Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Hotuba ya Freeman Mbowe. Amuonya Vikali Rais Magufuli

Mbowe Mungu ampe maisha marefu ni kiongozi mwenye busara na hekima anayeheshimika ndani ya nchi na nje ya nchi kwenye hotuba zake ameongea ukweli operesheni #UKUTA maandalizi yanaendelea kama ilivyopangwa hakuna kurudi nyuma.
AMEEEEEN AMEEEEEN AMEEEEEN
 
hivzo pHD zenu zinatsaidia nini sasa wakati watu wanalia njaa tu mtaani
kwa hyo unataka kumaanisha elimu aliyonayo tundu lissu haisaidii chochote kisa tu mtaani kuna njaa wekiwemo wananchi wa jimbo lake
 
Hotuba ya Freeman Mbowe:Naweletea Live Updates sehemu ya kwaza ya Hotuba hii.Sehemu ya kwanza pia wanahabari wamealikwa na Sehemu ya pili ni kikao cha ndani.

Updates:
-Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

-UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia


-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola
Ccm wanaendelea na siasa kama kawaida,wajumbe wa mitaa wa ccm wanapita nyumba hadi nyumba kuandikisha wanachama na kuchukua namba za kadi za kupiga kura hapa hapa DSM,juzi msururu wa pikipiki na bendera za ccm Kawe.Hivyo wana ukawa msidanganywe na kauli eti siasa zimesimama,nanyi mjipange kuwa na wajumbe wa kila nyumba 5 Tanzania nzima.Maandamano hayatasaidia dawa ni kwenda katika grass root haswa vijijini.


Ben Saanane
 
Kabla tarehe 1/9 usishangae viongizi wengi wa CDM wakaswekwa lupango.
 
Hahahhaha huyu mchagga ni hatari mbona sioni sehemu alipo jipa jukumu hata moja?

Hahahaha eti Lissu anabaki makao makuu kuandaa mashitaka ... Sasa kwanini na yeye asiandamane?
 
Mwambie mwenyekiti ajumuike na sisi kwenye maandamano siyo tupigwe sisi yeye akituangalia kwenye TV tu na familia yake
Mwambie na baba jessica ckuhiyo aje akiwa na polisi na yeye ashike kirungu na bunduki kuzuia maandamano c kila cku tu yeye anakaa kwenye tv na kudai hajaribiwi wakati hata kushika rungu hajui
 
Mbowe Mungu ampe maisha marefu ni kiongozi mwenye busara na hekima anayeheshimika ndani ya nchi na nje ya nchi kwenye hotuba zake ameongea ukweli operesheni #UKUTA maandalizi yanaendelea kama ilivyopangwa hakuna kurudi nyuma.
Si mkaandamane kelele za nn
 
Hahahhaha huyu mchagga ni hatari mbona sioni sehemu alipo jipa jukumu hata moja?

Hahahaha eti Lissu anabaki makao makuu kuandaa mashitaka ... Sasa kwanini na yeye asiandamane?
Kwanini baba jessica nae asishike rungu kuwasaidia polisi kuzuia maandamano???
 
Mimi Siku Hiyo nitakua nimepozi kideoni nacheka wana wanakula kichapo na kuswekwa kwenye kalandinga kwenda kusomewa mashitaka 26.Ila nitaenjoy Sana Kama DJ atakua mbele ili nishuhudie wanavyomkata makofi.
 
Ben ndio msemaji wa Chadema, makene yupo yupo tu hajui nini kinaendelea.
Makene wakati unaajiliwa ungesema wewe ni mchaga sasa unaona kazi zako anapewa mchaga mwenzao.
 
Kile kipengere kinacho zuia Mwanachama wa chadema kwenda mahakamani, mbona kina vunja katiba ya Nchi.. Mbowe na vifaranga wako usiwe na double standard katika mambo ya sheria
Wewe ndiye kifaranga cha lumumba pamoja na ukoo wako wa panya
 
Tatizo chadema imejaa vihiyo.
Huku dj huku kuna mtaalam wa sanaa
 
Back
Top Bottom