DOKEZO Hospitali ya Kairuki wahuni wachunguzwe. Kila mgonjwa wa Bima anaumwa Helicobacter pylori (H. Pylori)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
454
1,261
Helicobacter pylori (H. pylori) huu ugonjwa dawa zake bei zake ni kuanzia elfu 80. Hospital ya Kairuki hasa polyclinic Kairuki ya Mbezi Magufuli kila mgonjwa atakayepima choo wote wanaambiwa wana H. pylori. Ukiwa na Bima ya afya lazma uambiwe una H. pylori.

Nilipeleka mtoto wangu akaanbiwa hivyo mtoto wa miaka 3, wakampa madawa mengi aina km 5 afu zote za kumeza siky 14 hadi 30.

Shem wangu naye ambaye hatuishi nyumba 1 na yeye aliambiwa na H. Pylori, rafiki yangu hivyo hivyo.

Mimi mwenyewe jana nilipima nilikuwa siumwi chochote nikasema ngoja niwapime wakasema nina H. pylori.

Nikamchukua mtoto na mimi tukaenda kupima bochi na Kairuki kote tulikutwa hatuna hiyo H. pylori mtoto wangu amekutwa na matosi yanayompa homa basi.

Je, nyie hospitali ya Kairuki mmeamua kufanya biashara na miili yetu au?? Je, pesa ya bima ndiyo chanzo chenu cha mapato.

Serikali fatilieni hili swala. Wagonjwa wa bima kupewa madawa mengi na kuambiwa wanaumwa magonjwa mengi ili hospital wauuze dawa siyo fair.
 
hiyo hospitali kwa sasa wanafanya biashara ukienda hapo kupima magonjwa unaweza kupata msongo wa mawazo kwa majibu utakayopewa wanapiga hela hatari na wanajiona ni mabingwa kumbe ni wafanyabiashara hatari kwa miili ya binadamu
 
Maisha yamekuwa magumu siku hizi kila mtu anajiongeza pale alipo, kwenye maduka ya dawa wauzaji wanaongeza cha juu, huko hospitalini nako wanaangalia madawa ya bei mbaya ndio wanakusukumizia ugonjwa wake, ilimradi pesa itoke tu.
 
Hospitali zote za private zinafanya biashara..wapo hapo kumake profit..hela ngumu wanaitafuta hata kwa kukusingizia gonjwa ili wapige hela za vipimo na madawa..the rest utajua wewe na familia yako.

Hospitali za umma zinazotoa huduma wao nao hovyo tu huduma mbovu..foleni madawa hakuna yani hii nchi imelaaniwa kila kona.

Nakushauri nenda hospitali zaidi ya moja uweze ku confirm tatizo ndio utumie dawa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Helicobacter pylori (H. pylori) huu ugonjwa dawa zake bei zake ni kuanzia elfu 80. Hospital ya Kairuki hasa polyclinic Kairuki ya Mbezi Magufuli kila mgonjwa atakayepima choo wote wanaambiwa wana H. pylori. Ukiwa na Bima ya afya lazma uambiwe una H. pylori.

Nilipeleka mtoto wangu akaanbiwa hivyo mtoto wa miaka 3, wakampa madawa mengi aina km 5 afu zote za kumeza siky 14 hadi 30.

Shem wangu naye ambaye hatuishi nyumba 1 na yeye aliambiwa na H. Pylori, rafiki yangu hivyo hivyo.

Mimi mwenyewe jana nilipima nilikuwa siumwi chochote nikasema ngoja niwapime wakasema nina H. pylori.

Nikamchukua mtoto na mimi tukaenda kupima bochi na Kairuki kote tulikutwa hatuna hiyo H. pylori mtoto wangu amekutwa na matosi yanayompa homa basi.

Je, nyie hospitali ya Kairuki mmeamua kufanya biashara na miili yetu au?? Je, pesa ya bima ndiyo chanzo chenu cha mapato.

Serikali fatilieni hili swala. Wagonjwa wa bima kupewa madawa mengi na kuambiwa wanaumwa magonjwa mengi ili hospital wauuze dawa siyo fair.
Inasikitisha sana,hata maabara baadhi ukienda kupima ni u t i tu kama hakuna magonjwa mengine ambukizi.
 
Hospitali zote za private zinafanya biashara..wapo hapo kumake profit..hela ngumu wanaitafuta hata kwa kukusingizia gonjwa ili wapige hela za vipimo na madawa..the rest utajua wewe na familia yako.

Hospitali za umma zinazotoa huduma wao nao hovyo tu huduma mbovu..foleni madawa hakuna yani hii nchi imelaaniwa kila kona.

Nakushauri nenda hospitali zaidi ya moja uweze ku confirm tatizo ndio utumie dawa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
hospital za private hatari sana
 
Lipo tatizo kwenye private hospital ambalo serikali ipokuwa makini kwenye udhibiti na kufatilia viwango tutaharibu Taifa. Tucheze kote lakini sio afya!

Zipo trend nyingi za hatari za kutengeneza pesa kijanja huko ikiwemo, upasuaji wakati wa kujifungua kwa sababu nyepesi, majibu ya baadhi ya vipimo ili ufanyiwe matibabu ya gharama wakiona una uwezo kifedha mfano vipimo vya figo, matatizo ya uzazi kwa wanawake n.k

Hizi hospital nyingi zimekuja kusaidia vipimo na matibabu ya kisasa lakini kuna baadhi ya madaktari wasio waaminifu wanatafuta fursa za kupiga pesa humo humo bila kujali hatma za mgonjwa.

Serikali ipo unda utaratibu makini wa quality control, kufatilia trend ya matibabu n.k kuna hatari kubwa mbele afya za watu zikigeuka biashara! Bahati mbaya au nzuri hili tutaumia wote uwe waziri, mbunge whatever utaenda hizi hospital....
 
now tunatakiwa twende zaidi ya hospital 3
 
Kampuni za bima zinapigwa Sana aisee . Majuzi nilimsindikiza mtu hospital moja tu ya hadhi tu hapa dar ..yaani alipimwa vipimo hata ambavyo havihusiani na jumla ya vipimo vyote ni zaidi ya 2 mill halafu hajakutwa na kitu ...yaan inshort kipimo Cha fully blood picture tu kilitosha kugundua tatizo alilonalo...Na hapo ni vipimo, Bado gharama zingine Kama around 1 mill..At the end tukagundua ni janja ya hospital kuforce vipimo vya Bei na huduma ghali ili kuvuna pesa kutoka makampuni ya bima.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Halafu unamsikia mkuu wa nchi anapigia promo private sector .huu ni urefu wa kamba ndio maana Rais akiwa na uzarendo wa kupitiliza ma private sector yabaki kupiga miayo. Sijikatai ila Africans tuna matatizo makubwa hasa tunapopata upenyo wa ku corrupt mahala.
 
Back
Top Bottom