Hoseah na Richmond

mrishog

Member
Nov 7, 2007
7
0
Tumekuwa tukiandika mara nyingi lakini watu wanatupuuza wakifikiri sisi ni wachonganishi lakini ukweli ni kwamba TAKUKURU inaenda pabaya, morale ya wafanya kazi ipo chini.

Sasa twende kwenye hoja yenyewe.

1.Kuhusu uchunguzi wa Richmond na TAKUKURU Mambo yafuatayo yafahamike.

  • Taarifa iliyosomwa kwa vyombo vya habari ni taarifa ya Hoseah na wala siyo ya TAKUKURU. Kwani taarifa ya kweli ya uchunguzi Hosea aliiweka kando ikaandikwa taarifa nyingine ya kuvipa vyombo vya habari na kuwalinda marafiki zake.

  • Matokeo yake wachunguzi wote waliohusika na uchunguzi wa Richmond wakaamishwa makao makuu mara moja kuwaziba midomo. Jk afanye uchunguzi atabaini haya.

  • Mbaya zaidi wakati kamati ya Richmond ikiwahoji wahusika wote Hoseah kwa woga akamtuma mkurugenzi wake wa uchunguzi ndiye ahojiwe na badala yake, yeye akadanganya kwamba amekwenda kutibiwa India wakati alikuwa likizo chikago marekani kwa familia yake. Kamati ya bunge ya uchunguzi wa Richmond imebaini hilo.
Matumizi mabaya ya pesa.
Hoseah ana matumizi mabaya ya pesa , na ufisadi sasa anaufanya ndani ya TAKUKURU. Kwanza alitumia Tsh Mil 170 kukarabati nyumba ya mkurugenzi mkuu, na ukarabati huu haukuwa na tender yeye ndiye aliyechagua mtu wa kufanya kazi hii, sasa kituko ni kwamba baada ya hapo alimpatia rafiki yake huyo tender ya kuzunguka katika ofisi zote za TAKUKURU mikoani na kupiga rangi bila tender kupita , kwa kumwagiza mhasibu mkuu afanye malipo hayo. Sasa inakuja ajabu ni kwamba rafiki yake huyo ndiye anamjengea hekalu huko maswa –Mwanza. Hapo hakuna rushwa kweli, haya mambo ni ya kweli na uchunguzi ukifanyika yapo wazi.

Kama Ikulu inataka iangalia manunuzi yote yaliyofanya na Hoseah tangu aingie madarakani itagundua ukiukwaji wa tarataibu usio mfano na ukijaribu kuoji au kushauri tofauti anakupa adhabu ya kukuamisha.

Kama alivyosema Mwakiembe, watanzania wengi ni waoga, watu waliopo makao makuu wanayajua mengi kuliko sisi tulioko mikoani, lakini wanakaa kimya kwa kuogopa kuamishwa, sijuhi wanafikiri huku mioani tunaishi ndege tu.?

Mambo yanayomlinda Hoseah

  • Kwa sababu kabla ya hapa alikuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi kwa miaka 10, anajua madhambi yote ya viongonzi waliopo madarakani kiasi kwamba anaitumia hiyo kama insurance kwani wakimtoa atawalipua.

  • Baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu na Lilian Mashaka kuteuliwa kuwa naibu Mkurugenzi Mkuu kulitokea pengo la nafasi mbili za mkurugenzi wa uchunguzi na mkurugenzi wa elimu kwa umma, hivyo Hoseah alitumia nafasi hiyo kuteua watu wadhaifu katika nafasi hizo, watu ambao hawawezi kumbishia kwa jambo lolote.
Hii ina implication nyingi, kwanza kwa kumteua mtu dhaifu kuiongoza idara ya uchunguzi ambayo ndiyo kiini cha TAKUKURU inampa yeye nafasi ya moja kwa moja kuingilia shughuli zake. Na kwa kuwa mkurugenzi wa uchunguzi wa sasa (alex mfungo) siyo mwanasheria ni raisi kwake kumzidi ujanja.

Pili nafikiri watu mmeishona vipindi vya TV ambavyo mkurugenzi wa sasa wa elimu kwa umma amewakilisha PCCB, hata maswali yanamshinda kujibu huyu kweli ni mtu wa kuchagulia wakati PCCB ina watu makini wengi tu, wana TAKUKURU tuona aibu kweli kweli.

Ipo haja kwa bunge kuteua kamati kama ya Mwakyembe kwa ajili ya kuchunguza manunuzi na matumizi ya pesa yaliyofanyika TAKUKURU tokea Hoseah achaguliwe kuwa mkurugenzi mkuu kama yanafuata taratibu za PPRA.
 
Duh! Huyu jamaa anaongea kama chiriku..kumbe naye ni fisadi! Nakumbuka niliwahi hudhuria lectures zake pale chuo cha Tanesco Morogoro nikiwa kama PCB recruit. Wakati huo takrima ilikuwa kisheria sio rushwa, lakini yeye alikuwa akisema hadharani kabisa hiyo ni rushwa..nilijenga kweli imani naye sana..japo niliitosa PCB baadaye baada ya kuona kumbe usanii ni moja ya qualifications za kuwa huko...nikakosa qualifications.
Jamanii eee..mbona mafisadi wametuzunguka kila mahali? au nami ni mmoja wao bila kujijua?!!! Inasikitisha, inauma, inakera.....Watz wote tupigane vita hii mbaya.
MUNGU TUSAIDIE
 
Wote mnaoandika nimeona ni watoto wa KAMAZIMA, watu gani nyinyi msiotaka mabadiliko.

Lipi alilofanya Hoseah lililo tofauti na KAMAZIMA. Utaratibu mnaosema kuwa ametumia Hoseah na KAMAZIMA unatofauti gani.

Ninyi tunawajua, makosa yenu mnayajua, msilazimishe kuingia madarakani.

Wewe LILIAN MASHAKA na AWADHI MOHAMED hamkuridhika na mliyofanya kwa kumburuza KAMAZIMA.

Hoseah kweli ana msimamo na maamuzi. Je wakati wa KAMAZIMA mlitangaza hata zabuni moja?, wanafiki ninyi.

Wewe Mrishog usiwe mjinga kuwadanganya watu na kuitumia KAMATI YA MWAKYEMBE kuichafua TAKUKURU.

Wote tuko mikoani wewe nani?

Mrisho Shabani.
 
suala la RDC watu wametolewa Bangusilo,Mmliki wa RDC mbona hajatajwa??DR. Hoseah ni mtu makini sana,ila mammbo ya kuchafuana hayajaanza leo,nitaendelea kumtetea Hoseah sababu nafahamu utendaji kazi wake.Ni mchapakazi .suala la uadilifu sina uhakika nalo.
 
hata mimi namtetea hosea kwa kutupatia taarifa ya kweli kuhusu mkataba wa richmonduli.

na ole wenu mnaompinga mtakuja lipuliwa na hosea hizo dhambi zenu za kifisadi.

Enewei kwa akili ya kawaida inaonekana kuna mtu humu ndani anaongea na kujijibu mwenyewe ktk thread hii. Then nawasihi mheshimu kanuni za JF kutotaja majina ya members humu ohoo, kama mnabisha subirini Invisible akiamka mtaona.....
 
Si vizuri wana jf kupigana mikwala humu kama kuna mtu ana data zinazoonesha upande safi wa Hosea azimwage hapa ili zipingane na ripoti ya Dr. Mwakyembe. Kwa ufupi ni kujibu hoja moja baada ya nyingine ya ile ripoti inayomgusa Hosea.Wakati huohuo watu wasizuiwe kutoa uhuru wao wa maoni,kama yanavyolindwa na ibara ya 18 ya katiba. Maoni sio ushahidi na yanakanushika hivyo sio binding, acheni watu watumie midomo yao. Whats wrong with putting up an agrument? toa hoja usiogope kama hawaitaki wataikataa na ktoa sababu za kufanya hivyo. Lakini hoja si malumbano wala kutajana majina humu.Kila mtu ana uzuri na ubaya wake na ndio maaana Mrisho mpoto anasema "uzuri ni kipimo cha ubaya". Hayo ndio maoni yangu
 
JF

Nakuunga mkono kwa moja kubwa ulilosema 'UONGO WA BABA HUANGAMIZA FAMILIA, NA UONGO WA MWANASIASA HUANGAMIZA TAIFA'.

Mambo ya TAKUKURU ni usiri na unyeti, na wana MKUU wao ambaye ni Rais.TUMWACHIE RAIS AAMUE!

MRISHO SHABANI
 
Si vizuri wana jf kupigana mikwala humu kama kuna mtu ana data

Jamani katika dunia hii hakuna binaadam afananae na malaika. Hata huyo Mwakyembe anayeonekana safi, mkweli, jasiri leo ni kwa sababu hatujui madhambi yake au hajapata nafasi ya kufisadi. Tuombe Mungu JK amuone aingie kwenye cabinet tuuone usafi na uadilifu wake.
 
Hosea hawezi kutueleza ni vipi kamati ya Mwakyembe imeweza kupata ushahidi kibao wa ubadhirifu na ufisadi wakati yeye aliconclude kuwa Richmond safi?

Pia inabidi ajibu hizi tuhuma kuwa aliiweka kapuni ripoti ya ofisi yake na kuandika ripoti yake mwenyewe.

Pia itabidi aeleze kauli yake kuwa kuna rushwa nyingine ni za wakubwa sana na ofisi yake haiwezi kazi hizo.

Hosea inabidi ajiuzulu na ashitakiwe pamoja na Lowassa na AG.
 
Nawaombeni wa JF mimi nikiwa niko pamoja nanyi kuwapa ukweli wa mambo kwa ufupi.

Kashfa anazopewa Dr. Hoseah msingi wake ulianza 2006 wakati KAMAZIMA anakaribia kustaafu. Kuna kambi iliyojipanga kuhakikisha kuwa jina la DR.HOSEAH linafutika katika historia ya TAKUKURU na LILIAN MASHAKA anamrithi KAMAZIMA.

Ninayekupa hizi nilikuwa upande wa kambi ya KAMAZIMA na mipango yao yote naifahamu. Kwa hiyo JF inatumika ili kufanikisha mipango ya wafuatao:

1. LILIAN MASHAKA - MKURUGENZI MKUU aliyekuwa amemshawishi KAMAZIMA ili amririthishe.

Kamazima- aliahidi kutumia nafasi yake akiwa Jeshini kumshawishi RAIS kumpa nafasi hii.

2. AWADHI MOHAMEDI- Mwenye asili ya KIASIA (MWARABU) , alikuwa mshauri Mkuu wa KAMAZIMA na kupanga mipango ya kujipandisha vyeo haraka haraka ili arithi nafasi ya MKURUGENZI WA UCHUNGUZI.

Ni Mwanasheria asiyekuwa na uzoefu mzuri katika uchunguzi. Kwa maana ya kuwa hana
historia ya kuendesha hata kesi moja na kushinda.

3.DATA ZA WENGINEO: Kama ALEX KUHANDA, ROSE WANIHA (aliamua akimbie TAKUKURU baada ya jaribio kuu la kumwondoa Dr. Hoseah Desemba 2006 kushindwa).

Kwa kifupi niko tayari kuwapa DATA kwa undani na uchambuzi zaidi, ninawajua vizuri Dr. Hoseah na mali zake zote, LILIAN MASHAKA na mali zake zote, ROSE WANIHA na mali zake Zote, AWADH MOHAMED na wake zake wote alioishi nao wanaozidi wanne na kuendelea, na wote wanaotumia JAMBO FORUM kuwadaganya wana JF.

Kama kuna mtu ana DATA za kweli, uchunguzi ukifanywa kwa DR. HOSEAH uwaguse wote na uanzie wakati wa KAMAZIMA.

Nawashauri mjadala huu uko wazi na majina ya hao niliowataja na wengine ambao nimewahifadhi kwa leo.

Tuhuma zote za Dr. Hoseah kuhusu mali zake ni za uongo na zinaweza kuthibitishwa kwa maana ya kuwa nyumba inayodaiwa ni kuishi watu wote walioajiriwa 1997 waliikuta ipo huko Mbezi beach, hiyo ya Maswa ametumia mafundi na siyo Kampuni.

Sasa tafakarini wanaJF wenzangu, hivi tangu 1997 hadi 2006 asingekuwa na uwezo wa kujenga nyumba huko Maswa.

Nimefanya uchunguzi binafsi hadi Maswa na Tuhuma zote zina majibu ambayo mimi binafsi nazikubali.

Kumbukeni nimetoka Kambi ya KAMAZIMA na kukubali kufanya kazi na Dr. hoseah nafahamu kila kitu na si vinginevyo.

Ombeni kama ni Uchunguzi uanzie 1997 hadi leo ili mjue kuwa DR. Hoseah yuko makini zaidi.

Mrisho Shabani.
 
Hosea hawezi kutueleza ni vipi kamati ya Mwakyembe imeweza kupata ushahidi kibao wa ubadhirifu na ufisadi wakati yeye aliconclude kuwa Richmond safi?

Pia inabidi ajibu hizi tuhuma kuwa aliiweka kapuni ripoti ya ofisi yake na kuandika ripoti yake mwenyewe.

Pia itabidi aeleze kauli yake kuwa kuna rushwa nyingine ni za wakubwa sana na ofisi yake haiwezi kazi hizo.

Hosea inabidi ajiuzulu na ashitakiwe pamoja na Lowassa na AG.

Good, una mawazo mazuri mno na hata mimi pia niliwaza hivyo hivyo, Jiulize maswali yafuatayo kabla ya kutoa mwelekeo:-

1. Sheria zilizopo zinampa mamlaka Dr. Hoseah kumshitaki mtu mwenye kinga?

2. Kama Kamati ya Mwakyembe ilikuwa makini Kwa nini haikumhoji LOWASSA?

3. Dr. Msabaha katika maelezo yake amesema hivi 'Wakati naondoka Wizara ya Nishati na Madini October 2006, nilikuwa nimezuia malipo yeyote kwa RDC' Je, ni Mazingira gani yalikuwa yakitawala wakati Dr. Hoseah akitoa taarifa hiyo kwa umma!

4. Je, Dr. Hoseah angeweza kuwatuhumu viongozi kabla ya malipo kufanyika?

5. Kamati ilipata fursa kwenda Marekani, Je TAKUKURU waliwezeshwa kwenda Marekani kwa kuzingatia bajeti yao finyu?

6. Je, Dr. Mwakyembe akiombwa apeleke RIPOTI yake mahakamani anaweza kushinda kwa kutumia maoni aliyokusanya?

Ili tuhakikishiwe kuwa taarifa imefanywa kitaalam, KAMATI YA MWAKYEMBE iombwe kuipeleka kesi mahakamani hivyo hivyo ilivyo.

Kumbukeni kuwa KAMATI YA BUNGE ina kinga kwa makosa yoyote yanayotokana na kazi zake lakini DR. HOSEAH akimtuhumu mtu bila ushahidi kamilifu ni tatizo kubwa!

Tafakarini vizuri hayo.

MRISHO SHABANI
 
Asante sana wote mliochangia hapa nawe Mrisho pia asante kwa data zako. Nachofahamu mimi kila binadamu ana makosa yake alowahi kutenda katika maisha yake ambayo yanaelezea upande mwingine wa huyo mtu alivyo ambao hata yeye angependa wengine wasijua. Makosa haya yamefanyika kwa nyakati mbalimbali kulingana na maeneo tulikokuwa mfano.ubadhirifu kwenye pesa za umma humo shule za misingi,sekondari,vyama vya kiraia nk. Kikubwa hapa je.hao watu wamebadilika au je tabia hizo zimeendelea kuwa muhimili wa maisha yao.Hata sisi wana JF inawezekana tu kwakuwa hatujuani au kuna mtu hatujui vizuri inawezekana ni mafisadi wa kutupwa tukipewa serikali ila tu kwa kuwa hatuko huko.Siasa pia ina mengi saa nyingine ni kweli hujahusika kabisa lakini unaguswa na ndio maana ya mtego wa panya wataingia waliokuwamo na wasiokuwamo.Mimi niliwahi kuongoza chama fulani ambacho kabla yake kilikuwa mfu hata hivyo watu waliendelea kuamini kuwa chama kile kilikuwa na mamilioni japo walikuwa hawatoi michango ambayo ndio ilikuwa muhimili wa chama,pamoja na kutumia hadi pesa zangu mwenyewe kwa faida ya chama bado kuna watu walithubutu kusema kuna ufisadi. Sasa mambo haya tuangalie wapo watu kazi yao kuchafua wengine tu japo wao hawawajibiki,lakini kunapotokea uchunguzi wa kina kama ule wa Dr. Mwakyembe ndio maana sote tunadiriki kusema alaa kumbe. Hili la kusema Hosea alikosea kuifagilia Richmond liko wazi kabisa kwani ripoti yake ilichapwa kwenye vyombo vya habari na yeye mwenyewe kwa kauli yake aliongea na vyombo vya habari.

Huu ni udhaifu wa wazi anaopaswa kuwajibika nao,kwani alitudanganya watanzania,ila mengine zaidi ya hapo sote hatuyajui tukae kimya,kama yapo tuyaibue yafanyiwe uchunguzi Rais aamue.Ninyi wote mliokuwa na kambi PCB kila mmoja alikuwa na maslahi yake ambayo nia yake mnaijua wenyewe. Kwa nini muunde kambi kumshaiwshi Rais? macheni Rais aamue ndio maana nashawishika kusema wote nyie yaani KAMAZIMA CAMP na HOSEA Camp mlipotoka.Tuache kupigiana debe kwenye mambo ya kitaalamu.
 
Hosea hawezi kutueleza ni vipi kamati ya Mwakyembe imeweza kupata ushahidi kibao wa ubadhirifu na ufisadi wakati yeye aliconclude kuwa Richmond safi?

Pia inabidi ajibu hizi tuhuma kuwa aliiweka kapuni ripoti ya ofisi yake na kuandika ripoti yake mwenyewe.

Pia itabidi aeleze kauli yake kuwa kuna rushwa nyingine ni za wakubwa sana na ofisi yake haiwezi kazi hizo.

Hosea inabidi ajiuzulu na ashitakiwe pamoja na Lowassa na AG.

Ok, ushahidi wa kama kwenda Bungeni unaweza usiwe na sifa za kusimama mahakamani

Dr. Hoseah ndiye mwenye mamlaka aliyopewa na Rais na hili linaweza kuulizwa na RAIS kwani ndiye mwenye mamlaka juu yake.

Kwa kifupi taarifa ya Mwakyembe ingehitaji maelezo yake kama ilivyo kwa LOWASSA naamani Dr. Hoseah angetoa na si kwenye mtandao kama sisi tunavyofanya.

Au, unaweza kuomba 'appointment' kuja kuuliza maswali kama haya, naamini majibu yake mimi siwezi kutoa kwa kuwa uchunguzi ni siri na ukisema uchunguzi hata hiyo taarifa yake ni siri pia.

MRISHO
 
Asante sana wote mliochangia hapa nawe Mrisho pia asante kwa data zako. Nachofahamu mimi kila binadamu ana makosa yake alowahi kutenda katika maisha yake ambayo yanaelezea upande mwingine wa huyo mtu alivyo ambao hata yeye angependa wengine wasijua. Makosa haya yamefanyika kwa nyakati mbalimbali kulingana na maeneo tulikokuwa mfano.ubadhirifu kwenye pesa za umma humo shule za misingi,sekondari,vyama vya kiraia nk. Kikubwa hapa je.hao watu wamebadilika au je tabia hizo zimeendelea kuwa muhimili wa maisha yao.Hata sisi wana JF inawezekana tu kwakuwa hatujuani au kuna mtu hatujui vizuri inawezekana ni mafisadi wa kutupwa tukipewa serikali ila tu kwa kuwa hatuko huko.Siasa pia ina mengi saa nyingine ni kweli hujahusika kabisa lakini unaguswa na ndio maana ya mtego wa panya wataingia waliokuwamo na wasiokuwamo.Mimi niliwahi kuongoza chama fulani ambacho kabla yake kilikuwa mfu hata hivyo watu waliendelea kuamini kuwa chama kile kilikuwa na mamilioni japo walikuwa hawatoi michango ambayo ndio ilikuwa muhimili wa chama,pamoja na kutumia hadi pesa zangu mwenyewe kwa faida ya chama bado kuna watu walithubutu kusema kuna ufisadi. Sasa mambo haya tuangalie wapo watu kazi yao kuchafua wengine tu japo wao hawawajibiki,lakini kunapotokea uchunguzi wa kina kama ule wa Dr. Mwakyembe ndio maana sote tunadiriki kusema alaa kumbe. Hili la kusema Hosea alikosea kuifagilia Richmond liko wazi kabisa kwani ripoti yake ilichapwa kwenye vyombo vya habari na yeye mwenyewe kwa kauli yake aliongea na vyombo vya habari.

Huu ni udhaifu wa wazi anaopaswa kuwajibika nao,kwani alitudanganya watanzania,ila mengine zaidi ya hapo sote hatuyajui tukae kimya,kama yapo tuyaibue yafanyiwe uchunguzi Rais aamue.Ninyi wote mliokuwa na kambi PCB kila mmoja alikuwa na maslahi yake ambayo nia yake mnaijua wenyewe. Kwa nini muunde kambi kumshaiwshi Rais? macheni Rais aamue ndio maana nashawishika kusema wote nyie yaani KAMAZIMA CAMP na HOSEA Camp mlipotoka.Tuache kupigiana debe kwenye mambo ya kitaalamu.

Good, mawazo yako ni sahihi, RAIS anapaswa kuamua, na masuala ya kitaalamu yasiathiriwe na maslahi binafsi ya watu na kuifanya JAMII FORUMS ya kihuni zaidi.

Pia hata taarifa ya Mwakyembe nashawishika kusema kuwa iliingiliwa na HISIA na kundi fulani linaweza kuitumia ili kufanikisha malengo yake na si ya TAIFA.
 
ndugu yetu mrisho,
nakupa ushauri wa bure jaribu kusoma vizuri kuhusu suala la hiyo kampuni ya richmonduli hapa JF kabla ya kuja na utetezi wako kwa hosea.hapa kila kitu kiliwekwa wazi juu ya hii kampuni mara tu baada ya kushinda zabuni yake.kuwa huko marekani hakuna hiyo kampuni hata kabla ya hosea kufanya uchunguzi wake.lakini kitu cha kushangaza yeye akaja na majibu yake ya kuisafisha hii richimundoli.
Kama wewe ni mpambe wao,basi waliokutuma wamechelewa,rudi kawaambie jamaa wamekwisha amka
 
Good, mawazo yako ni sahihi, RAIS anapaswa kuamua, na masuala ya kitaalamu yasiathiriwe na maslahi binafsi ya watu na kuifanya JAMBO FORUM ya kihuni zaidi.

Pia hata taarifa ya Mwakyembe nashawishika kusema kuwa iliingiliwa na HISIA na kundi fulani linaweza kuitumia ili kufanikisha malengo yake na si ya TAIFA.

Ndugu Shabani

Ukweli uliousema imebidi nikkunge mkono na pia niongezee kwa undani ukweli ambao leo hii wengi wataubishia na kusema ni uwongo, lakini naomba hii posting idumu kwa muda wa miezi sita tu kama haya ninayoyasema hayatathibitika.

1. Dr. Mwakyembe 2. Dr. Mahalu
Hawa ni marafiki wa damu na ni lazima Mwakyembe afanye kila mbinu Mahalu apone kesi yake ya kuliibia taifa zaidi ya bilioni tatu. Aliyeshika bango la kumfunga Mahalu ni Dr. Hosea na uthibitisho ni pale Dr. Mwakyembe anapotoa recommendation kuwa uongozi wa PCB ubadilishwe. Kwa nini anakuwa so specific wala hasemi wawajibishwe wala kuadhibiwa yeye anasema wazi kuwa wabadilishwe. Na lazima Dr. Mwakyembe alipe fadhila kwa Dr.Mahalu kwa vile ndiye aliyempa scholarship kwenda ujerumani wakati Dr. Mahalu akiwa dean wa faculty ya sheria pale mlimani.

Dr.Mwakyembe amejishimbia shimo na uchu wake kupata sifa kwa kuwa-demonise wengine. Yeye kwa kushindwa kuficha hisia zake za ubinafsi na kushindwa kuelewa kuwa mazingara ya tume ake ni tofauti na ya PCCB ni ajabu sana. Yeye nia yake ni Dr. Hosea aondoke ili Dr. Mahalu angalau atafute mbinu mpya za kuponyoka kwa vile kwa Dr. Hosea ni jela tu!
 
menosugu,
Na wewe ni mgeni pia hapa,nsema hivi jamani someni tulikotoka ndio mje na hizi hadithi zenu.lakini ukisema JF walimdanganya hosea hapo nitakubaliana nanyi lakini kinyume na hapo mimi sipo,zaidi ya mfa maji haishi kutapatapa
 
Namfahamu mtu mmoja ambeya huyu Hoseah amemsolicit ampe hela iliafute kesi yake. Huyu jamaa anaandama watu akiwatishia kuwa atawashtaki wasipo mlipa hela. Hilo halina ubishi. sina lolote lakugain in his fall zaidi ya ku2ondolea tanzania element mbaya katika kitengo nyeti cha taifa.

Hoja ya kwamba Dr. Mwakyembe anamuandama ni upuuzi na hata kama ni kweli, it matters not. The fact is TAKUKURU ili toa ripoti ikisema Richmondis clean. That was a falsety considering they had 6months to investigate and full legislative powers.. Kama huu ndio ufanisi wa chombo kikuu cha kupapambana na rushwa, absi tumeisha. PIga Uwa.. Inabidi huyu jamaa awajibishwe... ili tupate TAKUKURU inayo wakamata mafisadi wakubwa na sio askari polisi wanaochukua hela ya chai kwasababu wanalipwa 100,000.
 
Mkuu! Haya yote yametoka wapi? Kinachozungumziwa si ripoti ya Mwakyembe? Hizo vita za ndani za TAKUKURU ukweli wengi hatuna hata haja ya kuzisikia. Kitu kinachogomba ni taarifa ya TAKUKURU na ile ya PPRA na sasa hii ya wakina Mwakyembe. Kama Mkuu una data za kuonyesha kuwa ile taarifa ya TAKUKURU ndiyo iliyokuwa sahihi na hawa wengine walichemsha, ueleze hivyo. Kuyaleta haya mengine kwa bahati mbaya yatazidi kujenga hisia jinsi hiyo idara ilivyo dysfunctional. Hii si sifa nzuri kwa kiongozi makini. Badala ya kumjenga Mkuu, utajikuta unamharibia. Ni ushauri wa bure tu.
 
JF

Nakuunga mkono kwa moja kubwa ulilosema 'UONGO WA BABA HUANGAMIZA FAMILIA, NA UONGO WA MWANASIASA HUANGAMIZA TAIFA'.

Mambo ya TAKUKURU ni usiri na unyeti, na wana MKUU wao ambaye ni Rais.TUMWACHIE RAIS AAMUE!

MRISHO SHABANI

Mkuu Mrisho,

hii siyo nchi ya mtu mmoja tu anayetakiwa kuachwa aamue anachotaka. Ni nchi ya waTanzania zaidi ya 38 million, na tumemwajiri Rais aiongoze nchi hii twende kwenye mafanikio. Anapoharibu mtu wa chini yake, si lazima kusubiri kisichosubirika na wengine wakae kimya tu. PCCB wamejiharibia,wamejishushia hadhi ya taasisi yenye nguvu na ya kuheshimiwa mbele ya jamii. Hatuwezi kuwa na confidence na utendaji wake tena hadi mabadiliko makubwa yafanywe kwenye uongozi.

Kwa kuificha kashfa ya Richmond, taasisi imefeli vibaya mbele ya jamii. hakuna utetezi unaoweza kuisadiai zaidi ya kuanza upya ujenzi wa credibility. Vita ya viongozi wenu humu haiwezi kuwajenga, bali inaonyesha picha chafu ya utovu wa nidhamu, no matter what you say. Kama ingekuwa mnathamini kazi kwa kutunza siri kama unavyosema, usingekuwa unaizungumzia vita ya personal iliyopo kati ya hao unaowataja hapa. Unge analyse kisayansi matatizo yanayoifanya taasisi isiweze kufanya vizuri.
 
Back
Top Bottom