Hospitali ya rufaa Bugando inaelekea kubaya!

Hospitali ya rufaa Bugando inaelekea kubaya!

mkuu mwanza kuna hospitali 2 kubwa ambazo ni bugando [catholic] na general hospital -- sekou toure [regional hospital], siamini kama hawa ni bugando ninaowafahamu mimi labda kama ulikwenda sekou toure ya serikali ukafikiri ni bugando
Kwa sasa Sekou Toure ina unafuu mkubwa ingawa kiwango chake pia hakiridhishi..Bugando ma-docta wengi wamekuwa wanafanya part - time kwenye clinic zao binafsi na wengine wameajiriwa private hspt..kwa hali ya sasa wanao uhuru mkubwa sana wa kufanya wanachojiamulia - sirikali na familia zao zinatibiwa india kwa nini wahangaike na BMC wakati kura bado miaka mingine minne mbele..
 
Inshu kama hizi inafaaaa kuweka na picha mkuu ili kuonyesha hali halisi. Haihitaji uchumi kuwa sawa kwenye inshu kama hizi, afya, elimu, miundo mbinu kweli tunahitaji kuwa na uchumi uliyotukuka ili kuboresha haya maeneo? Ni vipaumbele tu. Harafu wazee wanashangilia kama wamewekewa motor kwenye midomo yao wakati mkuu anamwaga upupu wa uchumi bila kujali kinachofanywa na serikali katika maeneo haya ni hatari kwa taifa letu.
 
Sina uhakika kwa undani zaidi. habari nilizosikia ni kwamba Kanisa Katoliki inafanya managementa, ajira ya watumishi inatoka serikalini. Wenye ufahamu zaidi!

ni ya kanisa serikali aihusiki hapo... msilaumu serikali bure...

 
juu ya BMC kuna mtu alikwisha lalamika tena juu ya hili...
 
Ninachojua mm,pale gov wanamiliki 25% nyingine ni catholic,
hvyo husiilaumu serikari sana. Maana hao masister na mapadri dairy wanazidi kuongezea majengo hapo bugando,na majuzi wameipaka rangi hiyo hosp, sasa hiyo hela inatoka wp? Badala ya kuboresha kwanza matibabu!
Ila siwezi bleam direct maana cjapata mgonjwa wa kwenda kumuona kwa hz cku za karibuni.
 
sidhani kama iko hivyo! Ubora umeongezwa, hayo si ya kweli
 
Kila kitu lawama ni kwa serikali. Hata yanayohusu kanisa bado mnailaumu serikali.

Hiyo hospitali ni ya Kanisa, waulizeni kanisa na si serikali.
 
hospitali zetu hazina hata matibabu ya antidote. Achilia mbali bei ya kufanyiwa hiyo CT scan.
Hospitali zetu ni kama model au vitu vya utani kwa walala hoi, na sehemu ya soko kwa wezi wanaojiita wasomi wa utabibu.
 
hivi kwanini serekali inawezekana ktk hospital za madhehebu ya dini na kuziacha hospital zake kuwa taabani huku hospital hizo zikiwa ndio nguzo ya Taifa? Ukienda Muhimbili,Amana,temeke na Hospital nyengine nyingi za Wlaya utakuta vitanda vimejaa wagonjwa na wengine kulala chini na huku dawa nyingi zikikoeskana lkn serekali hiyo hiyo imetumia billion moja kuipa Bugando kutoa huduma na huku hospital hiyo ikidhi kupewa misaada na kuicah muhimbili ho hae kinachosikitisha kwamba hizo hospital za madhehebu ya dini zinalipwa hizo fedha zmekuwa KAMA PRIVATE SECTOR Ukiwa huna hela no Matibabu

Swali lako ni la msingi. Lakini wewe si kila uchwao unaisifia serikali ya c.c.m humu? Leo kimekusibu nini?
Jijibu mwenyewe, form one wewe.
 
MS ur just awesome! FF huwa ana msemo wake "wanchekesha.."
 
hivi kwanini serekali inawezekana ktk hospital za madhehebu ya dini na kuziacha hospital zake kuwa taabani huku hospital hizo zikiwa ndio nguzo ya Taifa? Ukienda Muhimbili,Amana,temeke na Hospital nyengine nyingi za Wlaya utakuta vitanda vimejaa wagonjwa na wengine kulala chini na huku dawa nyingi zikikoeskana lkn serekali hiyo hiyo imetumia billion moja kuipa Bugando kutoa huduma na huku hospital hiyo ikidhi kupewa misaada na kuicah muhimbili ho hae kinachosikitisha kwamba hizo hospital za madhehebu ya dini zinalipwa hizo fedha zmekuwa KAMA PRIVATE SECTOR Ukiwa huna hela no Matibabu

Swali lako ni la msingi kabisa. Ninachoelewa ni kuwa serikali huwa inatoa ruzuku kwa hospitali zote za serikali na za kidini ambazo huwa zinaingia mkataba na serikali kutoa huduma kwa wananchi wote bila kujali dini zao. Tofauti kati ya hospitali za serikali na za kidini ni kuwa hospitali za dini huwa zina usimamizi mzuri zaidi wa pesa wanazopewa na pia huwa zinawekeza pesa zao kuziba mapengo yanayobaki ili kuboresha huduma. Hospitali za serikali zimegeuzwa kuwa mapango ya madaktari na wafamasia walafi ambao wanazifanya kuwa vijiwe vya kupata contact za wagonjwa kwa ajili ya kliniki zao binafsi. Suala la mtu kukataliwa matibabu kama hana pesa halichagui hospitali. Linatokana na sera ya taifa ya uchangiaji wa huduma. Wewe fanya utafiti mdogo tu wa kwenda MOI ukiwa na mgonjwa ambaye amevunjika miguu halafu uwaambie huna pesa uone kama watamfanyia upasuaji. Sana sana ukilazimisha utaishia kupasuliwa kichwa badala ya mguu.
 
Ni kwamba kinachotakiwa hapo ni huduma inayotakiwa kuwepo iwepo ukisema kwamba hatua zichukuliwe wakati watu wanakufa haisaidii sawa bibi kisusi
 
Ndio maana kila siku tunapiga kelele kuwa ile MoU kati ya serikali na makanisa ni ufisadi lakini ndugu zetu mnatetea. Sasa mabilioni yote yale ya ruzuku yanayotoka serikalini yanaenda wapi kama huduma ni mbovu kiasi hiki? Ndio maana baadhi ya wadau wanasema yale mabilioni yanaenda kuimarisha makanisa na si vinginevyo. Kwanza pamoja na ruzuku kubwa wanayopewa bado huduma zao ni ghali kama hospitali nyingine binafsi. Ni wakati sasa kwa serikali kuondoa hizi ruzuku kwa makanisa na kuimarisha hospitali zetu za serikali.
 
Jamani sisi amabao tuko kanda inayohudumiwa na hospital hii tume shachoka na uongozi wa hospital hiyo kwani hilo ndo tatizo kubwa. Mukurugenzi amekuwa ni zaidi ya Rais na jaji mkuu. Hufukuza wafanyakazi kama mende na hata taasisi anazopewa kushika uenyekiti wa bodi imekuwa ni kilio juu ya kilio. Acha watu wafe maana hakuna serikali.
 
Back
Top Bottom