Hotuba iliyonitoa machozi ya furaha

Fukua

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
546
479
Raisi wa JMT Mama Samia kwanza shikamoo.

Wadau wa JF na Watanzania wote, nina wasalimu kwa jina la JMT.

Mungu anaipenda Tanzania hata amekuchagua wewe Mama kuwa Raisi wetu.
Nimefurahi kwamba huwa unapitia maoni yetu hapa JF.

Nimefurahi kwamba una malengo ya kuijenga Tanzania Mpya ambayo pengine bila katiba Mpya Tanzania haitakuwa Mpya milele.

Mimi ni mkweli Mama, CHADEMA ni waungwana sana ni Watanzania wenzetu hupenda kuungana nasi CCM, lakini kwenye hili tatizo ni sisi CCM.

Sasa umetoa mwelekeo wako huu safi, tunakuahidi tutaungana nao kiasi kwamba hata wewe utashangaa. Watanzania hatushindwi kitu, hili ni dogo sana.

Ni kweli kabisa, tumetoka kwenye tanuru lililowaunguza Watanzania wengi bila kujali vyama vyao na sasa unaendelea kutuponya majeraha, mioyoni mwetu.

Ni ukweli pia, mtu/kiongozi asiyekubali kukosolewa, kushauriwa, na anajiona yeye anajua kila kitu, huyo ni mwendawazimu. Pia ni mwendakuzimu.

Umechagua njia sahihi ya maridhiano na itakufikisha mahali sahihi.

Siasa ni mchezo wa akili na maarifa na ukiambatanishwa na ukweli, huleta mafanikio chanya na siasa safi. Na tukiwa na siasa safi, tutapata maendeleo ya kweli. Kinyume chake ni kujidanganya wenyewe. Na mwisho, uongozi wako hautakuwa na tija kwa watu wako.

Kwa kweli Mama, nimeisikiliza hotuba yako ya leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, umeionyesha dunia kweli wanawake wanaweza. Kubwa zaidi kwangu, nimeisikiliza hotuba yako huku nikibubujikwa na machozi ya furaha.

Mimi kama mwananchi wako, umenigusa sana na ninaiona kwa dhati kabisa Tanzania Mpya iliyo njema, na wewe Mama ukiwa mwasisi wake, na naliona jina la Mama Samia likiandikwa kwenye mioyo ya Watanzania kwa miaka mingi ijayo.

Kama ulivyosema, wahafidhina hawaishi popote, bali watakubaliana na wewe kwa kuona matokeo mazuri.
Watanzania wenye mapenzi mema tunakuunga mkono hadi mwisho wa dahari.

Mungu akulinde na akutangulie katika uongozi wako, usijekuacha njiani bila kutufikisha kwenye Tanzania Mpya.
 
Ni ukweli pia mtu/kiongozi asiyekubali kukosolewa, kushauriwa, na anajiona yeye anajua Kila kitu huyo ni MWENDAWAZIMU Pia ni
Inategemea!

Si kila mwenye kukushauri lazima asikilizwe
 
Siku tukiacha kuridhishwa na maneno ya jukwaani bali vitendo bila maneno Bas tutapata maendeleo!!

Tunetengeneza kizazi cha hovyo kinachoridhika kwa maneno BADALA ya vitendo!!
 
Utofauti wa itikadi za kisiasa,kidini nk isichukuliwe kama ni uadui. Hongera SSH Kwa kutufanya wamoja.
 
Raisi wa JMT Mama Samia kwanza shikamoo.

Wadau wa JF na Watanzania wote, nina wasalimu kwa jina la JMT.

Mungu anaipenda Tanzania hata amekuchagua wewe Mama kuwa Raisi wetu.
Nimefurahi kwamba huwa unapitia maoni yetu hapa JF.

Nimefurahi kwamba una malengo ya kuijenga Tanzania Mpya ambayo pengine bila katiba Mpya Tanzania haitakuwa Mpya milele.

Mimi ni mkweli Mama, CHADEMA ni waungwana sana ni Watanzania wenzetu hupenda kuungana nasi CCM, lakini kwenye hili tatizo ni sisi CCM.

Sasa umetoa mwelekeo wako huu safi, tunakuahidi tutaungana nao kiasi kwamba hata wewe utashangaa. Watanzania hatushindwi kitu, hili ni dogo sana.

Ni kweli kabisa, tumetoka kwenye tanuru lililowaunguza Watanzania wengi bila kujali vyama vyao na sasa unaendelea kutuponya majeraha, mioyoni mwetu.

Ni ukweli pia, mtu/kiongozi asiyekubali kukosolewa, kushauriwa, na anajiona yeye anajua kila kitu, huyo ni mwendawazimu. Pia ni mwendakuzimu.

Umechagua njia sahihi ya maridhiano na itakufikisha mahali sahihi.

Siasa ni mchezo wa akili na maarifa na ukiambatanishwa na ukweli, huleta mafanikio chanya na siasa safi. Na tukiwa na siasa safi, tutapata maendeleo ya kweli. Kinyume chake ni kujidanganya wenyewe. Na mwisho, uongozi wako hautakuwa na tija kwa watu wako.

Kwa kweli Mama, nimeisikiliza hotuba yako ya leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, umeionyesha dunia kweli wanawake wanaweza. Kubwa zaidi kwangu, nimeisikiliza hotuba yako huku nikibubujikwa na machozi ya furaha.

Mimi kama mwananchi wako, umenigusa sana na ninaiona kwa dhati kabisa Tanzania Mpya iliyo njema, na wewe Mama ukiwa mwasisi wake, na naliona jina la Mama Samia likiandikwa kwenye mioyo ya Watanzania kwa miaka mingi ijayo.

Kama ulivyosema, wahafidhina hawaishi popote, bali watakubaliana na wewe kwa kuona matokeo mazuri.
Watanzania wenye mapenzi mema tunakuunga mkono hadi mwisho wa dahari.

Mungu akulinde na akutangulie katika uongozi wako, usijekuacha njiani bila kutufikisha kwenye Tanzania Mpya.
Aamen!
 
Back
Top Bottom