WAKATI vyama vya CCM na CUF vikijiandaa kuteua wajumbe wa kuunda kamati maalumu ya kuangalia mfumo wa kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, vyama ‘vidogo' vya siasa kisiwani hapa vimetishia kwenda mahakamani kupinga hatua hiyo.
Katibu Mkuu wa chama cha Tadea, Juma Ali Khatib alisema "nchi hii si ya CCM na CUF, tunatakiwa kujumuishwa kwenye mchakato huo na pia kupewa vyeo kwenye serikali hiyo.
Mabadiliko yoyote katika Katiba lazima yaangalie uwepo wetu." Khatib alisema vyama hivyo vya siasa vitakutana wiki hii kupanga taratibu za kupata msaada wa kimahakama katika kuhakikisha vyama vingine vya siasa vinapata nafasi kwenye serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa na kuongeza "serikali hiyo pia inatakiwa ijumuishe hata vyama vya kiraia kama walemavu".
Hata hivyo, Rashid Ahmed kutoka NLD ameungana na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama Cha Mapinduzi na Chama cha Wananchi wanaotaka kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuunganisha Wazanzibari.
Mwenyekiti wa Chama cha Muungano wa Wakulima Tanzania (AFP), Said Soud alisema "tumeshangazwa na CUF, kunapokuwa na matatizo tunakuwa pamoja, lakini kunapotokea fursa wanatutenga, hii haikubaliki lazima wote tuwepo kwenye serikali hiyo ya mseto." Vyama vingine vilivyo kwenye kundi hilo la vyama vidogo 16 vya siasa kisiwani hapa vinavyotaka kujumuishwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni pamoja na NCCR Mageuzi, UPDP na Chadema.
Asilimia kubwa ya Wazanzibari wameunga mkono hatua ya wawakilishi kutaka kuanzishwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya Uchaguzi Mkuu ujao. Ijumaa iliyopita, Baraza la Wawakilishi lilikubaliana kuunda kamati ya watu sita itakayofanya kazi na serikali katika kupanga namna ya kufanyika kura ya maoni ikiwa ni hatua ya kuwa na Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa.
Wawakilishi hao wamependekeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuendesha kura ya maoni na ikiwa matokeo yataonesha wananchi wanataka serikali hiyo ya umoja wa kitaifa, hatua itakayofuata ni kufanya mabadiliko ya Katiba kuruhusu kuwepo kwa serikali hiyo.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa ZEC, Salum Ali Said alisema Tume yake itaendesha kura hiyo ya maoni, lakini akasema kuwa kupatikane fedha za kutosha kwa ajili ya kufanyika kampeni ili watu waelewe kabla ya maoni hayo kukusanywa.
Ikiwa tutataarifiwa kuandaa kuchukua maoni ya wananchi, tutahitaji si chini ya bilioni mbili kwa ajili ya shughuli hiyo," alisema Said.
Source Habari Leo
Ijapokuwa mie naisupport hii hoja ya serikali ya mseto ila hawa akina soud na Juma khatibu haiwaitakii mema zanzibar.
Kabla hata serikali ya mseto haijaanza wanaanza lawama watu wengine sijui vipi kwani wao wakifanya jitihada wakapata kwanza hao wawakilishi ndipo wakaja katika uwakilishi katika serikali hawaoni wangelifanya la maana. Mtu unalilia representatio serikalini huna hata mwakilishi mmoja bungeni.
Either jamaa ni mamluki au basi tu wanataka madaraka wasiyoyatolea jasho