Ulimakafu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 31,824
- 13,781
Huwa siku zote naamini kuwa mwisho wa matatizo yote ya tiba ni hospitali yetu ya taifa Muhimbili.Lakini nimejikuta napata shaka hasa baada ya DCI Robert Manumba kuwa anahudumiwa na hospitali ya binafsi Aga Khan.Kwa kiongozi mkubwa kama huyu nilitaraji apate huduma zake MNH na ikishindikana apelekwe nje.Naambiwa kwa wenzetu waliopiga hatua, hata hospitali za jeshi huwa na huduma daraja la kwanza kabisa hasa inapotokea tatizo la afya kwa viongozi wa ngazi za juu.