Hotuba ya Kikwete kwenye sherehe za miaka 38 ya CCM imebeba ujumbe mzito

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 38 YA CCM, KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI, SONGEA - RUVUMA,
TAREHE 01 FEBRUARI, 2015

Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu na mjumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu;
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;
Ndugu Mike Mukula, Makamu Mwenyekiti wa NRM ya Uganda na ujumbe wake;
Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Oddo Mwisho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Waheshimiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa;
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM;
Ndugu Verena Shumbusho, Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Wenyeviti wa Jumuiya za CCM;
Viongozi, wananchama na wapenzi wa CCM;

Ina maana hakuna wahudhuriaje toka Zanzibar? Wapi Shein( Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar) Wapi Naibu katibu CCM Mkuu Zanzibar Vuai ? Au Itifaki haiwatambui?
 
Business as usual! Watanzania ni warahisi kama maharage ya mbea! Maji moja tu yashaiva. Tulidanganywa mwaka mmoja uliopita, na leo anakuja na ngonjera zilezile
 
Si jambo dogo.Kaneno kadogo kanakoweza kuwa na maana kubwa.Kaneno kadogo kanakoweza kuwa na matokeo hasi na chanya. Pamoja na jana kutokuwepo popote kwenye mkutano wa Maadhimisho ya CCM yetu, kutokana na kuumwa,nilimuangalia Mwenyekiti wetu luningani akihutubia. Ameongea mambo mengi. Ameipigia debe Katiba Pendekezwa waziwazi bila ajizi. Sio inshu!

Alipofika kuzungumzia uchaguzi mkuu wa mwaka huu,niliweka kikombe cha kahawa pembeni ili nisipitwe hata na neno la uzima moja toka kwa Mwenyekiti. Akasema mengi ya kichama na kisiasa.Lakini,kuna neno limenishtua. Neno "NATAKA" kwenye kauli hii: "Nataka Rais wa awamu ya tano atoke CCM". Ieleweke kuwa Rais Kikwete anataka.Si kwamba anapenda au anatarajia.Atataka. Neno zito.

Kutaka ni kuamua. Kuamua ni kupanga na kusimamia. Nakuhakikisha kuwa jambo linakuwa unavyotaka.Kutaka ni kuwa na uwezo wa kulifanya jambo husika. Mwenyekiti Kikwete ndiye Rais wa sasa wa Tanzania.Atakuwa na mamlaka na nguvu za kidola hadi pale Rais mpya atakapoapishwa. Akisema 'nataka' nani atabisha?

Naamini Mwenyekiti alikingikiwa na neno la kutumia tu.Hakupanga kutumia neno hilo.Angependa kusema anapendelea au anatamani badala ya kutaka. Kisiasa na kidemokrasia,huku yeye akiwa incumbent President, kusema 'nataka' si sawa. Wakuelewa na aelewe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ni kweli JK kwa hotuba ni kiboko tuje kwenye utekelezaji sasa....!!! ZERO!!!!!
Hiyo gharama walizotumia kuvalishana sare wangewalipa wakulima hela za mahindi waliyowakopa tangu mwaka Jana! Alafu wanawambia wauze mbuzi wakachangie mahabara kweli CCM hayondiyo maisha Bora mliyotuahidi? Nawananchi kwaujingawao wanashindwa kumuuliza mh. Mbona muda wako unaisha bila maisha bora? Wao wanashangaa viuno vya kina Komba!
 
Akihutubia kwenye sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa ccm, mwenyekiti wake aliwakumbusha wanaccm kwamba wana kazi kubwa ya kumtafuta mtu afaaye kuwa rais kwa sababu, mwalimu Nyerere alisema:Rais wa nchi hii aweza kutoka chama chochote lakini rais bora atatoka ccm.

Kwa maoni yangu maneno hayo ya Nyerere yataongoza kampeni za urais ccm 2015.

Ukawa kaeni chonjo kuukabili msemo huo ambao una kasoro kubwa.
 
Hata kama raisi akitoka ccm, tunapigania tuwe na wabunge wengi wa upinzani bungeni, halafu hapo ndo mtaona mtiti wake kama huyo raisi si atakimbia nchi!
 
Huyu Kikwete ni dhaifu sana hata akisema anataka mambo yataenda kombo tu... Kilichopo ni kuwa ashaona hali ni tete ndo maana anatumia kauli ya kulazimisha..... Lakini pamoja na hayo alishasimamia jambo lipi likatekelezwa kwa ufanisi??!Once dhaifu always dhaifu!!
 
Back
Top Bottom