Hotuba ya Rais wa TZ ya mwezi June

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Tumekuwa na tarbia na sasa naona imekuwa kama ada kwa kiongozi wa Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na wananchi wake kila inapofikia mwisho wa mwezi kwa nia ya kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanaoendelea nchini mwake.

Sasa wadau mlioko huko Tanzania napenda kuwauliza Vipi hotuba hiyo ya Rais ya mwisho wa mwezi June ameitoa? na kama ameitoa amezungumzia suala gani?

Tunaomba mtujuze mlioko huko Tanzania
 
Rudi nymbani bwana mkubwa tutafute uhuru uliopotea, hatuna rais huku bali tuna mtawala. Habari ndo hiyo!
 
Mmmmmh, nina wasiwasi na uzalendo wako, hata kukujibu kuhusu hiro hotuba ya huyo wa kujitetea sioni umuhimu! cha msingi jua tu kuwa Hatuna Raisi tuna mtawala kwa tiketi ya magamba
 
Labda mtoe dual citizenship naweza kufikiria kurudi. Lakini kurudisha passport ya Oman na kuchukua ya Tanzania ni sawa na kutema asali na kutamani pilipili.Poleni sana
kumbe we sio mwenzetu,umeshaukana uraia wako wa tanzania...bah!Umenisikitisha sana mkubwa,sasa kila mmoja wetu akiamua kutimka kukimbia matatizo ya nyumbani si ndo tutaiangamiza Tanzania yetu.,Rudi home tuungane kuikomboa nchi yetu bwanaa!
 
Hivi wewe bado unatamani kuitwa mtanzania? Sijakosa uzalendo naomba msije mkanihukumu! Nchi inayojengwa na wananchi na kuliwa na mafisadi, nchi yenye utajiri mkuuuuuuuuuuubwaaaaa unaowanufaisha wageni (zamani tukiwaita MAKABURU/WAKOLONI), wamerudi kwa staili ya UWEKEZAJI! Nchi inayotegemea kudra za mwenyezi Mungu kupata umeme, hata mimi nikipata mchongo, bila kujali umri wangu NASEPA!
 
Mkataa kwao ni mtumwa. Mimi ni mwarabu wa Omani, Zanzibar nilizaliwa tu na kusomea Bara.

Kwani nikivaa kama ninavyovaa nguo za asli yyangu basi nitaitwa mdini na pengine kukasa baadhi ya haki zangu.

Nyumbani ni Nyumbani. Huku nipo huru sana na nina wasaa.
 
Labda mtoe dual citizenship naweza kufikiria kurudi. Lakini kurudisha passport ya Oman na kuchukua ya Tanzania ni sawa na kutema asali na kutamani pilipili.

Poleni sana
Asali au pilipili inategemea tu unataka kuitumia wapi...................... WENZIO HUKU ASALI HATUWEKI KWENYE SUPU WALA KITIMOTO........... ni pilipili tuuu
 
Hata akitoa iyo hotuba labda atoe kwa maandishi kupitia magazeti tu kwa sababu akisoma kupitia vyombo vya moto haitawafikia wananchi kwa sababu hakuna UMEME masaa mengi sana Tanzania nzima.
 
Hata akitoa iyo hotuba labda atoe kwa maandishi kupitia magazeti tu kwa sababu akisoma kupitia vyombo vya moto haitawafikia wananchi kwa sababu hakuna UMEME masaa mengi sana Tanzania nzima.

Sasa vipi ya mwezi June kama ada ameshaitoa? au ndo usanii wa waDanganyika?
 
Mkataa kwao ni mtumwa. Mimi ni mwarabu wa Omani, Zanzibar nilizaliwa tu na kusomea Bara.

Kwani nikivaa kama ninavyovaa nguo za asli yyangu basi nitaitwa mdini na pengine kukasa baadhi ya haki zangu.

Nyumbani ni Nyumbani. Huku nipo huru sana na nina wasaa.

mkuu sasa km wewe si mtanzania maswala ya siasa za tz yanakuhusu nini? au wewe ni miongoni mwa wawekezaji mnasubiri JK atangaze uhuru wa wawekezaji ili ushangilie?
 
mkuu sasa km wewe si mtanzania maswala ya siasa za tz yanakuhusu nini? au wewe ni miongoni mwa wawekezaji mnasubiri JK atangaze uhuru wa wawekezaji ili ushangilie?

Nimewekeza saana Tanzania na ninataka kuja kugombea uwaziri huko hususan Tanzania Bara (Tanganyika)........joke.

Naipenda TZ na nasikitika sana nchi tajiri sana lakini wananchi maskini as'hat.
Uchumi unaliwa na wachache
 
Hivi wewe bado unatamani kuitwa mtanzania? Sijakosa uzalendo naomba msije mkanihukumu! Nchi inayojengwa na wananchi na kuliwa na mafisadi, nchi yenye utajiri mkuuuuuuuuuuubwaaaaa unaowanufaisha wageni (zamani tukiwaita MAKABURU/WAKOLONI), wamerudi kwa staili ya UWEKEZAJI! Nchi inayotegemea kudra za mwenyezi Mungu kupata umeme, hata mimi nikipata mchongo, bila kujali umri wangu NASEPA!
hapa ulikuwa unataka kusema nini vilee...!Acha ulimbukeni wewe,tena ondoa fikra potofu mtu wangu,usikimbie tatizo baki hapahapa tupambane na wanaoihujumu Tanzania/Tanganyika yetu ili siku moja iwe nchi ya maziwa na asali.Ujasiri wa kubaki nyumbani na kupambana utatuweka huru na tutakumbukwa na vizazi vijavyo.Acha ubinafsi!
 
Mkataa kwao ni mtumwa. Mimi ni mwarabu wa Omani, Zanzibar nilizaliwa tu na kusomea Bara.Kwani nikivaa kama ninavyovaa nguo za asli yyangu basi nitaitwa mdini na pengine kukasa baadhi ya haki zangu.Nyumbani ni Nyumbani. Huku nipo huru sana na nina wasaa.
Haya banaaa!
 
Barubaru,hiyo hotuba atamhutubia nani,Nchi iko gizani kwa sasa,nadhani hata yeye anajua fika ujumbe hautafika kwa walengwa.Lkn pengine sababu nyingine,ni kutokuwa na majibu ya uhakika na hasa hili la umeme.
 
Nimewekeza saana Tanzania na ninataka kuja kugombea uwaziri huko hususan Tanzania Bara (Tanganyika)........joke.

Naipenda TZ na nasikitika sana nchi tajiri sana lakini wananchi maskini as'hat.
Uchumi unaliwa na wachache

Karibu kwenye maandamano ya mwezi wa nane kani ndio kipindi umeme utakuwa hakuna kabisa na ndio tutakpo mwambia JK ajiuzuru na hatuna imani na waziri mkuu that is for sure waambia ALjazeera ajiaande kuja kwenye maandamano ya Nchi nzima ni kama ya Misri Mororco syria tunis. JK nchi imeisha mshinda wana tupeleka kwenye janga. Ngereja ni Mbuzi wa kafara anamlidia JK makosa yake ya Nishati na Madini ule wakati alikuwa waziri ndio mikataba yote mibovu ilipo sainiwa na JK alikuwa shaidi ambae sasa ni Mtawala wetu
 
Labda mtoe dual citizenship naweza kufikiria kurudi. Lakini kurudisha passport ya Oman na kuchukua ya Tanzania ni sawa na kutema asali na kutamani pilipili.

Poleni sana

Alikuwa ziarani nchi za nje. Nilidhani aliisoma huko huko. Nyie ndio mnatakiwa mtujuze.
 
Nimewekeza saana Tanzania na ninataka kuja kugombea uwaziri huko hususan Tanzania Bara (Tanganyika)........joke.

Naipenda TZ na nasikitika sana nchi tajiri sana lakini wananchi maskini as'hat.
Uchumi unaliwa na wachache

mkuu njoo bwana tumtoe huyu nduli natuikomboe nchi yetu.
 
mwezi May, Salva Rweyemamu alitoa press release kwamba mkuu hakuwa na jipya nasikia hata June hii Salva alitaka kutoa Press Release ila document imeliwa na Trojan so labda kesho atatoa Press Release kwa nini June hakukuwa na hotuba. Tanzania ya sasa mambo shaghalabaghala!
 
Back
Top Bottom