Hotel kubwa Morogoro kubomolewa

Hotel kubwa Morogoro kubomolewa

Ndio maana hii nchi haiendelei. Wachawi kila kona, Mtu unaweza ukadhani wachawi ni wale wanaoruka na ungo usiku, kumbe wengine wanatembelea Kilimo kwanza. Unaanzaje kubomoa jengo kama hilo. Kwani wao walikuwa wapi tangu msingi unaanza kuchimbwa?

Serikali iliyokuwepo haikuwa na meno sasa now n serikali mpya kila aliyetenda kosa atawajibika. Ikombolewe tuu sio eneo la majengo ni sehemu ya wazi tena linapita Bomba la Mafuta
 
Ahaaaaaa.
Mkuu kumbe ni maeneo yako hee!!!!!
Yule jamaa kapiga HELA ndefu sana mpaka sasa.
Bcoz even familia yake nasikia wanaishi kwa Obama.
By the way huku kwema kabisa mkuu.
Ila pale Ngemo bar pasivunjwe maana ugali wa pale na nyama choma saa mbili asubuhi ni balaaaaaa,yani unaenda town uko saaaaafi na lichupa la maji la lita moja na nusu.

Airtel pub ndo eneo langu napiga sana pultable pale, sema siku hizi kuna mziki una kelele sana
 
hao walijenga wamefanya makosa. lakini watendaji wa serikali walikuwa wapi kuzuia huu ujenz kuanzia ujenzi unaanza? kawaida ujenzi wa gorofa lazima halimashauri ijue na inginia wa halmashauri lazima ahusike. walikuwa wapi wote hawa? serikali isiishie tu kumbomolea huyo jamaa bali iende mbele zaidi kuwawajibisha waliohusika na uzembe huu. to sad.
Mjengaji na watoa vibali ni sawa na mtoaji na mpokea rushwa. Jengo livunjwe. Watendaji wawajibishwe.
 
Hivi kama kiwanja kapewa na manispaa na amekitafutia hati, kibali cha ujenzi anacho na kipo kihalali, taratibu zote kafuata..hawezi kuishitaki serikali na kudai fidia kama jengo likibomolewa?
Mjenzi na watoa vibali wachunguzwe. Ila jengo ni haki kubomolewa kama lipo kwenye kiwanja kisicho sahihi.
 
Waende Mtwara maeneo mengi tu yapo wajenge mahekalu kule
 
Hapo mmiliki anatakiwa akimbilie mahakamani kuweka pingamizi. Hakuna mtu aliye juu ya mahakama bana. Kuna jengo kama hili lilitaka kuvunjwa Masaki miaka ya 2007. Serikali yenyewe ili back down na mpaka sasa yale majengo yapo.... Duh kamji ka Morogoro kalishaanza kupendeza,sasa wawekezajai wooote watakimbia...
Mahakamani hata kama ulivunja sheria? Sheria haziangalii kiasi ulicho invest. Hata masikini wamevunjiwa, yeye nani asivunjiwe kama kiwanja si halali?
 
Wataisoma namba!huu uzembe wa watendaji,kutiana hasara tu,waliohusika na uzembe huo wafungwe jela miaka mia.iwe fundisho kwa matajir,kwa mara ya mwisho nimelala humo mwez october chumba 160000 tu.
Kweli kabisa...
 
Sina tatizo na kubomoa kama imejengwa eneo lisilo haki kujengwa, ila waanze na kunyoosha maelezo kwanza kuwa huwa wanakuwa wapi majengo hayo yakijengwa? Adhabu za uzembe kazini zianzie kwao...
 
Watanzania Tujifunze kuishi kwa kufuata sheria ndio tutaendelea, Huu ukanjanja ndio kama hivyo ikija serikali mpya mambo yanabadilika!

Kikwete alikuwa dhaifu, Magufuli ni muumini wa kufuata Sheria!

Sheria huwa zinafuatwa vizuri kwenye nchi zenye mipango, huwez kubomoa mali za watu kwenye nchi ambayo asilimia 80 haijapimwa, bongo hata leo hii ukinunua kiwanja mwaka kesho utaambiwa ni eneo la makaburi
 
Huyo mmriki nae boya tu atafanyaje uwekezaji mkubwa namna hii bila kufanya upembuzi yakinifu? hotel kubwa namna ile unaijenga juu ya bomba la mafuta?? no wonder pesa ya uwekezaji huo itakuwa ni dirtyMONEY

hii nchi ilikuwa imefika sehem ambayo pesa ni kila kitu
 
Imejengwa juu ya bomba LA mafuta LA TAZAMA no lazima ibomorewe tu

Kama ni kweli busara inatakiwa itumike, kwanini hio bomba lisipitishwe pembeni kwa gharama za mwenye hoteli? watu wangapi watapoteza kazi iwapo hiyo hotel itabomolewa? mbona mahakama iliwah kuamuru lile jengo karibu na ocean road libomolewe sababu linachungulia ikulu, lkin nadhan kikwete aliona ni ujinga sijui wakaipotezea, ifike pahala watu tuache roho mbaya ndo maana tunakuwa masikin, me sitaki kuamin kuwa morogoro imejaa kiasi cha kuitafuta hiyo hotel tu ndo haikufuata sheria?
 
Sina tatizo na kubomoa kama imejengwa eneo lisilo haki kujengwa, ila waanze na kunyoosha maelezo kwanza kuwa huwa wanakuwa wapi majengo hayo yakijengwa? Adhabu za uzembe kazini zianzie kwao...

Mbona mnatetea ufisadi!!! Naamini mwenye hiyo hoteli alipata kiwanja kiujanjaujanja na inawezekana pia hana kibali cha ujenzi wa Hoteli ya aina hiyo kwa sehemu kama hiyo, kwa wale wanaoijua vizuri Msamvu ya Morogoro. Imekula kwake ba watu wa aina hiyo.

Tuwe makini kuweka "assets" za kudumu kwenye maeneo yasiyo na uhakika.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Sheria huwa zinafuatwa vizuri kwenye nchi zenye mipango, huwez kubomoa mali za watu kwenye nchi ambayo asilimia 80 haijapimwa, bongo hata leo hii ukinunua kiwanja mwaka kesho utaambiwa ni eneo la makaburi
Huo ni upuuzi... Siwezi kumwaga pesa yangu kwenye sehemu yenye utata kama hiyo, muulize huyo mwenye hotel kama alipata hilo eneo kihalali kama sio kwa ufisadi!

Halafu kesho ukisiki kwa Ujenzi wa hiyo hoteli amezui mkondo wa maji na kusababisha mafuriko yaliangamiza roho kadhaa kwa raia wasio na Hatia sijui utasema nini!
 
Ww ni mtu wa ajabu sana, inawezekana ni wale watu ambao wana mawazo ya kusadikika hujawahi kujenga hata kibanda hujakumbana na changamoto za kununua maeneo yenye matatizo ilihali umeenda hadi jiji kutafuta ukweli, mm sitetei watu wasiofuata sheria lkin ujue kuna watu wanaonewa sana kwene masuala ya ardhi ukiwa hujawahi kukumbana na hizo kadhia mshukuru Mungu wako lkin usituletee theory za darasanai hapa.
 
Alivyosema Rais mstaafu Mkapa wewe ni mmoja wao. Hotel ya thamani KUBWA hivyo mwenyewe alipaswa kujua kama hapo alipojenga ni halali. Naamini ni pesa yake ilimpa kiburi. Ngoja aisome namba.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Hii serikali ya awamu ya 5 tusipokuwa makini itakuwa ya kibabe na kikatili sn!
Busara zinahitajika kwa suala la kujenga juu ya Bomba la Mafuta (Tazama) na eneo la wazi.
Mf. Kuna kuhamisha bomba kwa gharama za mjenzi au kujenga Handaki ardhini kwa ajili ya repair and Maintenance.

Ujinga mwingine wa serikali tusishabikie hovyo hovyo, walikuwa wapi wakati anajenga?
 
Inasemekana hii ni ya yule bosi wa fedha wa zamani
 
Back
Top Bottom