Hotuba nzima ya Mwalimu Nyerere alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin

..na askari waliokwenda mstari wa mbele tuwaiteje?

..kuna vijana waliomaliza form 6 wakaenda jkt na kutoka huko wakaenda vitani.

..wapo makamanda walioongoza vita hiyo. Je, tunawakumbuka?

..kwa mfano yuko Gen.Tumainieli Kiwelu ambaye alipewa jukumu la ku-mobilize jeshi la kutekeleza operation ya kuondoa majeshi ya Amini ktl ardhi yetu. Je, tunamuezi? Je, kuna ipo kambi ya jeshi iliyopewa jina lake?

..yuko Brig.Ahmed Kitete [ rip]ambaye vitabu mbalimbali vinamtaja kama operation commander wa zoezi la kuyafukuza majeshi ya uvamizi. Je, tunamuenzi?

..yupo Kanali Rajabu aliyeongoza kikosi cha wahandisi kujenga daraja la muda ili askari wetu na vifaa vyao wavuke mto Kagera. Iddi Amini alilipua na kuvunja daraja la mto Kagera. Je, tuna kumbukumbu naye?

..Kwa ujumla, kuna kumbukumbu yoyote kwa ajili ya tukio hili? Tunawakumbuka waliopoteza maisha? Tunawatunza mashujaa waliorudi, haswa waliopata vilema?
Hii nayo ni kazi yako ,si kila kitu akimalize yule aliyekupatia hotuba ya Mwalimu Nyerere , kutukumbusha watu muhimu waliolisaidia Taifa letu Tanzania. Tusinung'unike tu tusaidiane pale tunapoona mapumgufu.
 
Nakumbuka wakati huo Niko sekondari hamasa ilikuwa kubwa sana sio wapiganaji tuu, bali hata wafanyakazi,wakulima na sisi wanafunzi. Mkulima kuchangia magunia ya mahindi haikuwa hoja wala mfugaji kutoa ng'ombe pia haikuwa ajabu.
Nchi ilikuwa moja na wala hakukuwa na ubaguzi wa dini, wala kabila na maeneo.
Tuwe wakweli jee nchi ikiangukia vitani Leo tutakuwa salama kweli na hizi chuki za ndani?
Siku hizi, si taifa moja tena.
Mfano taifa stars, walifanikiwa kuwagawa Watz.
Mwendo wa wao na sisi.
 
Tuwekee na audio mkuu
..Rafiki yangu amenitumia hotuba hii nikaona itapendeza kama nita-share na wana JF.

TANGAZO LA VITA LA MWALIMU NYERERE DHIDI YA IDDI AMIN WA UGANDA:

" Ndugu wananchi nimewaomba hapa niwaelezeni jambo ambalo kwa sasa wote mnalijua, lakini si vibaya nikalieleza. Nitajitahidi kulieleza kwa kifupi.

Wakati nilipokuwa Songea katika ziara kuanza juma la pili la mwezi uliopita, ilitangazwa habari kutoka Uganda kwamba jeshi la Tanzania limeingia Uganda na limechukua sehemu kubwa na linaua watu ovyo. Siku hiyo ulipotangazwa uongo huo nilikuwa nimealikwa chakula na vijana wetu pale Songea. Kwa hiyo jioni nikachukua nafasi hiyo kukanusha uongo huo. Na kwa kweli kuwashutumu na kuvishutumu vile vyombo vya habari duniani ambavyo vimependa sana kutangaza uongo wa Amin. Bora atamke uogo na wao hurukia na kuutangaza kana kwamba ni kweli. Huo ndio uliokuwa uongo wake wa kwanza na aliendeleaendelea.

Baadaye akabadilika sura ya uongo wa pili katika shabaha hiyohiyo kwamba Watanzania bado wako Uganda wanapiga watu huko wanauwa na sasa wanasaidiwa na majeshi kutoka CUBA huo ndio ulikuwa uongo, nao tuliukanusha.

Kwa hiyo alivyozidi kusema habari hizo za uongo tuliendelea kuzikanusha na kuzipuuza. Kwa kweli tulikanusha na kupuuza uongo mzima. Lakini Alhamisi akatuma ndege zikaja Bukoba. Hizo ndege zilikuwa ndege za kivita. Vijana wetu wakazitupia risasi zikaruka. Siku hiyo zikarudi tena. Vijana wetu wakazitupia risasi zikakimbia, moja ikaangushwa siku hiyo ya Alhamisi.

Ijumaa zikaja ndege za kivita eneo la Kyaka, zikatupa mabomu. Vijana wetu wakazitupia risasi mbili zikaangushwa. Wakati huo huo kwa bahati mbaya ndege zetu zilizokuwa zinatoka hapa Dar Es Salaam kwenda Mwanza. Kwa bahati mbaya zilikosea katika kutua katika hali ya giza kwenye kiwanja cha Mwanza. Hizi ndege zilikosea na zilitaka kujaribu tena kutua lakini zinakwenda kasi sana, ziligeukia Musoma ili nadhani kutaka zirudi tena zije zijaribu kutua.

Katika maeneo yale tangu Idi Amin alipokwisha kutangaza uongo huo, ni dhahiri tunapuuza ule uongo lakini hatuwezi kupuuza yote. Kwa hiyo vijana wetu walikuwa wameisha ambiwa kwamba ndege za kivita zikionekana zipigwe katika miji yote. Kama zile za Bukoba zilivyopigwa, na za Kyaka zilivyopigwa, hizi nazo zilipofika Musoma kwa bahati mbaya wakadhani ni za adui, zikapigwa. Tukapoteza ndege tatu. Lakini katika mambo ya kivita mambo ya vita ajali zinatokea. Vijana hawa walikwisha ambiwa zikionekana ndege wapige. Wangeliziachia wanajuaje pengine ni za adui. Kwa hiyo ikatokea bahati mbaya hiyo. Matukio hayo hayakutangazwa kwasababu hatukutaka jambo lenyewe kulipa uzito mno. Tulisema akiendelea kuleta hizi ndege zake tutaendelea kuziangusha. Yeye ataendelea kuongopa lakini hizi ndege tutaziangusha kila zinavyokuja. Uwezo wa kuziangusha upo na mwenyewe alijua kwamba uwezo upo ni vizuri akijua yeye.

Tulikuwa tunaepuka kulipa uzito jambo hili ambalo mwanzo wake ni uongo kabisa kwa kuzua. Kwa hiyo uongo wake akaendelea na tukazidi kuukana na haya matukio ambayo yalikuwa ni ya kweli nasema hatukuyatangaza kwa sababu hiyo niliyoeleza.

Sasa Jumatatu ndipo akavamia nchi yetu. Akaingiza majeshi yake kwa nguvu kubwa yakachukua kasehemu kakubwa, yakaingia ndani mpaka Kyaka. Hii tulitangaza kwasababu ilikuwa jambo la kweli. Yeye kama kawaida yake akakana, akasema haikutokea hivyo. Akaendelea kusema tu kwamba Watanzania wao ndio wapo Uganda ndio wamechukua sehemu za Uganda. Akakana ukweli huo. Lakini tutawaeleza jamaa pamoja na Mabalozi waliopo Dar Es Salaam kwamba huu ndiyo ukweli. Huyu mtu amevamia nchi yetu.

Sasa jana ametangaza mwenyewe kwamba ni kweli majeshi yake yameivamia nchi yetu na yamechukua sehemu hiyo ya Tanzania iliyo kaskazini mwa mto Kagera, na kwamba tangu sasa eti sehemu hiyo ni ya Uganda na itatawaliwa kijeshi kama inavyotawaliwa Uganda. Ndivyo alivyotangaza mwenyewe. Sisi ametusaidia katika kutangaza kutangaza jambo hilo kusudi sasa, kwa sasa ubishi uishe, iwe tena hatuna tatizo la kuwaambia watu wenye akili duniani ni nini kimetokea.

Sasa hiyo ndiyo hali, tafanye nini. Tunayo kazi moja. Watanzania sasa ni kumpiga. Uwezo wa kumpiga tunao. Sababu ya kumpiga tunayo. Na nia ya kumpiga tunayo. Tunataka dunia ituelewe hivyo kwamba hatuna kazi nyingine, na tunawaomba marafiki zetu wanaotuambia maneno ya suluhu waache maneno hayo.

Kuchukua nchi ya watu wengine siyo kwamba majeshi yamekosea njia, lakini kusema sehemu hiyo nimeichukua ni kutangaza vita na nchi ule ingine na si sisi tuliofanya hivyo. Amefanya mwendawazimu, na amefanya hivyo katika jambo ambalo aliwahi kutangaza zamani, aliwahi kusema zanamini kidogo kwamba mpaka wa haki ya Uganda na Tanzania ni mto Kagera na siku moja atachukua sehemu hiyo. Ametimiza hivyo sasa. Rafiki zetu kama ni marafiki wa kweli watataka tumwondoe mtu huyu, hawawezi kutuomba suluhu au jambo la ajabu kabisa kwamba tuondoe turudishe majeshi yetu. Tuyarudishe wapi?

Kwa hiyo nasema tunayo kazi moja, hatukupenda kufanya hivyo. Maadui zetu ni mabeberu na kwa sasa hivi wako kusini. Serekali ya Afrika hata kama tunapokuwa hatupendi vitendo vya viongozi wao hatuwahesabu kwamba ni adui zetu. Na kama Amin angekuwa anasema tu kwamba Tanzania ni adui wetu sisi tungeendelea kumpuuza kama ni maneno tu, lakini kufanya hasa kitendo cha uadui sasa tumfanye adui. Na amekuja mwenyewe ameingia Tanzania mwenyewe na mtu huyu ni mshenzi, ameua watu wengi sana. Kwa hiyo nasema tunayo kazi moja, tutampiga.

Vijana wetu wako mpakani sasa hivi, wako kule. Wako kule mapambano yanaendelea. Sasa haya si mapambano ya vijana wa TPDF ni yetu wote. Kwa hiyo ninachowaombeni wananchi wote kwanza ni kuelewa hiyo kazi iliyo mbele yetu. Pili, tuwasaidie vijana, kila mtu kwa mahali alipo. Tutaendelea, kila tunavyoendelea tutaeleza nini la kufanya, na nani afanye nini tutaelezana wakati wote.

Tunamuondoa huyu nyoka katika nyumba yetu. Tunawaomba mtulie.Katika mambo haya ya vita na hasa kama watu mlikuwa mmezoea amani mnaweza kubabaika sana. Msibabaike, tulieni, fanyeni kazi kama kawaida, eleweni vitendo tutakavyovifanya. Mtaona vitendo tutakavyofanya tangu sasa mpaka hapo kazi itakapokuwa imekwisha. Lakini mjue vitendo hivyo kazi yake ni ni hiyo moja ya kumpiga mshenzi huyu aliyekuja katika nchi yetu. Asanteni sana. " -- Julius Kambarage Nyerere

cc Jasusi, Nguruvi3, Shwari, Kichuguu, Pascal Mayalla, Kiranga, Nyani Ngabu, tindo, BAK
 
Kwa jinsi mkoa wa kagera ulivyoaribiwa hasa misenyi na Bukoba mkoa huu ungekuwa mbovu Sana.

Lakini mkoa umesimama na kurecover Kwa muda mfupi.

Na kuwajulisha watz zaidi ya 1500 waliuawa Kwa kuvamiwa katika wilaya za Bukoba na misenyi.
Huku kiwanda cha kagera sugar kikilipuliwa kabisa
 
Nataka kuwaeleza jambo ambalo mnalijua lakini si vibaya nikalieleza. Ni vibaya ndio, unapoteza muda, ya nini utueleze jambo ambalo umesema tunalijua? Horrible communication skills...

Watanzania wametungua ndege tatu zao wenyewe, Nyerere anasema "wangefanyaje, vipi kama angekuwa adui... ajali zinatokea... walikuwa wamepewa order ya kutungua..."

Kama kuna order ya kutungua ndege yeyote itakayoonekana angani kwa nini unaweka ndege zenu angani?

Halafu unasema hamkutaka kuyatangaza haya ya kutungua ndege zenu wenyewe kwa vile hamkutaka kulipa suala hilo uzito. Raia (sijui ndege za jeshi, sijui za raia) wamekufa? Ndege tatu zimeangushwa? Unasema si jambo zito? Most horrendous communications skills ever...

Hata Marekani huwa wanajitungua wenyewe kwa bahati mbaya lakini huwezi kusikia rais wa nchi inayojielewa kama ile anasema "sasa wangefanyaje... ajali vitani kawaida..."!

Halafu war declaration makini lazima zieleze alternative steps ulizochukua kuepuka vita... Nyerere anasema hatutaki kusikia mambo ya suluhu!

The most terrible war declaration speech in all of history.

Eti ndege za Amin tulikuwa tunazitungua kwa risasi!

Nikupongeze kwa kuwa na ujasiri wa kwenda kinyume na mawazo ya kadamnasi. Najua hilo siyo jambo dogo.

Ni kweli, kuna mswali ya kujiuliza kuhusu zile ndege zetu zilizotunguliwa. Maelezo aliyotoa Mwalimu yanaleta maswali mengi baadhi ni hayo uliyoyaorodhesha. Swali la kwanza ni? Je zilikuwa za abiria au za kijeshi?

Pili tukumbuke wanasemaga historia huandikwa na washindi (History is written by the victors). Kwa maana hiyo ni muhimu kuwa makini tunapojadili haya mambo ili kuujua ukweli halisi usio na chenga ya uzalendo au propaganda.

Niliwahi kuambiwa sehemu hiyo ya Kagera ambayo Idd Amin anashutumiwa kutaka kuichukua tayari kwa kiasi kikubwa ilikuwa na muingiliano sana na Waganda. Kwa akili ya kawaida, ilikuwa haimake sense kwa Amin kwenda kuipiga mabomu ili kuichukua. Ukweli ni upi?

Pia tukumbuke Amin na Nyerere walikuwa wanafanana sana. Najua wengi mnaweza kushtuka kwa hili nililosema lakini ukiangalia misimamo yao kuhusu mambo ya kimataifa, walikuwa (au walitakiwa kuwa) upande mmoja. Inafika wakati unajiuliza, tofauti zao hasa zilikuwa ni nini na kitu gani hasa kilikuwa chanzo hasa cha ugomvi wao? Ndiyo maana nikasema tuwe makini na wakweli tunapojadili mambo ya historia kama haya. Vitu vingine watu wanaogopa kusema wanabaki kunong'onezana tu.

Haina tofauti sana na tofauti za Magufuli na Lissu. Inawezekana kabisa wajukuu zetu wakafundishwa kuwa Lissu alikuwa kibaraka wa mabeberu, ila je huo ndiyo ukweli? Tayari kuna ambao wanajisahaulisha na wanataka tusahau harakati zote za Lissu za miaka yote kupinga mikataba mibovu. Wakati anafanya hayo wao walikuwa upande wa pili wakimfungulia makesi. Na sasa tayari wameanza kutamka maneno hayo ya ukibaraka bila aibu, sasa waza miaka 40 kutoka sasa watasema nini juu yake.

Historia huandikwa na washindi. Kumbukeni hilo.
 
Sio sababu ya msingi hiyo

Egypt Rais wao kidemokrasia kateswa mpaka Kafia Kizimbani ( Mohamed Mursi) na walikuwa wanampenda kweli kweli lakin haijafanya wasiwe na Mapenzi na Team yao ya Taifa

Kwa hoja yako inaonekana wengi wenu hamjui tofauti ya Taifa na Serikali
Watanzania ni wanafiki wa kiwango cha SGR, humu jukwaani kuna watu walikuwa hawataki Taifa Stars ifuzu eti kwa kigezo kwamba Makonda ndio kiongozi wa kamati.

Hatuichukulii kwa uzito maana ya neno uzalendo, waafrika wenzetu wanajua kuweka mipaka kati ya Taifa na Serikali.

Utotoni tukiwa shule za msingi kulikuwa na zile bendi za shule, mkiwa mstarini kabla hamjatawanyika kwenda madarasani bendi ya shule iliongoza nyimbo za kizalendo.

Hawa vijana wa smartphone na instagram hawajapitishwa katika misingi ya uzalendo, ndio maana hawaelewi maana na uzito wa bendera na wimbo wa Taifa.
 
nashangaa starz inapigwa tatu mtu anaandika,nashukuru Mungu.
 
Watanzania ni wanafiki wa kiwango cha SGR, humu jukwaani kuna watu walikuwa hawataki Taifa Stars ifuzu eti kwa kigezo kwamba Makonda ndio kiongozi wa kamati.

Hatuichukulii kwa uzito maana ya neno uzalendo, waafrika wenzetu wanajua kuweka mipaka kati ya Taifa na Serikali.

Utotoni tukiwa shule za msingi kulikuwa na zile bendi za shule, mkiwa mstarini kabla hamjatawanyika kwenda madarasani bendi ya shule iliongoza nyimbo za kizalendo.

Hawa vijana wa smartphone na instagram hawajapitishwa katika misingi ya uzalendo, ndio maana hawaelewi maana na uzito wa bendera na wimbo wa Taifa.

..Mohamed Ali alikataa kwenda vitani Vietnam akipinga vitendo vya ubaguzi dhidi ya watu weusi.

..Je, kufanya hivyo alikuwa amekosa uzalendo kwa nchi yake?

..Siyo kweli kwamba vijana hawaipendi nchi yao. Kinachowakwaza ni ubaguzi, udhalilishaji, na ukatili, unaofanywa dhidi ya wafuasi na viongozi wa upinzani.
 
Utotoni tukiwa shule za msingi kulikuwa na zile bendi za shule, mkiwa mstarini kabla hamjatawanyika kwenda madarasani bendi ya shule iliongoza nyimbo za kizalendo.

uzalendo my foot, zile nyimbo za mstarini zilikuwa propaganda za chama tu... Ooh, Zidumu fikra za Mwenyekiti, Oooh, Kambona kaolewa Ulaya, Oooh mabeberu this makabaila that... wakati the whole existence of Tanzania ilikuwa bankrolled by the West, Tanzania was the biggest recipient of foreign aid in all of Sub-Saharan Africa, Nyerere kafukuzwa Ikulu na wanajeshi kutoka Calito Barracks, akafanyaje? Akaita ndege za Beberu Mwingereza zike kumuokoa.

Kambona akaenda pale Mlalakuwa kutuliza wanajeshi. Baadae shuleni tunaimbishwa Kambona kaolewa na mabeberu. Kumbe wametofautiana siasa za vijiji vya ujamaa!

Hawa wakina Bernard Membe wanaosema imendikwa wapi Rais wa CCM hapingwi, Tundu Lissu anaepigwa risasi kwa kukosoa dola, Kinana ambae hamuogopi mwenyekiti wa chama, ndio kina Oscar Kambona wa leo hawa, tunaambiwa ni maajenti wa mabeberu kumbe wanasiasa wenzao tu wametofautiana au wamewazidi hoja...

So much for "Baba wa Taifa..." Watanzania wamekufa, wamepigana makombora wenyewe kwa uzembe wa Brigedia aliyesema tungua chochote cha angani halafu akaweka ndege zetu angani, Mwalimu unatutangazia kwa mara ya kwanza, husemi hata pole wananchi, pole wanajeshi, unasema "sasa wangefanyaje, wametumwa kutungua...ajali kawaida...."

Eti una jambo la kutuambia ambalo tayari tunalijua, ndege zetu tumezitungua wenyewe! Tunalijua vipi wakati umesema lilifanywa siri?? Na kama tunalijua tayari then you are wasting out time and national attention re-telling it to us again!!!! hahahaaaaaa... Afrika hatuna bahati ya viongozi wanao think logically...
 
Habari kubwa ya kwangu ya kwanza kuisikia live tena nikiwa bado mtoto mdogo sana ni ile ya ndege iliyoua marais wawili wa Rwanda na Burundi. Nakumbuka sana wazazi wangu walikuwa makini sana kufuatilia habari ile. Aidha nakumbuka niliambiwa kuwa Nyerere alikuwa amemuhifadhi Obote hali iliyompa mashaka sana Idd Amin. Upo uwezekano kuwa aliyeanzisha chokochoko ni Nyerere!
 
Nakumbuka wakati huo Niko sekondari hamasa ilikuwa kubwa sana sio wapiganaji tuu, bali hata wafanyakazi,wakulima na sisi wanafunzi. Mkulima kuchangia magunia ya mahindi haikuwa hoja wala mfugaji kutoa ng'ombe pia haikuwa ajabu.
Nchi ilikuwa moja na wala hakukuwa na ubaguzi wa dini, wala kabila na maeneo.
Tuwe wakweli jee nchi ikiangukia vitani Leo tutakuwa salama kweli na hizi chuki za ndani?
Tutawaachia akina musiba na genge lao la ubaguzi
 
K
Nakumbuka wakati huo Niko sekondari hamasa ilikuwa kubwa sana sio wapiganaji tuu, bali hata wafanyakazi,wakulima na sisi wanafunzi. Mkulima kuchangia magunia ya mahindi haikuwa hoja wala mfugaji kutoa ng'ombe pia haikuwa ajabu.
Nchi ilikuwa moja na wala hakukuwa na ubaguzi wa dini, wala kabila na maeneo.
Tuwe wakweli jee nchi ikiangukia vitani Leo tutakuwa salama kweli na hizi chuki za ndani?
Saizi Mkuu kuna mpasuko sana,Siasa ya vyama vingi imeleta tofauti japo mambo mengi ya kitaifa huwa tunakuwa pamoja mfano ni matamshi ya Jaguar
 
..imenibidi nitafute hotuba ya Amiri Jeshi Mkuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
K

Saizi Mkuu kuna mpasuko sana,Siasa ya vyama vingi imeleta tofauti japo mambo mengi ya kitaifa huwa tunakuwa pamoja mfano ni matamshi ya Jaguar

..tatizo kuna ndugu zetu ambao bado hawakubaliani na mfumo wa vyama vingi.

..hao ndio wanaosababisha mpasuko tunaoshuhudia nchini kwetu sasa hivi.
 
"Nataka kuwaeleza jambo ambalo mnalijua lakini si vibaya nikalieleza." Ni vibaya ndio, unapoteza muda, ya nini utueleze jambo ambalo umesema tunalijua? Horrible communication skills...

Tanzania imetungua ndege tatu zao wenyewe, Nyerere anasema "wangefanyaje, vipi kama angekuwa adui... ajali zinatokea... walikuwa wamepewa order ya kutungua..."

Kama kuna order ya kutungua ndege yeyote itakayoonekana angani kwa nini unaweka ndege zenu angani?

Halafu unasema hamkutaka kuyatangaza haya ya kutungua ndege zenu wenyewe kwa vile hamkutaka kulipa suala hilo uzito. Raia wako wamekufa (sijui za jeshi, sijui commercial flights?) Ndege tatu zimeangushwa? Unasema si jambo zito? Most horrendous communications skills ever...

Hata Marekani huwa wanajitungua wenyewe kwa bahati mbaya lakini huwezi kusikia rais wa nchi inayojielewa akasema "sasa wangefanyaje... ajali vitani kawaida..."!

Halafu war declaration makini lazima ieleze alternative steps ulizochukua kujaribu kuepuka vita... Nyerere anasema "hatutaki kusikia mambo ya suluhu"! The most terrible war declaration speech in all of history.

Eti ndege za Amin tulikuwa tunazitungua "kwa risasi"!!
Aisee!
 
uzalendo my foot, zile nyimbo za mstarini zilikuwa propaganda za chama tu... Ooh, Zidumu fikra za Mwenyekiti, Oooh, Kambona kaolewa Ulaya, Oooh mabeberu this makabaila that... wakati the whole existence of Tanzania ilikuwa bankrolled by the West, Tanzania was the biggest recipient of foreign aid in all of Sub-Saharan Africa, Nyerere kafukuzwa Ikulu na wanajeshi kutoka Calito Barracks, akafanyaje? Akaita ndege za Beberu Mwingereza zike kumuokoa.

Kambona akaenda pale Mlalakuwa kutuliza wanajeshi. Baadae shuleni tunaimbishwa Kambona kaolewa na mabeberu. Kumbe wametofautiana siasa za vijiji vya ujamaa!

Hawa wakina Bernard Membe wanaosema imendikwa wapi Rais wa CCM hapingwi, Tundu Lissu anaepigwa risasi kwa kukosoa dola, Kinana ambae hamuogopi mwenyekiti wa chama, ndio kina Oscar Kambona wa leo hawa, tunaambiwa ni maajenti wa mabeberu kumbe wanasiasa wenzao tu wametofautiana au wamewazidi hoja...

So much for "Baba wa Taifa..." Watanzania wamekufa, wamepigana makombora wenyewe kwa uzembe wa Brigedia aliyesema tungua chochote cha angani halafu akaweka ndege zetu angani, Mwalimu unatutangazia kwa mara ya kwanza, husemi hata pole wananchi, pole wanajeshi, unasema "sasa wangefanyaje, wametumwa kutungua...ajali kawaida...."

Eti una jambo la kutuambia ambalo tayari tunalijua, ndege zetu tumezitungua wenyewe! Tunalijua vipi wakati umesema lilifanywa siri?? Na kama tunalijua tayari then you are wasting out time and national attention re-telling it to us again!!!! hahahaaaaaa... Afrika hatuna bahati ya viongozi wanao think logically...
Kwanini usiwe kiongozi kwa niaba yao?
 
Back
Top Bottom