi adi hii hotuba ya leo bungeni kenya kiukweli hotuba ya leo kenya imebeba hisia halisi za sisi kushikamana na ndugu zetu wakenya yani hotuba imesheheni misamiati ya kiswahili yenye upatanishi na upendo wa hali ya juu.

Mitano tena kwa Mama Samia.
 
Yaani huyu mama yupo makini,anatumia lugha kwa ufasaha,amewateka wafanyabiashara na wanasiasa wa Kenya ipasavyo.

Kuna wasumbufu waliokua hawataki ushirikiano katiyetu na Kenya wakajizolea sifa ziso msingi. RC wa Tanga bwana Shigela aibu yako.

Alizungumzia hata suala la bandari kwa chuki siku za mwisho wa uhai wa JPM wakati mama Samia akiwa ziara Tanga.
Narudia aibu yako Shigela. Haya funga hiyo mipaka sasa
 
Yaani huyu mama yupo makini,anatumia lugha kwa ufasaha,amewateka wafanyabiashara na wanasiasa wa Kenya ipasavyo..
Yan in the short period of time Mama Samia ametoa speech ambazo ni "memorable" yani zinaweza hata kusikilizwa na vizazi vijavyo wakati mwndazake hana speech hata moja ambayo ni memorable kwa kizazi kijacho!!!! Shame!!!
 
Midume mizima kujitekenya na kujichekeshachekesha!

Vimaneno kama vya kwenye khanga. Maandiko mengi yanareflect mtu alikotoka. Bila shaka mwandishi katoka jamii za waimba taarabu.
 
Midume mizima kujitekenya na kujichekeshachekesha!
Vimaneno kama vya kwenye khanga. Maandiko mengi yanareflect mtu alikotoka. Bila shaka mwandishi katoka jamii za waimba taarabu.
Mbn sindano inakuingiiaa hvooo,, tuliza mshono
 
Mkuu tulifokewa mno!!acha tupate japo faraja!!yaani rais alivyokuwa akiongea na wananchi wake utafikiria LAULENT KABIRA, alivyokuwa akiongea na waasi!

Aliowakamataa!!ni kufoka tu na vitisho!!juzi siku ya maya mosi wafanyakazi hawakupandishiwa mshahara lakini alivyowajibu wameridhika, ndio uongozi huo!!
 
Midume mizima kujitekenya na kujichekeshachekesha!
Vimaneno kama vya kwenye khanga. Maandiko mengi yanareflect mtu alikotoka. Bila shaka mwandishi katoka jamii za waimba taarabu.
Jamii ya wafugaji imelaumiwa,muimba taarabu humtaki sema unataka muimba singeli au
Mpe mtu muda ndio utoe tathmini
 
Midume mizima kujitekenya na kujichekeshachekesha!
Vimaneno kama vya kwenye khanga. Maandiko mengi yanareflect mtu alikotoka. Bila shaka mwandishi katoka jamii za waimba taarabu.
Mkuu kuna mitanzania inasikitisha sana!
 
Midume mizima kujitekenya na kujichekeshachekesha!
Vimaneno kama vya kwenye khanga. Maandiko mengi yanareflect mtu alikotoka. Bila shaka mwandishi katoka jamii za waimba taarabu.
Yule mwengine alitoka kwenye jamii ya mziki wa kufokafoka?
 
Back
Top Bottom