Hotuba ya Mpendazoe alivyomvaa Mkapa Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Mpendazoe alivyomvaa Mkapa Bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 31, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huu ulikuwa ni mojawapo ya mchango wa Mpendazoe August 1, 2009 Bungeni (msisitizo wangu)

  Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Uteklezaji wa Azimio la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali kma lilivyowasilishwa na Serikali

  Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nadhani nitachangia kwa kifupi Taarifa hii ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira.

  Mheshimiwa Spika, cha kwanza kabisa naomba niunge mkono taarifa hii na mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati na mimi nadhani nitaongezea jambo, nadhani litakuwa jambo moja na zaidi nitazungumzia suala la miiko ya uongozi na kumomonyoka kwa maadili katika nchi yetu. Nadhani ni jambo ambalo litakuwa siyo rahisi sana kulizungumza. Nirudie kusema, kwa kawaida ni rahisi sana kuuzunguka mbuyu, lakini ni vigumu sana kuukumbatia. Lakini leo nataka kuthubutu kuukumbatia. Lakini nadhani siwezi kuukumbatia peke yangu. Naomba kwa kuanza nimnukuu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kitabu chake cha Nyufa cha mwaka 1995, alisema hivi, nanukuu kwa ridha yako:

  �Sasa Tanzania inanuka rushwa, tunataka kiongozi anayejua hivyo, ambaye atasema rushwa kwangu mwiko. Mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa na wanamjua watu wa rushwa watamjua hivyo. Lakini hatutaki aishie hapo tu, maana haitoshi wewe mwenyewe uwe mwaminifu. Unaweza wewe mwenyewe ukawa mwaminifu kabisa kabisa lakini una shinikizo la ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako. Kwa hiyo, sio inatosha wewe kuwa mwaminifu tu, lakini uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa zako kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena. Utawaambia jamaa na rafiki zako kwa dhati kabisa, Ikulu ni mahali patakatifu. Mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza kuwa pango la wahalifu, walanguzi. Na hakuna Serikali mahali popote duniani inayoendeshwa bila miiko.�

  Ndio kitu ambacho ninaomba nikiongezee katika yale ambayo yamezungumzwa katika Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini.

  Mheshimiwa Spika, katika Isaya 1:1-10 inaeleza, wakati huo wana wa Israeli, walishuhudia nchi yao ilikuwa inaporwa, utajiri wao unaporwa na wageni. Lakini cha ajabu kabisa walikuwa wakishangilia uporaji wa rasilimali zao wenyewe; ni jambo la kushangaza sana. Lakini katika Isaya 24:1-2, inasema hivi...

  Mheshimiwa Spika, naenda kwenye Kiwira. Kama alivyo Kuhani, ndivyo waumini watakavyokuwa. Nchi yoyote hapa duniani wananchi watakuwa waadilifu na waaminifu kama viongozi wao ni waadilifu na waaminifu. Katika ubinafsishaji wa mgodi wa Kiwira, katika ukurasa wa nne wa Ripoti ya Kamati, umeonyesha wamiliki makampuni manne na wanaohusika pale wameonyeshwa. Lakini kauli ya Serikali iliongezea mmiliki mwingine na alikuwa ameonyeshwa wa kwanza pale katika Kauli ya Serikali. Mmiliki huyo ni Anbern.

  Mheshimiwa Spika, naomba nikukabidhi, kama utakubali, nyaraka zinazoonyesha mmiliki huyo Anbern ni nani na mlolongo mzima unaoonyesha jinsi ubinafsishaji ulivyofanyika na ninaomba Watanzania wafahamu na ndugu zangu wengine ambao wameniona mimi labda nina sababu zangu binafsi katika suala hili. Lakini ninataka nizungumze, hoja yangu ni kutaka kuwa na utaratibu wa kuwajibishana wakati, kama mtu aliyepewa dhamana kubwa na wananchi, akienda kinyume na maadili na miiko ya uongozi, tusimwonee haya. Hiyo ndio hoja yangu.

  Ukurasa wa nne wa Taarifa ya Kamati, umeonyesha wale wamiliki, kwa kifupi hao wote ni ndugu na marafiki. Ndio nilisema katika kuukumbatia huu mbuyu, nimeomba ninukuu maneno ya Hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere, inawezekana ikawa rahisi kuukumbatia. Lakini ninachotaka kusema, kama hatutazingatia maadili, viongozi tunaopewa dhamana kubwa, ninakuhakikishia nchi yetu miaka mitano, kumi ijayo, tutakuwa na maadili ya ajabu sana, kitu ambacho ni kibaya tutasema ni kizuri na tutakitetea kwa sababu maadili yamemomonyoka.

  Mheshimiwa Spika, unaonaje Israel? Utajiri wao unachukuliwa lakini wao wanashangilia! Unaonaje leo Tanzania, Viongozi tuliowapa dhamana kubwa ya kuongoza wanapoamua kujitajirisha wao wenyewe na tunasema wasiguswe! Wakisemwa, wanakejeliwa; hapana! Hayati Mwalimu, alisema tujali miiko ya uongozi na tukijali miiko ya uongozi tutafika mahali ambapo nchi yetu kweli na rasilimali zetu kweli zitawanufaisha Watanzania.

  Haiwezekani anapatikana mtu tunampa dhamana, anaanza kugawa utajiri wa nchi yetu kwa rafiki na familia yake, haiwezekani. Tufike hapo tukubali kwamba hilo nalo tuliangalie na sisi Watanzania tubadilike. Kama hatutabadilika na tabia hii hatutakuwa tofauti na enzi za Israel, wakati uchumi wao unachukuliwa wao wanashangilia. Ni afadhali kwamba Kuhani alivyo ni sawa na Waumini ni afadhali kidogo, kuliko waumini wawe sawa na Kuhani. Ni afadhali Kuhani awe sawa na Waumini, lakini ni vibaya sana Waumini kuwa sawa na Kuhani. Kuhani alivyo ndivyo waumini walivyo. Kama Kuhani akianza kuwa mbadhirifu na wengine wataanza kufuata hivyo hivyo, ni afadhali hiyo, kuna wengine watakataa; kuna kikundi ambacho walikuwa wanasema ni wale wale wanaotaka kusema leo.

  Mheshimiwa Spika, wengine wanaweza wakakataa lakini hatari iliyokubwa ni kwamba, akipatikana Kuhani kutokana na jinsi waumini walivyo, ambapo kama waumini wakawa wameharibika, tunapata Kuhani aliyeharibika, nchi itakwisha kabisa.

  Kama Watanzania leo hatutajali maadili ya kuwawajibisha viongozi wanaokiuka miiko na tukasema hakuna tatizo lolote, nchi yote itaoza. Wananchi watasema jambo lolote ni sawa. Nchi nzima ikianza kuliona jambo lolote la uovu ni sawa, atapatikana Kuhani kutokana na jinsi waumini walivyo, itakuwa ni hatari zaidi. Kwa hiyo, tuzuie hilo. Hilo tulizuwie na ombi langu, Viongozi wa Awamu ya III najua walifanya mambo makubwa sana.

  Mheshimiwa Spika, mimi wakati tunakwenda kwenye uchaguzi, nilitaka hata kusema kwamba Rais Mkapa aendelee na wengine ambao walikuwa humo waendelee kwa sababu wamefanya mambo makubwa, hakuna cha ajabu hapo, ni kweli kabisa! Lakini ndani ya pazia hilo kuna matatizo ambayo tunayaona hapa na ni lazima tuyarekebishe na tuyaweke wazi watu wajue na tujue kwamba haya hatuyataki tena. Tukiyaficha kama watu wengine wanavyosema kwamba tusioneshe hiki kitu, hapana! Ni lazima kitu kifahamike, where there is no pain there is no gain. Ni jambo linaloumiza, lakini tukilikubali litaleta faida kubwa sana.

  Mheshimiwa Spika, naomba waliohusika, waliokuwa Viongozi wa Awamu ya III, tuliyoiheshimu sana wajitokeze wawaombe msamaha Watanzania. Vinginevyo Serikali ya Awamu ya IV ambayo iliapa kuilinda Katiba, haikuapa kulinda Serikali ya Awamu ya III, isiwaonee haya wote waliohusika katika tatizo hili, waliokuwa viongozi. Ninarudia, Serikali ya Awamu ya IV ambayo ina heshima kubwa sana sasa hivi, haikuapa kuilinda Serikali ya Awamu ya III na Serikali ya Awamu ya III haikuapa kuilinda Serikali ya Awamu ya II, waliapa kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa hiyo, Serikali ya Awamu ya IV iliyo na heshima kubwa sana isione haya kuwaonea haya wale waliohusika na ubadhirifu au na ubinafsishaji ulio holela wa Mgodi wa Kiwira, waliokuwa Viongozi wa Awamu ya III. Kama hawatataka kujitokeza na kuwaomba msamaha Watanzania.


  Mheshimiwa Spika, ngoja nimalizie basi. Ninashukuru kwa kunikumbusha nirudi pale, basi nilichokuwa ninaomba ni kuhitimisha mchango wangu. Basi nilikuwa ninaomba wale waliohusika katika ubinafsishaji holela wa Mgodi wa Kiwira ambao walikuwa ni Viongozi, itakuwa ni heshima kubwa sana hata kwao wakisimama wakieleza na ikiwezekana wakawaomba msamaha Watanzania na itatusaidia sana. Ahsante sana.
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Jamaa alikuwa anaangalia mbali!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyu mtu ana hali fulani ya boldness!...Hata kama anaigiza, basi its to the best of his ability!
  Lakini namsifu kwa courage ya kubadilisha maneno kuwa vitendo, tofauti na wengine wengi wanaolalama tu bungeni, but they dont move an inch to cement and reinforce their allegations!
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Imetulia sana hii hotuba
   
 5. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yote mazuri aliyosema, lakini kwa nini amekimbia lindo kupisha wezi?
   
 6. N

  Ngala Senior Member

  #6
  Mar 31, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wana kishapu mbuge wenu kadhihirisha kwa unjano na kijani si lolote mbele ya maslahi ya umma kaitosa ccm. Ombi langu endapo atagombea ubunge toka ccj mpeni kura za kishindo ili ccm wajue kuwa ukaidi wao umefikia tamati. Upinzani nawaomba mpeni msaada wa hali na mali arudi bungeni aongeze nguvu ktk Slaa family
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  umewahi kusoma kitabu kinachoitwa "Art of War".. ambacho kimetumiwa kwa miaka elfu kadhaa katika nadharia mbalimbali za vita?
   
 8. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Bora kakimbia hujaona wezi wanaanza kumuiba mbwa wa ulinzi then ndo wanavunja na kuiba?, lindo limegeuzwa ghala la vitu vya wizi sasa asubiri nini, bora wahi huko vinapoibiwa
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh.tutasikia habari za Mpendazoe kila kona,mpaka tukome wenyewe.
   
 10. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WASUKUMA wangetakiwa watoe wabunge kama huyu Mwana Tungu.Ni kabila kubwa lakini wabunge wao wengi wamekuwa YES MEN,hali ya uchumi mikoa hii ni duni,though wana samaki,gold,mifugo na mazao mengi.
  Watu hawa ni decent,lakiki serikali ya SISIM imewachukua hawa for granted.
   
 11. N

  Ndeshingio Member

  #11
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Huyu jamaa, ni mzuri nakubaliana na wanaJF wenzangua anatakiwa kupewa support kusudi aongeze nguvu kwenye Slaa family
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa vyo vyote vile Mh. Mpendanzoe ameonyesha njia??
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kidogo ana hali fulani ya kutoogopa ila bado sina cha kusema juu ya chama hiki maana sijaweza kujua kwa sasa naendelea na utafiti wangu
   
 14. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Shukran MMKJ kwa kutukumbusha kauli zinazoonyesha kuwa kuna sauti zenye "sanity" (sijui neno zuri la kiswahili, labda "uzima wa akili") na ujasiri, aghalabu chache, katika jamii hii inayoonekana kukubaliana na uozo wa kutupwa unaojidhihirisha katika kada za juu za CCM. Naamini mtu yeyote mwenye akili timamu na dhamira iliyonyooka kabisa hawezi kukaa kwa amani ndani ya chama hicho.

  Huu ndio wakati muafaka kwa wapambanaji wote waliojipambanua kuinuka na, kwa pamoja, kuhamasisha umma kutokubaliana na mfumo wa kifisadi unaooendekezwa na uongozi wa juu nchini kupitia chama na serikali yake. Nimemshangaa Selelii kumuona Mpendazoe kama mtu aliyejinyonga. Ina maana yeye na wenzake bado wanathamini zaidi kurudishwa bungeni kwa gharama yoyote ile hata kwa kuadhiriwa kama kulikowapata baada ya kelele nyingi za Richmond! They are not serious. Inabidi wajue kuwa hivi sasa hawana karata ya maana tena ndani ya chama. Ama waendeleze mapambano kwa nguvu zaidi hadi kuleta mapinduzi au wanywee na kungojea kutemwa tena kwa aibu zaidi. Mpendazoe did the wise thing.
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mh tumwombee mema mana mh nchi hii inawenyewe labada iwe katumwa ila kama kajituma mwenyewe kazi ipo
   
Loading...