Kodi kwa biashara ya mihadarati???
Naona kama TRA wanakimbia vishindo bila kujua ni vya nini.
Ninaona kushitakiwa kwa rushwa pekee, kunaweza kuongeza ujasiri na kuzalisha wezi zaidi. Kesi kama mara nyingi kama si zote, serikali hupoteza..
Maoni yangu, hii mikiki mikiki ya hosea kuisafisha serikali iionekane imechukua hatua iendelee. Lakini watanzania tunahitaji zaidi ya hapa:-
Kwanza majina ya waliochota Stanbic yawekwe hadharani kwa sababu, yanajulikana na wala siyo kwamba yakisemwa yataharibu upelelezi wakati ni order ya sku moja na kesho benki ya Stanbci wanatoa details na vielelezo vya accounts zote zilizobeba sandarusi.
Tunahitaji kwamba fedha zote zilizotolewa escrwo zirudishwe mara moja na zile za Tanesco zirudi tanesco.
Hatua ya kuwachukulia watumishi wa umma pekee, unawaacha kina singa, ruge na wengine wasio watumishi wa umma ni udhaifu mbaya na ni kulea mafisadi na uhusiano hujumu wa viongozi na majizi.
Kukimbiilia kudai kodi ni kutakatifisha fedha haramu!.