Hospitali ya KKT Nyakato Mwanza inakera kubambika gharama kubwa kwa wanaojifungua

Amaniwood

Member
Mar 23, 2022
26
47
Habari zenu wapendwa.

Nina kero niliyokutana nayo hivi karibuni katika hospitali ya KKKT Nyakato Mwanza baada ya kumpeleka mgonjwa wangu kujifungua.

Awali tulipoanza cliniki walitupokea vizuri na kwa ushawishi mkubwa sana kuwa garama zao za kujifungua kwa njia ya kawaida ni Tshs. 56,500 huku kujifungua kwa njia ya upasuaji ni Tshs. 450,000.

Lakini chakushangaza zaidi nikuwa mgonjwa wangu alipo fanikiwa kujifungua kawaida garama zimekuja kuwa kubwa kinyume na matarajio tulio kuwa nayo hadi kufikia Tshs.263,300. Kiasi ambacho kusema ukweli kilitusumbua sana kukipata kwa wakati huo. Hivyo ikalazimika hadi kutumia hela ambayo nilikuwa nimeitenga kwaajili ya manunuzi ya chakula cha mzazi.

Kusema ukweli niliumia sana na kukwazika sana hata baada ya kuzungumza na uongozi sikuweza kupewa majibu yanayo ridhisha. Kilicho nikera zaidi nikwamba, niliomba bili mapema ili endapo kama kuna kitakacho kuwa kimeongezea niweze kuchakalika kukikamilisha kabla ya muda wakuruhusiwa kufika. Chaajabu sikupewa bili mapema bali walisubiri hadi ule muda wa jioni ulipo fika ndio nifanyiwa kushtukizwa.

Ukweli sijawahi kukutana na huu usumbufu kwa uzao wangu wote. Pia kulikuwa na mgonjwa mwengine ambaye alikuja nyuma yetu ilishindikana kuondoka sababu ya kuzidishiwa garama ili hali na yeye alijifunguwa kawaida.

Uongozi unao husika na usimamizi wa hizi hospitali za KKKT waliangalie vizuri jambo hilu vinginevyo hospitali hii ya KKKT Nyakato Mwanza haiwatendei haki wagonjwa.

Asante
 
Kupewa bill mapema isingewezakana,gharama halisi zinajulikana wakati wa kuruhusiwa.Ila kwa ushauri Sekou Toure kulingana na Sera ya Afya huduma hiyo ni bure.
 
Back
Top Bottom