HOTUBA ya Seif Sharrif na Majibu yake kuhusu Maridhiano Zanzibar!

Ingekuwa bora Seif na Amani waweke bayana kile walichokubaliana badala ya maelezo ya juu juu wanayoyatoa kwani wananchi wengi hatujui kile walichokubaliana. Hii taarifa imejaa porojo. Historia ya Unguka na Pemba tunaifahamu...Maalim twambie mlichokubaliana na rafikiyo Amani na si kuanza longolongo. Hii biashara ya kutaka eti Amani aongezewe sijui miaka miwili kukamilisha kazi aliyoianza haina mantiki. Katiba haisemi hivyo na kubadili katiba si suala la kutoa tamko tu.

Kama 'maridhiano' ni kati ya CUF na CCM (na si kati ya Seif na Amani) basi hata atakayechaguliwa kushika wadhifa wa urais wa Zanzibar atakuwa na jukumu la kutekeleza makubaliano hayo. Kitendo cha Seif kuwa na wasiwasi wa kutotekelezwa kwa 'maridhiano' baada ya Amani kuondoka madarakani kinaweza kutafsiriwa kuwa ni urojo wa 'maridhiano' hayo.

Undumilakuwili wa Seif na Ibrahim utadhihirika wakati na baada ya uchaguzi kwani CCM itaendelea kucheza rafu kwa kutumia migongo yao nao wataendelea kulia kilio cha mbwa mdomo juu.....kama huamini subiri na utanambia!
hongera sana ustaz umenena yale yaliyo moyoni kwangu ndoto yako ndio ndoto yangu, hawa cuf wanachezewa makidaMAKIDA NA CCM HATA SIKU MOJA HAWATAKUBALI KUFANYA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI HUKO ZENJ WANAJUA WAKIKUBALI MAMBO YAFANYWE KIDEMOKRASI YA KWWELI WATASHINDWA VIBAYA SANA WATAPOTEZA MADARAKA YAO,NA WANAJUA FIKA WAKIONDOSHWA MADARAKANI HAWATARUDI TENA MPK KIAMA WANANCHI WAMECHOKA KUFA NA NJAA ,NAHAWA KINA SEIF WANALIJUA HILO ILA WANASIASA ASILIMIA KUBWA NI WANAFIKI SEIF AMEDANGANYWA ANAWASALITI WATUWAKE NA WANANCHI WOTE WALIOMUONA KAMA MKOMBOZI WAO KUMBE NDUMILA KUWILI,CCM HAWAAMINIKI HATA KIDOGO,FUNIKA KOMBE MWANAHARAM APITE,WATAJUTA MA CUF PANAPO UHAI MUNGU ATUWEKE AMIN IKIFIKA NOVEMBA MWAKA HUU MTAUONA USALITI WA CCM NA HAPO NDIO ITAKUA MWISHO WA SEIF NA CUF YAKE WATAKAPOPIGWA GOLI LA KISIGINO KAMA CHAGUZI ZOTE ZILIZOPITA,HAPO NDIPO SEIF ATAKAPOPIGWA MAWE MTENDENI NA KILA KONA YA UNGUJA NA PEMBA,KAMA HAMUAMINI TUOMBE UHAI KWA MAULANA HAPO BAADA YA UCHAGUZI MTAYAKUMBUKA MANENO YANGU.
 
Baada ya mapinduzi ya mwaka 1964, Nyerere ndiye aliyempa hifadhi Sultani wa Zanzibar. Baada ya kuuawa kwa Karume, Nyerere ndiye aliyewahifadhi wakina Babu wakati wakina Ussi, Hanga wananyongwa Zanzibar.

Wakati wa utawala wa kigandamizi wa Karume I, ( Zanzibar walikuwa wakipigwa king'ora jioni wasimame, hakukuwa na uhuru wa kuvaa n.k.) wazanzibari wengi walihamia bara ambako waliishi bila kubughudhiwa au kubaguliwa. Wakati kila siku tunasikia kilio cha wapemba kubaguliwa Zanzibar, hatukisikii kutoka kwa wazanzibari waishio bara. Wazanzibari wamepewa uwaziri hata katika wizara zisizo za muungano, wamepewa uongozi wa taasisi kubwa na nyeti nchini, wamefundisha chuo kikuu bila kujali kama ni wangazija au wazanzibari, wameuguzwa katika hospitali bara bila kubaguliwa, wamesoma katika shule za bara bila kubaliwa, wanaendesha teksi bila matatizo, wanafanya biashara bila matatizo n.k.

Halafu leo bila aibu kuna watu wanaweza kusimamama na kudai watu wa bara hawaitakii mema Zanzibar! Kama hatuwapendi wazanzibari si tungeanza kuwabana na kuwashughulikia wale kibao walioko bara? Watu wa bara wangependa amani na utulivu uwepo Zanzibar maana siasa za chuki zinazoendelea huko zinatuaibisha wote.

Amandla......
 
Baada ya mapinduzi ya mwaka 1964, Nyerere ndiye aliyempa hifadhi Sultani wa Zanzibar. Baada ya kuuawa kwa Karume, Nyere ndiye aliyewahifadhi wakina Babu wakati wakina Ussi, Hanga wananyongwa Zanzibar.

Wakati wa utawala wa kigandamizi wa Karume I, ( Zanzibar walikuwa wakipigwa king'ora jioni wasimame, hakukuwa na uhuru wa kuvaa n.k.) wazanzibari wengi walihamia bara ambako waliishi bila kubughudhiwa au kubaguliwa. Wakati kila siku tunasikia kilio cha wapemba kubaguliwa Zanzibar, hatukisikii kutoka kwa wazaznibari waishio bara. Wazanzibari wamepewa uwaziri hata katika wizara zisizo za muungano, wamepewa uongozi wa taasisi kubwa na nyeti nchini, wamefundisha chuo kikuu bila kujali kama ni wangazija au wazanzibari, wameuguzwa katika hospitali bara bila kubaguliwa, wamesoma katika shule za bara bila kubaliwa, wanaendesha teksi bila matatizo, wanafanya biashara bila matatizo n.k.

Halafu leo bila aibu kuna watu wanaweza kusimamama na kudai watu wa bara hawaitakii mema Zanzibar! Kama hatuwapendi wazaznibari si tungeanza kuwabana na kuwashughulikia wale kibao walioko bara? Watu wa bara wangependa amani na utulivu uwepo Zanzibar maana siasa za chuki zinazoendelea huko zinatuaibisha wote.

Amandla......

Kwanza huko kumsifia kwako Nyerere naona unazungumza uzushi, huyo Nyerere ndio mpangaji wa hayo mapinduzi ya Zanzibar.

Pili huo ubaguzi wa Zanzibar sio kama ndio kibali cha kupoteza taifa zima ati kwasababu kuna ubaguzi?

Tatu sio wazanzibari tuu ndio waliohamia bara, kuna wamasai na makabila mengine sana yako Zanzibar.Hii hoja haina mshiko ati kuwa ndio kielelezo kama vile munasaidia Zanzibar.Tanzania ambayo ni nchi masikini duniani, asilimia kubwa ni Tanganyika.Kwa hiyo unaweza kusema Tanganyika ni nchi masikini duniani, uwezo wa kujisaidia wenyewe hamunao.

Sasa suala la Zanzibar acheni wenyewe wazanzibari walitatue, dilini na huo ufisadi na umasikini hadi umalize na pengine inshallah mukisha tatua hayo ...na Zanzibar itakuwa ishafix matatizo yake.
 
Hapa inabidi umlaumu nyerere kwa muungano usioeleweka, kumbuka kwamba mzenji ana serikali mbili mikonono mwake (SMT na SMZ).

Nyinyi wabongo mna serikali moja tu (SMT), kwa muundo wa muungano huu alouweka nyerere ni kwamba mzenji akijitawala bara anatumia uhuru wake wa kikatiba kwamba yeye ni mtanzania na anakubalika katika katiba ya smt, tatizo linakuja kwamba mtanganyika akija zenji anajikuta anakamatwa na katiba ya SMZ na kubanwa.

Narejea tena, hili sio kosa letu wazenji ni kosa la nyerere na kujifanya kwake ujanja mwingi. Kama mnataka usawa huo mnaouzungumzia ili na sisi tukija bara tubanwe na katiba yenu ningewashauri mpiganie Tanzania iwe na muungano wa serikali tatu au uvunjwe, kuhusu serikali moja haimo kwenye ajenda yetu wazenji.
 
Kibunango, kwa vijana wa leo wanaposoma historia ya biashara ya utumwa wengi wao wanawaona weusi wa Marekani na Carribean kama ndio vielelezo vya biashara hiyo na kudhania kuwa Waarabu hawakuhusishwa sana na biashara hiyo kwani huko uarabuni hakuna weusi wengi!! Ukweli ni kwamba waarabu waliwasafirisha watumwa wengi sana kwenda uarabuni lakini wengi wao waliuawa na pia wanaume walikuwa wanahasiwa[ castrated]. Hivyo huwezi kuwaona weusi wengi arabuni waliotokana na uzao wa watumwa!!

Ukienda Basra, Iraq kuna wa-Iraq kibao(mamilioni) wenye asili ya Afrika Mashariki. Fuatili uchaguzi mwaka huu utaona kina 'Obama' wengi tu maeneo ya Basra wamechukua fomu kugombea nafasi za uongozi.

Kiswahili kilikuwa lugha ya kufundishia ngazi ya shule ya msingi hapo Basra mpaka mwaka 1970, ambapo serikali ya Iraq ikaona bora kuwaunganisha Wa-Iraq wote kwa kuliondoa somo kama somo la kufundishia.

Nini tunajifunza, kuwa kizazi kilichotokana na utumwa weusi wapo kibao mpaka leo kusini mwa Iran, sehemu za Basra Iraq, Yemeni, Omani k.n kwa kutoa mifano michache.

Hivyo utumwa ulishirikisha watu wote wa dunia, kuanzia maeneo ya maziwa makuu ya Afrika(yaani Wabara waliuza wenzao), waarabu, waingereza(Bofya Black people Museum Liverpool, HSBC bank n,k), wareno, wahispaniola n.k

Hivyo duniani yote iliona kipindi hicho biashara hiyo kuwa halali, mpaka wazungu walipofanya mapinduzi ya kiviwanda na kimabenki kwa mtaji wa hela chafu(money-laundrying) wa biashara ya utumwa na opium (madawa ya kulevya) wakaanza kampeni ya kupinga vita utumwa.

Kampeni hii iliongozwa na waingereza waliokuwa wa kwanza kufanya mapinduzi ya kiviwanda. Na wengine pia wakafuata kuharamisha utumwa kufuatana na kiwango chao cha maendeleo ya kisasa.

Hii leo mtumwa mpya ni mfanyakazi(employee) na mmiliki wa watumwa wa kileo ni (mwajiri a.k.a employer). Kwa Afrika employee anapewa mshahara mdogo kiasi hawezi kukidhi mahitaji yake muhimu ya familia yake. Pia huko ulaya employee anadanganya kwa kukidhi mahitaji yake kwa kutumia debit cards, credit cards, store cards, overdraft limits za mabenki kwa vile pia mshahara wake haumtoshi, ulaya na marekani mfanyakazi ni mtu aliyezungukwa na madeni chungu mbovu.

Hivyo suala hili la utumwa limevishwa kilemba cha ukoka oh huyu ni mfanyakazi au msaidizi wangu, mtoto wa kazi, shamba boy, house girl listi ni ndefu.
 
Kwanza huko kumsifia kwako Nyerere naona unazungumza uzushi, huyo Nyerere ndio mpangaji wa hayo mapinduzi ya Zanzibar.

Pili huo ubaguzi wa Zanzibar sio kama ndio kibali cha kupoteza taifa zima ati kwasababu kuna ubaguzi?

Tatu sio wazanzibari tuu ndio waliohamia bara, kuna wamasai na makabila mengine sana yako Zanzibar.Hii hoja haina mshiko ati kuwa ndio kielelezo kama vile munasaidia Zanzibar.Tanzania ambayo ni nchi masikini duniani, asilimia kubwa ni Tanganyika.Kwa hiyo unaweza kusema Tanganyika ni nchi masikini duniani, uwezo wa kujisaidia wenyewe hamunao.

Sasa suala la Zanzibar acheni wenyewe wazanzibari walitatue, dilini na huo ufisadi na umasikini hadi umalize na pengine inshallah mukisha tatua hayo ...na Zanzibar itakuwa ishafix matatizo yake.

Uwe unatumia kidogo akili alizokupa mwenyezi. Wamasai, wajaluo, na wengine kwanza hawakuhamia Tanganyika, Tanzania au German East Africa maana wakati huo hizo nchi hazikuwepo. Hauwezi kuwafananisha na wahamiaji wa sasa.Wazanzibari wengi (sio wote) waliondoka zanzibar kuhamia bara kwa sababu maisha chini ya Karume I yalikuwa ni magumu na ya kigandamizi. Hawa walipokewa na watu wa bara bila ubaguzi au kutengwa. Wenzako, pengine ni babu zako, hadi leo wanamshukuru Nyerere kwa hili.

Sitafuti shukurani za wazanzibari kama wewe bali napinga nyinyi kudai kuwa watu wa bara wanawaona kijicho na wangependa muendeleze tofauti zenu. Ukweli ni kuwa watu wa bara tunajua matatizo yeyote yatakayotokea Zanzibar atakayelipia ni bara!

Amandla........
 
kumradhi sana lakini hizi takwimu zako ni vichekesho sana! baada ya mapinduzi mtafaruku ulikuwa mkubwa sana znz na hiyo iliwasababishia baadhi ya wazanzibari kukimbia ili kunusuru maisha yao, kumbuka kwamba hii hali hutokezea popote duniani, (penye mauaji hapakosi wakimbizi), sasa sijui ulipenda raia wabaki tu na wauliwe?, ukitaka tuingie deep sana utagundua kwamba hata huyo nyerere ana mkono wake kwenye mapinduzi ya zenji hili halipingiki. sasa hii ni kusema kwamba nyerere alitafuna halafu akapuliza.

tukiongelea kesi ya uhamiaji, hata zenji kuna mitaa imejaa watanganyika na wala habughudhiwi mtu kwa asili yake. ningekuomba utembelee kijiji kimojja zenji kinaitwa "dole", kijiji hiki kizima kimetawaliwa na watu wenye asili ya morogoro na amini usiamini hakuna hata mmoja kati yao aliekuja kwa njia ya utumwa, walikaribishwa na wazanzibari na wapo mpaka leo na wengi wao wamejikita na maadili ya kizanzibari na ni wanakilimo wazuri wa ndizi.

Na msipotoshe maana halisi ya zanzibar. wazanzibari asilia wapo, acheni kudanganya watu kwamba asili ya wazanzibari ni watanganyika na mataifa mengine.
 
Sitafuti shukurani za wazanzibari kama wewe bali napinga nyinyi kudai kuwa watu wa bara wanawaona kijicho na wangependa muendeleze tofauti zenu. Ukweli ni kuwa watu wa bara tunajua matatizo yeyote yatakayotokea Zanzibar atakayelipia ni bara!

Amandla......

Sasa munachokiogopa ni nini kuwachia Zanzibar ikajichagulia na kufanya maamuzi inayotaka?

Hili la Tanganyika kusimama mstari wa mbele kupinga na kuionea kijicho Zenji ipo, na si leo tuu.Hii ipo tokea huko zama za Nyerere, huyu mzee wenu alikuwa hapati usingizi kwa kufuatilia na kupanga mbinu za kuzorotosha uchumi wa Zanzibar.

Na waliofuata baada yake wote aliwapika waendeleze sera hiyo ya kuhakikisha Zanzibar haiji juu.Na hichi ndio chanzo cha kuwa muko mstari wa mbele kudai maridhiano yawekwe wazi.

Sisi huku visiwani tunawaamini hao Karume na Seif, wala hatuna pressure...tunasubiri mchezo hadi mwisho tujue ngoma imekwendaje.Lakini hatuweki bayana, ule mkutano wa Nov 5 utabaki siri hadi finali.

Munataka tueke siri yaje yale ya Jumbe sio? :D
Hii maridhiano ni chenga ya kisigino, tutaendeleza hapo hapo mshikiamano tuu...ukitoka mshikamano ni mseto na ubwabwa, na wala hamupati kitu...ubwabwa ni wazenji pekee!
 
Ukweli ni kuwa watu wa bara tunajua matatizo yeyote yatakayotokea Zanzibar atakayelipia ni bara!

Amandla........
Kumbe Fundi ni mtu wa Bara!!! Ahsante sana kwa hisia zenu hizo. Sasa achaneni na hilo la historia tu-deal na yaliyopo na tugange yajayo. Mtafaruku upo Zenj. Miafaka na juhudi za CCM/CUF katika vikao vyao vya pamoja zimegonga ukuta. tatizo kubwa ni kuundwa kwa Serikali ya Mseto wakati huu ambapo kuna Serikali halali iliyoshinda katika uchaguzi wa 2005. Msingi mkubwa wa maridhiano ya Wazanzibari ni kuwa na Serikali ya pamoja (CUF/CCM) ambayo itasimamia na kufanikisha kutekelezwa kwa yale yatakayoleta maridhiano (ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi kwa salama na amani na kukubliana juu ya Kiongozi atakayepata ridhaa ya walio wengi kutokana na uchaguzi huo ).Serikali hiyo haipo na haiwezi kuwepo katika kipindi hiki kinachomalizika Oktoba 2010. Ni kwa namna gani, Fundi(Mtu wa Bara) na wenzio kama wewe walio Bara mnafikiri Wazanzibari wanahitaji kuitumia kutimiza dhamira zao na kujenga mshikamano na kuzika chuki na uhasama. Tupe mawazo ya kujenga.
 
kumradhi sana lakini hizi takwimu zako ni vichekesho sana! baada ya mapinduzi mtafaruku ulikuwa mkubwa sana znz na hiyo iliwasababishia baadhi ya wazanzibari kukimbia ili kunusuru maisha yao, kumbuka kwamba hii hali hutokezea popote duniani, (penye mauaji hapakosi wakimbizi), sasa sijui ulipenda raia wabaki tu na wauliwe?, ukitaka tuingie deep sana utagundua kwamba hata huyo nyerere ana mkono wake kwenye mapinduzi ya zenji hili halipingiki. sasa hii ni kusema kwamba nyerere alitafuna halafu akapuliza.
tukiongelea kesi ya uhamiaji, hata zenji kuna mitaa imejaa watanganyika na wala habughudhiwi mtu kwa asili yake. ningekuomba utembelee kijiji kimojja zenji kinaitwa "dole", kijiji hiki kizima kimetawaliwa na watu wenye asili ya morogoro na amini usiamini hakuna hata mmoja kati yao aliekuja kwa njia ya utumwa, walikaribishwa na wazanzibari na wapo mpaka leo na wengi wao wamejikita na maadili ya kizanzibari na ni wanakilimo wazuri wa ndizi.
Na msipotoshe maana halisi ya zanzibar. wazanzibari asilia wapo. acheni kudanganya watu kwamba asili ya wazanzibari ni watanganyika na mataifa mengine.

Takwimu zipi unazozipinga? Mbona hamna unapoziweka wazi? Au neno takwimu lina maana tofauti bara na unguja kama ilivyo nyanya? Nielewavyo mimi takwimu ni statistics.

Wengi waliokimbia Zanzibar baada ya mapinduzi hawakuishia Tanzania Bara bali waliendelea hadi uingereza na Oman. Walioishia Tanzania bara ni wale walioondoka wakati wa utawala wa Karume I. kwa mfano, wahindi wengi walihama kukimbia uwezekano wa mabinti zao kuolewa kwa nguvu, kitu ambacho kiliishapewa baraka na utawala wa wakati ule. Ni uongo kudai kuwa mauaji Zanzibar yalitokana na mapinduzi ya mwaka 1964 tu. Baada ya uchaguzi wa mwaka 1961 watu 68 waliuawa katika fujo zilizotokea. Napo mtamlaumu Nyerere? Hata baada ya mapinduzi ni Nyerere ndiye aliyeipa hifadhi meli ya Sultan baada ya kenya kumkatalia. Ni Nyerere huyo huyo ndiye alimzuia John Okello asirudi Zanzibar ambako pengine mauaji yangeendelea. Tofauti na mnavyotaka tuamini, aliotaka muungano zaidi alikuwa ni Karume maana alikuwa na wasiwasi wa waarabu kurudi na kumlipizia. Ndiyo maana hata aliposhauriwa ahusishe watu zaidi alikataa. Ukweli mwengine ni kuwa bila serikali ya JMT watawala wa Zanzibar wangetumia mkono mzito zaidi kuwashughulikia wapinzani ambao wao waliwaona kama vibaraka vya waarabu.

Mbona hili la wutumwa linawasumbua sana. Sijawahi kupinga kuwa kuna watanganyika (nyinyi kwa vile mnawapenda sana mnawaita machogo) wengi tu waliohamia kwa ridhaa yao. Wanyamwezi wengi tu wako huko mnakoita mashambani. Na sio wote walikuja kwa kuribishwa bali wengi walikuja kujitafutia riziki yao katika mashamba ya karafuu. Pamoja na haya haiwezekani kabisa kuwa katika wazanzibari weusi walioko huko sasa hivi hakuna waliotokana na utumwa. Na haiwezekani kabisa kuwa katika hao waarabu waliokuwepo hakuna ambao ndugu zao walihusika na biashara ya utumwa. Huku ni kujidanganya.

Nimefika Unguja na Pemba na ninajua kuwa bado tofauti za rangi zina nafasi kubwa katika jamii. Machungu yaliyotokana na mapinduzi si rahisi kuyasahau kirahisi.

Tatizo ninaloliona mimi ni kuwa manataka kukwepa historia na kulaumu wengine kwa mapungufu yenu. Bila kuangalia historia yenu, kukiri mlipokosea, kuomba msamaha mliowatendea uovu, hamtakuwa na amani ya kudumu. Na safari hii mtakapobebeana majambia hao mnaowaita machogo watawaangalia tu maana watakuwa wamejifunza kutokana na historia kuwa hamna shukrani. Nawahikishia mtakuja kumkumbuka na kumlilia Nyerere.

Amandla......
 
Sasa munachokiogopa ni nini kuwachia Zanzibar ikajichagulia na kufanya maamuzi inayotaka?

Hili la Tanganyika kusimama mstari wa mbele kupinga na kuionea kijicho Zenji ipo, na si leo tuu.Hii ipo tokea huko zama za Nyerere, huyu mzee wenu alikuwa hapati usingizi kwa kufuatilia na kupanga mbinu za kuzorotosha uchumi wa Zanzibar.

Na waliofuata baada yake wote aliwapika waendeleze sera hiyo ya kuhakikisha Zanzibar haiji juu.Na hichi ndio chanzo cha kuwa muko mstari wa mbele kudai maridhiano yawekwe wazi.

Sisi huku visiwani tunawaamini hao Karume na Seif, wala hatuna pressure...tunasubiri mchezo hadi mwisho tujue ngoma imekwendaje.Lakini hatuweki bayana, ule mkutano wa Nov 5 utabaki siri hadi finali.

Munataka tueke siri yaje yale ya Jumbe sio? :D
Hii maridhiano ni chenga ya kisigino, tutaendeleza hapo hapo mshikiamano tuu...ukitoka mshikamano ni mseto na ubwabwa, na wala hamupati kitu...ubwabwa ni wazenji pekee!

Ndiyo hiki kinachoniudhi. Victim mentality. Uchumi wa Zanzibar ulitegemea zaidi zao la karafuu baada ya biashara ya watumwa kupigwa marufuku. Sasa Nyerere alidumaza vipi zao hili? Ni yeye ndiye aliyewazuia kupalilia mashamba yenu? Ni yeye aliyewazuia kuhakikisha ubora wake ili liweze kushindana na karafuu kutoka Indonesia? Kilichodumaza hilo zao ni dhana kuwa kazi hiyo ni ya kitwana inayostahili kufanywa na machogo wakati waungwana wakinywa gahwa na kucheza dhumna. Sasa hivi utalii una nafasi kubwa katika uchumi wa Zanzibar. Lakini miaka yote hii mmeshindwa kuendeleza viwanja vyenu vya ndege na bandari zenu, vyote vikiwa chini ya uongozi wa SMZ! Lakinibadala ya kushikana mashati wenyewe kujua kulikoni mnabaki kulaumu uongozi wa bara! Badala ya kuendeleza na kupanga mikakati juu ya rasilmali kibao mlizonazo mnabaki kutoka mapovu kinywani kugombania mafuta ambayo hata kupatikana bado! Yote haya ni kutokana na tabia ya kupenda mteremko.

Mnachojidanganya ni kuwa watanganyika wanajali kinachoendelea Zanzibar. Ukiondoa viongozi wa chama tawala na wale waliokuwa katika Muungano, watu wa bara wengi wasingejali hata huo Muungano ungevunjika leo. Jiulize ni asilimia ngapi ya watu wa bara waliowahi kutembelea Zanzibar ndipo utajua umuhimu wa Zanzibar kwa watu wa bara. Mwanzo ilikuwa kisingizio pasipoti lakini leo watu wa bara wanaweza kuingia wanavyotaka. Wangapi wamefanya hivyo?

Wewe udhika lakini ukweli nishasema.Huwezi kuepuka kuwa hamujaweka mguu Zanzibar.

Nchi ili iendelee jambo la mwanzo ni uongozi, na Zanzibar hamuachi wananchi wakachagua viongozi wenye uwezo na wanaotakiwa.Sasa uongozi ukikosekana, na sababu ya kukosekana ni Bara.Unataka tuseme nini?

Wewe mstari wa mbele kudai pongezi, 1995 wazanzibari wakaona Salmin hafai kuwaongoza.Nyerere alifanya nini?Usiku wa manane yuko Zanzibar akitumia vyombo vyenu vya dola kuhakikisha demokrasia inapindwa.

Huo ni mfano mmoja tuu, mengine utakuwa unaijua na nakupa home work ufanye uchambuzi.

Sasa usitutupie lawama sisi, wakati kila uchaguzi ukikaribia manuari na majeshi yenu munayaleta visiwani Zanzibar kuhakikisha maamuzi ya wazanzibari hayafuatwi.

SASA HUKO UNAKUITA NINI?AU NIMEKOSEA NINI KUSEMA KAMA MUNAWEKA MGUU NA KUDUMAZA ZANZIBARI?
 
Acha uongo.
1. Mwaka 1995 Nyerere hakuwa Rais wa JMT. Rais wa JMT alikuwa mzanzibari mwenzemu na ni yeye ndiye aliyekuwa na amri juu ya vyombo vya dola na sio Nyerere.
2. Nyerere peke yake asingeweza kupindisha matokeo ya uchaguzi kama wazanzibari wote walikubaliana nayo. Kukubali kuwa aliweza kufanya hivyo ni kukubali udhaifu wenu na msivyoaminika. Mngekuwa watu wa msimamo, Nyerere asingefua dafu.
3. Manowari na majeshi ya JMT yana haki ya kuwa Zanzibar wakati wowote. Mbona bara yapo na watu wanapiga kura bila uoga? Toa ushahidi wa kuonyesha kuwa majeshi hayo yamewahi kutumika kupindisha uchaguzi. Ingekuwa ni hivyo kwa nini wameshindwa kufanya hivyo Pemba ambako kuna watu wachache kuliko Unguja?
4. Hivi wanaokataa wapemba kuchukua nafasi ya uongozi ni watu wa bara? Waliosema, mpemba kushika utawala Zanzibar ni sawa na mbwa kuingia msikitini ni watu wa bara?
5. Katika baraza la mapinduzi kuna watu wa bara wangapi? Kwenye bunge la JMT kuna wabunge wangapi kutoka Zanzibar? Idadi yao inaendana na proprtion yao ya idadi ya watu?
6. Watu wa bara wangapi wamewahi kushika uongozi katika SMZ? Zakia Meghji, mzanzibari mwenzako, mbona aliwahi kuwa waziri wa utalii na mali asili? Wizara ambayo si ya Muungano!

Don't flatter yourself, hauwezi kunipa homework mtu ambae hata historia ya ulikotoka huijui.

Amandla......
 
Ukienda Basra, Iraq kuna wa-Iraq kibao(mamilioni) wenye asili ya Afrika Mashariki. Fuatili uchaguzi mwaka huu utaona kina 'Obama' wengi tu maeneo ya Basra wamechukua fomu kugombea nafasi za uongozi.

Kiswahili kilikuwa lugha ya kufundishia ngazi ya shule ya msingi hapo Basra mpaka mwaka 1970, ambapo serikali ya Iraq ikaona bora kuwaunganisha Wa-Iraq wote kwa kuliondoa somo kama somo la kufundishia.

Black Iraqis Fight Discrimination in The Middle East - Basra

Submitted by Editor on Tue, 2009-08-25 09:01

blackiraqi.jpg

The burden of their ancestors continues to haunt black Iraqis from the southern province of Basra.
Some continue to refer to black Iraqis by their ancestral name – slave. It is a long-standing insult for a group which has lived in Basra for centuries, but whose roots lie in Africa.
Black Iraqis from Basra have long faced discrimination because of the colour of their skin.
While some have become influential local entertainers and artists, many are labourers with limited upward mobility. No black Iraqis serve on provincial councils or in parliament.......

African slaves are believed to have arrived in Iraq from East Africa around the fourth century. The slaves became known as Zanj – a derogatory term that is still used today.
Descendants of slaves in Basra rose up against the Abassid government between AD 869 and 883 in what was coined the Zanj Rebellion.

kwa habari kamili bofya hapa:http://www.planbinsider.com/world-stage/black-iraqis-fight-discrimination-middle-east-basra

Hawa walikuwa uarabuni hata kabla ya mtume Mohammed kuzaliwa na hadi leo hawajakubalika! Halafu watu mnataka kutuambia kuwa wakina Seyyid Said walijihesabu wa-Zenj!

Amandla........
 
Acha uongo.
1. Mwaka 1995 Nyerere hakuwa Rais. Rais wa JMT alikuwa mzanzibari mwenzemu na ni yeye ndiye aliyekuwa na amri juu ya vyombo vya dola na sio Nyerere.
2. Nyerere peke yake asingeweza kupindisha matokeo ya uchaguzi kama wazanzibari wote walikubaliana nayo. Kukubali kuwa aliweza kufanya hivyo ni kukubali udhaifu wenu na msivyoaminika. Mngekuwa watu wa msimamo, Nyerere asingefua dafu.
3. Manowari na majeshi ya JMT yana haki ya kuwa Zanzibar wakati wowote. Mbona bara yapo na watu wanapiga kura bila uoga? Toa ushahidi wa kuonyesha kuwa majeshi hayo yamewahi kutumika kupindisha uchaguzi. Ingekuwa ni hivyo kwa nini wameshindwa kufanya hivyo Pemba ambako kuna watu wachache kuliko Unguja?

Don't flatter yourself, hauwezi kunipa homework mtu ambae hata historia ya ulikotoka huijui.

Amandla......

Fundi naona unapoteza muda wako bure - unabishana na mjukuu wa Sultani Jamshid bin Abdullah - mpaka leo uchungu wa mapinduzi ya mwaka 1964 bado unamnyima usingizi, masikini.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995, Nyerere hakuwa Raisi wa Tanzania, hakuwa Mwenyekiti wa CCM na hakuwa Jemadari Mkuu wa majeshi - hivi vyeo vyote vilishikwa na Mzanzibari.
 
Kama Mwinyi ni mzanzibari basi sawa...sisemi kitu mie :D
 
Takwimu zipi unazozipinga? Mbona hamna unapoziweka wazi? Au neno takwimu lina maana tofauti bara na unguja kama ilivyo nyanya? Nielewavyo mimi takwimu ni statistics.

Wengi waliokimbia Zanzibar baada ya mapinduzi hawakuishia Tanzania Bara bali waliendelea hadi uingereza na Oman. Walioishia Tanzania bara ni wale walioondoka wakati wa utawala wa Karume I. kwa mfano, wahindi wengi walihama kukimbia uwezekano wa mabinti zao kuolewa kwa nguvu, kitu ambacho kiliishapewa baraka na utawala wa wakati ule. Ni uongo kudai kuwa mauaji Zanzibar yalitokana na mapinduzi ya mwaka 1964 tu. Baada ya uchaguzi wa mwaka 1961 watu 68 waliuawa katika fujo zilizotokea. Napo mtamlaumu Nyerere? Hata baada ya mapinduzi ni Nyerere ndiye aliyeipa hifadhi meli ya Sultan baada ya kenya kumkatalia. Ni Nyerere huyo huyo ndiye alimzuia John Okello asirudi Zanzibar ambako pengine mauaji yangeendelea. Tofauti na mnavyotaka tuamini, aliotaka muungano zaidi alikuwa ni Karume maana alikuwa na wasiwasi wa waarabu kurudi na kumlipizia. Ndiyo maana hata aliposhauriwa ahusishe watu zaidi alikataa. Ukweli mwengine ni kuwa bila serikali ya JMT watawala wa Zanzibar wangetumia mkono mzito zaidi kuwashughulikia wapinzani ambao wao waliwaona kama vibaraka vya waarabu.

Mbona hili la wutumwa linawasumbua sana. Sijawahi kupinga kuwa kuna watanganyika (nyinyi kwa vile mnawapenda sana mnawaita machogo) wengi tu waliohamia kwa ridhaa yao. Wanyamwezi wengi tu wako huko mnakoita mashambani. Na sio wote walikuja kwa kuribishwa bali wengi walikuja kujitafutia riziki yao katika mashamba ya karafuu. Pamoja na haya haiwezekani kabisa kuwa katika wazanzibari weusi walioko huko sasa hivi hakuna waliotokana na utumwa. Na haiwezekani kabisa kuwa katika hao waarabu waliokuwepo hakuna ambao ndugu zao walihusika na biashara ya utumwa. Huku ni kujidanganya.

Nimefika Unguja na Pemba na ninajua kuwa bado tofauti za rangi zina nafasi kubwa katika jamii. Machungu yaliyotokana na mapinduzi si rahisi kuyasahau kirahisi.

Tatizo ninaloliona mimi ni kuwa manataka kukwepa historia na kulaumu wengine kwa mapungufu yenu. Bila kuangalia historia yenu, kukiri mlipokosea, kuomba msamaha mliowatendea uovu, hamtakuwa na amani ya kudumu. Na safari hii mtakapobebeana majambia hao mnaowaita machogo watawaangalia tu maana watakuwa wamejifunza kutokana na historia kuwa hamna shukrani. Nawahikishia mtakuja kumkumbuka na kumlilia Nyerere.

Amandla......

Hizo takwimu nilizoquote kwa rangi nyekundu ndio vichekesho japo hazina nambari lakini zinabaki kuwa ni takwimu kwa vile umetumia neno wengi(majority). hivi nikuulize ni nchi gani ambayo kunatokea mauwaji watu wasikimbilie nchi jirani? hii ni sheria ya kimaumbile na huwezi kuchukulia hiki kama ni kigezo cha ukarimu wa wabara kwa wazanzibari.(Mungu awalinde)lakini hata nyinyi mkianza kuuwana basi mtakimbilia zanzibar na kenya hivyo hii haiwezi kuwa ni hoja.

Chukua mfano huu hapa unaweza kufanana na hoja yako hii.Ireland walitawaliwa,kuonewa na kukandamizwa sana na waingereza lakini raia wa kawaida walikimbilia kwa hao hao madhalimu wao wa kiingereza kutafuta usalama wao na huku wakijua kwamba muingereza ndio adui yao.Hivyo wazanzibari kukimbilia bara kwenye matatizo haiondoi uhalisi wa kwamba bara hawezi kuwa adui yetu.

Hoja ya wahindi: hapa naona unajichanganya tena,kwenye mabandiko yako mengine,wahindi na waarabu unawatoa kwenye uzanzibari lakini hapa unawatamka kama wazanzibari kwakuwa tu wamekimbilia bara,tukamate lipi?

Kuhusu kesi ya Okello, ndugu ifatilie tena kesi ya okello kukimbizwa na nyerere usiuzuge umati wa JF. Soma tena mapinduzi ya Zanzibar.

Nakubaliana na wewe kwamba Karume aliungana na bara kwa kupata ulinzi, lakini baada ya kifo chake nini kiliendelea?

Kama Nyerere hakuupenda muungano je kulikuwa na haja gani ya kuunganisha vyama? Au utatwambia kwamba na vyama alitaka jumbe viunganishwe? acheni siasa za shule ,tuongeleeni uhalisi wa mambo jamani!
 
Takwimu zipi unazozipinga? Mbona hamna unapoziweka wazi? Au neno takwimu lina maana tofauti bara na unguja kama ilivyo nyanya? Nielewavyo mimi takwimu ni statistics.

Wengi waliokimbia Zanzibar baada ya mapinduzi hawakuishia Tanzania Bara bali waliendelea hadi uingereza na Oman. Walioishia Tanzania bara ni wale walioondoka wakati wa utawala wa Karume I. kwa mfano, wahindi wengi walihama kukimbia uwezekano wa mabinti zao kuolewa kwa nguvu, kitu ambacho kiliishapewa baraka na utawala wa wakati ule. Ni uongo kudai kuwa mauaji Zanzibar yalitokana na mapinduzi ya mwaka 1964 tu. Baada ya uchaguzi wa mwaka 1961 watu 68 waliuawa katika fujo zilizotokea. Napo mtamlaumu Nyerere? Hata baada ya mapinduzi ni Nyerere ndiye aliyeipa hifadhi meli ya Sultan baada ya kenya kumkatalia. Ni Nyerere huyo huyo ndiye alimzuia John Okello asirudi Zanzibar ambako pengine mauaji yangeendelea. Tofauti na mnavyotaka tuamini, aliotaka muungano zaidi alikuwa ni Karume maana alikuwa na wasiwasi wa waarabu kurudi na kumlipizia. Ndiyo maana hata aliposhauriwa ahusishe watu zaidi alikataa. Ukweli mwengine ni kuwa bila serikali ya JMT watawala wa Zanzibar wangetumia mkono mzito zaidi kuwashughulikia wapinzani ambao wao waliwaona kama vibaraka vya waarabu.

Mbona hili la wutumwa linawasumbua sana. Sijawahi kupinga kuwa kuna watanganyika (nyinyi kwa vile mnawapenda sana mnawaita machogo) wengi tu waliohamia kwa ridhaa yao. Wanyamwezi wengi tu wako huko mnakoita mashambani. Na sio wote walikuja kwa kuribishwa bali wengi walikuja kujitafutia riziki yao katika mashamba ya karafuu. Pamoja na haya haiwezekani kabisa kuwa katika wazanzibari weusi walioko huko sasa hivi hakuna waliotokana na utumwa. Na haiwezekani kabisa kuwa katika hao waarabu waliokuwepo hakuna ambao ndugu zao walihusika na biashara ya utumwa. Huku ni kujidanganya.

Nimefika Unguja na Pemba na ninajua kuwa bado tofauti za rangi zina nafasi kubwa katika jamii. Machungu yaliyotokana na mapinduzi si rahisi kuyasahau kirahisi.

Tatizo ninaloliona mimi ni kuwa manataka kukwepa historia na kulaumu wengine kwa mapungufu yenu. Bila kuangalia historia yenu, kukiri mlipokosea, kuomba msamaha mliowatendea uovu, hamtakuwa na amani ya kudumu. Na safari hii mtakapobebeana majambia hao mnaowaita machogo watawaangalia tu maana watakuwa wamejifunza kutokana na historia kuwa hamna shukrani. Nawahikishia mtakuja kumkumbuka na kumlilia Nyerere.

Amandla......

Fundi naona unapoteza muda wako bure - unabishana na mjukuu wa Sultani Jamshid bin Abdullah - mpaka leo uchungu wa mapinduzi ya mwaka 1964 bado unamnyima usingizi, masikini.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995, Nyerere hakuwa Raisi wa Tanzania, hakuwa Mwenyekiti wa CCM na hakuwa Jemadari Mkuu wa majeshi - hivi vyeo vyote vilishikwa na Mzanzibari.

si mlimpa cheo kisicho rasmi cha ubaba wa taifa au? labda nikuulize alikuja kufanya nini kwenye kamati ya dharura ya pale kiswandui kabla kutangazwa matokeo ya urais?,mkitaka msitake mguu wa tanganyika unaiathiri sana zanzibar!
 
Back
Top Bottom