Hospitali nzuri kubadili meno ya bandia, Dar es Salaam

Brone

New Member
May 15, 2021
1
0
Hali zenu Ndugu zangu hakika mpo sawa kiafya kwa uwezo wa Mungu Kikubwa Naomba mnijuze hospital nzuri yenye huduma za Kubadilisha meno Na kuweka bandia inagharimu kiasi gani cha pesa.

Naombeni Msaada mwenye kujua, Nipo Dar Es salaam.
 
Kwa nn usiende muhimbili wana kitengo kizuri sana cha meno na kuna maspecialist wa kutosha
 
Zipo kibao Kuna magomeni pale Kuna jengo wameandika meno bandia kabisa kama sijakosea ni mwembechai katikati..

Kuna nyingine hapo magomeni usalama pale kituoni utumishi house kwa pembeni inaitwa "omega dental " wako kama floor ya pili ivi.

Kuna nyingine ipo mabibo karibu na ibungu bar pale relini kabisa wanayo hyo huduma ni mama clinic wako njema jina nimesahau ukifika tu mabibo mwisho Kuna Bar maarufu inaitwa ibungu au new ibungu kwa mbele iko hyo clinic Ina gorofa kadhaa usawa huo huo wa barabar
 
Back
Top Bottom