HOTUBA ya Seif Sharrif na Majibu yake kuhusu Maridhiano Zanzibar!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
MARIDHIANO NA MUSTAKBALI WA ZANZIBAR

Na Seif Sharif Hamad

UTANGULIZI

Zanzibar inapita katika mojawapo ya vipindi muhimu sana vya historia yake ya kisiasa. Nuru mpya ya matumaini imechomoza kupitia Maridhiano ya Wazanzibari. Hatua hii imekuja kufuatia mkutano na mazungumzo ya kihistoria kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Amani Karume, na mimi nikiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) huko Ikulu ya Zanzibar , Novemba 5, 2009 yaliyokuwa na lengo la kujenga mustakbali mpya wa siasa Zanzibar .

Mazungumzo hayo yalifuatiwa na hatua ya kijasiri ya CUF ya Novemba 7, 2009 ya kwenda hadharani kutangaza kumtambua Rais Karume na Serikali anayoiongoza na kukubali kushirikiana na kufanya naye kazi pamoja kwa maslahi ya Zanzibar na watu wake.

Pamoja na hatua hiyo kuonekana kuwachanganya wana-CUF pale ilipotangazwa kwao kwa mara ya kwanza, lakini viongozi wa CUF tukiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba, hatukuyumba wala kurudi nyuma na tukaamua kufanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wanachama kupitia mikutano ya hadhara na vikao vya ndani hadi kufikia hatua ya sasa ambapo wana-CUF takriban wote sasa wanakubaliana na hatua zinazochukuliwa. Ushiriki mkubwa na wa aina yake wa wana-CUF katika kilele cha sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 zilizofanyika kisiwani Pemba ni ushahidi tosha wa hali hiyo ninayoieleza. Nataka nitumie fursa hii kuwashukurukwa dhati wana-CUF wote kwa kutuelewa na kutuunga mkono katika hatua zetu hizi tunazozichukua.

Kwa upande wake, Rais Amani Karume naye amehutubia mkutano wa hadhara wa CCM Novemba 22, 2009 na kutoa hotuba iliyotoa mwelekeo mpya wa mahusiano ya kisiasa hapa Zanzibar . Pamoja na mambo mengine, alitangaza kwamba milango iko wazi kuweza kuzungumza jambo lolote lenye maslahi na Zanzibar na watu wake. Hotuba zake za hivi karibuni alipokuwa katika ziara rasmi kisiwani Pemba na baadaye katika matukio mbali mbali ya Sherehe za Mapinduzi zimeendelea kusisitiza azma yake ya kujenga Zanzibar mpya yenye umoja, maelewano, mshikamano, amani, utulivu na maendeleo kwa watu wake wote.

Nafurahi kuona hotuba zetu, mimi na Rais Karume, tukiwa ndiyo viongozi wakuu wa kisiasa hapa Zanzibar zimesaidia kuyazamisha maridhiano haya katika nyoyo za wafuasi wa vyama vya CCM na CUF na pia katika nyoyo za Wazanzibari wote. Zanzibar inashuhudia hali ya matumaini ambayo haijapata kuonekana kwa miaka mingi.

Kiwango cha kuaminiana kimekuwa cha juu kabisa na hatua ya karibuni ya Rais Amani Karume kutangaza kuwateua viongozi wawili waandamizi wa CUF, Mhe. Juma Duni Haji na Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi imepokelewa kwa furaha kubwa kuwa ni hatua sahihi katika kuimarisha maridhiano yaliyofikiwa.

Umuhimu wa hatua tunazochukua umeonekana kutokana na kauli mbali mbali za viongozi wa ndani na hata nje ya nchi, taasisi zisizo za kiserikali na jumuiya mbali mbali za kiraia, wasomi, viongozi wa dini na wengine wengi za kupongeza hatua hizo. Nachukua fursa hii kuwashukuru wote hao kwa kutuunga mkono katika hili. Lakini na mimi pia naungana na Rais Karume katika kumpa shukrani nyingi na za pekee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa salamu zake za pongezi kwetu ambazo siyo tu zilibeba ujumbe mzito kwa wale wote wanaobeza hatua tuliyochukua lakini pia zilikuwa zimeambatana na ahadi yake kwamba anatuunga mkono kwa hatua tunazochukua na kwamba tutegemee kila msaada tunaouhitajia kufanikisha yale tuliyoyakusudia. Binafsi nimefarijika sana na ahadi yake hiyo kwani hapana shaka yoyote kwamba msaada wake unahitajika sana .

Ukiacha salamu hizo za pongezi, Wazanzibari wengi wameifurahia hatua tuliyochukua na wana matumaini makubwa kuwa itafungua milango mikubwa zaidi ya mashirikiano. Bila shaka wapo pia vidudu mtu wachache ambao wanafanya kila juhudi kutaka kuturudisha kule kule tulikotoka kwa sababu tu ya kujali maslahi yao . Natoa wito kwa wananchi wote kwamba wawapuuze na nawahakikishia kwamba mimi na Rais Karume tumekubaliana kuwa hakuna kurudi nyuma katika hatua tuliyoianzisha. Ni nia yetu kuona kuwa tunaitumia fursa hii kuirudisha Zanzibar katika nafasi yake iliyokuwa nayo huko nyuma ambayo ilipotea kutokana na kuendekeza kwetu tofauti zetu badala ya yale yanayotuunganisha. Time has come to make Zanzibar great and proud of herself again.

ZANZIBAR ILIKOTOKA
“Ipigwapo zumari Zanzibar , hucheza walioko katika Maziwa Makuu.” Huu ni usemi wa kihistoria unaoeleza nafasi kubwa viliyokuwa nayo visiwa vyetu katika kusarifu na kushawishi mwenendo wa mambo katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Hizo zilikuwa zama za Zanzibar kuvuma kutokea upande huu wa magharibi ya Bahari ya Hindi kuelekea ndani ya Bara la Afrika hadi mashariki ya Congo na pia kuelekea sehemu za kaskazini kwenda Bara Arabu, Bara Hindi na Mashariki ya Mbali na pia kupenya hadi Ulaya na Marekani.

Udogo wa visiwa vya Zanzibar haulingani na umuhimu wake katika historia ya Afrika Mashariki, Bahari ya Hindi, Arabuni hadi Mashariki ya Mbali. Umuhimu huo ulitokana na maendeleo makubwa yaliyokuwa yamepigwa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za maisha. Na hali hiyo haikuja kwa bahati mbaya bali ilitokana na ustaarabu uliojengeka karne nyingi sana zilizopita. Inatambulika, kwa mfano, kwamba Zanzibar , au Dola ya Zinj, ndiyo dola kongwe kuliko zote katika eneo lote la Afrika kusini ya jangwa la Sahara .

Watu wa visiwa vya Zanzibar walitoka sehemu mbali mbali: Afrika ya Mashariki na Kati , Iran , Arabuni, Bara Hindi, Ngazija, Mashariki ya Mbali, Ulaya n.k.

Zanzibar inaelezwa kutajwa kwa majina tofauti tangu miaka 500 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (a..s.). Uvumbuzi wa karibuni wa mapango ya watu wa kale katika ukanda wa Mashariki Kusini wa kisiwa cha Unguja unaonesha kuwepo kwa makaazi ya watu tokea zama za mawe ziitwazo kama ‘Stone Age’. Katika kitabu maarufu chenye kumbukumbu za wasafiri wa kale wa Ugiriki waliotembelea mwambao wa Afrika Mashariki kiitwacho Periplus of the Erythrean Sea kilichoandikwa mwaka 100 A.D. (kabla ya Nabii Issa), Zanzibar imetajwa kwa jina la ‘Menouthias’ ikiwa tayari ni nchi yenye watu mchanganyiko tena walio na ustaarabu wakiwa wanavaa nguo za hariri. Huko Oxford, imeonekana ramani ya wasafiri wa Kiarabu iliyotayarishwa Karne ya 11 ambayo inaonesha visiwa vya Zanzibar na mji mkuu wake ukiwa Unguja Ukuu.

Kwa muda mrefu, Zanzibar ilikuwa imegawanyika katika falme mbali mbali, mpaka ilipofika mwaka 1500 ulipoanzishwa utawala wa Mwinyi Mkuu akiwa ndiyo alama ya utawala wa kienyeji Visiwani. Mwinyi Mkuu wa mwisho, Ahmed bin Muhammed bin Hassan el-Alawy alifariki 1873. Mwaka 1503 Wareno waliivamia Zanzibar kupitia Unguja Ukuu na wakaitawala kwa muda mrefu wakifanya vitimbi vya kila aina. Waomani kwa maombi ya wenyeji walikuja katika Dola ya Zinj na kupambana na Wareno na hatimaye wakafanikiwa kuwatimua. Sayyid Said bin Sultan alifika Zanzibar mwaka 1828, na kutokana na kuvutiwa na mandhari yake mwaka 1832 akaifanya Zanzibar kuwa makao makuu ya utawala wake badala ya Muscat .

Katika kipindi hiki Zanzibar iliweza kujitambulisha na kutambuliwa kama Dola huru katika ulimwengu. Zanzibar ikawa kituo muhimu cha kisiasa, kiuchumi na kibiashara katika Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi.. Kutokana na umuhimu wake, Madola makubwa yalifungua Ofisi za Kibalozi mjini Zanzibar : Marekani (1837), Uingereza (1841), Ufaransa (1844), na baada ya hapo Ureno, Utaliana, Ubelgiji na Ujarumani zikafuata.

Madola ya Ulaya yalipoanza njama za kinyang’anyiro cha Afrika kwa lengo la kuigawanya kuwa katika makoloni yao , Zanzibar iligombaniwa baina ya Waingereza na Wajarumani. Baada ya vuta nikuvute, mwaka 1890 iliwekwa chini ya Himaya ya Kiingereza (Protectorate) katika Mkataba uliotiwa saini kati ya Mfalme wa Kiingereza na Sayyid Ali bin Said na kwa kutambua hadhi tofauti ya Zanzibar , masuala yake yalikuwa yakiendeshwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje (Foreign Office) ya Uingereza. Mwaka 1913, masuala ya utawala wa Zanzibar yalihamishwa kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje (Foreign Office) na kupelekwa rasmi Ofisi ya Makoloni (Colonial Office).

Kidogo kidogo, harakati za kuanzisha mfumo wa Utawala wa sura ya kikoloni zikaanza pale ilipotungwa Sheria (Order-in-Council) ya 1926 iliyoanzisha Baraza la Kutunga Sheria (LegCo) na Baraza la Utawala (ExCo). Ni katika kipindi hicho ambapo mfumo wa uwakilishi wa kikabila ulianzishwa ukiwaweka kando Waafrika na Washirazi na hivyo kupanda fitina za mifarakano chini ya sera ya Waingereza ya ‘wagawe uwatawale’ (divide and rule). Ilichukua miaka 20, hadi mwaka 1946, ambapo Mshirazi wa kwanza, Sheikh Ameir Tajo, aliteuliwa kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria akifuatiwa na mwenzake, Sheikh Ali Shariff Mussa, aliyeteuliwa mwaka 1948.

Miaka ya 50 ilishuhudia harakati za kudai uhuru kwa kuundwa vyama vya ukombozi: Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kilichoasisiwa 1955 na Afro Shirazi Party (ASP) kilichoundwa 1957. Katika kipindi cha miaka saba ya mchuano mkali wa nani anafaa kukabidhiwa Uhuru wa Zanzibar, kulifanyika chaguzi nne ambazo ni Julai 1957, Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963. Chaguzi hizo zilishindwa kuwaweka pamoja Wazanzibari na badala yake zikawa chachu ya kugawika kwa jamii kati ya mapande mawili yenye nguvu takriban sawa sawa. Hali ikazidi kukorogeka pale vyama hivyo vikuu navyo vilipopasuka ambapo Afro Shirazi Party ilimeguka na kupelekea kuanzishwa Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) mwaka 1959 na Zanzibar Nationalist Party nayo ikapasuka na kupelekea kuanzishwa Umma Party mwaka 1963. Zanzibar ikawa inaelekea katika Uhuru ikiwa ni jamii iliyogawanyika.

Uingereza ilikabidhi Uhuru kwa Zanzibar tarehe 10 Desemba 1963 chini ya Sultani na Serikali ya ZNP/ZPPP. ASP hawakuubali Uhuru huo na tarehe 12 Januari, 1964 ilifanya Mapinduzi na Zanzibar ikatangazwa kuwa Jamhuri.

Haya niliyoyaeleza ni mukhtasari tu wa historia ya Zanzibar unaoonesha vipindi mbali mbali ambavyo nchi ilipitia katika ujenzi wa Taifa.

Lakini pamoja na misukosuko ya kisiasa tuliyokumbana nayo, ni vyema ikaeleweka na hususan kwa vijana wa leo kwamba Zanzibar hii imeweka rekodi mbali mbali za kujivunia na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu na ustaarabu. Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha taa za umeme za barabarani na mitaani (zikiitwa taa za stimu) kabla ya miji ya London na New York ? Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake mwaka jana, Bwana Mark Green, wakati akitoa hotuba yake ya kuaga, alisema meli za Marekani zilikuwa zikitia nanga katika bandari ya Zanzibar kuja kununua mafuta ya nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia taa zao za barabarani wakati Zanzibar ikiwa inatumia umeme. Sayyid Said bin Sultan alipeleka Balozi wa kwanza wa Zanzibar nchini Marekani, Ahmed bin Nu’man mwaka 1840.

Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na sarafu yake katika Afrika kusini ya Sahara zilizoanzishwa wakati wa Tawala za Kishirazi ambazo zilichimbuliwa katika maeneo ya Unguja Ukuu, Mkumbuu na Mtambwe Mkuu katika miaka ya tisini. Baadaye katika mwaka 1908, ikawa tena nchi ya kwanza katika eneo hili kuanzisha sarafu za noti zake wenyewe (rupia za Zanzibar ) ambazo ziliendelea kutumika hadi 1936 ilipoanzishwa sarafu ya shilingi ya Afrika Mashariki chini ya Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki.

Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza katika eneo hili kufunga mikataba ya kibiashara na nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa na Jiji la Hamburg (kabla ya kuanzishwa kwa Shirikisho la Ujarumani). Zama hizo, nchi yetu pia ilikuwa na mahusiano ya kibiashara na nchi za Arabuni , India , China , Malaysia na visiwa vya Java na Sumatra (ambavyo sasa ni Indonesia ) na kupitia mahusiano hayo, iliweza kujenga utamaduni na ustaarabu wa kipekee.

Wakati Zanzibar inapata uhuru wake, ilikuwa nchi ya pili katika Afrika kwa ukubwa wa wastani wa pato la wananchi wake, na ya tatu kwa kiwango cha elimu na pia ikiwa na taasisi 17 za fedha zikiwemo benki na kampuni za bima.

Haya yalikuwa katika kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya 1964 lakini hata baada ya Mapinduzi, nafasi ya Zanzibar katika Afrika haikupotea. Ilikuwa nchi ya kwanza katika Afrika kusini ya Jangwa la Sahara kuanzisha televisheni ya rangi na pia ikitoa huduma zote muhimu za jamii bure kwa wananchi wake. Ilifikia wakati ambapo Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar , Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, alitangaza hadharani kwamba hakukuwa na nchi yoyote iliyokuwa ikiidai Zanzibar bali Zanzibar ndiyo iliyokuwa ikizidai baadhi ya nchi malimbikizo ya madeni yanayotokana na uuzaji wa karafuu zake.

Nimeamua kuchukua muda mrefu kidogo kuyadondoa haya ili tujue wapi nchi yetu ilikotoka na kwa vipi migogoro ya kisiasa iliyokuja kuvigubika visiwa vyetu na wananchi wake ilikuja kutuathiri vibaya na kuyapoteza mengi kati ya haya.


CHAGUZI: SUMU YA UMOJA WA WAZANZIBARI

Sina haja ya kurejea historia ya chaguzi mbali mbali zilizofanyika hapa Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi ili kuthibitisha hoja yangu kwamba chaguzi zimekuwa ndiyo sumu ya umoja wa Wazanzibari.

Ni bahati mbaya sana kwamba maendeleo ya kisiasa ya harakati za kudai uhuru wa Zanzibar yaliyoshika kasi kuanzia uchaguzi mkuu wa mwanzo visiwani wa 1957 yaliibua hisia kali zinazotokana na matukio ya vipindi mbali mbali vya historia ambavyo viliambatana na mapambano ya kitabaka na hivyo kupelekea siasa za wakati huo kugubikwa na wimbi la chuki, hasama na kutoaminiana lililokuwa limejikita kwa miongo kadhaa. Vyama vya siasa vilipokuja kuundwa havikuweza kukwepa athari hii na matokeo yake yakawa ni mapambano ya vuta nikuvute ambayo yalipelekea vurugu na fujo zilizoambatana na roho za watu kupotea. Kila kitu katika maisha ya Mzanzibari kikawa ni siasa. Shughuli zote za maisha ya kila siku zikawa zinafanywa kwa misingi ya vyama vya siasa. Jamii ya Zanzibar ikawa imegawanyika kati kati.

Bila shaka mbali na matukio hayo ya kihistoria, pia kulikuwa na athari mbaya za baadhi ya nchi jirani na za mbali ambazo zilikuwa na khofu kubwa na umaarufu wa Zanzibar , nchi ambazo ziliamua kujipenyeza katika siasa zetu na kuchochea na hata kuikoleza mifarakano iliyokuwepo.

Kabla ya Mapinduzi, chaguzi zikitegemea wingi wa viti ili kupata mshindi wa kuunda serikali. Wingi wa kura haukuwa kigezo cha ushindi. Pamoja na kwamba utaratibu huu ulilalamikiwa na ASP kwa kule kupata kwake viti vichache wakati ikiwa na kura nyingi, wingi huo bado ulionesha kwa wastani mgawanyiko wa takriban nusu kwa nusu ya ushindi wa vyama vya wakati huo.

Katika mtiririko wa historia ya kisiasa ya Zanzibar , kielelezo kikubwa cha ukosefu wa kuaminiana kinaonekana katika uendeshaji wa uchaguzi na matokeo yake. Kama nilivyoeleza kabla, Zanzibar ilifanya chaguzi nne kabla ya Mapinduzi ya 1964 ambazo ni zile za Julai 1957, Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963 na imeshafanya chaguzi tatu tokea mfumo wa vyama vingi uliporudishwa yaani 1995, 2000 na 2005.

Katika chaguzi hizo zote zilizowahi kufanyika Zanzibar , ukiacha uchaguzi wa mwanzo wa 1957, hakujawahi kutokea uchaguzi wowote ambao washiriki wake waliridhika kikamilifu na uendeshaji wake na wakayapokea kwa moyo mkunjufu matokeo yake. ASP ililalamikia uendeshaji na matokeo ya chaguzi za Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963 na katika kipindi hiki cha kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi tokea mwaka 1992, CUF imelalamikia uendeshaji na matokeo ya chaguzi za 1995, 2000 na 2005. Kikubwa kinachokosekana ni imani kwa taasisi zinazoendesha na kusimamia chaguzi.

Ikiwa tunakubaliana na ukweli huu, ni wazi kwamba bila ya kushughulikia kiini hiki cha migogoro isiyokwisha katika siasa zetu basi ufumbuzi wa dhati na wa kudumu wa migogoro ya kisiasa hautapatikana.

Naamini kwa dhati kabisa njia mojawapo ya kujengeana imani kati ya kambi mbili kuu za kisiasa visiwani Zanzibar ni kuzifanya kambi hizo zifanye kazi kwa pamoja katika uendeshaji wa nchi.

Tafakuri ya kina ya hali ya mambo inavyokuwa wakati wa uchaguzi na pia dalili za kheri zilizooneshwa na Rais Amani Abeid Karume za kutaka kujenga mustakbali mpya wa kisiasa Zanzibar zilitufanya tuone haja ya kushirikiana naye ili kuwaunganisha Wazanzibari wawe kitu kimoja huku tukiamini kwamba katika umoja, tutaweza kuyafikia yale makubwa ambayo tumeshindwa kuyafikia kwa kule kufarikiana kwetu.


MARIDHIANO: FURSA ZILIZOKO MBELE YETU

Mmojawapo wa Marais wa Marekani anayeheshimika sana katika nchi yake na duniani kwa jumla, Abraham Lincoln, aliwahi kusema kuwa ‘A house divided against itself cannot stand’ yaani ‘Nyumba iliyogawanyika haiwezi kusimama’. Haya ni maneno yenye hekima kubwa sana . Ni wazi kwamba Zanzibar imepiga hatua kubwa za maendeleo katika sekta mbali mbali lakini ni jambo lisiloweza kupingika kwamba kama tutaendeleza umoja na mshikamano tunaouonesha hivi sasa na kufikia hatua ya kufanya kazi pamoja basi kuna faida na fursa nyingi na kubwa sana zinazoweza kutumiwa vyema kwa ajili ya kuiendeleza mbele zaidi nchi yetu na watu wake. Miongoni mwa faida za wazi za Maridhiano ni pamoja na:

1. Kisiasa: Kuondosha siasa za utengano, chuki, ubaguzi, uhasama, ugomvi na visasi miongoni mwa wananchi wetu na kuleta siasa za umoja, maelewano na mashirikiano.

2. Kiusalama: Kuondoa khofu na wasiwasi kwa kufuta viashiria vinavyoweza kuwa chanzo cha fujo na ghasia na ambavyo vingeweza kutumiwa hata na maadui wa Tanzania kuhatarisha usalama wetu na badala yake kuleta hali ya amani na usalama ambayo inavifanya hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya kazi zao katika hali ya utulivu na ushirikiano na wananchi wote.

3. Kiuchumi: Kuondoa hali iliyokuwepo ya sehemu ya wananchi kujiona hawashirikishwi au hawapaswi kushiriki katika harakati za ujenzi wa nchi na kuwaleta pamoja wananchi wote ili kwa pamoja tushiriki katika ujenzi wa Zanzibar mpya.

4. Kijamii: Kuondoa hali ya utengano na kutoaminiana miongoni mwa wafuasi wa vyama tofauti vya siasa na kuwafanya wapendane na washirikiane katika shughuli zote za kijamii wakijua kuwa wote ni wananchi wa nchi moja.

Tukizitumia vyema faida hizo zilizoletwa na maridhiano, tutaweza pia kuzitumia vizuri fursa zilizopo mbele yetu ili kuyabadili maisha ya watu wetu. Binafsi naamini kuwa sasa ile ndoto yetu ya muda mrefu ya kuifanya Zanzibar kuwa ni Hong Kong ya Afrika Mashariki itaweza kutimia ndani ya muda mfupi kabisa. Naamini Wazanzibari wote sasa watakunjua nyoyo zao na kila mmoja atapigana kikumbo na mwenzake katika kuona anatoa mchango mkubwa zaidi wa kuikwamua Zanzibar katika umasikini ambao hauna sababu ya kuwepo. Ubunifu na ari ya kutenda ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Mzanzibari.

Zanzibar ina utajiri mkubwa wa watu wake wenye vipaji na nafasi kubwa kubwa katika kila pembe ya dunia. Hawa tukiwatumia vyema na kuwapa fursa wanaweza kutoa mchango mkubwa kwa kushirikiana na Wazanzibari wenzao walio ndani kuijenga upya Zanzibar .

Tukijituma na kujitutumua itakiwavyo, Zanzibar inaweza kurudia nafasi yake ya kuwa kituo kikuu cha biashara na harakati za uchumi katika Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi. Zanzibar ina nafasi ya kuwa kituo kikuu cha huduma katika eneo hili. Tunataka kuona Uwanja wa Ndege na Bandari ya Zanzibar zinakuwa tena mlango wa kuingilia na kutokea Afrika Mashariki. Tunataka na tunapaswa kuona ndege za mashirika ya kimataifa zikitua na kuruka kutokea Zanzibar na pia meli zikitia nanga na kung’oa kupitia Zanzibar . Tunaweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza Zanzibar kwa kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wetu na pia kusaidia kuifanya Zanzibar izalishe na kuuza nje bidhaa. Tukizitumia vyema fursa zilizopo Zanzibar itakuwa johari na siyo tena jeraha katika Afrika. Vijana wetu wasio na ajira watapata ajira zenye kipato cha kuwatosha wao na familia zao. Mababu zetu waliweza huko nyuma na sisi tunaweza tena ikiwa tutaikumbatia fursa ya maridhiano tuliyo nayo. Tusiruhusu kidudu mtu yeyote akaingia kati kuturudisha kule tulikotoka.


MARIDHIANO NA CHANGAMOTO ZAKE

Wakati tukizungumzia faida na fursa hizo, tuna pia changamoto kadhaa zinazoyakabili maridhiano haya. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na:

1. Matumaini makubwa yaliyojengwa na Wazanzibari bila ya kujali vyama vyao wakiamini kwamba hatua ya viongozi wawili wakuu wa kisiasa kukutana na kukubaliana kuzika tofauti zao itapelekea mabadiliko makubwa katika maisha yao na ujenzi wa mustakbali mpya wa nchi yao .

2. Viongozi wabinafsi kutoka pande zote mbili wanaojali maslahi yao zaidi kuliko maslahi ya nchi na watu wake ambao wameanza kufanya fitina zenye lengo la kuyavuruga mafanikio yaliyopatikana.

3. Muda mfupi uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao ambapo Maridhiano yanapaswa yawe yamejengewa msingi wa kuhakikisha kuwa yanaimarika na kuendelezwa..

Binafsi nimekuwa nikitafakari sana changamoto hizi na naamini tunapaswa kuzitafakari na kuzijadili kwa lengo la kuona tunazikabili vipi. Ni maoni yangu kuwa tukifanya haraka ya kukimbilia uchaguzi ambao nilishaeleza hapo awali kwamba umekuwa ndiyo chanzo cha kuvurugika kwa umoja wetu, kuna hatari ya kuyapoteza yote niliyoyaeleza.. Hatuwezi kukwepa uchaguzi maana ndiyo njia ya kidemokrasia ya kuwapata viongozi wetu lakini tumeshafanya chaguzi saba za vyama vingi Zanzibar , nne kabla ya Mapinduzi na tatu tokea 1992, na zote zimeshindwa kutupa umoja. Kwa Zanzibar na katika kipindi hiki, maridhiano ni muhimu zaidi kuliko uchaguzi. Tutapaswa kwenda katika uchaguzi lakini naamini tutakuwa na uchaguzi mzuri zaidi baada ya kufanikiwa kujenga msingi madhubuti wa maridhiano.

Hatuwezi kukwepa ukweli kwamba wapo watu wanaokodolea macho fursa ya kutaka kuchukua madaraka ya juu ya Zanzibar , yaani nafasi ya Urais na ambao hawayapendi maridhiano. Miongoni mwao wako wanaotumia vyombo vya habari kukuza habari za kuleta chokochoko na kuzibana taarifa zenye mtazamo wa umoja. Wako pia waliotuma ujumbe kwenda Tanzania Bara kueneza uzushi kwamba lengo la maridhiano haya ni kuvunja Muungano. Watu wa aina hii hawawezi kuisaidia Zanzibar na kwa hakika ni maadui wa umoja wa Wazanzibari.

Kwa msingi huo basi, na baada ya kutafakari, mimi binafsi naungana na wale wanaotoa wito wa kuchukuliwa hatua ya kusogeza mbele kidogo uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mwaka huu kwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja au miaka miwili ili kutoa nafasi kwa Rais Amani Karume kuchukua hatua zaidi za kukamilisha kazi njema aliyoianza. Naelewa mwenyewe juzi katika hotuba yake ya kilele cha sherehe za Mapinduzi amesema kwamba anakamilisha kipindi chake na Katiba ya Zanzibar hairuhusu kipindi cha tatu. Nakubaliana naye na sipendekezi kuondolewa kwa ukomo wa vipindi viwili kwa mtu anayeshikilia madaraka ya Urais wa Zanzibar . Ila namuomba sana akubaliane na matakwa ya Wazanzibari walio wengi kama yalivyokwisha oneshwa kupitia taarifa na kauli mbali mbali kwamba kipindi chake cha pili tukiongeze muda kidogo ili tusiipoteze fursa ya kihistoria ambayo ameianzisha yeye.

Natoa wito kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa pande zote mbili, Serikali na Upinzani, kulitafakari hili na kutupa Wazanzibari kile tunachokitaka. Kwa upande mwengine, nawaomba Wazanzibari tuungane pamoja kumtaka Rais Amani Karume aweke upande dhamira yake ambayo najua anaiamini sana ya kuondoka madarakani mwaka huu na badala yake akubaliane nasi juu ya haja ya kuendelea kuubeba mzigo huu tunaotaka kumtwisha na atuvushe pale ambapo waliomtangulia walishindwa kutuvusha.

Ahsanteni sana.


_______________________________
Mada hii iliwasilishwa katika Kongamano la Kitaifa kujadili Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar tarehe 14 Januari, 2010 katika Ukumbi wa Salama wa Hoteli ya Bwawani, Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF).



Updates: # 1

MAJIBU KWA HOTUBA YA MAALIM SEIF SHARRIF
Gazeti la Raia Mwema na Lula Wa Nzela

LIMEFANYIKA jaribio dhaifu la hadaa ya kisiasa; jaribio ambalo maelfu ya Wazanzibari wameliamini na kulikubali na bila ya kujali itikadi zao na mirengo yao ya kisiasa, wamelikumbatia kama ukweli na kuandamana kuliunga mkono.

Jaribio hilo ni lile la kupotosha historia ya Zanzibar ili kujipa alama bora za kisiasa. Jaribio hilo limefanywa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharrif Hamad katika hotuba yake ya kuelezea juu ya “maridhiano na mustakabali wa Zanzibar”.

hamad_1.jpg


Seif Sharrif Hamad

Kwa mtu yeyote aliyesoma hotuba hiyo ya Maalim Seif, ukweli mmoja unajionyesha wazi kama mwili wa mbuni aliyejificha kichwa chake mchangani, na kama mwangaza wa radi, hotuba hiyo imefunua ulaghai wa kisiasa ambao mtu makini anaweza kuuona toka mbali na kuukwepa.
Nasikitika wananchi wa Zanzibar katika kile kinachodhaniwa kuwa ni umoja wao, wamekumbatia historia hii mpya ya Zanzibar; historia ambayo kiukweli ni mpya!

Historia isiyo na doa ya Zanzibar

Kitu cha kwanza ambacho tunakiona katika historia hii mpya ya Zanzibar kwa mujibu wa Maalim Seif, ni historia isiyo na “doa” ya Zanzibar. Katika historia yake, Maalim Seif anaielezea Zanzibar katika mwanga wa uzuri wa paradiso. Anadai kuwa Zanzibar, licha ya udogo wake kama kisiwa, ilikuwa na umuhimu mkubwa katika eneo la Afrika ya Mashariki, Uarabuni, Bahari ya Hindi na Mashariki ya Mbali. Anadai kuwa umuhimu huo “ulitokana na maendeleo makubwa yaliyokuwa yamepigwa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za maisha.”

Katika ‘maendeleo haya’ utumwa hautajwi wala kuhusishwa! (nitaliangalia hili mbele zaidi kwa wakati huu yatosha kuliweka mawazoni kama utumwa ni sehemu ya maendeleo ambayo Maalim Seif anaisifia Zanzibar!).

Mojawapo ya vitu vingine vya kihistoria ambavyo Maalim Seif amevionyesha katika kutangaza utukufu wa Zanzibar ni madai kuwa “Zanzibar inaelezwa kutajwa kwa majina tofauti tangu miaka 500 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (Yesu Kristo). Uvumbuzi wa karibuni wa mapango ya watu wa kale katika ukanda wa Mashariki Kusini mwa kisiwa cha Unguja unaonyesha kuwepo kwa makazi ya watu tokea zama za mawe ziitwazo ‘Stone Age’.

Katika kitabu maarufu chenye kumbukumbu za wasafiri wa kale wa Ugiriki waliotembelea mwambao wa Afrika Mashariki kiitwacho Periplus of the Erythrean Sea, kilichoandikwa mwaka 100 A.D. (kabla ya Nabii Issa), Zanzibar imetajwa kwa jina la ‘Menouthias’ ikiwa tayari ni nchi yenye watu mchanganyiko tena walio na ustaarabu wakiwa wanavaa nguo za hariri.”

Sasa alivyozungumza kwa uhakika ni kana kwamba wasomi wote duniani wanatambua kuwa “menouthias” ndiyo Zanzibar! Bila ya shaka Wazanzibari waliomsikia na kumsoma hivyo walifurahia mioyoni mwao kuwa kweli Zanzibar inatajwa katika maandishi ya kale.

Sitoshangaa kama watu wa Bara ambao hawajui historia yao waliinamisha vichwa vyao kwa sababu hawajui kama eneo lao linatajwa mahali popote au historia yao ndiyo imeanza mwaka 1884 au wanafikiria Bagamoyo ndiyo sehemu ya kale zaidi!

Kama Maalim Seif angependa kuwaambia ukweli wa Zanzibar juu ya miji ya kale na jamii za kale zilizowahi kutajwa kwenye maandishi ya kale, angewaambia watu wake juu ya mji wa kale wa Rhapta! Najua wengine mnajiuliza “ze what?”!

Katika kitabu hicho hicho cha maelezo ya safari za majini za kale katika bahari ya Hindi, kunatajwa vile vile mji wa Rhapta ambao tunaambiwa ulikuwa ni mji pwani ya Azania umbali wa usafiri wa kama siku mbili toka visiwa vya Menouthias.

Mmoja wa wataalamu wetu wa mambo ya kale Prof. Felix Chami anaweza kulielezea hili kwa kina kuwa siyo Zanzibar peke yake ambayo ina historia ya kale na kuwa watu wake walikuwa wakiishi katika jamii na kufanya biashara vizuri tu.

Ujio wa utawala wa Sultani

Katika historia yake hii mpya ya Zanzibar, Maalim Seif anadai kuwa “Mwaka 1503 Wareno waliivamia Zanzibar kupitia Unguja Ukuu na wakaitawala kwa muda mrefu wakifanya vitimbi vya kila aina. Waomani, kwa maombi ya wenyeji, walikuja katika Dola ya Zinj na kupambana na Wareno na hatimaye wakafanikiwa kuwatimua.” Katika hili tunaona mambo mawili yanayotajwa kwanza ni uvamizi wa Wareno (ambao kwa yeyote aneyejua historia haukukoma kwa visiwa hivyo tu) na pili “maombi ya wenyeji kwa Waoman”.

Kwamba Wareno walikuwa na vitimbi ni maneno machache; kwani historia yao inajulikana hadi Mombasa na Lamu. Tunapoambiwa kuwa wenyeji waliomba Oman ije kuwasaidia kuwaondoa Wareno, hatuambiwi ni wenyeji gani hao? Lakini wakati huo huo ni lazima tukumbuke kuwa utumwa ulikuwepo!

Yawezekana wenyeji waliotaka Oman kuja kuwaondoa Wareno walikuwa ni watumwa? Je watumwa walifaidika vipi na ujio wa Wa-Oman?

Balozi za kigeni huko Zanzibar

Maalim Seif anatuelezea katika hii historia mpya ya Zanzibar kuwa “Katika kipindi hiki Zanzibar iliweza kujitambulisha na kutambuliwa kama Dola huru katika ulimwengu. Zanzibar ikawa kituo muhimu cha kisiasa, kiuchumi na kibiashara katika Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi.. Kutokana na umuhimu wake, madola makubwa yalifungua Ofisi za Kibalozi mjini Zanzibar : Marekani (1837), Uingereza (1841), Ufaransa (1844), na baada ya hapo Ureno, Utaliana, Ubelgiji na Ujarumani zikafuata.”

Mzanzibar ambaye hajui historia ya Zanzibar na mtu wa bara ambaye anayasoma maneno haya anaamini kabisa kuwa balozi hizo zilifunguliwa kwa sababu ya Zanzibar “kujitambulisha na kutambuliwa kama dola huru katika ulimwengu”.

Bahati mbaya ni kuwa kuna historia ambayo Maalim Seif hakutaka kuikiri hadharani inayohusiana na kufunguliwa kwa balozi hizo Zanzibar na siyo sehemu nyingine katika eneo letu hili. Naomba ruhusa nimkumbushe sehemu hii ya historia yetu.

Mwaka 1822 Sultan wa Oman, Sayyid Said Bin Sultan aliingia mkataba ujulikanao kama Mkataba wa Moresby. Mkataba huu, pamoja na mambo mengine, ulipiga marufuku uuzaji wa watumwa kwa nchi za Kikristu kutoka katika himaya yote ya Sultani huyo. Ni kutokana na mkataba huo na mingine iliyofuatia ndio nchi za Marekani, Uingereza , Ufaransa n.k zilipoamua kuanzisha ofisi zao za ubalozi huko ili kuhakikisha mojawapo ya mambo mengi kuwa Sultani wa Zanzibar anaheshimu makubaliano ya Moresby, Hamilton n.k

Ukiangalia tarehe ya kuanza kwa balozi hizo kama Maalim alivyoonyesha (1837) unaweza ukafikiria ni kwa bahati nzuri tu kuwa ndani ya miaka kama saba nchi mbalimbali za Kimagharibi zimefungua balozi zao huko?

Ikumbukwe kuwa mwaka 1832 (wanahistoria wengine wanaweka tarehe ya mbele kidogo) Sultani wa Oman alihamishia maskani yake kutoka Omani na kuwa Zanzibar makao makuu. Kutokana na ukaribu wake na nchi hizo za Magharibi Zanzibar hatimaye ilifanikiwa pole pole kukomesha utumwa na utumishi wa kulazimisha (servitude).

Omani, hata hivyo, ambayo tunaambiwa ndio walikuwa watu wema kwetu, waliendelea na hali hiyo kwa namna moja au nyingine hadi mwaka 1870 kufuatia mapinduzi yaliyomuingiza Sultan Qabus na Saudi Arabia yenyewe chini ya Mfalme Faysal ilifanya hivyo mwaka 1869!

Hii ni muhimu kuelewa kwa sababu ni sehemu ya Historia ya Zanzibar, na ni historia yetu vile vile. Hatuwezi kuikana, kujificha kwa haya au hata kuitaja kwa jina.

‘Uhuru’ wa Zanzibar ni uhuru?

Jambo jingine ambalo Maalim analielezea ni kuwa “Uingereza ilikabidhi uhuru kwa Zanzibar tarehe 10 Desemba 1963 chini ya Sultani na Serikali ya ZNP/ZPPP. ASP hawakuukubali uhuru huo na tarehe 12 Januari, 1964 ilifanya Mapinduzi na Zanzibar ikatangazwa kuwa Jamhuri.”

Wapo watu wanaoamini kabisa kuwa huu kweli ulikuwa ni “uhuru wa Zanzibar”. Ndio hawa ambao bado wanapata shida kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar na ulazima wa kwanini yalitokea. Unaweza kuliona hilo katika hotuba hiyo ya Maalim Seif.

Utaona mambo makubwa matatu ambayo ni sehemu ya historia ya Zanzibar hayatajwi kabisa na kama hilo hapo juu yanatajwa kama kwa kupita.

Kwanza ni suala la utumwa na pili ni utawala wa Sultani wa Zanzibar na kama wananchi waliokuwa watumwa au watu weusi walinufaika na utawala huo.

Ndugu zangu, tunapotaka kujenga Zanzibar mpya na Tanzania mpya tuipendayo, hatuna budi kuwa wakweli kwa historia yetu. Tusiikane au kuona ni vibaya kuikiri. Wamarekani walikuwa na utumwa, Wamarekani walipigana wenyewe kwa wenyewe na zaidi ya nusu milioni walikufa.

Wamarekani walikuwa na ubaguzi wa rangi licha ya Katiba yao kutangaza usawa wa binadamu wote na haki zao. Leo hii Wamarekani wameweza kumchagua mtu mweusi kuwa Rais wao miaka chini ya hamsini tu tangu vurumai za mwamko wa haki za watu weusi nchini humo!

Bila ya kura za watu weupe Obama asingeweza kuwa Rais wa Marekani! Watu weusi wa Marekani ni kama asilimia 12 tu ya Wamarekani wote! Kwa maneno mengine, watu weupe ambao wamekuwa wakiangaliwa vibaya na kubebeshwa lawama za utumwa na ubaguzi na watu weusi walikubali historia yao na kuikumbatia na kujitokeza kumchagua mtu mweusi.

Hii ni historia yetu!

Hii ina maana kwetu leo hii. Waarabu, Wahindi, Washirazi na watu weusi wa Zanzibar na Tanzania Bara, ni lazima watambue kuwa hata tukimbie vipi, hata tujifiche vipi na hata tukwepe vipi, historia yetu imefungamana milele. Hata kina Maalim wasipotaja utumwa wasidhanie kuwa basi utafutika katika historia!

Na pia ni lazima tutambue kuwa kama taifa hatuwezi kuwabebesha Waarabu na Waoman wa leo mzigo wa dhambi ya utumwa na kuwaona kuwa ni waonevu juu yetu.

Kama vile Marekani, natambua wapo watu ambao bado hawamuoni mtu mweusi kuwa ana haki sawa na kumheshimu. Wapo watu weupe Marekani ambao hadi leo hii hawamtambui Obama kama Rais wao! Sitoshangaa wapo kati yetu uzao wa Wa-Oman na Waarabu wengine ambao wanaona watu weusi bado ni duni!

Na katika upotofu Fulani, wapo watu weusi ambao wanaamini kabisa kuwa bila ya wao kukubaliwa na Waarabu hao au na Washirazi, basi siyo binadamu hasa. Na wengine wamefikia hata kujiita “Waarabu” ili waonekane kukubalika. Huu ni upumbavu.

Waarabu wa Tanzania ni wananchi wenzetu na wana haki zote kama Watanzania wengine. Hawana haki au utu zaidi kwa sababu ya Uarabu wao.

Watu wenye asili ya Omani ambao vizazi vyao vimegawanyika Zanzibar na Oman wasijione kuwa wao ndiyo Waarabu hasa kulinganisha na Waarabu waliochangia damu na Wamanyema na Wanyamwezi wa Bara!

Wahindi ambao hawajachangia damu yoyote na watu weusi na wana vizazi Tanzania na India wasijifikirie kuwa wao ni watu bora zaidi na kuwa watu weusi bado ni maboi wao!

Nayasema haya ili ijulikane kwamba Tanzania tunayoitaka ni Tanzania yetu sote - historia ya Zanzibar ni historia ya Tanzania. Huu upuuzi wa kutaka kufanya watu wa Bara ni duni kwa sababu hawana historia ya taa za barabarani na televisheni za rangi, ni lazima ukome hata ukitolewa na wanasiasa tunaowapenda.

Huu mtindo wa “Zanzibar ilikuwa pepo na mapinduzi yakaharibu”, ni mtindo tunaopaswa kuukataa kwa nguvu zetu zote!

Ndiyo maana ni muhimu kujua kama kina Maalim Seif wanatambua ulazima wa mapinduzi yale na kuyakubali si kwa ajili ya kupata pointi za kisiasa bali kifalsafa na kimaadili. Ni lazima tujue kama kina Seif wanaweza kusema kuwa waliona matatizo yoyote ya utawala wa Sultani huko Zanzibar au wao bado wanaamini kuwa Sultani alionewa tu.

Na ndiyo maana katika haya pia mimi ninaamini kabisa kuwa mojawapo ya mambo ya kupatana Zanzibar ni lazima suala la Sultani lizungumzwe siku moja na kuhitimishwa, kwa sababu tunajua hadi leo hii Sultani wa Zanzibar hajakikana kiti chake cha Usultani wa Zanzibar na watoto wao bado wanaendelea kujitambua kuwa ni wana wa Sultan (Prince na Princesses).

Wote hawa ndugu zangu ni sehemu ya historia yetu na wakati umefika tuache kujitenga kwa mambo ya kijinga tukifirikia kuwa tunachofanya ni hekima na busara na ni uzalendo. Zanzibar haiwezi kukaa katika kivuli cha Sultani anayesubiri siku moja arudi na kukalia kiti chake!

Wananchi wa Zanzibar wasikubali hadaa ya maneno ya kisiasa, wasikubali kuimbiwa zumari za uongo na wao wakacheza.

Zanzibar ina historia yake na historia hiyo ina mazuri na mabaya yake kama vile ilivyo historia ya Uingereza, Japani, na China!

Historia hiyo ya Zanzibar ni historia ya Azania! Ni historia ya Tanzania yetu leo hii. Katika hili hatuna sababu ya kuomba radhi na Wazanzibari wasifikirie kuwa tutawaonea wivu. Wao ni sehemu yetu, sehemu ya damu yetu; kwani hatuwezi kamwe kuandika historia ya Tanganyika au Mwambao wa Afrika ya Mashariki bila kuandika historia ya Zanzibar.

Wana CCM Zanzibar wameliabisha taifa

Kitendo cha uongozi wa CCM Zanzibar kukubali na kukumbatia uongo kwa kisingizio cha “Zanzibar moja” ni cha hatari kwa muafaka wa taifa; kwani kinalenga kudhoofisha muungano na Rais Kikwete na Watanzania wasipoangalia ni ujumbe mkubwa wa kisiasa ambao matokeo yake hata kichaa anaweza kuyatabiri.

Wana CCM wa Zanzibar na Watanzania wa Zanzibar watambue kuwa wao ni sehemu ya jamhuri yetu, historia yetu ni historia yao na historia yao ni yetu. Tofauti za kisiasa na kimtizamo ni tofauti zinazozungumzika (hata leo hii majimbo ya Marekani na hata Uingereza wanazungumzia tofauti zao za kisiasa na kiutawala)

Katika kutafuta sifa za kisiasa, Rais wa Zanzibar asilipeleke taifa kwenye uchaguzi mbaya kwa kukumbatia uongo.

Vinginevyo, Dk. Karume atajikuta anafifisha na kudunisha na kudharau damu ya wale waliokufa katika mapinduzi na kufanya mapinduzi yale kuwa hayana maana yoyote! Historia itamhukumu vibaya sana akiendelea na maamuzi anayofanya sasa.

Kina Maalim wasitugawe sasa kwa historia wakifikiri wanatutendea hisani. Na nimeudhika kuona wana CCM wameingia katika mtego huu huko Zanzibar kiasi cha kupepea uongo kwa kanga zao za kijani na njano!

Ninaona fahari kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Ninaona fahari ya kujua historia yetu kama taifa.

Naomba niishie hapa. Nitajibu hoja zake za kisiasa alizozitoa wiki ijayo, inshallah.

 
Maalim Seif said:
Waomani kwa maombi ya wenyeji walikuja katika Dola ya Zinj na kupambana na Wareno na hatimaye wakafanikiwa kuwatimua. Sayyid Said bin Sultan alifika Zanzibar mwaka 1828, na kutokana na kuvutiwa na mandhari yake mwaka 1832 akaifanya Zanzibar kuwa makao makuu ya utawala wake badala ya Muscat .

..naona Maalim Seif is in denial kuhusu biashara ya Watumwa iliyokuwa ikifanywa na watawala wa Kiarabu wa Zanzibar.
 
Zanzibar iliyokuwa British Protectorate toka mwaka 1890 ilikuwa ni koloni la Omani ndani ya himaya ya Waingereza kabla ya kilichoitwa uhuru wa mwaka 1963.

  • Je, Sultani wa Oman alikuwa na influence gani Zanzibar baada ya kuundwa kwa cheo cha Sultani wa Zanzibar mwaka 1957 ?
  • Je, yasingetokea mapinduzi ya mwaka 1964, mahusiano kati ya Zanzibar na Oman yangechukua sura gani chini ya Sultani Jamshid ibn Abdullah ?
  • Je, huo uhuru wa Zanzibar ungekuwa na maana gani kama Kiongozi Mkuu wa Zanzibar angeendela kuwa Sultani au mwakilishi wake ?
Naona kama vile Waingereza na Waoman wangekuwa tu kama vile wanapokezana vijiti - kaazi kweli kweli.
 
Inashangaza katika historia nzima "fupi" ya Zanzibar.. neno utumwa hata halikuingia mawazoni kwa maalim; anaamini kabisa watu weusi wote walioko Zanzibar walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha ya kheri visiwani humo na kuwa watu wote walioishi Zanzibar waliishi kama watu sawa na huru! This in history is known as revisionism!

In the compacted political history of hon Seif, slavery never happened and there is no evidence of its existence in the beautiful islands of Zanzibar!
 
..na katika watawala wa Zanzibar anaazia pale kwa Mamwinyi tu.

..ukichunguza vizuri kauli za Maalimu ni kwamba anashabikia sana zile tawala zilizoshamiri kutokana na biashara ya Watumwa.
 
Maalim Seif ameelezea vyema historia ya Zanzibar. Kuna watu wanauliza kuhusu biashara ya utumwa. Wakazi wa Afrika Mashariki alishiriki sana kuuza wenziwao waliowateka ktk vita vya kikabila kuwauza kwa wafanyabiashara ya utumwa toka Ulaya na Arabuni. Hivyo hakuna wa kulaumiwa maana wote walishiriki ktk kufanikisha biashara hii ya utumwa.

Ukiangalia barani ulaya hususan benki ya HSBC (Hong Kong Shangai Banking Corporation) mtaji wake ulitokana na biashara ya utumwa na kuuza opium China. Ulaya walivyoona wameshapata mitaji, wakaanza kuharamisha biashara ya utumwa na kusafisha hela chafu walizopatia mtaji kufanya biashara ya mabenki.

Tukirudi kwenye hili la kubadilisha au kupindisha katiba, inaonekana kuna baadhi ya watu wanataka kuhodhi maamuzi mazito kupitia kura za wabunge au wawakilishi. Ikiwa hoja ya maridhiano imezama vizuri ndani ya nyoyo za Wazanzibari basi yeyote atakaye mpokea Mh. Rais Karume ataendeleza hayo maridhiano bila wasiwasi wowote.

Pia ktk kipindi hiki cha kuendea uchaguzi oktoba 2010, CCM Zanzibar na CUF watakuwa wamerekebisha kasoro zote zilizozungumziwa ktk maridhiano na mazungumzo ya faragha kati ya Mh. Rais Karume na Maalim Seif wa CUF.

Pia nimependa imagination ya Maalim Seif kuifanya tena Zanzibar kuwa nchi ya asali, maziwa na tende kama Singapore au Macao (Macau).
 
Maalim Seif ameelezea vyema historia ya Zanzibar. Kuna watu wanauliza kuhusu biashara ya utumwa. Wakazi wa Afrika Mashariki alishiriki sana kuuza wenziwao waliowateka ktk vita vya kikabila kuwauza kwa wafanyabiashara ya utumwa toka Ulaya na Arabuni. Hivyo hakuna wa kulaumiwa maana wote walishiriki ktk kufanikisha biashara hii ya utumwa.

Ukiangalia barani ulaya hususan benki ya HSBC (Hong Kong Shangai Banking Corporation) mtaji wake ulitokana na biashara ya utumwa na kuuza opium China. Ulaya walivyoona wameshapata mitaji, wakaanza kuharamisha biashara ya utumwa na kusafisha hela chafu walizopatia mtaji kufanya biashara ya mabenki.

Tukirudi kwenye hili la kubadilisha au kupindisha katiba, inaonekana kuna baadhi ya watu wanataka kuhodhi maamuzi mazito kupitia kura za wabunge au wawakilishi. Ikiwa hoja ya maridhiano imezama vizuri ndani ya nyoyo za Wazanzibari basi yeyote atakaye mpokea Mh. Rais Karume ataendeleza hayo maridhiano bila wasiwasi wowote.

Pia ktk kipindi hiki cha kuendea uchaguzi oktoba 2010, CCM Zanzibar na CUF watakuwa wamerekebisha kasoro zote zilizozungumziwa ktk maridhiano na mazungumzo ya faragha kati ya Mh. Rais Karume na Maalim Seif wa CUF.

Pia nimependa imagination ya Maalim Seif kuifanya tena Zanzibar kuwa nchi ya asali, maziwa na tende kama Singapore au Macao (Macau).

kwa vile hakuna wa kulaumiwa hivyo historia haitajwi tena? fikra za namna hii ni fikra za denial; sasa wale walionunuliwa watumwa (acha waliouza au walionunua) wao hawana wa kumlaumu bali kushukuru?
 
Maalim Seif vipi tena?

Hizi sanamu si zipo Zenji?



Sanamu za wa Binadamu wakati wa biashara ya utumwa sanamu hizi zinapatikana Kisiwani Zanzibar.
 
Macho yangu yana makengeza(macho mkasi) nikijitahidi sana kuaangalia hiki kinachoitwa maridhiano hapa ya ccm na caf siyaoni kabisa. Ninachoona ni maridhiano ya Seif na Amani. Hatari inayokikabili chama cha caf ni kuondoka kwa Amani, kama jitihada haitafanyika kuweza kuweka hiki kinachoitwa maridhiano katika maandishi kupitia vikao au wawakilishi wa hivi vyama, kuna kila dalili za caf kuwa imeingizwa kingi. Hii itadhihirika mara tu baada ya uchaguzi mkuu ujao. ---YANGU MACHO!!---
 
Inashangaza katika historia nzima "fupi" ya Zanzibar.. neno utumwa hata halikuingia mawazoni kwa maalim; anaamini kabisa watu weusi wote walioko Zanzibar walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha ya kheri visiwani humo na kuwa watu wote walioishi Zanzibar waliishi kama watu sawa na huru! This in history is known as revisionism!

In the compacted political history of hon Seif, slavery never happened and there is no evidence of its existence in the beautiful islands of Zanzibar!

Maana ya historia fupi (ni siyo comprehensive)...unataja yaliyo muhimu kwa dhamira yako ...unashindwa kufahamu hilo

Utumwa siyo muhimu kama utumwa wa kifikra uliofuata baada ya mapinduzi na uonevu uliombatana na mapinduzi

Bravo seif kwa kuwaunganisha wazen..hawa ndio vidudu mtu wasiotamani maelewano kwenye taifa lenu..angalia kalamu zao na vinywa vyao! hatari kama moto

Msiwasikilize (maana hawatachoka kuwagawa) kazeni kamba ya umoja wa ki-zanzibar hata muwe wamoja na mjitoe katika uonevu na kuwa mfano wa taifa lenye kusimamia ustaarabu maziwa makuu.
 
Ingekuwa bora Seif na Amani waweke bayana kile walichokubaliana badala ya maelezo ya juu juu wanayoyatoa kwani wananchi wengi hatujui kile walichokubaliana. Hii taarifa imejaa porojo. Historia ya Unguka na Pemba tunaifahamu...Maalim twambie mlichokubaliana na rafikiyo Amani na si kuanza longolongo. Hii biashara ya kutaka eti Amani aongezewe sijui miaka miwili kukamilisha kazi aliyoianza haina mantiki. Katiba haisemi hivyo na kubadili katiba si suala la kutoa tamko tu.

Kama 'maridhiano' ni kati ya CUF na CCM (na si kati ya Seif na Amani) basi hata atakayechaguliwa kushika wadhifa wa urais wa Zanzibar atakuwa na jukumu la kutekeleza makubaliano hayo. Kitendo cha Seif kuwa na wasiwasi wa kutotekelezwa kwa 'maridhiano' baada ya Amani kuondoka madarakani kinaweza kutafsiriwa kuwa ni urojo wa 'maridhiano' hayo.

Undumilakuwili wa Seif na Ibrahim utadhihirika wakati na baada ya uchaguzi kwani CCM itaendelea kucheza rafu kwa kutumia migongo yao nao wataendelea kulia kilio cha mbwa mdomo juu.....kama huamini subiri na utanambia!
 
Kwa muda nilikuwa natafuta chanzo cha kugawika kwa jamii ya kizanzibari, kwa hiyo angalau nimesoma kitu ambacho ni general case kwa migogoro yote ya Afrika imetokana na sera za kikoloni za kugawanya watu.

Hii ni case sawa na Hutus na Tutsis na mifano mengineyo iliyo na mizizi ya kikoloni.

Aidha kwa Zanzibar ni rahisi sana kurekebisha hili, na tungeliomba Watanganyika mkajiengua na kukaa kando na kutupa muda tukadili na masuala yetu bila ya chokochoko zozote.

Nukuu:
**Ni hisia yangu kuwa Tanganyika haipendi kuona maendeleo yoyote ndani ya visiwa hivyo.Naweza kuwa totally wrong, lakini sioni haja ya mtu ambae si mzanzibari kusimama mstari wa mbele na kuvuruga jitihada hizi za Seif na Karume.
**Nashauri na naunga mkono uchaguzi upelekwe mbele, na Mh.Karume apewe muda wa ziaida kama alivyopendekeza Maalim Seif.Ndani ya muda huo kufanyike heavy updates za katiba kuruhusu ushirikishwaji wa vyama vya kisiasa na uundaji tume huria ya uchaguzi.
**Pengine na sheria ziongezwe ukali kwa wabadhirifu au wachafuaji wa uchaguzi Zanzibar.
 
Kwa muda nilikuwa natafuta chanzo cha kugawika kwa jamii ya kizanzibari, kwa hiyo angalau nimesoma kitu ambacho ni general case kwa migogoro yote ya Afrika imetokana na sera za kikoloni za kugawanya watu.

Hii ni case sawa na Hutus na Tutsis na mifano mengineyo iliyo na mizizi ya kikoloni.

Aidha kwa Zanzibar ni rahisi sana kurekebisha hili, na tungeliomba Watanganyika mkajiengua na kukaa kando na kutupa muda tukadili na masuala yetu bila ya chokochoko zozote.

Nukuu:
**Ni hisia yangu kuwa Tanganyika haipendi kuona maendeleo yoyote ndani ya visiwa hivyo.Naweza kuwa totally wrong, lakini sioni haja ya mtu ambae si mzanzibari kusimama mstari wa mbele na kuvuruga jitihada hizi za Seif na Karume.
**Nashauri na naunga mkono uchaguzi upelekwe mbele, na Mh.Karume apewe muda wa ziaida kama alivyopendekeza Maalim Seif.Ndani ya muda huo kufanyike heavy updates za katiba kuruhusu ushirikishwaji wa vyama vya kisiasa na uundaji tume huria ya uchaguzi.
**Pengine na sheria ziongezwe ukali kwa wabadhirifu au wachafuaji wa uchaguzi Zanzibar.

Japo nakubaliana na wewe kwenye vipengele vingi lakini uongeze kuwa wazanzibar wenye kutaka madaraka kwa kutumia system iliyopo i.e. Dodoma kuamua rais wa Zenj ni kikwazo kwa maelewano ya wazanzibar

1. Wazenj wenye kutaka madaraka wanashikiana na wabara kwa kutumia system mbovu kujustify thier politic desire and ends..hilo mliangalie kwa uzuri zaidi
2. Wa Tanganyika wanaopenda mgawanyike hawafaidi na chochote isipokuwa tu kuwafaidisha marafiki zao wazenj wanaopenda madaraka kwa kutoa habari za uwongo kujustify their desire and political ends
3. Mimi naenda zanzibar mara kwa mara ila ikifika karibu na uchaguzi sitii mguu kwa hofu ya kuonekana mamluki...napendekeza wazanzibar waamue watakayo bila tone la influence kutoka Bara...peace.
 
CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimependekeza uchaguzi mkuu wa mwaka huu uahirishwe visiwani hapa ili Rais Amani Abeid Karume aongoze kwa miaka miwili zaidi.

Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ikiwa ni siku tatu tangu Rais Karume kutangaza kutokuwa na nia ya kubadilisha katiba na kuongeza kipindi kingine cha uongozi.

Akiwasilisha mada kuhusu mustakabali wa Zanzibar na maridhiano, Maalim Seif alisema Rais Karume anapaswa kubaki madarakani kwa muda huo, ili akamilishe kazi ya kumaliza tofauti za kisiasa aliyoanza kuifanya.

“Baada ya kutafakari, mimi binafsi naungana na wale wanaotoa wito wa kuchukuliwa hatua ya kusogezwa mbele kidogo uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka huu. Aongezewe kipindi cha kati ya mwaka mmoja au miaka miwili, ili kutoa nafasi kwa Rais Karume ya kukamilisha kazi njema aliyoianza,” alisema Maalim Seif.

Katika kongamano hilo, Maalim Seif alisema Zanzibar haiwezi kukwepa kufanyika uchaguzi, lakini kabla ya uchaguzi lazima kujengwe misingi madhubuti ya maridhiano, ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki.

“Hatuwezi kukwepa uchaguzi maana ndiyo njia ya demokrasia ya kuwapata viongozi wetu, lakini tumeshafanya chaguzi saba za vyama vingi Zanzibar na zote zimeshindwa kuleta umoja wa Wazanzibari,” alisema.

Hata hivyo, alisema maridhiano yaliyofikiwa kati yake na Karume kuna baadhi ya watu wameyapokea kwa kinyongo kutokana na malengo yao ya kisiasa ya kurithi nafasi ya urais baada ya Rais Karume kumaliza muda wake.

“Hatuwezi kukwepa, ukweli ni kwamba wapo watu wanaokodolea macho fursa ya kutaka kuchukua madaraka ya juu ya Zanzibar ya nafasi ya urais, ambao wamekuwa hawayapendi maridhiano tuliyofikia,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, aliongeza kuwa watu hao wamekuwa wakieneza taarifa za uongo kwamba maridhiano waliyokubaliana kati yake na Rais Karume yamelenga kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Watu wa aina hii hawawezi kusaidia Zanzibar na kwa hakika ni maadui wa umoja wa Wazanzibari,” alisema Maalim Seif na kuwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa tayari kufanikisha azma ya mabadiliko ya katiba kumuwezesha Rais Karume kubakia madarakani.

Pamoja na Rais Karume kutoa msimamo wake kuwa anakamilisha kipindi chake cha uongozi na hana nia ya kuongeza kipindi kingine, Maalim Seif alimuomba akubaliane na matakwa ya wanaotaka aongeze muda wa kubakia madarakani.

Hata hivyo, katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wanachama wa CUF, Maalim Seif hakueleza idadi ya Wazanzibari wanaotaka katiba kufanyiwa mabadiliko ili Rais Karume aongezewe muda isipokuwa alisema milango ya neema kwa Zanzibar itafunguka na kuwa kituo cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.

“Natoa wito kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa pande zote mbili, serikali na upinzani, kulitafakari hili na kutupa Wazanzibari kile tunachotaka. Naomba Wazanzibari tuungane pamoja kumtaka Rais Amani aweke upande dhamira yake ya kutokuwa na nia ya kuongeza muda,” alisema Maalim Seif.

Hata hivyo, wajumbe katika mkutano huo walisema suala la kubadilisha Katiba ya Zanzibar na kumuwezesha Rais Karume kubakia madarakani bado lina mtihani mgumu kwa vile linahusu Katiba ya Muungano na ya chama tawala - CCM.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona, Mohammed Kassim Abdallah alisema mabadiliko ya katiba yafanyike haraka ili Rais Karume aendelee kubakia madarakani na uchaguzi wa mwaka huu uahirishwe.

Katika kongamano hilo mwanasheria Ali Omar Juma alisema kwamba suala la Zanzibar kubadilisha katiba kumuwezesha Rais Karume kubakia madarakani haliwezekani bila ya kupata baraka ya Serikali ya Muungano na chama chake.

Akichangia mada hiyo alisema Zanzibar haina mamalaka kamili kama nchi na ni tofauti na Rwanda au Burundi, hivyo si rahisi kubadilisha katiba bila ya kuhusisha Katiba ya Muungano na ya CCM, kwa vile Zanzibar imepoteza mamlaka yake baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima, January 15,2010
 
Well nilikuwa sijamaliza bado, kuna suala jengine ambalo watanganyika wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwanini mzanzibari hapendelei kupoteza utaifa wake na kujivunia utanzania.

Nafikiria Maalim Seif amejaribu sana kujibu suala hili, kwa kuonesha records muhimu ambazo Zanzibar iliweza kuziweka katika dunia kiasi ambacho unaweza kumwambia mtu mimi ni mzanzibari na akafahamu kama unatoka kwenye nchi iliyopata ustaarabu kwa miaka mingi sana.

Tanzania ambayo ni 90% Tanganyika, haina record yoyote ambayo mimi kama mzanzibari naweza kukaa mbele ya dunia na kujivunia.Labda ufisadi na umasikini au ufukara!Ni vipi nitaweza kujivunia utaifa huu, wakati taifa langu la Zanzibar lina pretty good records za kuheshimika kabisa.

Shukurani za dhati kwa Maalim Seif kwa kuweka mbele records hizo za Zanzibar, ambazo tunatarajia zitaweza kurudishwa.

Natanguliza samahani kwa wale nitakao rusha sparks humo :D
 
Katika kitabu maarufu chenye kumbukumbu za wasafiri wa kale wa Ugiriki waliotembelea mwambao wa Afrika Mashariki kiitwacho Periplus of the Erythrean Sea kilichoandikwa mwaka 100 A.D. (kabla ya Nabii Issa)

1. Tangu lini Anno Domini imekuwa KABLA ya kuzaliwa Kristu?

2. Hauwezi ukazungumzia historia ya Zanziba bila kuzungumzia utumwa. Hao mnaosema kuwa wenyeji walishiriki watuambie ni kabila gani walikuwa na soko la watumwa ambako binadamu walikuwa wakipigwa mnada kama mbuzi? Watuambie ni kabila gani lilikuwa likiwahasi wale waliowateka vitani? Watuambie ni kabila gani ambalo lili m-dehumanise binadamu mwenzao kama walivyofanya hawa waarabu na wazungu? Msitake kuandika historia upya kwa kutaka kujikomba kwa hao mnaoona wamewazidi. Angalau wazungu wameosha utu wa kujutia biashara hii haramu na dhalimu. Kwa mtu anayejiita mmoja wa viongozi wakuu wa kisiasa Zanziba kuinyamazia ni incomprehensible.

Amandla.........
 
3. Mimi naenda zanzibar mara kwa mara ila ikifika karibu na uchaguzi sitii mguu kwa hofu ya kuonekana mamluki...napendekeza wazanzibar waamue watakayo bila tone la influence kutoka Bara...peace.

Unataka kutuambia wanaokuona mamluki ni watu wa bara waishio Zanzibar au vibaraka wao? Na hao wanaotaka kuwatenga wanzanzibari wenye asili ya ungazija ni wabara vile vile?

Amandla.........
 
The first electric street lighting employed arc lamps, initially the 'Electric candle', 'Jablotchkoff candle' or 'Yablochkov candle' developed by the Russian Pavel Yablochkov in 1875. This was a carbon arc lamp employing alternating current, which ensured that both electrodes were consumed at equal rates. Yablochkov candles were first used to light the Grands Magasins du Louvre, Paris where 80 were deployed -- improvement which was one of the reasons why Paris earned its "City of Lights" nickname. Soon after, experimental arrays of arc lamps were used to light Holborn Viaduct and the Thames Embankment in London - the first electric street lighting in Britain. More than 4,000 were in use by 1881, though by then an improved differential arc lamp had been developed by Friederich von Hefner‑Alteneck of Siemens & Halske. The United States was swift in adopting arc lighting, and by 1890 over 130,000 were in operation in the US, commonly installed in exceptionally tall moonlight towers.
The first street in the UK to be lit by electric light was Mosley Street, in Newcastle-upon-Tyne. The street was lit by Joseph Swan's incandescent lamp in February, 1879.[3] The first in the United States, and second overall, was the Public Square road system in Cleveland, Ohio, on April 29, 1879.[4] Wabash, Indiana holds the title of being the third electrically-lit city in the world, which took place on February 2, 1880. Four 3,000 candlepower Brush arc lamps suspended over the courthouse rendered the town square "as light as midday."[5] Kimberley, South Africa, was the first city in Africa to have electric street lights - first lit on 1 September 1882. In Latin America, San Jose, Costa Rica was the first city, the system was launched on August 9, 1884, with 25 lamps powered by an hydroelectric plant [6]. Timişoara, in present-day Romania, was the first city in mainland Europe to have electric public lighting on the 12 of November 1884. 731 lamps were used. In 1888 Tamworth, New South Wales, Australia became the first location in the Southern Hemisphere to have electric street lighting, giving the city the title of "First City of Light".[7]
Nimeitoa hapa;[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Street_light[/ame]

Actually, the first electric light was the arc discovered by Humphrey Davy in 1800, with "invisible fluid" flowing through two sticks of wood charcoal. Pencils of hard carbon were later introduced to replace the charcoal. An arc lamp invented in 1847 by W.E. Staite was a great improvement over Davy's theory, and Charles F. Brush made other improvements so that by 1878 small Brush arc lights were sold to Wanamaker's big store in Philadelphia, as well as others.

The first electric lights installed for illuminating a public street were two thousand candle power Brush arc lamps set up on poles in the public square in Cleveland in 1879. A year later the Brush arcs were illuminating some of the streets of New York City and then spread to other cities.


kutoka hapa:http://genealogytrails.com/ill/adams/history/aqesl.htm

The spice trade in Zanzibar greatly increased the country's prosperity and the extravagance of its sultans, which can be noticed in the fine buildings and palaces which characterise the capitol Stone Town. In 1883, Sultan Barghash, who wanted to emulate the opulence of Indian palaces, ordered the building of Beit el-Ajaib, the House of Wonders, the first building in Zanzibar to feature electric lighting. Barghash also introduced other developments, such as the first clean water system, electric street lighting, roads and a police force.

Kutoka hapa:http://www.zanzibar-holiday.com/brief_history.html

Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha taa za umeme za barabarani na mitaani (zikiitwa taa za stimu) kabla ya miji ya London na New York ? Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake mwaka jana, Bwana Mark Green, wakati akitoa hotuba yake ya kuaga, alisema meli za Marekani zilikuwa zikitia nanga katika bandari ya Zanzibar kuja kununua mafuta ya nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia taa zao za barabarani wakati Zanzibar ikiwa inatumia umeme.
Hizo taa za stimu anazozingumzia Maalim ziliwekwa lini? Kama ni baada ya 1883, New York tayari walikuwa nazo tangu 1880.

Wawindaji wakubwa wa nyangumi kihistoria walikuwa watu wa Norway, Iceland n.k. Wamerekani wawaache wote hao waje kununua mafuta ya nyangumi Zanziba kuwashia taa za mitaani kwao? Zanziba ambao hawakuwa na historia ya kuwinda nyangumi!


Ilifikia wakati ambapo Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar , Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, alitangaza hadharani kwamba hakukuwa na nchi yoyote iliyokuwa ikiidai Zanzibar bali Zanzibar ndiyo iliyokuwa ikizidai baadhi ya nchi malimbikizo ya madeni yanayotokana na uuzaji wa karafuu zake
Nchi gani hizo ambazo Zanziba ilikuwa ikizidai na ni kiasi gani ilikuwa ikidai? Zanziba ingedaiwaje wakati uwezo wa kukopa kama nchi kutoka nchi nyingine hakikuwa nao? Kwani leo wanadaiwa kiasi gani na NCHI ipi ya kigeni?

Amandla........
 
Nina mashaka na maridhiano haya;

Karume uchaguzi wa 1995 aliuona na malalamiko ya CUF aliyajua

Karume uchaguzi wa 2000 aliuona na malalamiko ya CUF na machafuko mbalimbali aliyaona na mengine yawezekana alishiriki kuyaunda.

Karume huyohuyo alishiriki kikamilifi katika uchaguzi wa 2005 na kushinda kwa hila, kama CUF walivyokuwa wakilalamika.

Muda wote huo hakuona umuhimu wa kufanya maridhiano hadi sasa anapomaliza muhula wake!
Angekuwa muungwana na makini, angeingia madarakani mwaka 2000 akiwa na dhamira ya kumaliza matatizo hayo, au basi baada ya kuwa madarakani mwa miaka 5 ya mwanzo, angeanza miaka yake 5 ya mwisho na dhamira hiyo.

Kuna msemo "UNAVUTA SHUKA WAKATI KUMESHAKUCHA"

Wanyambo husema "weijuka kulega enjura necha"

Nahisi kunaweza kuwapo na ajenda ya siri; anyway - all the best
 
Mabadiliko ya kifikra ndio kitu cha msingi na hili linaonekana wazi kwa Maalim na hata kwa Karume. Pamoja na mapungufu kadhaa katika hili la Maaalim Seif na Karume, naamini ni mwanzo mzuri na kwa hakika tunapaswa kuwaunga mkono.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom