We hear you loud and clear Mzee Es.
Sina shaka ulipokuwa unaandika hayo maneno ni kama damu ilikuwa inachemka kabisa ndani ya mishipa yako.
Watawala tulionao sasa hivi bado wanayo nafasi nzuri ya kugeuza mambo wakitaka iwe hivyo. Sijui kama Kikwete anaridhishwa na utendaji na mwenendo mzima wa serikali yake sasa hivi. Kama anataka awe kiongozi wa kukumbukwa na sio wa kupita tu, basi inabidi ajizatiti kikweli katika mambo mhimu yanayoweka dosari - rushwa, upatikanaji wa huduma za mhimu kwa haki kwa kila mtu- shule, afya n.k. Aachane kabisa na maswala ya chama chake tu ndio kiwe kinara wa kila kitu. Inafaa kabisa awe ni rais wa waTanzania, hayo mambo ya chama awaachie akina Makamba. Matatizo mengi sasa hivi yanajionyesha kuanzia kwenye chama na kusambaa hadi bungeni, serikalini, na hadi hata kwenye sheria. CCM imeanza kuwa mzigo usiobebeka!
Kwa kuanzia, ni mhimu watumishi wote serikalini wawe na malengo na viwango vya kazi wanazozifanya, na wayafikie hayo malengo- vinginevyo wawajibishwe. Mambo ya kusema ninakwenda kazini bila hata ya kujua kipimo cha kazi unachotakiwa kukikamilisha haileti maana.
Nadhani turudi nyuma kama taifa na tujiwekee wajibu na utaratibu unaoeleweka. Sasa hivi tunajiendea tu bila ya kuwa na dira madhubuti.
Kama matatizo yetu yanaanzia kwa mtu binafsi na kusambaa hadi kwenye watekelezaji wetu wakuu, basi hatuna budi kufumua mfumo mzima wa utaratibu huu. Pa kuanzia ni katika shule zetu wanakoandaliwa wakulima na wafanyakazi wa kesho. Hawa wafanyakazi waliomo katika mkondo huu wa leo tusukumane nao hivyohiyo, wengine watabadilika tu wakishaona kuwa upuuzi hauvumiliki tena katika utendaji wao.