Jamani katika dunia hii hakuna binaadam afananae na malaika. Hata huyo Mwakyembe anayeonekana safi, mkweli, jasiri leo ni kwa sababu hatujui madhambi yake au hajapata nafasi ya kufisadi. Tuombe Mungu JK amuone aingie kwenye cabinet tuuone usafi na uadilifu wake.
Nawaombeni wa JF mimi nikiwa niko pamoja nanyi kuwapa ukweli wa mambo kwa ufupi.
Kashfa anazopewa Dr. Hoseah msingi wake ulianza 2006 wakati KAMAZIMA anakaribia kustaafu. Kuna kambi iliyojipanga kuhakikisha kuwa jina la DR.HOSEAH linafutika katika historia ya TAKUKURU na LILIAN MASHAKA anamrithi KAMAZIMA.
Ninayekupa hizi nilikuwa upande wa kambi ya KAMAZIMA na mipango yao yote naifahamu. Kwa hiyo JF inatumika ili kufanikisha mipango ya wafuatao:
1. LILIAN MASHAKA - MKURUGENZI MKUU aliyekuwa amemshawishi KAMAZIMA ili amririthishe.
Kamazima- aliahidi kutumia nafasi yake akiwa Jeshini kumshawishi RAIS kumpa nafasi hii.
2. AWADHI MOHAMEDI- Mwenye asili ya KIASIA (MWARABU) , alikuwa mshauri Mkuu wa KAMAZIMA na kupanga mipango ya kujipandisha vyeo haraka haraka ili arithi nafasi ya MKURUGENZI WA UCHUNGUZI.
Ni Mwanasheria asiyekuwa na uzoefu mzuri katika uchunguzi. Kwa maana ya kuwa hana
historia ya kuendesha hata kesi moja na kushinda.
3.DATA ZA WENGINEO: Kama ALEX KUHANDA, ROSE WANIHA (aliamua akimbie TAKUKURU baada ya jaribio kuu la kumwondoa Dr. Hoseah Desemba 2006 kushindwa).
Kwa kifupi niko tayari kuwapa DATA kwa undani na uchambuzi zaidi, ninawajua vizuri Dr. Hoseah na mali zake zote, LILIAN MASHAKA na mali zake zote, ROSE WANIHA na mali zake Zote, AWADH MOHAMED na wake zake wote alioishi nao wanaozidi wanne na kuendelea, na wote wanaotumia JAMBO FORUM kuwadaganya wana JF.
Kama kuna mtu ana DATA za kweli, uchunguzi ukifanywa kwa DR. HOSEAH uwaguse wote na uanzie wakati wa KAMAZIMA.
Nawashauri mjadala huu uko wazi na majina ya hao niliowataja na wengine ambao nimewahifadhi kwa leo.
Tuhuma zote za Dr. Hoseah kuhusu mali zake ni za uongo na zinaweza kuthibitishwa kwa maana ya kuwa nyumba inayodaiwa ni kuishi watu wote walioajiriwa 1997 waliikuta ipo huko Mbezi beach, hiyo ya Maswa ametumia mafundi na siyo Kampuni.
Sasa tafakarini wanaJF wenzangu, hivi tangu 1997 hadi 2006 asingekuwa na uwezo wa kujenga nyumba huko Maswa.
Nimefanya uchunguzi binafsi hadi Maswa na Tuhuma zote zina majibu ambayo mimi binafsi nazikubali.
Kumbukeni nimetoka Kambi ya KAMAZIMA na kukubali kufanya kazi na Dr. hoseah nafahamu kila kitu na si vinginevyo.
Ombeni kama ni Uchunguzi uanzie 1997 hadi leo ili mjue kuwa DR. Hoseah yuko makini zaidi.
Mrisho Shabani.