Hospitali ya Mkoa wa Singida ipo hoi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya Mkoa wa Singida ipo hoi!

Discussion in 'JF Doctor' started by MADORO, Jan 20, 2012.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hospitali ya Mkoa wa Singida ipo hoi hakuna hata panadol za kutuliza maumivu, dawa za kawaida kabisa katika hospitali, vituo vya afya, na Zahanati. Kuna Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu amefika hospitalini amebanwa na kifua akaambiwa akanunue dawa ili aje kuchomwa Sindano.

  Turudi nyuma kidogo jana watu walikuwa wanamsifia Mbunge wa Jimbo hilo kuwa anatumia pesa nyingi kusaidia. Vipi juu ya suala hili, mbona hospitali ipo hoi muda mrefu.

  Hivi Mbunge mwenyewe ana taarifa kuwa watu huwa wanaugua? atafikishiwa vipi taarifa, kila mara yupo nje ya nchi kushughulikia biashara zake na kurudi kuja kujisifu kuwa anachangia mihela yote kila kitu utadhani serikali haifanyi wajibu wake kwa watu wa Singida. Anyway serikali wajibikeni haraka kwa Tatizo la Singida Mjini Hospitali ya Mkoa sasa ni Critical Issue.

  HERI PUNDA MZIMA KULIKO FARASI MGONJWA
   
 2. I

  Isango R I P

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa hali ilivyo kwa sasa, Manispaa ya Singida ni ya kuhurumiwa. Ifike mahali wananchi wa Singida mjutie uamuzi wa kuambiwa ninyi ndio kambi ya CCM. Pamoja na kukosekana dawa, michango iliorodheshwa kwa ajili ya kusajili wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza, au wale wanaoendelea, au wanaoanza kidato cha kwanza. Sijui hatima ya watu hawa......... any way walichagua ovyo, wanaongozwa ovyo, wasaidieni kupunguza malalamiko ya ovyo!
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu majukumu ya Serikali usitake kumbebesha Mohamed Dewji. Kama mbunge kafanya sehemu yake! Mohamed Dewji, ni mbunge wa kwanza Tanzania ambae atumii posho na mshahara wake! Zote zinakwenda Jimboni kwake.

  Labda utuambie Tundu Lissu, kafanya nini cha maana Mkoani Singida?
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  huyu mara nyingi hata akimpa mtu juisi au akimnunulia mt u soda anapost kwenye website zake ndio maana watu wanamuona kuwa ni mzuri style yake ni kama ya eng manyanya
   
 5. m

  mtamba Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Watu wa singida wana hasara kumbwa hawajui wapi wapeleke malalamiko yao kunamtu kaniambia kuna barabara mbili zimekwanguliwa tena nimuhimu zinaelekea kwa mbunge wao zina miezi mitatu hazijatengenezwa ni vumbi tu. Watu wanaofanya biashara maeneo hayo wanalalamika biashara zao zinaharibika na vumbi singida kuna upepo mkali sana .
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  singida kwenyewe walivyo nyuma,wanasikitisha
   
 7. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Hilo tatizo limetokea ktk hospitali nyingi za serikali,kuna hali mbaya kwa takribani miezi mitatu sasa, usimlaumu Mh. MO, Funding ya sekta ya Afya si jukumu la Mbunge.
   
 8. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena vyema, hospitali zote za serikali Hali si shwari, dawa hakuna na huko MSD ndo
  Usiseme hawana lolote ni kitengo cha wakubwa
  Huwezi kukisemea lolote.......
  Serikali
  Legelege
   
 9. m

  mtamba Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Wewe utakua ni mazalalalalala huwatakii mwema ndugu zako nani wakumliza waziri maswali kama hayo kama si mbunge wajimbo ili waziri atoe maelezo ili ndugu zetu wapate huduma.kitu kingine hatuhitaji msaada kutoka kwa mbunge,yeye tumemtuma kutuwakilisha bungeni sio kutsaidia maana narudia tena temutuma kutuwakilsha sisi wanainchi tunalipa kodi kila tuingipo dukani sasa yeye kwanini aseme ametusaidia bilini 6 kwahio tuache kwenda madukani kununua vitu kama tuna mtu wakutusaidi,mahitaji yetu. Hembu ajipambanue yeye ninani tuelewe kwani tumeshindwa kumjua yeye ninan niserkali auni mfazili wa serkali kwa sababu anafanya kazi za mtawala, na ninani niserkali na nanini mbunge?usikute ww unakudanya kodi zetu kwa leo nishie hapo.
   
 10. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Lissu anaiamsha serikali itimize jukumu lake la msingi ambalo ni kurejesha kodi iliyokusanya toka kwa wananchi kwa kutoa huduma za msingi.
   
 11. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna tatizo kubwa kitaifa. Fungu linalotengwa na serikali kwa kila kituo huko MSD halitoshelezi hata nusu ya mahitaji,kuna mfumko wa bei za dawa kila kukicha lakini fungu ni lilelile kwa miaka zaidi ya minne.
  Ongeza na ubabaishaji wa MSD ni balaa tupu,kuna items nimekuwa nikiagiza hapa kwangu kila mara huu mwaka wa 3 sasa lakini siletewi kisa out of stock msd !
  Hilo ni tatizo la kitaifa,sio Singida pekee si Mh MO pekee.
  I wonder,itafika siku ya kufikiria kubinafsisha hizi huduma.
   
 12. M

  MADORO Senior Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hatumuandiki Mohamedi Dewji kwa kuwa na wivu na pesa zake. Tunahoji Ikiwa anajisifu kila kitu amefanya yeye, imekuwaje hivi vidogo havionekani? anajitapa anasaidia sekta ya afya lakini hospitali haina panado, anajisifu anasaidia elimu na kutaja mabilion lakini wanafunzi hawana madawati wanakaa chini. Hana aibu kijana huyu ameahidi kumalizia Ujenzi wa Namfua hadi sasa hajaleta hata tofali moja, akaahidi anamalizia pagara la CCM linalotia aibu katikati ya mji lakini hadi sas hajaleta hata kopo moja la rangi, akadanganya wananchi kuhusu kuleta nyasi uwanja wa Namfua za Milioni 300, akasema zimeshakuja, kumbe alikuwa anadanganya ili vijana wetu wasio na cha kuahidi wakataliwe na wapiga kura. Atekeleze wajibu wake aliomba kwa hiari yake hakuna aliyemlazimisha. Kama alijua hana nafasi ya kwenda bungeni kupeleka matatizo ya wananchi alikuwa na kiherehere cha nini kuwadangaya watu eti kwa sababu ya pesa zake?
   
 13. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Tuambie huyo wa chadema kafanya nini??
   
 14. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hili tatizo ni kubwa sana na limekumba hospitali nyingi.kama mdau alivyosema hapo juu kuna maeneo kadhaa ambayo ni chanzo cha ukosefu wa dawa.tuanze na msd,hawa jamaa wameshindwa kutoa huduma kama ilivyokusudiwa na wanahitaji mshindani(hawa ni tanesko ya pili).huwezi ukaagiza dawa na vifaa tiba MSD ukavipata vyote,lazima neno out of stock litokee.sometimes unaweza kuambiwa bidhaa iko in lakini haipo kwenye bohari ya kanda yako,mfano bidhaa ipo MSD Dar lakini MSD tabora haipo hivyo itakubidi uisubiri kwa siku kadhaa.cha kusikitisha huwezi kwenda kufanya manunuzi kwa watu binafsi(wazabuni) bila kuwa na list ya out of stock kutoka MSD,hapa ndipo tatizo linapokuja kwa sababu waganga wakuu hawakubali kujiingiza kwenye matatizo ya manunuzi na badala yake ni bora waache hospitali hazina dawa mpaka pale MSD watakapo kuwa nazo au watakaposema dawa hizo hazipo.kwa ufupi chanzo cha ukosefu wa dawa kwenye mahospitali ni MSD kushindwa kutoa bidhaa kwa wakati na kwa ukamilifu na pia utaratibu mrefu wa manunuzi ya dawa.
  pili kuna baadhi ya halmashauri wanaendekeza ufisadi,yaani dawa hazinunuliwi mpaka wahakikishe wanapata 10%,hapa ndipo nenda rudi za hapa na pale zinapoanzia mpaka hospitali zinakaukiwa na dawa.
  nasikitika kuona mganga mkuu kiongozi,katibu wa wizara ya afya na mawaziri wao wanashindwa kushughulikia maswali ya msingi kama haya badala yake wanakaa kuhamisha interns kutoka muhimbili kwenda sehemu nyingine kisa wamedai posho zao.ndio maana hawatakiwi kuendelea kuwepo pale wizarani kwani wameshindwa kuwahudumia watanzania,hawana uchungu kwa sababu hawatibiwi singida !!!!wananchi waeleweni madaktari wana mambo mengi ya kuwaeleza la sivyo wote wataishia kubadilisha fani kama hamis kigangwalla.
   
 15. N

  NILLA J New Member

  #15
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani singida kuna mkuu wa mkoa kuna mbunge inamana wote hao wanashindwa kuikumbusha serikali yetu juu ya hili swala?mbona mbunge wa morogoro mjini huwa anaenda kutembelea hospitari ya mkoa mara kwa mara na anafuatilia hadi utendaji wa kazi na kuweka mambo mengine sawa?inamana hata mbunge na mkuu wa mkoa hawajawahi kufika hapo hospitali,jamani hata siku moja moja awe anaenda kuwasalimia wagonjwa ambao ni wananchi wake atajua kero nyingi na ataweza kutatua
   
 16. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Kwa wananchi wa kawaida wanapokosa huduma bora lawama zao huzielekeza kwa watumishi wa idara ya afya. Wasichokijua ni kwamba chanzo ni hao 'baba na mama zao' wanaowaona miungu watu na watetezi wao.
  TRULLY,
  KUFANYAKAZI KWENYE SEKTA YA AFYA SERIKALINI NI MORE THAN TO BE FRUSTRATED...
  NDO MAANA WENGINE HUAMUA BORA LIENDE!
   
 17. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mbona hali kama hii ipo hospital zote za serikali nchini ushuhuda ni nao nenda Morogoro, Iringa, songea utakuta hali kama ya Singida. Afu utakuta nje ya hospital hizi kuna pharmacy kubwa ndo wafanyabiashara wakubwa wa madawa. Serikali yetu imekufa haina kitu, tangu mzungu aachie MSD haina kitu hadi panya wataingia pale msd
   
 18. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Dah! It is very sad, Sijui ni kwanini now days naifananisha Tanzania yangu na pre-jehanam. Kulala gizani ni kawaida kabisa siku hiz, by any means tanzanian should die "kama si kwa risasi, mabom(mbagala&g.mboto), magomjwa,mafuriko,ajali(mf. Mv ice lander) basi hata mfumuko wa bei wafe kwa njaa" hii ndiyo kauli mbiu ya uongozi wa nchi yetu japo haijawekwa waz. Bongo hapa hapa ilipo serikal tembea mahospitalin na mashulen utizame, utafurah mwenyewe utakayo yakuta. Aah mpaka inachosha, acha nikapiganie uhai na usalama wa maisha yangu.
   
 19. M

  MADORO Senior Member

  #19
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mnaosema Mbunge wa Singida Mjini (Mohamed Dewji) afike hospitalini, kwani yupo Tanzania? BUngeni kwenyewe ambako anapaswa kwenda kuwakilisha wananchi haendi. Anajua hili mnalosema ni tatizo kwake sio Tatizo. Mkuu wa Mkoa naye bado yupo kwenye foleni ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa anadai pesa za Malipo ya kuzoa takataka katika manispaa na kampuni yake tata ya PAVICO, Mkurugenzi wa Manispaa anawambia subiri tujadiliane na Meya, Meya ana Elimu ya darasa la Nne, ukimuuliza anasema haya tuwaachie wataalamu. Hebu niambieni ufumbuzi utapatikana? Hata kama ni huko MSD, au hata kama Wizara haijatekeleza vema kazi zake bado anahitajika mfuatiliaji. Dewji kwanza hasumbuki anawashangaaa akina zito wanaobishanana mawaziri anaona kama wanaigiza vile
   
Loading...