Siwez kubali hoja mfu...wewe lete ushahidi kuwa alipewa hizo hoja na ccm na si kubwabwaja tu.....maana mnataka tukubali mambo kinadharia huku mkiongozwa na chuki....nani asiyejua kuwa zitto alianzisha hoja juu ya mgodi wa buzwagi? Unataka nikubali kishabiki shabiki tuu....no way
Maskini….!!!!!!!! Mh. Zitto haaminiki tena. Hoja ya Buzwagi ilimpatia uaminifu na umaarufu mkubwa sana baina ya uuma wa Tanzania. Lakini ndio mwanzo wa matatizo ya kisiasa kwa Zitto. Wengine mtaani kwetu huku wanadai ule umachachari wako Mh uliutumia kama "fursa" kupata ukwasi ulionao leo. Kuna mambo yanajadiliwa sana kuhusu wewe na hii ni kutokana na ukweli kuwa ulipendwa sana na wananchi na wependa mabalidiliko hilo halina ubishi. Ila miongoni mwa mambo ambayo nahisi yamemmaliza Mh Zitto na kufikia hapo alipo leo yaliyotumiwa na watawala kumu-attack kwa ufupi yanaaminika yakawa:
1.
Direct bribe: Baada ya hoja yake ya BUZWAGI kuonekana ni shubiri na inaingilia maslahi ya watawala hakukuwa na njia nyingine nzuri zaidi ya kuhonga kumtuliza. Watawala inawezekana wali-win kumshawishi Mh. Zitto kupokea pesa ili afunge mdomo. Inawezekana alishawishika kukubali labda kwa sababu ya umaskini (tamaa) ama umri wake kwa wakati huo. Pengine Zitto ali "overlook consequences" za dhambi aliyokuwa akiifanya labda watawala walimuhakikishia hakuna wa kufahamu dili ile ikiwa ni pamoja na kupeana fedha (uchawi wa kidhungu) nje ya nchi ama hata kuamini kuwa ikitokea ikabainika hakutokuwa na ushahidi wa kutosha yeye kuhukumiwa. Akasahau aina ya watu aliodili nao na ikasababisha watawala kunogewa na msaada wake hata kuanza kumtumia kukivuruga chama cha chake kwa nguvu ya pesa (hapa sio rahisi kuamini kuwa alilifanya bila kujua mwisho wake ni kukilegeza ama kukiua chama). Na kwasababu hii naamini kabisa kuna watu (wahanga wa mpango haramu) ndani ya CHADEMA aliwaingiza kwenye mpango wake na CCM bila hata ya wao kujua. Lazima tujiulize kama alianza kuvaa viatu darasa la tatu je ukwasi huu alionao leo ameutoa wapi????? Private investigation (uswisi na Jersey) na safari za nje kama sokoni, hii pesa anaitoa wapi?? Na posho bungeni hataki?? Mh. Zitto hebu acha utoto watanzania wanakupenda sana hebu wajibika kwa kusema ukweli.
2.
Reciprocal relationship: Msingi wa "approach" hii imefichwa na neno "uzalendo" eti TAIFA KWANZA VYAMA BAADAE!!. Hapa nimelenga makubaliano kati ya Mh Zitto na "Mkulu wa kaya" kwamba naenda kufunga mdomo na/au kukivuruga chama (CHADEMA) lakini na wewe "Mkulu wa kaya" lazima unifanyie mambo kadhaa.
a) Ujenzi wa daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji- Mwandiga pale katika mkoa wa Kigoma. Unaweza tu ukaliamini hili kirahisi ukilinganisha na juhudi za mkulu kurekebisha baadhi ya mambo hasa miundombinu (kwa kisingizio cha ILANI ya CCM) na safari za viongozi wa kitaifa wa CCM za mara kwa mara kule Kigoma. Hili sio baya sana (indirect bribe) maana lina faida kubwa kwa watu wake wa Kigoma na Jimboni kwa ujumla lakini linamuondelewa sifa ya kuwa kiongozi sio tu CHADEMA bali ni katika chama chochote cha siasa hapa nchini.
b) Uenyekiti wa CHADEMA: Hili liko sambamba na (a) hapo juu. Yawezekana walimuahidi kumsaidia kikimkakati na kimtandao Mh Zitto kuwa mwenyekiti wa CHADEMA. Pengine aliyetangulia kuomba msaada huu ni Zitto mwenyewe akiamini kuwa anasitahili kuwa mwenyekiti wa chama chake. Lengo ikiwa ni kuleta mbinu mbadala na endelevu ndani ya chama ili 2015 chama kitwae maadaraka. Nadhani kwa hili CCM wako radhi watoe kila walichonacho ili mpango huu ufanikiwe kwa sababu wanajua fika kabisa kuwa CHADEMA chini ya Mh. Zitto ni sawa na TLP ya Mrema kwamba wanaamua chochote wakati wowote kwa kuilinda CCM na masilahi yake kwa ujumla. Na kwa msingi huo basi tunatarajia Zitto kuwa financed na watawala kwa kiasi chochote anachotaka ili kucomplete mission lengwa. Hapa nitasema Zitto na CCM wameamua kuviziana, CCM wakiamini chini ya Zitto CHADEMA wataiua huku Zitto nae akisubiri tu mpango ufanikiwe awageuke CCM maana swahiba wake "Mkulu" atakuwa ameshang'atuka. Na kwa sababu hiyo nachelea kusema tena Mh Zitto hana sifa ya kuwa kiongozi sio tu CHADEMA bali ni katika chama chochote cha siasa hapa nchini.
Sababu hii ya pili nadhani ndio ilioleta ukaribu sana Kati ya Zitto na Mkulu hadi kupitiliza pengine hata ndio chimbuko la msigano na kutoaminika ndani ya CHADEMA na baya zaidi kwa Zitto ni kupoteza mvuto wake sio tu kwa wapenzi na wanachama wa wa-CHADEMA bali kwa watanzania wengi walioichoka CCM na wanaotaka mabadiliko wakiamini wamewasalitiwa na "SHUJAA WAO''.