Hospitali kupandishwa daraja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali kupandishwa daraja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by taffu69, Oct 26, 2010.

 1. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwenye mikutano ya kampeni inayoendelea kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 31, kati ya ahadi nyingi anazotoa Kikwete ni kuzipandisha daraja hospitali kadhaa kwenye maeneo ambayo amekuwa akifanya mikutano yake ya kampeni. Ahadi hizo zinajumuisha kufanya baadhi ya hospitali za mikoa kuwa za rufaa na za wilaya kuwa za mikoa

  Kinachonitatiza katika ahadi hiyo ni vigezo vinavyotakiwa kutimizwa kabla ya kupandisha daraja hospitali ama zahanati. Naomba wajuzi wa hii fani ama eneo hili wanifahamishe mambo yanayotakiwa kutekelezwa ili kuweza kupandisha hadhi hospitali ama zahanati.
   
 2. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hizo lisikusumbue kichwa kwani propaganda za kisiasa. Huwezi kupandisha hadhi kwa kutangaza tu pasipo maandalizi kama madaktari bingwa, vifaa, majengo n.k.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  haaa kumbe ndo hivyo basi atafanya kweli kunakipindi alisema cuba wameahidi kumpa madaktari bingwa, huku yeye hawaaandai wakwake!
   
 4. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hilo ni tatizo la wanasiasa wa sisiemu kujifanya wao ndio wataalamu wa kila kitu, badala ya kutoa ahadi za kisera wao wameng'ang'ania kunadi ahadi za kipropaganda. unaposema utapandisha hospitali zote za mkoa kuwa za rufaa unatizama vipaumbele gani? Je hicho ndio kipaumbele? vipi kuhusu wataalamu?
   
 5. P

  Preacher JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  madaktari wa Kitanzania wanataka kuboreshewa maslahi yao - ikiwemo mishahara, marupurupu, vifaa bora vya kufanyia kazi, mahali bora pa kulala wagonjwa wanaowatibu' vyakula vya hospital kuboresha afya za wagonjwa hao; barabara/njia bora za kuwafikisha hao wagonjwa hospitalini muda muafaka - [sio kufika wameshakufa shauri ya foleni; ugumu wa usafiri toka vijijini-wilayani-mikoani wanapotoka] uwezo wa wagonjwa hao kusafiri wanapopata hizo rufaa - IN SHORT JK AMESHINDWA - AANZIE GRASS -ROOT LEVEL KUREKEBISHA NDIO AJE JUU KUPANDISHA HIYO HOSPITAL DARAJA-

  AHADI HEWA AU FEKI...............WHICHEVER - NA UONGO - WATANZANIA HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIII
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Usihofo...Shekhe Y ataweka amajini yake kwenye hospitali zote
   
 7. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuhusu hizi hospitali zimepandishwa sasa hadhi kwenye vichwa vya wapiga kura baada
  31 oktoba 2010 zitashushwa hadhi nakurudia hali ile ile au zitakuwa chini zaidi .Samaha
  ni wapiga kura kama nimewakwaza kwa hili manake hii ni siri ya mgombea wetu Shemej
  iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Tulivyokuwa vijana mara nyingi tukipigana tulikuwa tunatumia ngumi, mieleka, na hata Kung fu kwa wale waliojifunza, lakini kuna wakati unagundua kuwa umeshadundwa na mpinzani wako anaelekea kukumaliza, basi hapo ndipo unapotoka kwenye utaratibu wa kawaida uliozoeleka wa ngumi kwa ngumi na kuangalia pembeni kama kuna gongo linalofaa karibu halali yako kumtwanga nalo, kama hakuna na amekutaiti hapo chini basi meno nayo huwa silaha nzuri sana ya kujikwamua, sasa je kwa hali ilivyo mnategemea JK afanye nini? Jana ameahidi Hospitali ya Tumbi-Kibaha kuwa ya mkoa wakati tayari inafanya kazi za kimkoa kama..Tumbi Special Disignated Hospital na hii ilianza zamani tu pia bado inapewa mgawo wa pesa za matumizi mkubwa kuliko hospitali zingine za Mikoani sababu ikiwa majeruhi wengi wa Morogoro road wanaletwa pale Tumbi kabla ya kupelekwa Muhimbili, hivyo basi ukiangalia uhalisia wa ahadi ya Tumbi Hospital kuwa ya Mkoa ni kwamba amechezesha jina tu lakini hakutakuwa na badiliko lolote zaidi ya yale majengo yanayoendelea sasa hivi na uwepo wao wa madaktari wa Cuba na ma-specialist wazawa watakuwa walewale waliopo hivi sasa na ni vigumu kuongeza wengine kwani wazawa wengi wanakimbilia nje kufuata malipo mazuri, Vifaa vya kazi nafikiri vitaendelea kuwa vile vile ingawa vinazidi kuzeeka na hakuna bajeti mpaka sasa iliyopitishwa na Shirika la Elimu ambayo inayoonyesha kuwa vitanunuliwa, na kwa upande wa service Tumbi hospital sasa hivi haina tofauti na hospitali zingine za mikoa kwani inafanya kazi zote zinazotakiwa kimkoa na hata zaidi kwani wao tayari wana hao madaktari wa Cuba kwa ajiri ya mifupa tofauti na hospitali zingine za mikoa hazitoi huduma hiyo na hata hivyo Quality yao nao wote imeendelea kuwa ya kimkoamkoa...kaulize pale Martenal Death Rate sasa hivi ikoje and why? kwa ujumla hii ngoma ya JK sasa hivi ni Noo formula usaniii kwa kwenda mbele na ahadi zisizo ndizo
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wasisahau na hii Hospitali

  Dripu dirishani
  [​IMG]
  p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal { margin: 0cm 0cm 0.0001pt; font-size: 12pt; font-family: "Times New Roman"; }div.Section1 { page: Section1; }
  Pichani Mkazi wa Kijiji cha Gomelo, Kata ya Kisaki , Tarafa ya Bwakila, Wilaya ya Morogoro
   
 10. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hapa Mwanza leo akiwa katika Uwanja wa Sahara jimbo la Nyamagana ameahidi kuipandisha Hospitali ya mkoa ya Mwanza sekou Toure kuwa ya Rufaa na Bugando ambayo ni mali ya RC kuwa itakuwa hospitali maalum ya rufaa.
   
Loading...