Hospitali ya rufaa Bugando inaelekea kubaya!

Bwana discoverer, nilichosema ni kwamba kuna tatizo la Oxygen kwa wiki kama 3 sasa....Mipango ya kuwa na source yao ya Oxygen inaweza kuwepo ndio lakini, tayari tatizo limetokea na roho zimepotea!!! Kila mahali kuna mipango, au umesahau kwamba tuliambiwa Kigoma itageuzwa kuwa Dubai?? Anyway tusitetee ujinja, tatizo la msingi lipo na linahitaji ufumbuzi wa haraka sana!
 
...........hakuna tofauti na muhimbili, hizi hospital hovyo sana. Hata sijui kwa nini wanafanya hivi? Sio kwamba pesa hamna, pesa ipo sema uongozi ni hovyo sana kuanzia ngazi ya taifa hadi huko hospital.
 
Kaka Mponda umesikia hayo???? Angalia hivi karibuni mnakwenda bundeni anza kutafuta majibu. Na hilo utashindwa? kwa sababu ukweli dalili zinaonnyesha majukumu yameanza kukushinda. kumbuka hivi sasa jamaa zetu kina Mh. Tunu Lisu, Mh. Zitto. Na huyo wa Bilicanas wanakusanya data umejiandaa?
 
Hivi sisi watanzania tuna matatizo gani hata Hospitali ya rufaa kama Bugando tunayotegemea kuwa na wasomi na watu wenye uelewa ndo hii!!
je tatizo letu ni Uelewa, Umaskini, au roho mbaya tu, au tumekata tamaa, au labda elimu tunayopata shuleni si yenyewe. mambo tunayoyofanya si ya kawaida to a rational person. Nafikiri kila mmoja wetu tujipe muda tujiulize, we have something seriously wrong ambacho tunatakiwa kukijua ili kifanyiwe kazi. vinginevyo tusishangae hata tukibadilisha utawala tukaendelea na business as usual. this is very confusing and frustrating watu kufa kwa sababu tu ya oxygen??!!! What a shame!!!!

Haya ndo matatizo ya professionals kuimbiwa siasa na wao kukubali kuicheza siasa na kuweka taaluma pembeni!!. Kilichopo ni kwamba wataalamu wetu wametupa taaluma zao wamekazana kunengua siasa, huku wakimuangalia mchezeshaji kama anawasifia kuwa wananengua vizuri. Tutarajie mengi zaidi!!
 
Kaka Mponda umesikia hayo???? Angalia hivi karibuni mnakwenda bundeni anza kutafuta majibu. Na hilo utashindwa? kwa sababu ukweli dalili zinaonnyesha majukumu yameanza kukushinda. kumbuka hivi sasa jamaa zetu kina Mh. Tunu Lisu, Mh. Zitto. Na huyo wa Bilicanas wanakusanya data umejiandaa?

Mkuu umenena vyema, muda wa kurudi bondeni umekaribia, huyu Waziri naona kazi ishamshinda, nimepita hospitali ya mkoa Kilimanjaro, hawana chumba cha upasuaji, hili lilijadiliwa kwa kirefu kikao cha bunge kilichopita, wabunge wakiomba ipewe udharura, hadi leo hakuna lolote, wajawazito wanalazimika kupelekwa hospitali ya rufaa KCMC, kule wanalipia huduma...hata ukiumia huwezi kushonwa pale Mawenzi kwani hata chumba kidogo cha upasuaji, minor theatre, hakuna. Mponda jiandae kujibu haya. Uliahidi kufuatilia na hata kufika na kujionea, kwa habari za uhakika hata mwakilishi hujatuma!
 
Kaka Mponda umesikia hayo???? Angalia hivi karibuni mnakwenda bundeni anza kutafuta majibu. Na hilo utashindwa? kwa sababu ukweli dalili zinaonnyesha majukumu yameanza kukushinda. kumbuka hivi sasa jamaa zetu kina Mh. Tunu Lisu, Mh. Zitto. Na huyo wa Bilicanas wanakusanya data umejiandaa?
mpond aalihonga kamati ya bunge kupitisha bajeti yake

period and he knows it
 
mpond aalihonga kamati ya bunge kupitisha bajeti yake

period and he knows it

Umenena vyema! Hata mh Kingwangalla aliwahi kuandika kwenye wall yake kule fb.... Tumeburuzwa kupitisha bajeti ya Afya...
 
Hata Muhimbili ni vivyo hivyo. Hakuna mahali nafuu katika nchi hii chini ya Serikali hii legelege. Umefanikiwa kuyaona ya Bugando, nasi tunayafahamu ya Muhimbili, ukiyaweka kwenye mizani yote ni uozo tu. Ndiyo maana waziri kavimba ngozi tu anakimbizwa India tena kila gazeti linaandika, TV zote zinaonesha na simu zinapigwa nchi nzima kuelezea tuikio hilo. Hii ina maana kuwa hospitali zetu hata ile ya Taifa ni hoi na haziaminiki na serikali yenyewe inayokuwa tayari kupoteza mabilioni ya shilingi kumpeleka waziri India kutibiwa ukurutu!!!
 
Hali inasikitisha katika hospitali ya Rufaa Bugando. Watanzania tunatarajia nini kutoka serikali yetu kama watumishi kuanzia wa ngazi ya chini hadi madaktari mabingwa wanapakimbia kutokana na maslahi duni pamoja na vitendea kazi.

Ni takribani mwaka hospitali hii ambayo watanzania wa lake zone ndiyo referral kwao Haina citscan. Mashine hii imeharibika na serikali ndiyo yenye jukumu la kununua imetelekeza wananchi wake.

Staff wengi wameondoka, kusimama kazi kwa kukosa mshahara. Watarudi kazini iwapo watalipwa mishahara.

Hali ya wodini ni tete. Wagonjwa wamelazwa chini, blanket zimechoka, wagonjwa wananyeshewa mvua na uchafu uliokithiri. Hii inatisha.

Huduma ya oxygen. Kuna uhaba mkubwa wagonjwa waliolazwa ICU wako hatarini na wengi wamepoteza maisha kwa uzembee huu

Daktari moja wagonjwa 300 kwa siku.

Hii ni ndio maisha bora ya mtanzania akiwa anatimiza miaka 50 ya uhuru wake.

Wenye information zaidi wachangie, tuweze kuokoa uozo huu. Nawasilisha.
 
Mkubwa! Yani tuna hasara kubwa sana ndani ya hii serikali legelege kama hii ya jk. Yani sitamani hata niambiwe ni nchi yangu ndiyo hii. Natamani Sudan ile mpya ya kusini.
 
Hivi hii hospitali wameirudisha kwa Catholic au bado. Je ni kwanini serikali isiombe msaada wa vifaa??. Kama ni ya catholic Bishop anaweza kuongea na Catholic Hospital za nje wakapata vifaa hasa kama hapa USA kuna hospital za St. Luke
 
Si Bugando tu.Hali ni mbaya hospitali zote nchini.Mwezi uliopita nilienda kumuona rafiki yangu wodi ya mifupa hospitari ya mkoa Dodoma<sasa ni ya rufaa>Niliyoyakuta huko aibu kuyaandika humu!
 
Hali inasikitisha katika hospitali ya Rufaa Bugando. Watanzania tunatarajia nini kutoka serikali yetu kama watumishi kuanzia wa ngazi ya chini hadi madaktari mabingwa wanapakimbia kutokana na maslahi duni pamoja na vitendea kazi.

Ni takribani mwaka hospitali hii ambayo watanzania wa lake zone ndiyo referral kwao Haina citscan. Mashine hii imeharibika na serikali ndiyo yenye jukumu la kununua imetelekeza wananchi wake.

Staff wengi wameondoka, kusimama kazi kwa kukosa mshahara. Watarudi kazini iwapo watalipwa mishahara.

Hali ya wodini ni tete. Wagonjwa wamelazwa chini, blanket zimechoka, wagonjwa wananyeshewa mvua na uchafu uliokithiri. Hii inatisha.

Huduma ya oxygen. Kuna uhaba mkubwa wagonjwa waliolazwa ICU wako hatarini na wengi wamepoteza maisha kwa uzembee huu

Daktari moja wagonjwa 300 kwa siku.

Hii ni ndio maisha bora ya mtanzania akiwa anatimiza miaka 50 ya uhuru wake.

Wenye information zaidi wachangie, tuweze kuokoa uozo huu. Nawasilisha.

Hata muhimbili hospitali ya taifa wagomjwa kibao wanalala chini na hakuna vyandarua. Daktari mmoja wagonjwa 300 ndo uwiano wa nchi yetu. Pamoja na hayo serikali inapaswa kuchukua hatua kuboresha mazingiya ya hospitali hiyo kwa kuwa inategemewa na watu wengi sana wa kanda ya ziwa na mikoa ya jirani kama Tabora.
 
mkuu mwanza kuna hospitali 2 kubwa ambazo ni bugando [catholic] na general hospital -- sekou toure [regional hospital], siamini kama hawa ni bugando ninaowafahamu mimi labda kama ulikwenda sekou toure ya serikali ukafikiri ni bugando
 
Badala ya kusubiri mchango wa serikali ambao hautolewi katika muda muafaka, kwanini wababe wa kivita wa mwanza wasimuite upya fund raising specialist akaja kwenye harambee? Au anahitajika kujenga kanisa tu?
 
Back
Top Bottom