Hotuba za Rais Samia zawagusa wanasiasa na wafanyabiashara

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,830
2,417
Wakati hotuba za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alizozitoa nchini Kenya zimeibua mjadala mitandaoni ikielezwa zimeleta matumaini na kujawa hekima, busara na haiba, leo anatarajiwa kuzungumza na Baraza la Wazee wa mkoa wa Dar es salaam.

Viongozi na wafanyabiashara mbalimbali nchini Tanzania kupitia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wameeleza namna hotuba za Rais Samia zilivyoleta mshikamano na Kenya.

MO DEWJI (mfanyabiashara)
"Ninajisikia kutiwa moyo sana na matumaini ya kushuhudia kurudishwa kwa uhusiano wa pande mbili kati ya Kenya na Tanzania"

FREEMAN MBOWE (mfanyabiashara).
"Dunia imeona, imesikia na inasubiri vitendo. Hongera Mama. Tanzania uharibifu ni mkubwa zaidi. Rejesha tabasamu la haki, uhuru na demokrasia. Tunakusubiri"

JANUARY MAKAMBA (mwanasiasa)
"Ziara hiyo imekuwa mafanikio mazuri ya uhusiano huu muhimu. Hotuba yake kwa kikao cha pamoja imemvutia kila mmoja.

#kaziiendelee #kaziiendelee
 
Ile ripoti ya ukaguzi BOT ambayo aliagiza kuanzia Jan hadi March itasomwa lini? Bandari nk., lakini hatujasikia waliobambikiziwa makesi kuachiwa na wamejazana huko magereza?
Ni vyema mama samia ajipambanue kwa vitendo zaidi
Shida anaongea kuliko vitendo
 
Back
Top Bottom