Hongereni NSSF kwa kufanya hivi


Game Theory...
Kama huyo MD wa NSSF ni muislam tumpe zake pongezi! Lakini kama ni Mkristo tomzomee kwa nguvu zetu zote!
 
niliwai kuandika post juu ya Nssf na mashirika kama haya. huu ni mfano mzuri lakini sidhani mtu akifanya wajibu anaotakiwa kufanya anatakiwa apate hongera. haki ya polisi kama mfannyakazi yeyote ni kuapta makazi bora na wajibu wa NSSF wanakusanya pesa za wadau ni kusaidia katika kwenye mambo kama haya.

Pilii hii ni part ya solution sio solution kamili . sababu nyumba hizi si mali ya ya hao polisi. Je hao polisi wakistaaafu wataenda kushi kwenye nyumba gani? Kwa sababu mashirika kama haya yanakusanya hela kwa ajili ya pension za wadau lilenge kwenye miradi amabayo mstaafu kweli akistaafu hata akiwa hana pesa ataona shirika lilimfaaa.
 


Kujenga nyumba kwa ajiri ya jamii ni vyema sana na ninatoa suport kubwa kwa NSSF. Na pia kama wengine walivyosema MIFUKO yote ya hifadhi za jamii yaani PPF, PSPF , NHIF, CWT LAPF, yote inatakiwa kutoa mifano ya kuigwa kwa manufaa ya jamii. Kwani kwa mfano Chama Cha Walimu kinakusanya pesa nyingi sana, lakini hakijawahi kuwekeza kwenye nyumba za walimu wakati ndiyo wanaotoa hizo pesa!!! Hivi kingeamua hata kujenga nyumba Mbili kila Wilaya kwa mwaka kingeshindwa??? .Viongozi walioko huko wamelala na kujinufaisha wenyewe.

Kuhusu gharama halisi ya project ni muhimu sana kuuliza kwani ufisadi mkubwa hufanyika huko, Hao Auditors unaosema '' Most of them they are good as nothing'' Most auditors niliokwisha kutana nao wakishapewa fupa tu, huandika report nzuri ya kumsifu mwajiri wao kwa wakati huo ambaye huwa ni Mkurugenzi wa hizo kampuni au mashirika. Kwanza Auditor ni wewe MD ndiyo unawapa kazi, na wakikuharibia next year huwapi kazi!!! What do you expect.!!!

Umeomba akupe mfano wa matumizi mabaya ya pesa za project !!! Ina maana wewe upo Tz hii au huwa unafunga masikio pindi anayetuhumiwa anapokuwa kipenzi chako??!! Project ya kununua Magodown pale ubungo toka NSSF na Manji kwa Bil. 3 na kuyakarabati kwa pesa ya NSSF Bil. 9 na kuyauza kwa NSSF kwa Bil. 40 siyo matumizi mabaya hayo ya pesa za project??????!!!

Tusiwe biased wakati tunataka kutoa ukweli ili tusaidie taifa letu. Hata kama mtu ni kipenzi chako, akiharibu mwambie ukweli, na akifanya vizuri mpe haki yake.
 

mwamuuu,punguza mwamu chonde chonde watajua haokama kakayo huyooo!!!
 
chama cha walimu ni trade union na kazi yake ni kuwatetea walimu na kadhalika lakini hawakusanyi hela za kutosha kujenga...
kato lao ni dogo sana
 


Duh hiyo kali
$ 1.3 + $ 5.6 = $ 6.9, Sold for $ 6.5
Profit: $6.5 - $ 6.9 = $ -0.4 Mil, Tsh - 700,000,000/= ( Loss)
Excluding Labour+allowances za wasimamizi, extra duty and misleneous

Na wasiwasi aliyeuziwa anauhusiano na viongozi wa NSSF
 
Last edited:
chama cha walimu ni trade union na kazi yake ni kuwatetea walimu na kadhalika lakini hawakusanyi hela za kutosha kujenga...
kato lao ni dogo sana



Mmnnnn E bwana unasema wanakusanya kidogo??

Wanakata 2% of the salary ya kila mwalimu Tanzania. Tuchukue mfano mmoja wa walimu wa kima cha chini kabisa wanolipwa 150,000/= kwa mwezi 2% x 150,00 = 3000/= na kuna walimu zaidi ya 100,000/= the minimum you can get ni 300,000,000/= kwa mwezi, hapo tumeacha wenye mishahara ya hadi 600,000/= siku hizi wapo wengi tu.

Huoni wangeweza kuwekeza hizo pesa, na wakawa wanajenga nyumba za kuwapangisha walimu wanaohangaika kila kukicha nyumba???? kujenga lile jengo mwalimu house kunamsaidia nini mwalimu.
 
hawa nssf wanajipendekeza tu kwa polisi,kwanini wasijenge nyumba pale manzese ili watu waishi sehemu nzri
 
wanajua polisi hawatawapelleza kwa ufisadi wao wa kula mafao ya waliokufa na wasiodai
 
wanajua polisi hawatawapelleza kwa ufisadi wao wa kula mafao ya waliokufa na wasiodai

Ndiyo maana jana wamefungua jengo la PCCB lililojengwa na NSSF ili PCCB nayo isiwafuatefuate wanapokula hizo deal zao
 
hawa nssf wanajipendekeza tu kwa polisi,kwanini wasijenge nyumba pale manzese ili watu waishi sehemu nzri

Ungeliza ungeambiwa

mbona husemi nyumba za kule Tabata au siyo nyumba zile

ningekutonya kuhusu nyumba lakini unaonekana jeuri sasa utakula Jeuri yako
 
Ndiyo maana jana wamefungua jengo la PCCB lililojengwa na NSSF ili PCCB nayo isiwafuatefuate wanapokula hizo deal zao

unajua sina hata la kukujibu

na ile University of Dodoma ili iweje? wafanyakazi wa NSSF wasome bure?

Daraja..watumie wanachama wa NSSF peke yao au vipi?

kazi kweli kweli
 
unajua sina hata la kukujibu

na ile University of Dodoma ili iweje? wafanyakazi wa NSSF wasome bure?

Daraja..watumie wanachama wa NSSF peke yao au vipi?

kazi kweli kweli

GT,
kwa hili naungana na wewe 100% kuwapa NSSF pongezi. Wanakotoa hizo pesa sitaki kujua, lakini wanaonesha kwamba wanawajali wananchi. Wameanza na Polisi, PCCB, Chuo kule Dodoma na itafika wakati watawafikia wananchi wengine, kila safari ina mwanzo.
 
 
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…