Hotuba ya Zitto Kabwe - Kigoma: 21 Desemba 2013

Hotuba ya Zitto Kabwe - Kigoma: 21 Desemba 2013

ZZK usiingie humu kinyemela-hebu kuwa brave enough ku-exchange notes na wana JF.Umeiga tabia mbaya ya wanasiasa uchwara na wanasiasa majambazi kuandaa na kugharamia 'mapokezi' yao wenyewe. How long are you going to sustain this? Are your bankrollers permanent? Grow up bimbo!
 
Hotuba iliyojaa woga pia ina busara zake.Msibeze.Ushauri umefanyiwa kazi
ni mwanamke pekee ambae hishindwa na huchoshwa na mateso ya mumewe na huamua kukimbia.....mnamnyanyasa na kumfanyia vituko zitto ili asalimu amri na kumbia ili mpate ajenda itakayowapa huruma ya wananchi? sasa kasema haondoki na takuwa mwisho kuondoka CHADEMA kwa elimu yako duni ya india hebu nikusaidie kuichambua hyo kauili na nikupe maana yake.
i) anaposema yeye ni mtu wa mwisho kuondoka anamaanisha utaondoka wewe utamwacha chadema
ii) anaposema ataondoka kwa hiari yake maana yake hakuna mwenye ubavu wa kumfukuza ndani ya chama

wewe kama mwanaume na kwa sifa ya uanaume ya kusimamia maamuzi unasimama wapi katika kauli hizo?? ni vyema mkaacha kuhubiri chuki mkaishi kwa amani. mmeshindwa mmevuna aibu dogo kawapiga bao la kisigino.
 
Kwa ujumla hotuba yako Zitto ni nzuri japo umejaribu kuwa 'diplomatic/philosophical' huku ukitumia 'figurative language' yenye kuweka taswira ya kwamba ulikuwa unaongea kwa ujumla tu hukulenga chama chako cha chadema. Lkn ukiangalia matukio ya hivi karibuni juu yako ndani ya chadema utaona kwamba bado ulikuwa unakinanga chama chako na uongozi wake. Hebu nirejee mstari huu katika hotuba yako ya leo 'Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa'. Kwa nukuru hiyo inaonyesha ama unasema taifa letu chini ya serikali ya ccm linaongozwa kwa demokrasia ya juu,kitendo ambacho kinapaswa kuigwa na vyama vyote kikiwemo chadema,cuf, tlp, nccr etc. Hapo umekinanga/umekikosoa chama chako indirectly! Labda useme ulimaanisha nini hapo km siyo kupigia debe ccm na serikali yake unayodai unaipinga kwa ufisadi mikataba mibovu ya madini na kwa kukosa uwazi na uwajibikaji!

mawazo yako mwingine anaweza kusema kivingine duh..........umewaza na umeandika kama una hakika,
 
Hotuba iliyojaa woga pia ina busara zake.Msibeze.Ushauri umefanyiwa kazi

ikiwa ukilala ukiamka unamuwaza zitto basi ujue anakutawala bila wewe kujua. sidhani kama zitto anahangaika na wewe

kwa hapa wewe ndie tatizo.....................mbowe na slaa wanakutumia vizuri
 
vifaranga na mama zao hawatoipenda hii...kitu wanatamani ni kuona jamaa ana-retaliate kama mvuta bangi flani hivi...its unfortunate, it wont happen that way!
 
Katika picha zote na hata jukwaa alilolutumia hakuna bendera ya CHADEMA,hata kwenye maandamano ya wafuasi wa Zitto na pikipiki hakuna bendera ya CHADEMA,na ikumbukwe Zitto amejitapa sana kuwa anakipenda CHADEMA na angependa hata mtoto wake aje kuwa CHADEMA,Mbunge wa CHADEMA na unayehubiri mapenzi kwa chama unakosaje hata bendera moja ya chama kwenye mkutano wako?? Huu sio unafiki??!!

Tukisema kuwa mkutano huu umeratibiwa kwa maelezo maalum na pia kuandaa hadhira mathalani wasibebe bendera wala alama yoyote ya chama Tutaongea?? Tukisema mkutano huu ni wa mamluki dhidi ya CHADEMA tutakosea??!! Zitto ni mtu wa ajabu sana!!

Kwenye hotuba yake amelialia kutokuaminiwa ila kweli inajulikana kuwa matendo ya mtu ya kutilia shaka au maouvu ndio hufanya mtu asiaminike,imani hainunuliwi bali inatengenezwa kwa hiyo matendo ya Zitto ndio yanafanya uonekane msaliti

Kigoma inahistoria chafu ya kutoa wanasiasa wanafiki,wazandiki na wachumia tumbo na Zitto nathubutu kusema ni mmoja wao,Kigoma ingebaki kutoa wacheza mpira na wanamziki kama wakina Kaseja,Maulidi,Ali Kiba n'a wengine lakini si viongozi wa siasa,kwani ni wezi wa fikra na imani za walalahoi kwa maslahi yao binafsi n'a watu wanaowatumikia!!!
Nimesoma hotuba yote na zzk amenifanya niamini kuwa alienda Kigoma na jimboni kwake kwa wale waliompigia kura na si kwa wanachama wa CHADEMA. Ameifanya kuwa ziara ya mbunge kwa wananchi wake bila kujali iyikadi za kisiasa. Hivi wewe ulitaka bendera za nini wakati huohuo sisi wanachama tunahoji: "hii ziara imeratibiwa na nani" mara aangalie "asivunje katiba ya chama".

Hebu for once tukubali kuwa hotuba yake ilikuwa objective na amezungumza ya moyoni kwa mtazamo wake. Kuna watu hapa hapa JF wangeona bendera za CDM bado wangeendelea kumuita mnafiki na mhaini. ZZK does not have to prove himself to any one but the people who voted for him. Let him continue to be the politician that he is. I never used to like this guy but now I do!
 
Naweza kumfananisha Obama, pengine atakuja kuwa miongoni mwa viongozi bora kabisa baran afrika!

Kama ile tuzo ya MO Ibrahim ingekuwa inatolewa hata kwa viongozi wengine kama vile mawaziri, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa basi huyu kijana (zzk) angeichukua zaidi ya mara tatu!

Big up zzk umetoa mfano kwa akina Slaa, Lema, Msigwa, Mbowe na wengine wengi!

Live long ZZK!
 
hotuba za zitto ni za kishenzi sana..huku anajisifu, huku anajikweza,huku anajishusha,huku anawapa sifa watu, huku anajipa sifa yeye......anajiapiza kuamua mwenyewe,na anajiapiza kuamuliwa na wtau wake.Anajisifu kuwa kajenga malagarasi,barabara,etc na kupiga marufuku wengine wasijifu kwa hilo.....ila anasahau CCM nao wanajitangaza hivyohivyo..

Na barabara za kigoma pia zipo chini ya mfuko wa MCC na wahisani wengine baada kuhost wakimbizi, na miradi mingine ya kimataifa....Pengine kaongea na CCM ajifiche huko ,ila sijui ataongea vipi na Bush ili ajifiche ktk kazi za MCC....kwani MCC ndio walitoa hela inayojenga hadi barabara za Sumbawanga kwa mara ya kwanza.

Zitto asiyeyushe wajinga kwani hata km asingezaliwa mikoa hiyo sasa hivi ilikuwa iwekwe barabara tuu,hata EA wenyewe pia wangeweka.

Kwa ujumla ni kichaa......
 
Naweza kumfananisha Obama, pengine atakuja kuwa miongoni mwa viongozi bora kabisa baran afrika!

Kama ile tuzo ya MO Ibrahim ingekuwa inatolewa hata kwa viongozi wengine kama vile mawaziri, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa basi huyu kijana (zzk) angeichukua zaidi ya mara tatu!

Big up zzk umetoa mfano kwa akina Slaa, Lema, Msigwa, Mbowe na wengine wengi!

Live long ZZK!
Mkuu umesema ukweli kabisa. Wakati viongozi wengine wametumia muda kwenye majukwaa kuendelea kumponda ZZK, yeye amezungumza na wananchi wake bila kujaribu kuchafua chama. Pamoja na madhaifu ya kibinadamu aliyo nayo (kama walivyo kina Slaa, Mbowe, Lema nk) Nimempenda huyu kijana bure kabisa. Ameonyesha ukomavu wa kisiasa.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu bariki CHADEMA!
 
hotuba ya mh zitto z. Kabwe - kigoma – 21 desemba 2013

leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji.

Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa kigoma na zao la ujiji.

Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na jimbo la kigoma mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa chadema mwaka 1995. Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994.

Wakati watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa ujiji, watu wa kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.

Na nchi yetu tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya msingi kigoma na baadaye shule ya sekondari kigoma.

Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya kigoma. Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa 'asante salim' vilivyokuwa vinatengenezwa na kampuni ya bora shoes. Vililinunuliwa na mama coretha furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa kisangani mwanga. Mama coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu. Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania.

Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote. Jamii hii ya watu wa kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.

Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama elimu, afya, maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini. Demokrasia inahusu maendeleo.

Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya maendeleo ikiwemo daraja la malagarasi, uwanja wa ndege wa gombe-mahale, barabara za lami na upanuzi wa bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha usafirishaji mwandiga.

Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la taifa, bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa kigoma katika uchumi wa tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.

Lakini tukumbuke pia kuwa demokrasia ni uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa serikali inawajibika kwa wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa taifa' lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma dodoma kusemea watanzania wote na sio kigoma tu.

Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo serikali kuwa na hisa kwenye migodi, tanzanite kumilikiwa na watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani.

Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza rais kufanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana. Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa waziri mkuu. Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu.

Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu.

Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu.

kutoaminiana
ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli.

Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu. Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa. Ni majanga! Juzi bungeni mwanasheria mkuu wa serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko uswisi. Huu ulikuwa ni uongo.

Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko tanga na nilikutana nao mara nne. Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa kamati maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria.

Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya mwanasheria mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya kutoaminiana.

Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo. Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo taifa litaongozwa.

demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli
juzi nilipoingia bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge tundu lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule.

Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.

Na hapo ni muhimu muelewa wanakigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu; kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi. Ninawaona si wanakigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu.

Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni 2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini tanzania.

Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).

Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa - robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka kigoma mpaka dar-es-salaam!

Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu. Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!

Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.

Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa tanzania.

Mungu ibariki tanzania.
cc: TAYADI
 
Last edited by a moderator:
Zitto msiwaamini wanasiasa hata wakiwa wa upinzani mwezi wa 10 Tabora leo nwezi wa 12 kigoma anataka watu wa mwamini! anaakili huyu kweli au unafki tu

Lazima utajitia mimba mwaka huu,kijana wa watu hana mawazo ya gongo km Mzinzi wako na mporaji wa wake za watu,ZZK kijana mdogo lakina anawakalisha wahafidhina wote
 
Utajitekenya na kucheka mwenyewe kwani upeo wako wa kuchambua unakutuma hivyo na umeshagota lakini kwa watu makini na wenye kuchambua na kuangalia mambo kwa upana wanaona kasoro za kipumbavu na unafiki wa waratibu wa huu mkutano na anayepinga hoja yangu angekuja au atakuja na majibu postive na sio utendaji wa kasuku au roboti!!

Wakatabahu!

Unye,utapka hata ufe kabsa,CDM no one like ZZK
 
Nimepanda hapa ''Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta,lakini
uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia''.. Viva Zitto
 
Imetolewa na ofisi ya mbunge _ Tabata Dar! Ofisi iko Dar na siyo Mwandiga. Ikitantabuye Zitto ulasaze!
 
Back
Top Bottom