Hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi

Mheshimiwa Spika, alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb), alizua tafrani kwenye familia ya Ben Saanane baada ya kusikika maneno kama “huyu mwenzetu aliyetangulia mbele za haki”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa Kauli, endapo maneno haya yalikuwa ni ya bahati mbaya kutamkwa au kwa kuwa Waziri Mkuu alitumia hekima na busara zake kufikisha ujumbe kuwa Ben Saanane amekwisha fariki?
 
Mheshimiwa Spika, Wakati Serikali imetumia gharama kubwa sana kumtafuta faru John, Serikali hiyo hiyo haionekani kufikia ukomo katika juhudi za kutoa taarifa za hatma ya suala hili la Ben Saanane. Na taarifa tulizonazo ni kuwa hata kikundi cha Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), ambacho Ben Saanane alikuwa ni Katibu wake, walipoanza kufuatilia miili ya watu 7 iliyozikwa kando ya Mto Ruvu, walibaini kuwa miili ile imefukuliwa na kupelekwa kusikojulikana haswa mara baada ya kupaza sauti ya kutaka kufanyike vipimo vya DNA ya miili ile 7 ya mto Ruvu.
 
Pamoja na Mh Lema kunyanyaswa na polisi wakubwa lakini amekuwa MTETEZI MKUU WA MASILAHI YA MSINGI YA POLISI MAKURUTA , polisi wadongo mwangalieni Mh Lema kwa jicho la 3 .

Ninao uhakika kwamba hali zenu zitabadilika sana baada ya Mh Lema kutwaa uwaziri kamili wa Mambo ya ndani mnamo Decemba 2020 baada ya serikali mpya ya UKAWA kuapishwa kwa mbinde.
 
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kuwa bodi ya Parole, ifike mahali iwaachilie wafungwa wote waliofungwa wakati wa Nyerere na Wakati wa Mwinyi na hata wakati wa Mkapa ambao wana zaidi ya miaka 10 mpaka 15 magereza. Kwani ni imani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa watu hao wameshajifunza kiasi cha kutosha. mtu amekaa jela miaka 25, na ana miaka zaidi ya 65 akipata msamaha kisha akawa huru, kweli mtu huyo anawezaje kuwa mhalifu tena?
 
Mheshimiwa Spika, Wakati Serikali imetumia gharama kubwa sana kumtafuta faru John, Serikali hiyo hiyo haionekani kufikia ukomo katika juhudi za kutoa taarifa za hatma ya suala hili la Ben Saanane. Na taarifa tulizonazo ni kuwa hata kikundi cha Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), ambacho Ben Saanane alikuwa ni Katibu wake, walipoanza kufuatilia miili ya watu 7 iliyozikwa kando ya Mto Ruvu, walibaini kuwa miili ile imefukuliwa na kupelekwa kusikojulikana haswa mara baada ya kupaza sauti ya kutaka kufanyike vipimo vya DNA ya miili ile 7 ya mto Ruvu.
Haya mambo yanachanganya, sielew kwann serikal imekaa kimya tu
 
Mheshimiwa Spika, Serikali inayojivunia mapato yatokanayo na makosa ya barabarani, inakosa uhalali wa kutuma salamu za rambirambi pindi ajali na vifo vinapotokea
 
Mheshimiwa Spika, Serikali inayojivunia mapato yatokanayo na makosa ya barabarani, inakosa uhalali wa kutuma salamu za rambirambi pindi ajali na vifo vinapotokea..........G.Lema 9/5/2017 Bungeni
 
Nasikia Hotuba hii wamezuia isisomwe bungeni...

Anyway Hotuba Nzuri sana nimeisoma Vizuri sana ila Mh.. umesema Jela mnavuliwa nguo na kupekuliwa masaburi Je Na Wewe walifanya kwako Maana umesema ni kwa Wafungwa na Mahabusu...Pole sana
 
Hotuba imejaa utetezi wa mambo ya Lema binafsi jinsi anavyoshindana Na sheria za nchi Na anavyodhibitiwa yeye kwa kukosa maadili Kama kiongozi.

Amejitambulisha yy mwenyewe ktk hotuba yote kwakweli huu ni ubinafsi uliyopindukia.

Ni vyema akatupisha apite kuleeee..
 
Hotuba za bajeti zingelenga bajeti kwa maana matumizi ya fedha katika wizara husika zinazohitajika kifungu hadi kifungu.Budget ni financial plan.
Bila kujadili kwa undani matumizi ya fedha, kutasababisha kupitisha jambo bila kuwa na uhakika nalo.Wabunge walio wengi wamesikika wakilalama kuwa bejeti ya mwaka jana imekamilika kwa asili mia 30 tu.Kuna haja gani ya kupitisha kitu kisichotekelezwa?
 
Imeniuna pale niliposikia princess mawazo! Mungu amjalie kwa hekima aliyoonesha MP! Wabirah taufiq!
 
Back
Top Bottom