Hongereni wenye kazi nzuri na msiokua na maisha ya shida

Superleta

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
466
538
Hongereni wenye kazi nzuri na msiokua na maisha ya shida

Kuna watu mna bahati sana mmezaliwa mnakuta wazazi wenu wapo vizuri kiuchumi mnakuzwa maisha mazuri kila kitu home kipo yaani ni mboga saba

Shule mmesoma nzuri na za maana, hamna kitu mlikosa maishani, hamzijuwi shida tokea mzaliwe hamjapitia misoto wala nini

Mkamaliza na elimu za juu mkapata kazi nzuri za hadhi zenu, wengine mkafika umri wa kubalehe na kukua mkafanyiwa connection na ndugu zenu au jamaa ambao wapo idara nyeti au vigogo wazito.

Kama umepitia maisha ya hivi mshukuru Mungu sana

Kama umepita misoto pia lakini sasahivi una kazi nzuri au maisha mazuri mshukuru sana Mungu

Ni wachache sana wanapata bahati kama zenu, Yes ni wachache mno.

Na sasa dunia ya sasa bila connection hutoboi sisi tusiojulikana wala tusio na connection na hatujulikani popote wacha tujidodoe na digrii zetu.....Inauma sana kupitia haya....
 
Sasa bwanamdogo cha kufanya ni wewe kujitoa kafara ili uzao wako usiishi maisha yako.

Hao unaoon wako vyedi baba au babu zao walijitoa kafara, wakahustle ili vizazi vyao virithi ukwasi.

Ukiendelea na masikitiko bila ya jitihada basi na mwanao nae atakua kama wewe.
 
Ridhika na unachopata halafu pambana kupata zaidi ya hicho kamwe usije ukajilinganisha na yoyote hapa duniani.

Ishi maisha yako.

Pambana kadiri uwezavyo narudia tena kamwe usitamani maisha ya wengine ishi maisha yako wala maisha yako yasikufanye mnyonge kwa walio nao.

Usiendekeze pombe,wanawake, starehe kuwa wa tofauti hata kama kundi kubwa la watu lisipo kuelewa as long as unajielewa mwenyewe inatosha.
 
Kwenye hali hiyo usichague kazi anza sifuri
Mimi pia ni muumini wa kuanza sifuri..ukijua tu kile unatakiwa kufanya ukaweka nia over a time huwez kuwa pale pale.
Nilichojifunza ni kwamba kulia lia hakutakaa kukubadilishie hali.
Mambo yakikuzidia, badala ya kulalamkka unatafuta chemba unalia kiume ukitoka hapo like nothing happened.

Sumu kubwa ya maisha ni kupenda kujionea huruma na vile kutaka watu wakuonee huruma hapo lazima upotee tu
 
Hata hao unaodhani wanaogelea kwenye raha nao wana matatizo yao,maisha ya hii dunia ni mafupi yaliyojaa stress tu.
Yan kwakifupi hao anaowaona wana raha ni kwamba wameamua kukubliana na changamoto walizo nazo na wamejijengea utayar wa kukabiliana nazo. Hakuna asiye na changamoto ni vile tu watu wameamua kuzipokea na kushughukika nazo. Angejua mapambano ya hao anaowataman unaweza ukaona bora ukae kwa kutulia
 
The three reality of life

1 • Life is not easy
2• Life is difficult
3• Life is difficult to everyone

Maumivu unayoyasikia sio kwako tu hata sisi tuliozaliwa hizo familia bora tunayasikia ,isipokuwa sisi tumeachagua kukaa kimya na kushukuru hivyo usiishi maisha ya kuamini kuwa sisi wenzako tunafuraha na Amani kukuzidi wewe, utajiumiza bure.
 
Hongereni wenye kazi nzuri na msiokua na maisha ya shida

Kuna watu mna bahati sana mmezaliwa mnakuta wazazi wenu wapo vizuri kiuchumi mnakuzwa maisha mazuri kila kitu home kipo yaani ni mboga saba

Shule mmesoma nzuri na za maana, hamna kitu mlikosa maishani, hamzijuwi shida tokea mzaliwe hamjapitia misoto wala nini

Mkamaliza na elimu za juu mkapata kazi nzuri za hadhi zenu, wengine mkafika umri wa kubalehe na kukua mkafanyiwa connection na ndugu zenu au jamaa ambao wapo idara nyeti au vigogo wazito.

Kama umepitia maisha ya hivi mshukuru Mungu sana

Kama umepita misoto pia lakini sasahivi una kazi nzuri au maisha mazuri mshukuru sana Mungu

Ni wachache sana wanapata bahati kama zenu, Yes ni wachache mno.

Na sasa dunia ya sasa bila connection hutoboi sisi tusiojulikana wala tusio na connection na hatujulikani popote wacha tujidodoe na digrii zetu.....Inauma sana kupitia haya....
Mtu kama Riz1 shida anazisikia tu.
 
Back
Top Bottom