Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Ndo maana Magamba hayampendi Mbowe! Baba Jesca kapigwa beat la kufa mtu. Eti leo wanawasambaza askari barabarani, ili iweje?
 
Tukimchekea uchwara tutavuna mavi,uchwara hajielewi kabisa yeye fukuza na teua
 
Matamko koko,Mbowe anaonesha kabisa kushindwa kabla ya maandamano yenewe
Amekana kuwa UKAWA hawakushirikishwa,lakini anasema watakaa na NCCR,hajaongelea NLD wala CUF watashiriki vipi zaidi ya kuwaomba CCm nao wamuunge mkono,
Kaonesha kuwa ni kiongozi hamnazo,baada ya kusema alitegemea Magufuli angewaamuru UVCCM waingie barabarani kupambana nao badala ya polisi.
Kuonesha kuwa UKUTA wamepania kufanya fujo,wamejiandaa kabisa na timu ya wanasheria ya kuwatetea wakikamatwa
Mbowe na wahuni wenziwe hawaatafanikiwa kuleta machafuko
 
kwa hyo unataka kumaanisha elimu aliyonayo tundu lissu haisaidii chochote kisa tu mtaani kuna njaa wekiwemo wananchi wa jimbo lake
Lissu haongozi Serikali. Elimu take inatumika kujenga misingi ya sheria. Kuhusu njaa mtaani muulize mwanasheria mkuu na serikali yake ni lini wataacha matamko watekeleze mpango wa maendeleo.
 
Serikali ione aibu hata kidogo tu kwa kukanyaga katiba
 
Watu wamekosa hoja kweli. Yaani wapuuzi kibao hoja yao wao wamebaki kusema kusema tu kuwa viongozi nao waende na familia zao kuandamana. Hii ni hoja mufilisi na ya kipuuzi. Leteni hoja za msingi.
It is very true.

Walete hoja ni kwa nini Mkuu wa nchi Kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi hii pale uwanja wa Taifa tarehe 4/10/2015 aliapa kuilinda na kuitii Katiba ya nchi, lakini hivi sasa anaisigina Katiba hiyo hiyo aliyoapa kuilinda.........

Inapotokea vyama vya siasa makini kama Chadema vinapotaka kuitetea Katiba ya nchi, eti wanaitwa wachochezi na Mkuu wa nchi anapiga mikwara kuwa atatumia vyombo vya dola 'anavyovimiliki' kuwashughulikia hao raia wema wasio na hatia ambao yeye anawaita kuwa wanaleta fyoko fyoko.....

Watanzania hivi sasa ndiyo tunapaswa kuzikumbuka hekima za hali ya juu za Mwalimu Nyerere kuliko wakati wowote huko nyuma.

Katiba hotuba yake kwa Taifa mwaka 1995 alisisitiza kwa hoja nzito kuwa Rais tunayemchagua ni lazima aitiii Katiba ya nchi aliyoapa kuilinda na Mwalimu akaendelea' kusisitiza kuwa Rais ambaye hataki kuitii Katiba ya nchi yetu Rais wa aina hiyo HATUFAI.......

Inashangaza kwa chama kama CCM ambao siku zote huwa wanasisitiza kuwa wataendelea kumuenzi Mwalimu kwa vitendo, lakini kwa hili la kuilinda Katiba ya nchi wanampuuza kupita kiasi!
 
Lissu haongozi Serikali. Elimu take inatumika kujenga misingi ya sheria. Kuhusu njaa mtaani muulize mwanasheria mkuu na serikali yake ni lini wataacha matamko watekeleze mpango wa maendeleo.
mmmh ina maana tundu lissu matatizo ya chakula jimboni mwake hawezi kutatua??
 
Mwambie mwenyekiti ajumuike na sisi kwenye maandamano siyo tupigwe sisi yeye akituangalia kwenye TV tu na familia yake
Nani amekuambia kwenye maandamano watu wanaenda kupigwa? Nani anapotosha kuwa maandamano ni vita kati ya Police na waandamanaji?
 
Kawaambieni waliowatuma nimjaribu Kawaambieni raisi Aliyepo madarakani hajaribiwi Kwanini wanasubiri tarehe 1/9 waamdamane Hata sasa....
 
Habari Mkuu,Ben saanane!!

Nasubiri updates za kina pamoja na Kauli rasmi ya Maandamano ya Tar 01.Asiishilie kuwataka wananchi katika maandamano tu,bali nitafarijika kama atasema tutakuwa Mstari wa mbele na wake zetu,Nategemea siku hiyo kumuona Mama Lowassa,Mama Mbowe,Mama Lissu na wake za viongozi woote wa UKUTA.
Kwani kila anayeandamna atakuja na mke wake?
 
Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia


-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola
Ujinga hawawezi kutudanganya tena this tm watakula kichapo
 
Back
Top Bottom