Hospitali ya rufaa Bugando inaelekea kubaya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya rufaa Bugando inaelekea kubaya!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SirBonge, Oct 18, 2011.

 1. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  -Bugando refferal hospital inahudumia mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Geita,Singida, Tabora na Dododoma.
  -Tarehe 2/11/2011 wanapanga kuadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa kwaake kwa mbwembwe kibao!

  Cha ajabu;
  -Wiki tatu sasa hospitali haina Hewa ya OXYGEN ambayo ni uhai wa mwanadamu, nimeshuhudia wagonjwa 6 wakifariki(katika ICU ya wakubwa) achilia mbali wodi za kawaida na ICU ya vichanga kwa kukosa OXYGEN.
  -Operesheni kubwa hazifanyiki-HAKUNA OXYGEN
  -Hakuna chupa za kupimia mkojo na makohozi-hivi ni vipimo rahisi sana ambavyo hata dispensary za mitaani wanafanya, iweje hospitali ya rufaa?
  -Hakuna kipimo cha CT scan kwa takriban miezi 8 sasa-mashine tunaambiwa ni mbovu.

  Uongozi ulichofanya;
  -Wafanyakazi wote watakatwa 2% ya mishahara yao kufanikisha Bugando day-hospitali kutimiza miaka 40, lakini haujafanya chochote kuhakikisha kwamba OXYGEN inapatikana muda wote.
  -Vyanzo vya habari vinasema kwamba wanadaiwa milioni 60 na TOL-(Tanzania Oxygen limited) ndo maana hawaletewi tena OXYGEN

  Nionavyo mimi;
  -Mkurugenzi ameshindwa kutekeleza majukumu yake
  -Sina uhakika kama wizara ya afya inajua hili
  -Sisi waandishi wa habari, tufanye uchunguzi wa ndani (siri) tupate majina ya waliopoteza maisha kwa uzembe huu pamoja na data zao za kitabibu tusaidiwe na wanasheria kuushtaki uongozi wa Bugando kwa UZEMBE!!
  -Wizara ya afya-huwa mnakagua maabara feki mtaani na kuzifunga-Je hamwoni kwamba Bugando inastahili kufungwa kwa UZEMBE HUU MKUBWA??
  Nawasilisha.....
  Chanzo-mimi mwenyewe nilitembelea Bugando! (niliumia sana)
   
 2. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah....mi sisemi sana ni magamba on action
   
 3. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kiukweli ni suala zito sn kwa hospitali kubwa km bugando ambayo ni tegemezi kwa cc wakaazi wa kanda ya ziwa, mi nadhani suala hili lipigiwe kelele za kutosha kiac kwamba wadau waamke na kuchukua hatua stahiki kulitatua kabla halijaleta madhara zaidi!
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280

  Umenena jambo la msingi sana. Wanasherehekea nini watu wanakufa. Upuuzi pote, makanisani, serikalini, watu sisi wenyewe, Tanzania is done. Hata makanisa jamani. Yesu shuka uone wanaojiita watumishi wako au unawaona, maana tunaambiwa hivyo. halafu eti hiyo ni univesity teaching hospital!!!! They are making competent doctors, shame!!!!!!!
   
 5. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mkuu umesahau kuwa hii ni serekali Legelege! Mimi wala sishangai nape kaenda mwanza kupiga domo hajui hilo.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hv hao wafanyakazi wameridhia kabisa kukatwa 2%
   
 7. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Viongoz weng watanzania wanapenda kujikwaza kuliko matendo yao,wanasubiri idadi kubwa ya watakaokufa ili serikali iseme tumeshutshwa
   
 8. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  nafurahi kuona habari za kichunguzi kama hizi, endeleeni kuuhabarisha umma wa watanzania ndani na nje. Na isiwe nguvu ya soda bali iwe ni kila siku mpaka wakuu watusikie
   
 9. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  yaani waandishi wetu wa habari wangekuwa japo wanafanya kwa asilimia 30 tu uchunguzi na kutoa habari kama hizi naamini kungekuwa na mabadiriko fulani, Big Up sana SirBonge!
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Serikali inayatambua haya madudu ndio maana wao wakiumwa kidogo wanakwea pipa kwenda India.

  Haya madudu yatakwisha pale tutakapofanikiwa kuindoa hii serikali legelege.
   
 11. a

  alph Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi sisi watanzania tuna matatizo gani hata Hospitali ya rufaa kama Bugando tunayotegemea kuwa na wasomi na watu wenye uelewa ndo hii!!
  je tatizo letu ni Uelewa, Umaskini, au roho mbaya tu, au tumekata tamaa, au labda elimu tunayopata shuleni si yenyewe. mambo tunayoyofanya si ya kawaida to a rational person. Nafikiri kila mmoja wetu tujipe muda tujiulize, we have something seriously wrong ambacho tunatakiwa kukijua ili kifanyiwe kazi. vinginevyo tusishangae hata tukibadilisha utawala tukaendelea na business as usual. this is very confusing and frustrating watu kufa kwa sababu tu ya oxygen??!!! What a shame!!!!
   
 12. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mhh!!! nchi hii!!!
   
 13. M

  Msindima JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatar, halafu wako bize kukimbizana na mwenge usiokua na faida yoyote.
   
 14. D

  Discoverer Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SirBonge kwanza inaonesha wewe si mwandishi na kama ni mwandishi basi si mwandishi makini au pengine masuala ya afya bado yanakutatiza.
  Ni kweli kwamba Bugando wanaweza kuwa wameishiwa Oxygen, umeongea na uongozi kuweza kujua tatizo ni nini? ni TOL, ni MSD au ni serikali,
  kwa kuwa ni hospitali ya rufaa manunuzi yote ya madawa huwa yanatoka serikalini. Ni mara ngapi Muhimbili Operation hazifanyiki kwa sababu tu maji hamna?
  Tumezoea kutaka majibu rahisi kwa maswali magumu.
  Sababu ya msingi ni kwamba Afya sio kipaumbele cha serikali yetu, Bajeti iliyotengwa kwa Afya ni kiasi gani, na hizi zonal hospitals zinapata kiasi gani?
  Kwa taarifa yako :
  Bugando hospital ina Oxygen concentrator ambayo ina extract oxygen from normal air na baada ya muda si mrefu watakuwa hawategemei tena TOL.
  Fanya utafiti kabla ya kukurupuka kupost, kwa tulioko bugando hali sio kama unavyosema wewe.
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Hii hosp ndio imekuwa hivi?
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu akihabarisha kupitia humu jf bado kwani waTZ wanaoingia humu hawafiki hata 2% ya waTZ yafaa na waandishi wetu wa habari toka vyombo mbalimbali kupita humu na kuchukua habar na kuzifanyia uchunguzi na baadae kuripoti kwa umma
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hili sio jambo la kushangaza hasa kwa serikali hii ya rais wa mambo ya nje ya jk, yapo mambo mengi sana sema tu waandishi wa habari wamejazana huku mijini. Ingekuwa na uwezekano tungemmbadilisha presida na hiyo oxygen kwenye hiyo kampuni
   
 18. D

  Discoverer Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndio kwenye tatizo, issue ya oxygen ni kwenye zone yote hospitali zimeishiwa! ndo maana nilimtaka mwanzisha thread afanye uchunguzi wa kina. TOL watakuwa ndio watuhumiwa wa kwanza kama kweli wamegoma kuleta Oxygen kwa sababu ya madeni though kwa jinsi nijuavyo wao wanasema wamepata technical problem. Ila Bugando tuna backup system ya Oxygen concentrator from natural air na nijuavyo karibuni wataanza ku supply hata hospitali za jirani.
  Priorities za Serikali ya CCM sio kwenye Afya hiyo naomba JF mjue hilo, Oxygen ndio the most prescribed drug in hospitals.
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Nchiii Hiiiiiii ni iko Dar Es Salaaaaaaaam Period

  Huku kwetu Mwanza siko Dar ingawa tuna toa resource za kutosha nchi hiii na wakubwa kuzigombani ila Hospital zetu kama ya bugando ndio kabisaaaa kila kitu Muhimbili Muhimbili inamaa nchi ni watanzania wote wakatibiwe Dar Es Salaaaaam Au??

  My Take;

  Nchi yetu igawanywe kimajimbo tuu maana wanapo igawa nchi na kuiongezea mikoa wakati mikoa iliyopo tu wanashindwa fikisha huduma muhimu kwa wananchi.

   
 20. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,725
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Hakuna haja ya kuhangaika nayo. Kwani kuna wiongozi wa ngazi za juu wanatibiwa hapo? India si kupo jamani?
   
Loading...