Suala la Palestina ni suala la kidini tena kwenye daraja za juu kabisa. Tofauti na wajinga wengi na Wanaharakati wanavyo jaribu kuwaaminisha watu.
Ukiangalia ardhi ya Palestine karibu kila dini wanajinasibisha napo, sababu Ile ardhi wameishi takribani mitume 14 ukiwaondoa wale maarufu. Mayahudi wanajinasibisha na Israeli kutokea kwa Yakubu, kwenda kwa Daudi mpaka kwa Suleyman, Wakristo kadhalika kule ndipo alipozaliwa Yesu, na sisi Waislamu wote duniani pale panatuhusu kwanza ndio sehemu ambayo kibla Cha kwanza kilikuwa kule, kadhalika msikiti wa pili kujengwa baada ya ule wa Makka ni masjidi Al-Aqsa. Kwahiyo huwezi kutenganisha ule mgogoro na udini.
Kilichowapeleka pale Wayahudi ni maandiko, tena yale yaliyomo katika agano la kale. Sasa msiwadanganye watu kuwa ni mgogoro wa ardhi, wakati Wayahudi wameenda pale kwa hayo maandiko.