Mkuu nami siamini sana juu ya hii tetesi ila naomba kutoa ufafanuzi kidogo. Kwa sasa ngazi ya TGTS D1 ni 532000 na TGTS E1 ni 720,000 kabla ya makato yoyote, lakini kwenye bajeti mpya mishahahara yote itapanda, kwa hiyo labda mleta mada anamaanisha kuwa TGTS E1 itapapanda toka 720,000 za sasa mpaka hiyo 850,000. Kwa maelezo yake ni kwamba serikali itawapandisha daraja moja moja kila mwalimu sambamba na hongezeko la kawaida yaani wale wanaostahilikuwa daraja la C sasa wanapelekwa D na kuendelea hivyo mpaka mwisho, kama wakiamua wanaweza na sio ajabu kwa serikali kupandisha mishahara ya kada moja na kuacha zingine, walishafanya hivyo kwa kada za afya na sheria. Kituko kikubwa kipo wizara za Kilimo na Mifugo, watu waliosoma chuo kimoja kozi moja na wameajiriwa siku moja na wizara moja ila idara tofauti wanatofautiana mishahara kwa zaidi ya mara tatu. Kwa mfano ngazi ya TGS D1 kwa idara za ugani na mafunzo ni 520,000 wakati wa idara ya utafiti wanapewa 1,400,000 wakati wamesoma kozi moja na kituo chao cha kazi ni kimoja. Kwa serikali hii hakuna cha kushangaa.