Labda tukueleze hivi ndio ufahamu. Kwani hao watumwa walitoka Zanzibar au walitoka kwengineko? Ukishajibu hili utafahamu kwanini historia ya Zanzibar ( hasa ukizungumzia ustaarabu) haina ulazima wa kujumuishwa na utumwa.
Kama ni msomaji wa historia utafahamu kuwa waliokuwa wakiuza binaadamu wenzao ni watu wa Bara na wakiwauzia Waarabu, Mzanzibari hakuwa akiuzwa wala akinunua mtumwa kutoka Bara.
NI upumbavu na upotoshaji wa kumuhusisha Mzanzibari yeyote na utumwa na badala yake ni sahihi kabisa kusema kuwa Watanganyika waliuzana wakati ule na sasa ............
Pole sana Mzee naona unajichanganya tu hapa, na yale usiyayajua. Nafikiri inabidi uwatake radhi wewe Wazanzibari. Wazanzibari wanajielewa na wengi wao ni kweli hawahusiani kabisa na mtiririko huo wa watumwa waliotolewa kutoka kwa Mtipu au sehemu nyengine za Bara. Wazanzibari walio wengi ni kutoka sehemu za vijijini (MASHAMBA) mote Unguja na Pemba, ni weusi na wenye asili ya Kiafrika-lakini asilani hawahusiani na kadhia ya utumwa. Ni kweli katika Wazanzibari wa leo wapo wale walioguswa na kadhia ya utumwa lakini ni wachache sana (miongoni wa wale wanaotokana na asili ya kiafrika). Hawa ni wale ambao hawana nasaba na vijijini (Mashamba ya huko)- Ni wale wa kuzikwa Mwanakwerekwe tu. Fundi jitahidi uielewe Zanzibar na Watu wake . Sote tunapinga Utumwa ni jambo baya la Kihistoria.Kwanza mzanzibari ni nani?
Watu wanaojiita wazanzibari sasa hivi wametokana na matunda ya wale waliokuwa wakiishi huko( waarabu, wahindi, wangazija, wanyamwezi, wanyasa n.k.). Wanajumuishwa wale waliokuwa wakijiita waungwana na wale waliokuwa watwana wao. Katika hao waliokuwa watwana wengi wao walitokana na watumwa. Kusema leo kuwa utumwa haukuwahusu ni kuwatukana matusi ya nguoni na ndiyo maana wengi wao hawawaamini mnapotoa machozi ya mamba na kujifanya kuwa ati kuwa nyie wote ni wazanzibari.
Amandla.......
Kwanza mzanzibari ni nani? Kuna kabila linaloitwa wazanzibari? Kuna "race" inayoitwa wazanzibari? Wau waliokuwa wakiishi Zanzibar walikuwa mchanganyiko. Walikuwepo waarabu, wahindi, wanyasa, wangazija, wafaransa, waingereza n.k. Wote hawa walijitambulisha kwa uasili wao na sio uzanzibari. Mwarabu alikuwa mwarabu, mtumbuka mtumbuka, mhindi mhindi, mnyasa mnyasa n.k. Huo utaifa wa uzanzibari ni kitu kigeni na wala si cha muda mrefu. Watumwa waliokuwa wakiuzwa Zanzibar walitoka kwenye bara la Afrika. Wengine walinunuliwa na watu waliokuwa wakiishi Zanzibar na walitumikishwa majumbani na kwenye mashamba. Wengine walisafirishwa kwenda uarabuni na baada ya biashara ya utumwa Afrika Magharibi kuwa ngumu,wengine walinunuliwa na wazungu na kupelekwa Marekani na kwengineko. Biashara ya utumwa kwa kiasi kikubwa ilifadhiliwa na wafanyabiashara wa kihindi ambao walitoa pesa kwa waarabu ( nadhani unatambua kuwa muarabu alikuwa mtu yeyote aliyekuwa na damu ya muarabu hata kama alichanganya kama Hamad bin Muḥammad bin Jumah bin Rajab bin Muḥammad bin Sa‘īd al-Murgab maarufu Tippu Tib) ambao walisafiri ndani kwenda kununua watu (hawa hawakuwa watumwa wakati huo) kutoka kwa baadhi ya makabila. Watu hawa wengine walitokana na matekwa wa vita baina ya makabila, watu ambao walionekana hawakubaliki katika makabila kwa sababu yeyote (wachawi, wezi n.k.) n.k. Wengine walichukuliwa kwa maelewano kuwa watasaidia kuwabebea mizigo hao wageni. Pamoja na kuyalaumu haya makabila kwa ushiriki wao katika biashara hii haramu ni lazima tukumbuke kuwa dhana ya kumnunua au kumuuza binadamu mwenzako ililetwa hapaa kwetu na waarabu na kwa wenzetu na waarabu pamoja na wazungu.
Watumwa hapa kwetu na sehemu nyingi tu duniani ( ulaya, asia n.k) ulitokana na matekwa wa vita, watu ambao walifanya uovu na sehemu nyingine madeni. Mtumwa hakupoteza utu wake. Kulikuwa na mipaka ya vitu ambavyo anaweza kufanyiwa na alikuwa na haki zake. Waarabu hao unaowatetea ndio walileta tafsiri ya binadamu kama bidhaa. Kwa kuwa alikuwa bidhaa, mwenye mtumwa alikuwa na haki ya kumfanyia chochote atakacho na waliwafanyia. Waliwatumia kama target katika mazoezi ya shabaha, waliwahasi, waliwanyang'anya watoto wao, waliwabaka na matendo mengine maovu. Kwa mtu yeyote kutetea hii biashara na kudai kuwa hao waarabu walichokileta ni uarabu ni beyond contempt. Hasa kama huyo jamaa anajiita mwafrika!
Hao unaowaita wastaarabu hata siku moja hawakujihesabu ni wazanzibari mpaka wimbi la waafrika kuanza kudai haki zao. Ingawa Sultan wa Oman alihamisha makao makuu yake Zanzibar haikuwa na maana kuwa Zanzibar ilitawala Oman. Zanzibar ilitawaliwa na kuingizwa katika himaya ya Oman. Hao unawaita wastaarabu walipobanwa na wazungu kukomesha biashara ya utumwa, na bandari yao kuzingirwa na kuziwa kusafirisha watumwa, walijenga mji wa Dar es Salaam ambao walitegemea utawapa nafasi ya kuendeleza biashara hiyo haramu bila kuingiliwa na wazungu. Hao unaowaita wastaarabu waliona ni haki yao kufanya watu kama mimi kuwa watumwa wao na ndiyo maana huko Saudi Arabia utumwa ulipigwa marufuku mwaka 1959!
Watu wanaojiita wazanzibari sasa hivi wametokana na matunda ya wale waliokuwa wakiishi huko( waarabu, wahindi, wangazija, wanyamwezi, wanyasa n.k.). Wanajumuishwa wale waliokuwa wakijiita waungwana na wale waliokuwa watwana wao. Katika hao waliokuwa watwana wengi wao walitokana na watumwa. Kusema leo kuwa utumwa haukuwahusu ni kuwatukana matusi ya nguoni na ndiyo maana wengi wao hawawaamini mnapotoa machozi ya mamba na kujifanya kuwa ati kuwa nyie wote ni wazanzibari. Mpaka hapo mtakapokiri na kuwaomba msamaha kwa yale mliyowatendea, hatutakuwa na imani na nyie kwa vile tunajua kuwa bado mnatuhesabu kuwa ni watwana wenu. Hilo hatutariruhusu lirudi kamwe. Kwa msemo wa vijana wa siku hizi, mlie tu.
Amandla.......
Jitahidi ujifunze uchambuzi wa mambo (analysis).they way i ve seen Karume kamuahidi kitu maalim ampigie debe abaki ikulu, Cha msingi maalim na karume watuweke wazi walijadili nini that day!
Pole sana Mzee naona unajichanganya tu hapa, na yale usiyayajua. Nafikiri inabidi uwatake radhi wewe Wazanzibari. Wazanzibari wanajielewa na wengi wao ni kweli hawahusiani kabisa na mtiririko huo wa watumwa waliotolewa kutoka kwa Mtipu au sehemu nyengine za Bara. Wazanzibari walio wengi ni kutoka sehemu za vijijini (MASAHAMBA) mote Unguja na Pemba, ni weusi na wenye asili ya Kiafrika-lakini asilani hawahusiani na kadhia ya utumwa. Ni kweli katika Wazanzibari wa leo wapo wale walioguswa na kadhia ya utumwa lakini ni wachache sana (miongoni wa wale wanaotokana na asili ya kiafrika). Hawa ni wale ambao hawana nasaba na vijijini (Mashamba ya huko)- Ni wale wa kuzikwa Mwanakwerekwe tu. Fundi jitahidi uielewe Zanzibar na Watu wake . Sote tunapinga Utumwa ni jambo baya la Kihistoria.
Pumba tupu, hivyo alivyoeleza Maalim imetosha.Ni wazi Zanzibar ilikuwa ni jamii moja sawa na sehemu nyengine yoyote ile.Kuja ukoloni wa kiingereza ndio jamii ilianza kugawika.Hii principle is applicable all over those old colonies.Nenda Rwanda, nenda Burundi...kote humo kulikuwa watu wanaishi fresh walikuja kugawanyika baada ya mkoloni.
Na hiyo principle ya wakoloni kugawa watu, ndio chanzo cha conflicts nyingi za barani afrika.Sasa wewe hapa kwenye hiyo story ndefu sijuwi unatuletea story gani?Zanzibar ni taifa kongwe kushinda Tanganyika, sasa hapo unataka kutuambia kuwa hili taifa miaka yote hiyo ilikuwa halina uongozi na watu wake walikuwa hawajitambulishi kwa uraia wao.???
Acha kasumba za Nyerere ndugu yangu, wazanzibari ni watu wanaoringia sana taifa lao la Zanzibar.Hadi leo wazanzibari hawajakubali kupoteza utaifa wao completely, hii ni kwasababu taifa lao wanaliona lina records nzuri za kumfanya mtu awe really proud of his or her own country.
Hata kama race ni nyingi Zanzibar, kuna sehemu ambayo hakuna?Hapo tanganyika kwani ni vipi?Makabila hayapo?Hakuna huyu mmasai na myakusa??
Mie niliwahi kutoa maoni, kama mtu sio mzanzibari tafadhali kaa kando waachieni hao jamaa wadili na matatizo yao bila ya chochoko.Matatizo yapo kila nchi, Rwanda hapo watu walichinjana na kutoana roho....na sehemu nyengine nyingi tuu hata nyie munazijua za hapo Tanganyika mukitiana mapanga kupigania mifugo.
Sasa hili la Zanzibar nalo halina tofauti yoyote, waacheni wazanzibari wafix problems zao.Kujiingiza kati kati ni kuonesha kuwa muna special interests in those islands...as it has been since Nyerere
Haujui hata asili ya vyama vyenu vya siasa? Kama wazanzibari ni wamoja kwa nini Salim Ahmed Salim alipingwa na wazanzibari wenzake? Hao mnaowaita Hizbu ni kutoka wapi? Zanzibar toka mwanzo haijawa jamii moja. Mwanzoni mlikuwa na watwana na waungwana, kabla ya uhuru mkagawanyika kikabila, chama cha weusi, chama cha waarabu n.k. Mapinduzi yalifanyika kwa msingi wa rangi. Masuala ya rangi yalichangia sana katika utawala wa Karume I. Au haujui kuwa wahindi walikimbia Zanzibar kwa kuogopa kuozeshwa kwa nguvu?SIZE]
Waarabu wengi walizaa na watumwa wao na watoto wao wakahesabiwa waarabu. Wangapi Zanzibar (waarabu, wahindi n.k.) ambao mababu zao walihusika na biashara ya utumwa? Wangapi katika nyie waarabu safi ambao wazazi wenu walikuwa na watumwa au walishiriki katika biashara hiyo? Mnataka kuniambia mashamba ya karafuu yote yalilimwa na watu huru? SIZE]
Lakini mbona hakuna lolote lile linaloashiria kuwa juhudi za sasa hivi za maridhiano zina dalili ya kuhatarisha special interests (kama unavyofikiria wewe) za Wa-tanganyika ( kumradh- Watanzania). Au unamaana interests za Wa-tanganyika ni kuona Wazanzibari wanagombana na kuhitilafiana kila siku.waacheni wazanzibari wafix problems zao.Kujiingiza kati kati ni kuonesha kuwa muna special interests in those islands...as it has been since Nyerere
Msitufanye wote wajinga. Kwa kukataa matatizo yaliyokuwepo na misingi yake hata siku moja hapatakuwa na suluhisho la kudumu.
Amandla.....
Lakini mbona hakuna lolote lile linaloashiria kuwa juhudi za sasa hivi za maridhiano zina dalili ya kuhatarisha special interests (kama unavyofikiria wewe) za Wa-tanganyika ( kumradh- Watanzania). Au unamaana interests za Wa-tanganyika ni kuona Wazanzibari wanagombana na kuhitilafiana kila siku.
Pamoja na maelezo yako mazuri ni vema ukajua hata Maalim Seif anajua nafasi ya utumwa katika historia ya Zanzibar. Ndio maana hata kwenye kuelezea historia ya Zanzibar aliweza kunukuu kauli ambayo iliashiria umaarufu wa Zanzibar katika utumwa... soma hapa chini
Kauli hii ilitokana na biashara ya utumwa na umaarufu na Zanzibar kipindi hicho. Na unaweza kuipata katika kitabu kilichoandikwa na Amin, Mohamed; Willetts, Duncan and Marshall, Peter. Kiitwacho Journey Through Tanzania, ukurasa wa 13.
Aidha sioni nafasi ya ushoga katika historia hiyo na kanisa la Anglikani, labda kama una maelezo yakinifu kuhusu hilo. Itakuwa ni jambo la maana iwapo utaweza kutuwekea hapa ili kupata ufahamu wake.
Kumbuka watumwa aliokuwa wakipelekwa Uarabuni walifanywa nini kabla ya kuondoka Zanzibar.
Amandla!!!. Mzee. Hivi sijui unafikiria idadi gani ya waarabu waliingia pale Zanzibar. Sijui walikuwa na uwezo gani hao waarabu kuzaa (watoto) na watumwa wao. Hatimaye wakawa wengi wakaunda ZNP na kuweza kuwapa kashkash ASP hata katika uchaguzi. Tuyasarif ya sasa sijui kwa mantiki hiyo hiyo hao watoto wa waarabu wanaweza kuwa na uwingi wa kiasi gani wakaiwezesha CUF kuisogelea kwa karibu mno CCM katika kura za uchaguzi. Achana na kasumba hizo, tuwape nafasi Wazanzibari wa leo watafute njia za kujenga Zanzibar mpya. Hilo ni jambo lao tuwaachie wenyewe.