Hotuba nzima ya Mwalimu Nyerere alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,023
..Rafiki yangu amenitumia hotuba hii nikaona itapendeza kama nita-share na wana JF.


TANGAZO LA VITA LA MWALIMU NYERERE DHIDI YA IDDI AMIN WA UGANDA:




" Ndugu wananchi nimewaomba hapa niwaelezeni jambo ambalo kwa sasa wote mnalijua, lakini si vibaya nikalieleza. Nitajitahidi kulieleza kwa kifupi.

Wakati nilipokuwa Songea katika ziara kuanza juma la pili la mwezi uliopita, ilitangazwa habari kutoka Uganda kwamba jeshi la Tanzania limeingia Uganda na limechukua sehemu kubwa na linaua watu ovyo. Siku hiyo ulipotangazwa uongo huo nilikuwa nimealikwa chakula na vijana wetu pale Songea. Kwa hiyo jioni nikachukua nafasi hiyo kukanusha uongo huo. Na kwa kweli kuwashutumu na kuvishutumu vile vyombo vya habari duniani ambavyo vimependa sana kutangaza uongo wa Amin. Bora atamke uogo na wao hurukia na kuutangaza kana kwamba ni kweli. Huo ndio uliokuwa uongo wake wa kwanza na aliendeleaendelea.


Baadaye akabadilika sura ya uongo wa pili katika shabaha hiyohiyo kwamba Watanzania bado wako Uganda wanapiga watu huko wanauwa na sasa wanasaidiwa na majeshi kutoka CUBA huo ndio ulikuwa uongo, nao tuliukanusha.


Kwa hiyo alivyozidi kusema habari hizo za uongo tuliendelea kuzikanusha na kuzipuuza. Kwa kweli tulikanusha na kupuuza uongo mzima. Lakini Alhamisi akatuma ndege zikaja Bukoba. Hizo ndege zilikuwa ndege za kivita. Vijana wetu wakazitupia risasi zikaruka. Siku hiyo zikarudi tena. Vijana wetu wakazitupia risasi zikakimbia, moja ikaangushwa siku hiyo ya Alhamisi.

Ijumaa zikaja ndege za kivita eneo la Kyaka, zikatupa mabomu. Vijana wetu wakazitupia risasi mbili zikaangushwa. Wakati huo huo kwa bahati mbaya ndege zetu zilizokuwa zinatoka hapa Dar Es Salaam kwenda Mwanza. Kwa bahati mbaya zilikosea katika kutua katika hali ya giza kwenye kiwanja cha Mwanza. Hizi ndege zilikosea na zilitaka kujaribu tena kutua lakini zinakwenda kasi sana, ziligeukia Musoma ili nadhani kutaka zirudi tena zije zijaribu kutua.


Katika maeneo yale tangu Idi Amin alipokwisha kutangaza uongo huo, ni dhahiri tunapuuza ule uongo lakini hatuwezi kupuuza yote. Kwa hiyo vijana wetu walikuwa wameisha ambiwa kwamba ndege za kivita zikionekana zipigwe katika miji yote. Kama zile za Bukoba zilivyopigwa, na za Kyaka zilivyopigwa, hizi nazo zilipofika Musoma kwa bahati mbaya wakadhani ni za adui, zikapigwa. Tukapoteza ndege tatu. Lakini katika mambo ya kivita mambo ya vita ajali zinatokea. Vijana hawa walikwisha ambiwa zikionekana ndege wapige. Wangeliziachia wanajuaje pengine ni za adui. Kwa hiyo ikatokea bahati mbaya hiyo. Matukio hayo hayakutangazwa kwasababu hatukutaka jambo lenyewe kulipa uzito mno. Tulisema akiendelea kuleta hizi ndege zake tutaendelea kuziangusha. Yeye ataendelea kuongopa lakini hizi ndege tutaziangusha kila zinavyokuja. Uwezo wa kuziangusha upo na mwenyewe alijua kwamba uwezo upo ni vizuri akijua yeye.

Tulikuwa tunaepuka kulipa uzito jambo hili ambalo mwanzo wake ni uongo kabisa kwa kuzua. Kwa hiyo uongo wake akaendelea na tukazidi kuukana na haya matukio ambayo yalikuwa ni ya kweli nasema hatukuyatangaza kwa sababu hiyo niliyoeleza.

Sasa Jumatatu ndipo akavamia nchi yetu. Akaingiza majeshi yake kwa nguvu kubwa yakachukua kasehemu kakubwa, yakaingia ndani mpaka Kyaka. Hii tulitangaza kwasababu ilikuwa jambo la kweli. Yeye kama kawaida yake akakana, akasema haikutokea hivyo. Akaendelea kusema tu kwamba Watanzania wao ndio wapo Uganda ndio wamechukua sehemu za Uganda. Akakana ukweli huo. Lakini tutawaeleza jamaa pamoja na Mabalozi waliopo Dar Es Salaam kwamba huu ndiyo ukweli. Huyu mtu amevamia nchi yetu.


Sasa jana ametangaza mwenyewe kwamba ni kweli majeshi yake yameivamia nchi yetu na yamechukua sehemu hiyo ya Tanzania iliyo kaskazini mwa mto Kagera, na kwamba tangu sasa eti sehemu hiyo ni ya Uganda na itatawaliwa kijeshi kama inavyotawaliwa Uganda. Ndivyo alivyotangaza mwenyewe. Sisi ametusaidia katika kutangaza kutangaza jambo hilo kusudi sasa, kwa sasa ubishi uishe, iwe tena hatuna tatizo la kuwaambia watu wenye akili duniani ni nini kimetokea.


Sasa hiyo ndiyo hali, tafanye nini. Tunayo kazi moja. Watanzania sasa ni kumpiga. UWEZO wa kumpiga tunao. SABABU ya kumpiga tunayo. Na NIA ya kumpiga tunayo. Tunataka dunia ituelewe hivyo kwamba hatuna kazi nyingine, na tunawaomba marafiki zetu wanaotuambia maneno ya suluhu waache maneno hayo.


Kuchukua nchi ya watu wengine siyo kwamba majeshi yamekosea njia, lakini kusema sehemu hiyo nimeichukua ni kutangaza vita na nchi ule ingine na si sisi tuliofanya hivyo. Amefanya mwendawazimu, na amefanya hivyo katika jambo ambalo aliwahi kutangaza zamani, aliwahi kusema zanamini kidogo kwamba mpaka wa haki ya Uganda na Tanzania ni mto Kagera na siku moja atachukua sehemu hiyo. Ametimiza hivyo sasa. Rafiki zetu kama ni marafiki wa kweli watataka tumwondoe mtu huyu, hawawezi kutuomba suluhu au jambo la ajabu kabisa kwamba tuondoe turudishe majeshi yetu. Tuyarudishe wapi?


Kwa hiyo nasema tunayo kazi moja, hatukupenda kufanya hivyo. Maadui zetu ni mabeberu na kwa sasa hivi wako kusini. Serekali ya Afrika hata kama tunapokuwa hatupendi vitendo vya viongozi wao hatuwahesabu kwamba ni adui zetu. Na kama Amin angekuwa anasema tu kwamba Tanzania ni adui wetu sisi tungeendelea kumpuuza kama ni maneno tu, lakini kufanya hasa kitendo cha uadui sasa tumfanye adui. Na amekuja mwenyewe ameingia Tanzania mwenyewe na mtu huyu ni mshenzi, ameua watu wengi sana. Kwa hiyo nasema tunayo kazi moja, tutampiga.

Vijana wetu wako mpakani sasa hivi, wako kule. Wako kule mapambano yanaendelea. Sasa haya si mapambano ya vijana wa TPDF ni yetu wote. Kwa hiyo ninachowaombeni wananchi wote kwanza ni kuelewa hiyo kazi iliyo mbele yetu. Pili, tuwasaidie vijana, kila mtu kwa mahali alipo. Tutaendelea, kila tunavyoendelea tutaeleza nini la kufanya, na nani afanye nini tutaelezana wakati wote.


Tunamuondoa huyu nyoka katika nyumba yetu. Tunawaomba mtulie.Katika mambo haya ya vita na hasa kama watu mlikuwa mmezoea amani mnaweza kubabaika sana. Msibabaike, tulieni, fanyeni kazi kama kawaida, eleweni vitendo tutakavyovifanya. Mtaona vitendo tutakavyofanya tangu sasa mpaka hapo kazi itakapokuwa imekwisha. Lakini mjue vitendo hivyo kazi yake ni ni hiyo moja ya kumpiga mshenzi huyu aliyekuja katika nchi yetu. Asanteni sana. " -- Julius Kambarage Nyerere


cc Jasusi, Nguruvi3, Shwari, Kichuguu, Pascal Mayalla, Kiranga, Nyani Ngabu, tindo, BAK, albuluushiy , JERUSALEMU , The Boss, Ghostshadow , Mtukudzi
 
Kambarage alikuwa Genius sana , hata kama ni propaganda alikuwa anazipanga na kupangika sio siku hizi Propangadist Mkuu wa Taifa ni Musiba hata kupangilia floor ya Mazungumzo hajui

Hayati Mzee Kingunge angekuwa hai angekuwa anatushushua sana au kutucheka tukikutana nae kwa namna tunavyopika propaganda kwa namna ambayo huhitaji walau cheti cha Ngumbaru kujua ni uongo
 
Nakumbuka wakati huo Niko sekondari hamasa ilikuwa kubwa sana sio wapiganaji tuu, bali hata wafanyakazi,wakulima na sisi wanafunzi. Mkulima kuchangia magunia ya mahindi haikuwa hoja wala mfugaji kutoa ng'ombe pia haikuwa ajabu.
Nchi ilikuwa moja na wala hakukuwa na ubaguzi wa dini, wala kabila na maeneo.
Tuwe wakweli jee nchi ikiangukia vitani Leo tutakuwa salama kweli na hizi chuki za ndani?
 
Kwanini asidhalikishwe wakati yeye anamdhalilisha Rais?
Kanali mstaafu, Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mwenyekiti mstaafu wa Kamati ya Ushindi ya Ccm kwa robo karne 1992-2017, Katibu Mkuu mstaafu wa Chama tawala anadhalilishwa na Mtangazaji wa zamani wa Chennel ten

Kweli hujafa hujaumbika
 
Tumeenda Egypt tu kuna wengine Mengi ya kwanza walikuwa Senegal, ya pili wakawa wa Algeria na ya tatu wakawa wa Kenya

Hakuna kabisa Uzalendo siku hizi


Kuna watu hata kile Kimbunga cha Madagascar kilivyotukosa kosa wakasikitika

..yote hiyo ni kwasababu watawala wanawatendea baadhi ya waTz kana kwamba ni haramu ktk nchi hii.

..wanapompandisha mtu kama Mbowe kwenye karandinga kana kwamba ni mhaini wanafikiri wapenzi, wafuasi, na wanachama wa chama chake wanajisikiaje?
 
..yote hiyo ni kwasababu watawala wanawatendea baadhi ya waTz kana kwamba ni haramu ktk nchi hii.

..wanapompandisha mtu kama Mbowe kwenye karandinga kana kwamba ni mhaini wanafikiri wapenzi, wafuasi, na wanachama wa chama chake wanajisikiaje?

Sio sababu ya msingi hiyo

Egypt Rais wao kidemokrasia kateswa mpaka Kafia Kizimbani ( Mohamed Mursi) na walikuwa wanampenda kweli kweli lakin haijafanya wasiwe na Mapenzi na Team yao ya Taifa

Kwa hoja yako inaonekana wengi wenu hamjui tofauti ya Taifa na Serikali
 
Sio sababu ya msingi hiyo

Egypt Rais wao kidemokrasia kateswa mpaka Kafia Kizimbani ( Mohamed Mursi) na walikuwa wanampenda kweli kweli lakin haijafanya wasiwe na Mapenzi na Team yao ya Taifa

Kwa hoja yako inaonekana wengi wenu hamjui tofauti ya Taifa na Serikali

..Egypt kuna makundi ya kigaidi.

..At least waTz wako waliosusia timu ya taifa kuliko kuwa extremists.
 
Back
Top Bottom