Hosni Mubarak taabani baada ya kung'olewa madarakani

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
MubarakMawazoMgonjwa.jpg
Gazeti la Al Masri al Youm linalochapishwa nchini Misri limeripoti kuwa hali ya kiongozi aliyeng'olewa mdarakani nchini humo Hosni Mubarak ni mbaya mno na kwamba dikteta huyo mepoteza fahamu.
Ripoti hiyo imesema Hosni Mubarak yuko chini ya uangalizi wa madaktari na kwamba hadi sasa haujachukuliwa uamuzi wa kumhamishia hospitalini.
Mwezi Machi mwaka uliopita dikteta huyo wa zamani wa Misri alilazwa katika Hospitali ya Heidelberg nchini Ujerumani ambako alifanyiwa upasuaji.
Baadhi ya vyombo vya kuaminika vya Misri vinasema hali ya kinafsi na kimwili ya Hosni Mubarak ni mbaya mno na inazidi kunyong'onyea siku baada ya siku.
 
SAFI SANA AKAPUMZIKE KWA MATESO MOTONI HUKO.......:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 
SAFI SANA AKAPUMZIKE KWA MATESO MOTONI HUKO.......:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:

Usiseme hivyo kiongozi. Hiyo ni roho ya kinyama, inayotaka binadamu mwenzako afe. Tumwombee afya njema alafu mengine yafuate.
Ni Mungu tu anayejua udhaifu au wema wake.
 
Mapenzi ya Mungu yatimilike si kama tutakavyo sisi, kama ni kufa basi ahadi yake itakuwa imefika lakini sishabikii afe kwani baada ya kifo ni hukumu na hakuna aliye na hakika kama leo akifa atauona ufalme wa Mungu.
 
Wacha afe tu, wana faida gani madikteta? Hata wa hapa bongo wakipatwa na maafa mimi kwangu baridi tu, hawana utu kwa nini tuwahurumie wanyama pori hawa ?
 
Usiseme hivyo kiongozi. Hiyo ni roho ya kinyama, inayotaka binadamu mwenzako afe. Tumwombee afya njema alafu mengine yafuate.
Ni Mungu tu anayejua udhaifu au wema wake.

aaaaaaaaaaaah!..kwani hata wewe unashindwa kujua udhaifu wa madikteta kama mubaraka,mse7,anna makinda,mramba,idd amin and the like..sasa nasema RIP Mubarak
 
Mapenzi ya Mungu yatimilike si kama tutakavyo sisi, kama ni kufa basi ahadi yake itakuwa imefika lakini sishabikii afe kwani baada ya kifo ni hukumu na hakuna aliye na hakika kama leo akifa atauona ufalme wa Mungu.

Hivi nyie mnafikiri pamoja na kulaumiwa kote maendeleo yaliyofikiwa na Misri chini ya Mubarak ni madogo???? ni basi wamemchoka tu...lakini misri ni kati ya nchi zenye maendeleo makubwa duniani....kama hamuamini ngojeni afe ili muone watakavyoanza kuhubiri sifa zake..na kwenye siasa za nje kama sio mubarak pale SUEZ CANAL na ISRAEL pangekuwa hapakaliki....ndo maana marekani wazee wa double standard walikuwa wanasema Mubarak is not a dictator ..wakati hao hao watakuambia Chiluba alikuwa dictator au Sadam...wakati wao wameshasababisha vifo vingi Iraq kukiko huyo Sadam...

Ndo maana Nyerere alijuwa hilo akawa anawaambia viongozi wenzake ...hata wananchi wakupende vipi na uwafanyie kila kitu kwenye utawala kuna kuchokwa ..ni lazima kuheshimu.... Presidential Terms...alisema hayo wakato anamshauri Kaunda aondoke kwa hiari akiwa bado anapendwa...Egyp walimpenda mubarak lakini wamemtosa.........Museveni hapo Uganda miaka 15 iliyopita walikuwa wanamuita mkombozi lakini sasa wameanza kumchoka....

Ni dhahiri kwa kiongozi ambaye ana ndoto za kuona kizazi chake kiendelee kuheshimiwa kwenye siasa ni muhimu aondoke kwa hiari ....kwa hali ya sasa Mubarak amewaharibia hata watoto wake mipango yao ya kisiasa....
 
Kwanini Nyerere alilijua hili baada ya kukaa ikulu takribani miaka 25?
mix with yours
 
Kwanini Nyerere alilijua hili baada ya kukaa ikulu takribani miaka 25?
mix with yours

Nyerere alidhamiria wazi kujiuzulu mwaka 1980....kwa dhati.....ukatumwa ujumbe kumuomba abakie na kati ya sababu kubwa walizotoa kubwa iliyomfanya abakie ilikuwa ni ile kuwa tumetoka vitani...alitakiwa arudishe nchi kwenye hali stable kiusalama na wakati huo pamoja na vita kwisha tulikuwa " tumeikalia Uganda ..Kijeshi.."....
Mwaka 1985 walitaka tena abakie akakakataa na katika hotuba yake aliwaponda waliokuwa wakimfuata kuwa abakie wana uchu wa madaraka ...wanataka abakie ili nao wabakie kwenye system.,na uganda majeshi yalikuwa kwa kiasi kikubwa yamesharudi yote kufikia mwaka 1984......akaondoka!

Ni wazi kuwa mara nyingine wanaochangia viongozi kubakia madarakani ni wapambe wao ambao huogopa mabadiliko kwa kuhofia nafasi zao...ndio maana pamoja na jahazi kuzama wapambe wa mubarak ....walikuwa wanamndannganya kuwa anakubalika hadi alipoona mwenyewe wananchi wameingia mitaani asiamini....,kuna SENAGAL yule mzee anafikisha miaka 90 karibuni...wapambe wanamtaka aendelee ......daktari wake binafsi amekataa alipoona wapambe hawataki ..akaamua kwenda kwenye vyombo vya habari kuwaambia kuwa afya ya rais ..hairuhusu tena ratiba za urais..na kuendelea na madaraka ni kuhatarisha maisha yake ambayo yeye amekabidhiwa kuyalinda..aka resign...what next detention....
MUGABE anafikisha miaka 90 karibuni na mpambe mkuu anayeogopa Mugabe kuondoka ni Mkewe na wasaidizi wa mzee wa karibu wanajuwa akiondoka wamekwisha.........
So msifikiri hata kama rais wa nchi yeyote anafikia kuona ameelemewa na hali yake haimruhusu kuendelea..anaweza kabisa akawa anataka kuondoka ..lakini watu wake wa karibu ndio huwa kikwazo..that is normal..ni lazima awe na ubavu wa kuwaambia kuwa nimechoka sasa napumzika!!!
 
MubarakMawazoMgonjwa.jpg
Gazeti la Al Masri al Youm linalochapishwa nchini Misri limeripoti kuwa hali ya kiongozi aliyeng'olewa mdarakani nchini humo Hosni Mubarak ni mbaya mno na kwamba dikteta huyo mepoteza fahamu.
Ripoti hiyo imesema Hosni Mubarak yuko chini ya uangalizi wa madaktari na kwamba hadi sasa haujachukuliwa uamuzi wa kumhamishia hospitalini.
Mwezi Machi mwaka uliopita dikteta huyo wa zamani wa Misri alilazwa katika Hospitali ya Heidelberg nchini Ujerumani ambako alifanyiwa upasuaji.
Baadhi ya vyombo vya kuaminika vya Misri vinasema hali ya kinafsi na kimwili ya Hosni Mubarak ni mbaya mno na inazidi kunyong'onyea siku baada ya siku.

He deserves it.Hii iwe fundisho kwa madikteta wengine kwamba haisadii sana kuwaibia wananchi wako na kuwafukarisha only to leave everything behind after you have died.Kikwete once said "anamuelewa mtu anayeiba T.sh.million 100,lakini hamuelewi mtu anayeiba Billion 100."Nina hakika hakuwa anajustify wizi.I concur with him katika hilo.Sina hakika hata hivyo kama mpaka sasa hajaiba Billion 100.
 
usiseme hivyo kiongozi. Hiyo ni roho ya kinyama, inayotaka binadamu mwenzako afe. Tumwombee afya njema alafu mengine yafuate.
Ni mungu tu anayejua udhaifu au wema wake.
hakuna cha kumwombea mema; na hapa bongo ee mora ebu waondoe mafisadi duniani
 
Some time I feel like others sometime I do feel the way I feel! I was in Egypt two yrs ago at CONRAD Hotel and some one (tax driver) told me 'many people think that all Egyptians are Muslims but not...there are many denominations and all are Egyptians".

In the real sense Mubarak overstayed on power and because of that he accumulated half of Egyptian’s wealth for himself and his children. Whether He dies today or tomorrow that wouldn’t matter to me! What matters is the equal distribution of Egyptians' wealth to all Egyptians. This is what Mwl Nyerere did.

The strike and endless demonstrations of Egyptians till Mubarak went out of Ikulu reminded me what the Tax driver told me 'All are Egyptians'.

The current divide and rule of our leaders in Tanzania does not make us feel 'All are Tanzanians'. It's amazing! There are Tanzanians above the rule of laws but time is coming soon where all Tshs reserved in the foreign banks will be returned for the benefit of ALL Tanzanians.
 
hakuna cha kumwombea mema; na hapa bongo ee mora ebu waondoe mafisadi duniani

Hapa ishu si UFISADI ila ni jinsi huyu mtu alivyo na hali mbaya na yuko katika hatari ya kufa. Kibinadamu, ni kumtakia afya Njema. Hii roho ya kutaka mtu aliye mahuti afe ni sawa na kuua.
Kwa maneno mengine, inaonakana kama wewe ungekukuwa ni mmoja wa timu ya madaktari ungefanya chochote kumpoteza. Na hili ndo ninalolikemea.
Kweli alikuwa dikteta, fisadi, nk na nguvu ya umma imefanya kazi yake. Jukumu la Wamisri limekamilika la kumuondoa madarakani na jukumu la kumwondoa au kumbakiza duniani sio la binadamu yoyote yule.

Get well soon Hosni Mubarak!
 
Back
Top Bottom