Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma imekuwa ya ndugu wa Madaktari, Manesi na Washkaji zao

Prince Chapee

Senior Member
Jul 31, 2017
179
126
Hospitali hii imekuwa ya ndugu wa madaktari, manesi na washkaji zao..

Tangu afe Magufuli huduma za hospitali Rufaa Mkoa wa Ruvuma zinatolewa kwa kujuana sana, ndugu wa watoa huduma hospitalini madaktari na manesi pamoja na washkaji zao wao kwa wao wanaingia na kutoka sisi wengine tumekaa tu kwenye mabenchi tukisubiri wamalize kuhudumiana.

Kama huna ndugu anayefanya kazi hospitali hii utasubiri sana kupata huduma.

Ukiwa na mkono mfupi bila kuwapa buku tano tano manesi fomu zako ziteleze bila vikwazo vya maskini wenzako waliopo kwenye foleni utasubiri sana.

Nimeandika kwa jazba tu, mimi siyo mwandishi wa habari.

Ofisi za malalamiko na zenyewe ni "malalamiko" hazina msaada wowote unaweza ukafa ukisubiri kuhudumiwa.

Ushauri wangu, nendeni na pesa hospitalini ili mpate angalau nafasi ya pili.


=============

UPDATES...

MAJIBU YA HOSPITALI


Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Ruvuma, Dkt. Charles Hinju anafafanua:

Kwa kawaida katika Taasisi yetu kuna maelekezo ya kutoa maoni kuuhusu Hospitalini hao, Wananchi wapo huru kwa kuwa ni Taasisi ya Umma, upande mwingine kuna Kamati inayosimamia ubora wa huduma zinazotolewa.

Hospitali ina vitengo vingi, labda huyo Mdau angefafanua ni sehemu gani alipokutana na changamoto hiyo ili iwe rahisi kutolea ufafanuzi.

Pamoja na hivyo kuna watu wanaosema vibaya kuhusu Hospitali ya Mkoa lakini wakati huohuo wengine wanatuma ujumbe wa kushuruku kwa kupata huduma nzuri.

Ningependa kuwaona watu wanaolalamika kuhusu huduma zetu, wakipata nafasi waje watueleza kwa kuwa uongozi wetu umekuwa ukisisitiza utoaji wa huduma bora.

Pamoja na hivyo, napokea maoni hayo, nitayafikisha kwenye uongozi ili tujipime tuone iwapo wapo kuna upungufu wowote na tuweze kuufanyia kazi.
 
Tatizo mnapenda bure bure sana.kila kitu bure ukiulizwa unaleta siasa hospital ya serikali
nendeni bank wakawape pesa bure nazo si za serikali pia
 
Nadhani kuna haja ya watu kuwa wazi kueleza na siyo jamiiforums.

Inauma na kikwazo Sana kwani nchi hii malalamiko ni mengi Sana watu wanataka Matibabu chapchap bila utaratibu na haswa wanapoambiwa issue ya malipo etc.

Moja. MTU aje aseme Mimi nipo hapa na sijapata matibabu au ndugu yangu hajapata matibabu,

mbili kutumia mtandao kila MTU anaeza mchafua mwenzake.

Tatu ikumbukwe kuwa Kwa sasa kila kitu ni system ya internet na sometimes haifanyi kazi na hatuna namna ingine ya kufanya kazi unless ni dharura.

Nne. Tafuta pesa nenda private kama hujaridhika na huduma, kuna peramiho, kuna mji mwema, kuna jeshini ruhuwiko, kuna hospital ya Dr Mushi hapo Kwanza mpya, kuna masista pale matogoro etc. Kuna ya mkoa kule mbele ya mkuzo etc.

Hii style ya jamiiforums wengi imewachafua bila uhalisia. Simply ni Ushamba Fulani.
 
Back
Top Bottom