Nyumba za NSSF: Balozi wa Shirika awaita potential customers mafala na mabwege

Bu'yaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,502
1,398
Kupitia balozi wa shirika, Steven Mengere, NSSF imesema mtu ambae hamiliki nyumba au atakufa hana nyumba basi ni fala, bwege na mbwiga. Na kwamba tutumie fursa waliyotuletea ya kumiliki nyumba.

Hebu tuchambue huu mradi halafu tuangalie ufala wetu na ubwege ukoje au nani kati yetu sisi na NSSF ndio fala na bwege.

Mradi mpya wa NSSF Kigamboni Dungu ni wa mpangaji mnunuzi. Lazima umalize malipo ndani ya miaka 15 ( miezi 180).

Bei za nyumba:

mil 131
mil 148
mil 192
mil 232
mil 492

Bei wamesema zinatofautiana kwa sababu ya material oliyotumika pamoja na ukubwa.

Lakini zote zina vyumba vitatu kasoro ile ya mil 500 yenye vyumba 4. Kwa hiyo hizi za mil 130, 150, 200, 240 zote kimsingi zinatofautiana kwa quality ya materials.

Kwa hiyo hii ya mil 130 ukinunua ni Mchina mtupu. Naongea kwa experience, NSSF wanashtakiwa mahakamani kwa kuuza nyumba mbovu kwa bei ya kilanguzi. The fact kwamba wanakuja kututangazia nyumba za mradi mpya zina tofauti ya material ina maana hawajajifunza! Wanaoishtaki NSSF wameleta evidence mahakamani kwamba wamelazimika kuzi overhaul na kujenga upya kasoro pagale na kwamba wanajuta kuzinunua na kwamba wamgeweza kujenga kivyao nyumba bora zaidi kwa unafuu zaidi.
(NSSF bisheni kama hamjashtakiwa mahakamani.)

Basi tuseme tunanunua ya juu kidogo bri kiwango cha kati labda ina ubora zaidi. Milioni 192

Milioni 192 minus 10% ya downpayment divide by 180 month = rent TSH 960, 000

960,000/= kwa mwezi, miaka 15 unalipa.

Hujajenga ya kwako mbali na hizi apartment za NSSF ? Kwenye kiwanja chako private, na muundo unaotaka wewe na mafundi wa kuwasimamia wenyewe? Tena ambayo utahamia baada ya miaka miwili mitatu au mitano ukichelewa sana halafu utamalizia taratibu bila stress ya kudaiwa 960, 000/= kila mwezi

Na unajuaje 10 years, 15 years from now utakuwa na kipato cha 960 000 kila.mwezi ya kulipia mafleti haya ambayo baadae yatakuja kuonekana kama. Mafleti ya Polisi Msimbazi choka mbaya manake si kila mtu ata keep up na maintenance. Ununue nyumba mafletini umekuwa Mhindi?

Steve Nyerere na NSSF msitumie lugha ya matusi wakati mradi wenyewe atakaeingia huo mkenge ndio anaweza kuwa fala zaidi.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
42,845
110,287
Hizi hela za watumishi wa umma ni tamu sana, zinaliwa namna hii kupitia miradi uchwara

Watu wanajenga hadi vighorofa kwa chini ya Milioni 100, tena hapo ni gharama yote kuanzia kiwanja, ujenzi wote

Dr. Wansegamila kale kamjengo chako si hakajazidi 100M hadi kukamilika?
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
15,686
13,194
Biashara ya nyumba ni ukichaa kwa tz, nyumba gharama kubwaaa kisa wameiba kipindi cha ujenzi
 

Juma1967

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
20,731
23,916
Kupitia balozi wa shirika, Steven Mengere, NSSF imesema mtu ambae hamiliki nyumba au atakufa hana nyumba basi ni fala, bwege na mbwiga. Na kwamba tutumie fursa waliyotuletea ya kumiliki nyumba...
Hamna picha?
 

Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
2,154
3,883
Watu wanakosa kabisa vitu vya maana wanakwenda kuhangaika na steve mpiga dili,ovyo kabisa .
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom