Hospitali ya Kamanga jirekebisheni

twende wote

Member
Mar 29, 2021
50
84
Hospitali yenu Ni nzuri kwa uwekezaji, Ila ni mbovu kabisa kwa huduma, hasa upande wa bima hasa za NHIF. Mnabambika madeni ya matibabu, mbaya zaidi huduma za wazazi wajawazito, Ni mbovu na wengi wanapoteza maisha ktk uzazi shida iko wapi?? Msipobasilika mtapoteza wateja, yatabaki maghorofa. Kama wapo inaowagusa watachangia hii mada
 
Ndio tatizo kuu LA watanzania wengi....unawekeza mabilioni kuyavutia macho na sio moyo...wekezeni kwenye huduma tutaitafuta hata mpaka vichochoroni huko. Kamanga hospital malalamiko ni mengi huko mitaani.
 
Ndio tatizo kuu LA watanzania wengi....unawekeza mabilioni kuyavutia macho na sio moyo...wekezeni kwenye huduma tutaitafuta hata mpaka vichochoroni huko. Kamanga hospital malalamiko ni mengi huko mitaani.
Ubahili utaiponza hiyo hospitali
Hoteli ukijenga nzuri chakula kiwe kizuri na wahudumu wawe wazuri.

Watu hawafuati majengo

Kama hawezi kuendesha akodishe law mahospitali mengine makubwa.wamlipe Kodi ya mwezi basi
 
Nitaongea na mmoja wa largest shareholder pale ila namna ya kuanza kumwambia ni ngumu. Kama vipi nitamueleza mwanae aongee nae
 
Kamanga hospital ya mwanza au kama ni hii wameishiwa hawana hata wateja sana siku hizi watu wanaamua kwenda kubanana Bugando tu kikubwa wapate matibabu mazuri, tatizo Kamanga wameleta vijana ambao hata kumshauri mgonjwa na kuongea naye hawajui hii hospitali itapitwa hata na st clara tu
 
Majungu hayo!! Madhaifu ya baba utamwambia mtoto? Hapana mwambie mhusika mwenyewe.
Mwanae yuko kwenye management ya biashara za mzee wake. Badala ya kumwambia Kikwete kuhusu mojawapo ya uwekezaji wake ukimwambia Ridhiwani kuna tatizo?
 
Back
Top Bottom