Hotuba ya Zitto Kabwe - Kigoma: 21 Desemba 2013

Hotuba ya Zitto Kabwe - Kigoma: 21 Desemba 2013

Nyerere: " Bwana Muyanka bin Haji, Kimya msidhani ni ishara ya amani" (Uongozi wetu na hatima ya TZ)
 
Huyu kwa kushambulia majukwaani hakuna anaemfikia,anajua sana kucheza na jukwaa,hongera kwa mtu ataesoma hiyo hotuba labda awe kalewa gongo ndio hatamuelewa Zitto kaongea vitu vya ukweli kabisa, bravoooo Zitto
 
Last edited by a moderator:
Vizuri, amefuata ushauri alopewa juzi (kwenye thread fulani) na Ben Saanane kwamba aangalie asivunje Katiba ya Chadema. Hotuba yake imefanya hivyo tunashukuru!
 
Kuna wengine wanasoma hotuba mara 3 ili wapate kosa watukane,wamekosa wanaleta majungu tu. Tutaanguka na kuinuka pamoja. Tutashnda tu hata kama sio leo au kesho.
 
Katika picha zote na hata jukwaa alilolutumia hakuna bendera ya CHADEMA,hata kwenye maandamano ya wafuasi wa Zitto na pikipiki hakuna bendera ya CHADEMA,na ikumbukwe Zitto amejitapa sana kuwa anakipenda CHADEMA na angependa hata mtoto wake aje kuwa CHADEMA,Mbunge wa CHADEMA na unayehubiri mapenzi kwa chama unakosaje hata bendera moja ya chama kwenye mkutano wako?? Huu sio unafiki??!!

Tukisema kuwa mkutano huu umeratibiwa kwa maelezo maalum na pia kuandaa hadhira mathalani wasibebe bendera wala alama yoyote ya chama Tutaongea?? Tukisema mkutano huu ni wa mamluki dhidi ya CHADEMA tutakosea??!! Zitto ni mtu wa ajabu sana!!

Kwenye hotuba yake amelialia kutokuaminiwa ila kweli inajulikana kuwa matendo ya mtu ya kutilia shaka au maouvu ndio hufanya mtu asiaminike,imani hainunuliwi bali inatengenezwa kwa hiyo matendo ya Zitto ndio yanafanya uonekane msaliti

Kigoma inahistoria chafu ya kutoa wanasiasa wanafiki,wazandiki na wachumia tumbo na Zitto nathubutu kusema ni mmoja wao,Kigoma ingebaki kutoa wacheza mpira na wanamziki kama wakina Kaseja,Maulidi,Ali Kiba n'a wengine lakini si viongozi wa siasa,kwani ni wezi wa fikra na imani za walalahoi kwa maslahi yao binafsi n'a watu wanaowatumikia!!!
 
Siasa za Kunyemeleana na siasa za kificho na kinafiki na za kibinafsi nayo ni Demokrasia! Nani angekupinga kama mawazo yako yangekuwa wazi! kwanini siasa za kificho?Kila mtu anaamini tofauti ya mawazo huru na ya wazi, mawazo yaliyofichama ni haramu, Unafiki ktk siasa nikujimaliza,
 
Hii Hotuba ya kufungia Mwaka!Zitto anajielewa,wakati wapinzani wake wanaongea kwa chuki!Zito ametulia tu:Zito generous politician
Nguruvi3
Mchambuzi
Mkandara
 
Last edited by a moderator:
Hizi ni zama za uwazi na uwajibikaji,tuacha ushabiki na unafiki,hotuba ya zzt hakuna kiongozi yyte wa chadema ambaye anaweza kutoa hotuba iliyojaa maneno ya busara kama hii.
 
Km hama majina bora aache kuzungumzia fedha sa uswiss zaidi ya hapo ni mipasho tu
 
Hotba ni nzuri sana imejaa busara sana na hikma kubwa hususan alipogusa na kutoa takwimu za KUTOAMINIANA ambako siku zote tunakubainisha kunazaa taifa la wenye kunung'unika bila kupata fursa ya kutoa madukuduku yao.

Viongozi wanajenga khofu kwa wanachama waogopwe ili yao yapite na sio viongozi kuogopa wanachama ambako ndioko kuliko na chimbuko la demokrasia,

Nafikiri Dr Slaa na Mbowe ni wakti wa kujifunza kutokana na busara hizi.

Hongera Zito kwa hotba nzuri na kubainisha malezi uliyopata toka kwa wazee wako
 
I like him (Zitto) for some reasons. Future yake ilikuwa nzuri sana ila tamaa ya mapande ya fedha yanafunika mema yake...kama kweli Zitto unaamini katka siasa zenye majawabu kwa kero za wananchi, siasa zitakazoleta unafuu wa maisha then kwanini unatumika visivyo? kwanini u-mwepesi sana wa kupokea hongo?.... Si kweli kuwa madini ya vitu inachimbwa na Watanzania pekee! Almasi ya Mwadui, Tanzanite inamilikiwa na wageni kwa kiasi kikubwa sana... Sera Mbovu za CCM na kiasi wanachokukatia kutoka ktk kiasi kinachotoroshwa inazorotesha mapambano ya kuikomboa nchi yetu... Sijui kama watakusamehe! Ila mimi nakupotezea kama SHIBUDA!!!
 
Katika picha zote na hata jukwaa alilolutumia hakuna bendera ya CHADEMA,hata kwenye maandamano ya wafuasi wa Zitto na pikipiki hakuna bendera ya CHADEMA,na ikumbukwe Zitto amejitapa sana kuwa anakipenda CHADEMA na angependa hata mtoto wake aje kuwa CHADEMA,Mbunge wa CHADEMA na unayehubiri mapenzi kwa chama unakosaje hata bendera moja ya chama kwenye mkutano wako?? Huu sio unafiki??!!

Tukisema kuwa mkutano huu umeratibiwa kwa maelezo maalum na pia kuandaa hadhira mathalani wasibebe bendera wala alama yoyote ya chama Tutaongea?? Tukisema mkutano huu ni wa mamluki dhidi ya CHADEMA tutakosea??!! Zitto ni mtu wa ajabu sana!!

Kwenye hotuba yake amelialia kutokuaminiwa ila kweli inajulikana kuwa matendo ya mtu ya kutilia shaka au maouvu ndio hufanya mtu asiaminike,imani hainunuliwi bali inatengenezwa kwa hiyo matendo ya Zitto ndio yanafanya uonekane msaliti

Kigoma inahistoria chafu ya kutoa wanasiasa wanafiki,wazandiki na wachumia tumbo na Zitto nathubutu kusema ni mmoja wao,Kigoma ingebaki kutoa wacheza mpira na wanamziki kama wakina Kaseja,Maulidi,Ali Kiba n'a wengine lakini si viongozi wa siasa,kwani ni wezi wa fikra na imani za walalahoi kwa maslahi yao binafsi n'a watu wanaowatumikia!!!

Ha ha ha duuuh!kasimama kama mwanakigoma,mwanadiplomasia,mtanzania
 
Ama kwa hakika, kijana amejitahidi kuwa mtanzania na sio mkigoma wa ujiji kwa livingstone ambako unaweza kupata nyumba bora ukapanga kwa 5000/= kwa mwezi ingawa utaikimbia mwenyewe ndani ya wiki moja ukakataa kutoa sababu! Dah! Anaweza kuwa msaliti kweli, lakini hotuba yake haionyeshi yuko hivyo. Anasemea taifa la walalahoi na anajua anachokifanya. Anaonyesha kakomaa kisiasa na kama ni sifa msifuni anapostahili, msimponde 100% kwani hastahili. barabara mulefu haikosi kona kama vile mwanamke muzuri hakosi kasoro. Hata Lucifer ambaye alikuwa nambari mbili baada ya Mungu kule mbinguni alikuwa na kasoro na bahati mbaya akatimuliwa kwa sababu ya kutaka kuwa kama Mungu Bosi wake. Tujifunze mfano huo vizuri maana kama kungekuwa na mapatano kati yao huenda dunia hii pangekuwa mahali pazuri pa kuishi maana dhambi usingekuwa msamiati tena ulio maarufu. Songa mbele Zitto, lakini patina na wenzako na uwe tayari kuheshimu utawala na misingi bora ya utawala, usifanye mambo ya hatari kwa kificho na wala usifungamane na watu wenye nia mbaya. Sio wote wanaokuzunguka ni marafiki wazuri kwako, kuna wengine wanafanya project against your efforts. Unaweza kuwa kiongozi bora lakini hakikisha unakuwa msafi kiakili kiutu na kimatendo ili wabaya wako washindwe kuingia kichwa kichwa kukuwekea mapingamizi. Huwezi kuwa malaika, lakini jitahidi kwani hata Mandela na Nyerere sio kwamba hawakufanya makosa, walifanya na tena mengine yaweza kuwa aibu hata kuyataja. Huo ndio ubinadamu, lakini ukubali kukosea pale unapoambiwa umekosea, na uombe radhi. Ningefurahi zaidi endapo katika hotuba yako angalau ungeweka wazi kama una mawazo gani kuhusu kuwa mwanachadema hai hata nje ya vyeo vya juu vya chama au umewapa njia nyeupe vyama vingine wakuchukuwe uende kwao ikiwemo ccm. nakushauri komaa na CDM kama JK alivyokomaa na EAC kwamba TZ ilikuwamo, imo na itaendelea kuwamo na kuzidi kuwa mwanachama mwaminifu siku zote. Mungu ajuaye kuufinyanga moyo wa binadamu na kuufanya uzaliwe upya kwa ubora kila siku na akusaidie zaidi kukujaza hekima na uadilifu. Amen.
 
Zitto msiwaamini wanasiasa hata wakiwa wa upinzani mwezi wa 10 Tabora leo nwezi wa 12 kigoma anataka watu wa mwamini! anaakili huyu kweli au unafki tu
 
Well said. Zitto anayekutakia mabaya ili upotee katika siasa za Tanzania huyo ni adui wa Tanzania na watanzania.
 
Back
Top Bottom