Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Raisi kazungumza kwa uzuri kabisa na kwa sentensi za kueleweka challenge zinazotukabili kwa mwaka huu mpya wa 2008, sikutegemea raisi aanze kutoa lecture kama mijadala ya kiacademics kama baadhi ya wapenda vyeti wanavyohusudu. instead raisi kazungumza kwa lugha yenye kueleweka, kazungumzia hali ya chakula, usalama,uchumi kama vile kukuza uchumi kwa asilimia 7.7 ambalo ni hatua nzuri ukilinganisha na hali ya sasa.

kuhusu kenya, hali bado ni tete, na busara ya hali ya juu inahitajika kuiweka nchi katika hali ya usalama, siyo kuwin cheap international politcs huku ukijeopardise chance yetu ya kuwasaidia wenzetu kurekebisha mambo.isitoshe kwa muda huu kabla ya raisi kukurupuka na kuzungumzia suala la kenya , Membe anatakiwa awe amefanya homework yake vya kutosha.

Bado kuna challenge, ila naona Muungwana ameanza kuadress issue vizuri, tumuunge mkono kwa yale mazuri anayoaddress na tumpinge kwa yale mazuri asiyoyadress au mabaya yawayoyoyote huku tukisaidia kuonyesha alternatives bila arrogance
 
1st January, 2008

RE:AN OPEN NEW YEAR LETTER TO ALL TANZANIANS AND AFRICAN PEOPLE OF GOODWILL


FELLOW EAST AFRICANS,

Our country THE REPUBLIC OF KENYA has been hijacked by the opponents of democracy namely Hon. Mwai Kibaki and the former Minister of Internal (in)Security Mr. John Michuki together with their club of rich Kikuyu mafia. It is very sad how Kenya has degenerated into chaos because of these two men together with some unpatriotic officials of the Electoral Commission of Kenya who refused to even look at evidence pointing to a massively rigged election.

As people lit fireworks and drank warm champagne last midnight to usher in the New Year, gunshots and the flow of warm blood of hundreds of peace-loving Kenyans denied the country such global happiness that they had planned to celebrate with a new president of their choice, Hon. Rail Odinga. Hon. Kibaki, Mr. Michuki and their friends working from/in State House, Nairobi today should know that all nefarious men of their type, such as Mobutu Sese Seko and Charles Taylor will one day face their days in court whether alive or dead. African dictatorships have never lasted forever, they have always come tumbling down at some point and Kenyans of our generation and beyond will never forgive them for giving the ongoing shoot-to-kill orders to the special security forces of the paramilitary General Service Unit(GSU) against their fellow countrymen in Kisumu. This is something that even retired President Daneil Arap Moi and the late Jomo Kenyatta who ruled for longer terms and wielded more power, never did.

Fellow Africans, Tanzanian men and women of goodwill, join us in spreading the news of how the unpopular regime in Nairobi today openly took advantage of Hon. Raila Odinga's peaceful politics, to swear in a man who lost hands down in Kenya's just concluded historic elections. Announce to all and sundry how this regime, faced with a genocide/ethnic cleansing on their hands at the moment, has even had the immoral audacity of asking Raila to be a good statesman and conceed defeat to Kibaki! What nonsense is this? How absurd can the power-hungry be? Why really should Raila, the legitimately elected president, Raila the people's choice in an election with the highest turn-out ever seen in these parts of Africa, accept this slap in the face to the democracy that he and others have built on blood, imprisonment and tears? Why?

Hon. Kibaki, why hasnt any world, African or even East African leader sent you a message of congratulation even after two days since you "won" the elections?

At the dawn of this new year, 2008, the wishes of the majority of the different tribes of Kenya to be led by Hon. Raila Amolo Odinga until 2012 cannot be respected by a few old men whose only fear is that a Raila presidency will audit their dubiously acquired wealth and bring them to books. If we give in to this "civilian coup" as Raila calls it, and let the new Kibaki regime eventually get their way, then what will be the point for future elections?

We might just as well accept the fact that Kenya awill now resurrecting the dictatorship of yesteryears in Africa even as the continent forges forward into the new millenium. In this context, we should find bo difference between Kibaki and the dictators of the past of the Great Lake region especially Idi Amin, Kamuzu Banda, Said Barre, Mobutu Sese Seko etc. Kibaki and his cronies are extremely evil and that is why Raila should not give up. If Raila gives up, Kenya will go down the drain because of the power hungry few. There may be no other Raila to leas us against these forces of evil in the future. Let us all rally behind him, for the sake of Kenya and other African democracies.

Let the hastily sworn-in Hon. Kibaki be the statesman not Raila because Raila already is a popular statesman in the eyes of Kenyans and the world. Let Hon. Kibaki just step down and accept the honest verdict of the Kenyan voters that they do not want his leadership. He does not have the mandate to rule. He knows deep in his heart that he is not the true heir to the Kenyan throne in the legal sense especially as evidence continues to come up on how his Party of National Unity (PNU) and some officials of the Electoral Commission of Kenya (ECK) rigged the December, 2007 elections. In the face of the laws of the Republic of Kenya, he is no different than the looters in the streets. He has looted the presidency from Kenyans by imposing himself even when Kenyans have rejected him, his vice president, 90% of his former cabinet ministers and his own political organization, the Party of National Unity (PNU). Just as the looters on the streets of Kenyan cities should respect the law of the land, so should the Kibaki regime. We are all equal before the eye of the law.

Fellow East Africans, Tanzanian men and women of good will, as we in the new deathstricken Kenya of Kibaki struggle on towards our political freedom by adopting Ukrainian techniques of compelling Kibaki to resign, join us and the international community in denying recognition to the false government in Nairobi today. Spread word to as many people as you can that the duely elected president of Kenya Hon. Raila Amollo Odinga has been blocked from office by Hon. Emilio Mwai Kibaki and his tiny group of business friends from his home province. I finish my plea to you all by supporting the views of the Chief European Union Election Observer in the December 2007 Kenyan presidential elections, Alexander Graf Lambsdorff who said the tallying process "lacked credibility" and reported very openly that Kenya's presidential poll was "flawed" and "fell short of international standards".

A KENYAN VOTER
 
Hajagusia kabisa matatizo ya Kenya au macho yangu yameenda haraka?

Very good observation. Kweli Mkuu wa kaya amelala, kwa sababu ninavyojua watu wa Kenya watakuwa comfortable kuingia Tanzania kama hali itaendelea kuwa mbaya, at least angesema kitu kama kuwaandaa wananchi kuipokea hali hiyo na namna ya kukabiliana nayo.
Nadhani the best way for himwas to say "happy new year", hayo mengine yote ni mepesi sana kwa wakati huu!
 
Nilitegemea hotuba ya mwisho wa mwaka ya mkuu wa nchi kwa wananchi wake ingekuwa na yafuatayo.
1. Kwa mwaka 2007 tulikuwa tumekusudia kufanya nini kwa figures sio blabla.
2. Tumefanikiwa kufanya nini na kwa asilimia ngapi.
3. Tulishindwa wapi na kwa nini.
4. Tunafanya nini ili kuweza kutimiza lengo letu?
5. Nini malengo yetu kwa mwaka 2008 kwa figures.
Ili iwe rahisi kwetu kufanya evaluation mwisho wa mwaka.
Lakini hotuba yenyewe imejaa majigambo tu. Tumefanya vizuri kwa kiwango gani? Hivi wanaoandaa hizi hotuba kama hizi hawaoni kuna mapungufu? Au bora liende wanafikiria tuu ni wapi pa kupata rushwa?
Mimi sioni jipya kwenye hotuba angesema tu watanzania nawatakia heri ya mwaka mpya
 

Duh! wewe unawaza mbali sana! Hicho unachoongelea wewe ni lugha ya kigeni kwao. Hapa kiichofanyika ni kutimiza wajibu wa kutoa hotuba siku ya kufunga mwaka na kukaribisha mwaka mpya.
 
Wameshamtumbukiza muheshimiwa kwenye crap of global warming, naona speech imejaa global warming effects zaidi ya uchumi.

Madhara ya mafuta Tanzania hawajaanza kuyaona bado, hapo ndio ikumbukwe umuhimu wa kuwa na reservs.

Hii speech ni longo longo tupu, yaani kama ana hutubia std 7
 
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWENYE UZINDUZI WA AWAMU YA PILI YA PROGRAMU YA KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA, DAR ES SALAAM, TAREHE 28 JANUARI, 2008
Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa;
Waheshimiwa Wabunge;
Waheshimiwa Mabalozi;
Waheshimiwa Viongozi wenzangu wa Siasa;
Wageni Waalikwa na
Ndugu Wananchi:
Awali ya yote napenda kukushukuru wewe, Mheshimiwa Waziri kwa kunialika na kunipa heshima hii kubwa ya kuzindua Awamu ya Pili ya Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma. Nafurahi kujumuika nanyi leo katika tukio hili muhimu linalotupeleka katika hatua ya juu zaidi katika jitihada zetu za kuboresha utumishi wa umma nchini.
Tangu miaka ya tisini (1990s) Serikali imekuwa ikifanya maboresho ya sekta ya utumishi wa umma. Maboresho hayo yamekuwa yakilenga katika kuubadili utumishi wa umma ili uwe mhimili imara wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika nchi yetu, badala ya kuwa kero na kizuizi cha jitihada za Serikali za kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo.
Mheshimiwa Waziri;
Kama ulivyoeleza kwenye hotuba yako, mipango yote ya kuboresha utumishi wa umma iliyokwishatekelezwa imezaa matunda yanayoonekana. Programu ya Kuboresha Utumishi Serikalini (Civil Service Reform Programme) imefanikisha lengo lake kuu la kuwa na Serikali ndogo, yenye ufanisi wa hali ya juu na inayolenga kutoa huduma bora kwa wananchi. Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuainisha upya majukumu yake.
Tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, hivi sasa Serikali imebakia na majukumu yake ya msingi yanayohusu utawala, ulinzi na usalama na usimamizi wa uchumi wa nchi. Maboresho hayo pia yamesaidia sana katika kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali. Ajira holela na ajira hewa Serikalini zimedhibitiwa.
Hali kadhalika, maslahi ya watumishi wa umma yamekuwa yanaboreshwa kwa kutambua ujuzi na uzoefu wa watumishi pamoja na kuzingatia uwezo wa Serikali kiuchumi. Muundo wa Serikali umeboreshwa na madaraka zaidi yamepelekwa kwenye ngazi za chini waliko wananchi wengi.
Hatua hizi zimesaidia katika kuimarisha na kuboresha utendaji wa Serikali pamoja na utoaji wa huduma muhimu kama vile maji, afya, elimu na nyinginezo.
Mheshimiwa Waziri;
Katika hotuba yako pia umeelezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Programu ya Kuboresha Utendaji Kazi Katika Utumishi wa Umma (Public Service Reform Programme). Programu hiyo ilizinduliwa rasmi mwezi Juni, 2000 na kumalizika Desemba, 2007.
Mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na ya kujivunia. Napenda kuitumia nafasi hii kukupongeza wewe Mheshimiwa Waziri na watumishi wote wa Ofisi yako kwa kazi nzuri mliyoifanya na mnayoendelea kuifanya.
Mafanikio yaliyokwishapatikana yametokana na juhudi zenu hivyo niruhusuni niseme hongereni sana na ahsanteni sana.
Ni jambo la kuleta faraja kuona mifumo ya kuboresha utendaji kazi katika taasisi za umma imewekwa na upangaji wa mipango na bajeti za Wizara, Idara na Wakala za Serikali nao umeboreshwa. Maslahi na mazingira ya kazi ya Watumishi wa Umma yameboreshwa na matumizi ya teknolojia ya kompyuta katika shughuli za Serikali yameongezeka. Mfumo wa wakala wa Serikali umeanzishwa kwa shughuli kadhaa za serikali na sekta binafsi imekuwa inahusishwa kwa baadhi ya shughuli. Mambo haya yameipunguzia serikali mzigo na kuongeza ufanisi.
Suala la maadili ya utumishi wa umma limepewa uzito stahili. Kanuni za maadili ya utumishi wa umma zimeandaliwa na mafunzo yamekuwa yanatolewa.
Mheshimiwa Waziri,
Wageni waalikwa;Lakini, pamoja na mafanikio hayo, bado kuna kazi kubwa ya kufanya mbele yetu. Licha ya jitihada zetu za kuboresha huduma tunayoitoa kwa umma bado kuna mapungufu ambayo hatuna budi kuendelea kuyatafutia ufumbuzi. Kwa mfano, bado kuna malalamiko mengi ya wananchi kuhusu huduma zisizoridhisha kwa baadhi ya Idara za Serikali.
Pia yapo malalamiko yahusuyo ubabaishaji na vitendo vya rushwa. Mengi ya malalamiko hayo yanaelekezwa kwenye sekta za elimu, afya, usalama wa raia, utoaji haki, mambo ya ndani na ardhi.
Vile vile bado kuna tatizo la tija duni katika utumishi wa umma. Baadhi ya sababu zinazosababisha kuendelea kwa hali hii ni kutokuwepo kwa mfumo mzuri wa uwajibikaji katika ngazi zote za taasisi za Serikali, uchache wa watumishi wenye sifa na uzoefu wa kutosha na uongozi usiokuwa mbunifu.
Mheshimiwa Waziri na Wageni Waalikwa;
Nimefurahi kusikia kwamba matatizo haya na mengineyo ambayo sikuyataja yamezingatiwa katika uandaaji wa Mpango wa Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Programu hii.
Nimetiwa moyo, kusikia kwamba kwa kiwango kikubwa uendeshaji wa programu hii utaamuliwa, kuendeshwa na kusimamiwa na taasisi za umma zenyewe na kwamba maboresho yatakayoidhinishwa yataingizwa kwenye mipango na bajeti za taasisi hizo kwa ajili ya utekelezaji. Matarajio yangu ni kuwa kila taasisi ya umma itachambua kwa makini maboresho yanayoihusu na kuyaainisha kwenye mipango yake na kuyatekeleza kwa ukamilifu ili kuboresha zaidi huduma kwa umma.
Nimefurahi pia kusikia kwamba tatizo la kutowajibika litashughulikiwa katika awamu hii ya maboresho. Hii ni pamoja na kuandaa utaratibu wa uwajibikaji wa taasisi zote za umma katika ngazi zote. Ombi langu kwenu ni kuwa tuharakishe uandaaji wa utaratibu huo ili ukamilike mapema. Tusichukue muda mrefu sana kwa kazi ya uandaaji. Naamini kuwa utaratibu huu tukiutekeleza vizuri utasaidia sana katika kuimarisha utendaji wa Serikali na kutoa huduma kwa wananchi kwa jumla. Ndugu Viongozi na Wageni waalikwa;
Jambo lingine ambalo napenda kulisisitiza hapa ni haki ya wananchi kupata huduma nzuri kutoka kwa watumishi wa umma na haki yao kudai huduma hiyo. Utumishi wa umma upo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Huduma itolewayo ni haki yao, siyo fadhila. Hivyo kila mwananchi anayo haki ya kudai kupatiwa huduma iliyo bora.
Na watumishi wa umma wanao wajibu wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ni kwa msingi huo nimefarijika kusikia kwamba mpango huu unalenga katika kuwawezesha wananchi na wateja kwa ujumla kuwa na uelewa wa upatikanaji wa huduma za umma na kufahamu haki zao za kupata huduma bora. Hili ni jambo jema, naomba tuliimarishe. Nafurahi pia kusikia kwamba katika awamu hii ya Programu kuboresha maslahi ya watumishi wa umma na kujenga utumishi wa umma wenye nidhamu na unaozingatia maadili.
Hili nalo ni jambo muhimu sana. Hakuna mafanikio bila nidhamu kazini. Na mtumishi wa umma asiyezingatia nidhamu na maadili ya kazi yake hawezi kuwa na ufanisi. Naomba suala la nidhamu na maadili tulipe uzito mkubwa zaidi ili kujenga uadilifu wa hali ya juu katika utumishi wa umma hapa nchini.
Mheshimiwa Waziri, Wageni Waalikwa;
Kuhusu kuboresha maslahi ya watumishi wa umma napenda kusisitiza mambo mawili. Kwanza, kwamba tumemekuwa tunayaboresha kwa nyakati mbalimbali lakini lazima tuendelee kuboresha. Pili, kwamba msingi wake ni tija yaani tija ya mtumishi mmoja mmoja na tija ya wengi katika taasissi na nchi nzima kwa jumla.
Sote tunatambua kuwa maslahi bora yanategemea sana kukua kwa uchumi wa nchi yetu. Pia yanategemea ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Uchumi unaokua kwa kasi na umakini katika ukusanyaji wa kodi ndivyo pekee vitakavyoiwezesha Serikali kuwalipa watumishi wake vizuri. Lazima tufanye hayo.
Hivyo, nawasihi ndugu zangu wote tuliomo kwenye utumishi wa umma tujitume zaidi, tufanye kazi kwa bidii na maarifa zaidi ili kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Kila moja wetu atimize wajibu wake ipasavyo, tena kwa wakati. Tusikwepe wajibu wetu na kwamba tuache tabia ya kutoa visingizio visivyokwisha kwa kutokutimiza malengo tuliyojiwekea.
Naamini sote tukiyafanya hayo nchi yetu itapiga hatua kubwa na ya haraka. Hii itatuwezesha kuboresha zaidi maslahi ya watumishi wa umma nchini mwetu.
Mheshimiwa Waziri, Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa;
Nafurahi kuona kwamba Mpango huu mpya umelipa umuhimu stahili suala la kuimarisha uongozi katika utumishi wa umma. Nchi yetu inahitaji viongozi makini, wabunifu, wanaoona mbali na wachapa kazi hodari.
Viongozi walio makini katika kusimamia utekelezaji wa mipango na maamuzi mbalimbali ya Serikali yahusuyo maeneo yao ya uongozi. Kwa sababu hiyo nimependezwa na uamuzi wa kuanzisha mfumo wa kutambua na kuandaa viongozi kupitia utaratibu wa mafunzo ya mara kwa mara. Bila ya shaka utaratibu huu utasaidia sana katika kujenga kada ya viongozi na watendaji bora wanaohitajika sana katika utumishi wa umma. Nawaomba muangalie uwezekano wa kuanzisha Chuo cha Taifa cha Uongozi kitakachotoa mafunzo kwa viongozi na watendaji kama njia mojawapo ya kuimarisha uongozi na utendaji Serikalini.
Mheshimiwa Waziri;
Ili Mpango wa kuboresha utumishi wa umma uweze kufanikiwa kuna mambo kadhaa ambayo hayana budi yafanyike. Kwanza, Ofisi yako lazima iendelee na kazi ya kuwaelimisha watumishi wa umma kuhusu umuhimu wa kubadilika kifikra na kimtazamo.
Hii inatokana na ukweli kwamba sehemu kubwa ya maboresho ya utumishi wa umma yanalenga katika kubadilisha taratibu, tabia na utamaduni wa kazi uliozoeleka kwa muda mrefu. Hivyo kubadilika kifikra na kimtizamo ni jambo la lazima. Lazima sisi tulio katika utumishi wa umma tubadilike.
Tuache umangimeza na kujiona kuwa sisi ni mabwana mkubwa na wananchi si lolote. Tutambue kuwa tupo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na siyo vingenevyo. Hivyo kazi ya kuwaelimisha watumishi ili kutambua wajibu wao huo iwe ni ya kudumu.
Nawaomba msichoke kuifanya. Pili, hakikisheni kuwa raslimali watu kwa maana ya watumishi wa umma, inaendelezwa. Shirikianeni na taasisi nyingine za umma katika kubuni na kutekeleza mipango ya mafunzo kwa kada mbalimbali za watumishi wa Serikali. Mazingira ya kazi duniani yanabadilika kila siku. Kila kukicha kuna mambo mapya. Hivyo watumishi wa umma nao wanastahili kujengewa uwezo utakaowawezesha kwenda na wakati.
Tunahitaji kuwa na watumishi wa umma wenye uwezo na ujuzi wa kutosha. Watumishi ambao wanajua wanalolifanya na siyo kubahatisha. Tujipange vizuri kuwawezesha watumishi wa Serikali kupata mafunzo stahiki yatakayowawezesha kufanya kazi zao kwa kujiamini na ufanisi mkubwa.
Mheshimiwa Waziri, Wageni waalikwa;
Tatu, hapana budi kuongeza kasi ya kuanzisha na kutumia teknolojia za kisasa za habari na mawasiliano katika shughuli za Serikali. Katika dunia ya leo mambo mengi yanaendeshwa kwa kutumia mtandao wa kompyuta. Serikali nyingi duniani zinaendesha mambo yake mengi kupitia mtandao wa aina hiyo (serikali mtandao).
Nasi hatuna budi kufanya hivyo kwani itasaidia sana katika kuboresha na kurahisisha mawasiliano ndani ya Serikali na baina ya Serikali na wananchi. Pia itapunguza urasimu ambao bado ni moja ya vikwazo vya ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.
Vilevile, itasaidia katika vita dhidi ya rushwa kwa sababu vitu vingi vitakuwa wazi na havihitaji mazungumzo ya ana kwa ana baina ya mtoa huduma na mpokea huduma.
Mheshimiwa Waziri na Wageni Waalikwa;
Programu hii tunayoizindua leo itakuwa ya manufaa kwa wananchi ikiwa tu mabadiliko tunayoyakusudia yataongeza ubora katika utoaji wa huduma kwa umma. Hivyo lengo letu kubwa liwe ni kuimarisha ubora wa hudumu tunazozitoa kwa Watanzania. Kama nilivyosisitiza katika hotuba yangu ya kuhitimisha sherehe za siku ya utumishi wa umma za mwaka jana, watumishi wa umma lazima tudhamirie kuhakikisha kuwa huduma za leo ni bora kuliko za jana na zile za kesho ziwe bora zaidi kuliko za leo.
Naamini tukifanya hivyo tutaweza kabisa kufikia lengo letu la kujenga utumishi wa umma mahiri, utumishi wa umma ulio adilifu na sikivu na utumishi wa umma unaoweka mbele maslahi ya umma. Nawasihi wote tuitumie programu hii ya maboresho kama nyenzo ya kutufikisha kwenye lengo letu hilo.
Hitimisho
Mheshimiwa Waziri; Viongozi na Ndugu Wananchi Wenzangu;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama nitamaliza hotuba yangu bila ya kuwashukuru wale wote waliojitolea kuchangia kwa hali na mali katika utekelezaji wa Programu hii.
Wenzetu hao ni pamoja na Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali za Uingereza, Canada, Denmark, Ireland na Japan. Aidha nawashukuru wengineo wote waliofanikisha Programu hii kwa namna moja au nyingine. Kwao wote nasema asanteni sana. Tunathamini sana mchango wao. Tunawaomba wandelee kutuunga mkono.
Baada ya kusema hayo, sasa ninayo heshima ya kutamka kwamba Awamu ya Pili ya Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma imezinduliwa rasmi.
Vile vile natamka kwamba Jengo la Mtandao na Tovuti Mpya ya Utumishi vimezinduliwa rasmi.
Ahsanteni kwa kunisikiliza!!

© Michuzi Tarehe: 28.1.08
 
Watumishi ziku hizi choka mbaya tu- sasa maboresho gani wakati Mshahara wa mwal. primary ni laki 1? Hivi kweli kama anaishi Dar na ana familia? hiyo laki kwa mwezi ataigawaje?
 
Msanii JK calls haya ni mafanikio ya awamu yake yeye .
 
Nimeenda kule Michuzi Blog- hii hapa hotuba ya JK 31st Jan. Anaongelea mambo sita,
1. Uhamiajia haramu (haswa Kagera)
2. Hali mbaya Uchumi Duniani
3. Ujio wa Bush mid Feb
4. Uchunguzi EPA (BoT)
5. Machafuko Kenya
6. Maadili ya Uongozi

Je kuna jipya? Mimi ningependa zaidi kuwe na mikakati ya kweli wakati anapoongea Maadili ya Uongozi- siyo tu maneno matupu ya kila siku! Pia anasema pesa za EPA baada ya uchunguzi wa miezi 6 zitarudishwa serikalini!

JF Mnasemaje?






 
Kama kweli anaipata Tanzania heshima kubwa mbona JK hasemi Kichata atakaa Tanzania hadi lini ?Kama atakaa masaa 2 bado si ziara ya Tanzania ila atakuwa kapita Tanzania . Je atalala Tanzania JK aweke wazi aache kutuyumbisha .
 
Kama kweli anaipata Tanzania heshima kubwa mbona JK hasemi Kichata atakaa Tanzania hadi lini ?Kama atakaa masaa 2 bado si ziara ya Tanzania ila atakuwa kapita Tanzania . Je atalala Tanzania JK aweke wazi aache kutuyumbisha .

George W atalala, na kwa habari niliyosikia, (kama haijabadilishwa) atapumzika pale Move-n-Pick.
 
Nimeisoma hotuba ya JK, naona amejibu baadhi ya hoja za JF, hasa ile ambayo ilikuwa ina suspect "Kituo cha kijeshi cha Marekani" Tanzania. Amekanusha na kusema ni uzushi! Ila kwa aslili, Mmarekani haiwezi kukupa kitu hivi hivi tu bila kudai kingine kwa mlango wa nyuma. (Kwa sababu wanasema "Be With us or against us" Yetu macho! Nyingine ni kuhusu sualala Balali, naona analizima kiaina. Hajasema kama Balali anarudi Tanzania ama la! Katuomba tusubiri kazi ya akina Hosea na Mwema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…