Hongereni CHADEMA Kwa Kuwang'oa Wasaliti

Hongereni CHADEMA Kwa Kuwang'oa Wasaliti

Wajinga ndio waliwao, endelea kuamini kuwa kila anayetofautiana na chama ni msaliti. Kafulira alifukuzwa CHADEMA na kuitwa sisimizi, mbona leo amepewa uwaziri kivuli na Mbowe ambae alimuona sisimizi alipokuwa CHADEMA?

Huyu unayemuita msaliti alisema vyama vya siasa vikaguliwe mkasema anatafuta umaarufu, mbona leo ripoti ya CAG kwa mwaka 2013 inaonesha kuwa CHADEMA ilipata hati yenye mashaka kutokana na kufanya manunuzi bila idhini ya bodi? Si mnasema CHADEMA inazingatia kanuni na taratibu, mbona kwenye manunuzi hizo taratibu hazizingatiwi? kuna tofauti gani sasa ya CHADEMA na CCM? hamka ndugu acha kutumika kama toilet paper.

Kwenye siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu, CHADEMA ilisema CUF ni CCM B na inafuata sera ya ushoga, mbona leo wako wote UKAWA? CUF imebadilika na kuacha kufuata sera za ushoga au CHADEMA ndio kigeugeu?

Aliondoa wagombea wetu watatu ili achukue mshiko kwa Mkono, Pinda, Dewji.....
 
kwa kitendo cha cdm kumfukuza naibu katibu mkuu nawapa hongera sana. zitto ukiangalia kwa macho manne ni dhahiri alikuwa msaliti
Ukitaka kujua Usaliti wake nikipindi kile umwambie twende kwenye mikutano ya Chama atatoweka kama mkaa uliowashwa moto utakachoona ni jivu tu
 
Sasa ni dhahiri kwamba Inteligensia ya CHADEMA ni moto wa kuotea mbali. Kama mliweza kumwondoa kabla ya kusababisha madhara je akiwa nje ndo ataweza kuwadhuru?

Kwa mujibu wa matendo, maneno na mwenendo sasa Naamini kwamba siku za CCM na wapambe wao zinahesabika. Hivi kweli hatukumbuki Maandiko yanavyosema Juu ya Usaliti na Uasi?

Shetani alipomuasi Mwnyezi Mungu alipata wafuasi wengi na akashangiliwa kwa MBWEMBWE kibao lakini baada ya muda mfupi tu Ukweli ulidhihiri.

Karibuni sana ACT-WAZALENDO tuwasikilize na mtupatie maneno ya kumfurahisha Mkoloni mweusi. Ikumbukwe kwamba Hata Kaburu na wakoloni walikuwa na Mamluki lakini siku ya kuwang'oa ilipofika walijiondokea bila Jasho.

Wasaliti huwa adhabu yao ni kuchomwa moto.... sheria ya nchi hii imelala sana
 
Kama ni msaliti kama mnavyoamini kwa nini msimuwache tuone jinsi atakavyoharibikiwa kama yuda iskariote.

Tumuache kwani kuna mtu amemshika huyo Mfalme wa ACT?
 
Naona mnaelekea kumsahau adui yenu mkubwa na kuwekeza nguvu nyingi kuishambulia ACT na kiongozi wake mkuu ndugu Zitto utadhani ndio chama tawala.

Unamjua Adui wetu ni nani?

Adui yetu ni CCM na mawakala wake wote.
 
Naona mnaelekea kumsahau adui yenu mkubwa na kuwekeza nguvu nyingi kuishambulia ACT na kiongozi wake mkuu ndugu Zitto utadhani ndio chama tawala.
Usijitoe ufahamu wa Kusahaulisha kwa ile pesa yenu mliompa yakuhujumu Chadema
 
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Utabiri kinzani na mchanganyiko:

NAVAA VIATU VYA "SHEIKH YAHYA" KWA MUDA.!

Apumzike kwa amani huko alipo mnajimu mkuu, ustaadh, mtaalamu wa nyota na anga za mbali, bingwa wa kusoma alama za nyakati, mtaalamu wa kuita na kufukuza majini marehemu Sheikh Yahya Hussein. Miaka kadhaa baada ya kifo chake leo naomba kurithi kazi yake japo kwa dadika chache.

Nimesoma interview ya leo ya ZZK na gazeti la JamboLeo ameeleza juu ya umakini wa usalama wa taifa. Amesema wanaopuuza usalama wa taifa ni watu ambao hawafikiri vizuri.

Kauli hii ya ZZK imenifanya nijaribu kuunganisha dots na hivyo kuweza kufanya utabiri wangu vzr.

Dot ya kwanza. Siku chache zilizopita maafisa wa juu wa Usalama wa taifa waliripotiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Ndg.Edward Lowassa na kuwa wanamuunga mkono kwny mbio zake za Urais. Usalama wanaodaiwa kumuunga mkono Lowassa ndio haohao ZZK anawasifia leo kuwa wako makini.

Dot ya pili. ZZK wakati anafukuzwa CHADEMA alisema ipo siku atakuwa kiongozi mkubwa nchini na eti chadema watamheshimu kwa hilo.

Dot ya tatu. Fedha nyingi na nguvu kubwa inayotumika kukitangaza chama cha ACT inatoka wapi?

UTABIRI.!

Mpango wa ZZK kuanzisha chama cha ACT wakati akiwa bado mwanachama wa CHADEMA ni mpango ulioratibiwa vizuri na usalama wa taifa wanaomuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa.

Lowassa is very strategic person. Anajua kuwa hawezi kupitishwa na CCM kugombea Urais. So ametafuta chama mbadala. Chama ambacho kitamfanya ashinde kirahisi.

Lowassa anajua kuwa akijiunga CHADEMA hatapokelewa na hata akipokelewa hawezi kupewa nafasi ya kugombea Urais. So ndoto yake itakuwa imekufa. Sasa afanyeje ili agombee nje ya CCM na kushinda?

Mbinu aliyotumia ni kuanzisha chama ambacho kitapata support CCM na upinzani. Na chama hicho ni ACT.

Alichofanya Lowassa ni kutafuta mtu mwenye ushawishi ndani ya CHADEMA ambaye akiondoka anaweza kuhama na wafuasi wengi. Na mtu huyo ni ZZK.

So ZZK kazi yake kubwa ni kuibomoa CHADEMA. Aondoke na wafuasi wengi wa CHADEMA kwa kadri iwezekanavyo. Ndio maana hadi sasa hatujasikia mtu kutoka TLP, UDP au PPT Maendeleo, kajiunga na ACT. Wengi tunaowasikia wametoka CHADEMA. Hiyo ndiyo kazi aliyopewa ZZK. Kuibomoa CHADEMA.!

Na wapo wabunge kadhaa wa CHADEMA watakaojiunga na ACT baada ya bunge kuvunjwa (baadhi majina tunayo). Wamehofia kujiunga sasa hivi kwa sababu watapoteza "kiinua mgongo" chao kama ilivyokua kwa Fredy Mpendazoe mwaka 2010. So baada ya bunge kuvunjwa mwezi July kuna utitiri wa wabunge wa CHADEMA watajiunga ACT.

Baada ya hapo Lowassa mwenyewe atajiunga ACT akifuatwa na mamia ya wabunge wa CCM na mawaziri lukuki. Wapo wafuasi na viongozi wa vyama vingine vya upinzani ambao nao watajuinga ACT. Kufikia hapo ACT kitakuwa chama tishio kwa CCM na upinzani maana kina wafuasi kutoka chama tawala na upinzani.

Wakati CCM na CHADEMA wakiwa kwenye taharuki ya mpasuko kwenye vyama vyao, ACT watatumia fursa hiyo kujinasibu na kujitafutia uhalali kwa wananchi. Ushawishi wa Lowassa na ZZK utawafanya watu wengi wajiunge na ACT kutokea CCM na Upinzani hasa CHADEMA.

Wakati wa uchaguzi ACT itapata kura nyingi kutoka kwa waliokua supporters wa CHADEMA na waliokua supporters wa CCM na vyama vingine vya upinzani. So ACT itapunguza kura za CCM na za CHADEMA kisha watachanganya pamoja na kudeclare ushindi.

Baada ya hapo Edward Lowassa atatangazwa Rais kupitia ACT na ndipo atamteua ZZK kuwa Waziri mkuu. Na hapo ndipo litakapotimia lile neno la ZZK kuwa "ipo siku nitakuwa kiongozi mkubwa nchini na CHADEMA wataniheshimu"

Mkakati huu unadaiwa kupangwa kwa ustadi mkubwa na Usalama wa taifa ndio maana ZZK amediriki kusema "wanaobeza usalama wa taifa hawajui kazi yake".

‪#‎MWISHO WA UTABIRI‬.
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Copy and paste...
Haya ndugu Rasheed tunasubiri kuona kama utabiri wako utakuwa na ukweli wowote.
 
Huu utabiri waweza kuwa kweli, act which historically at once was funded by ccm will betray the agreement contract btn the two parties.
 
Ccm wanahasiri sana na Ceo maana yale makubaliano yakuvuruga Chadema Yalishindikana
 
Wajinga ndio waliwao, endelea kuamini kuwa kila anayetofautiana na chama ni msaliti. Kafulira alifukuzwa CHADEMA na kuitwa sisimizi, mbona leo amepewa uwaziri kivuli na Mbowe ambae alimuona sisimizi alipokuwa CHADEMA?

Huyu unayemuita msaliti alisema vyama vya siasa vikaguliwe mkasema anatafuta umaarufu, mbona leo ripoti ya CAG kwa mwaka 2013 inaonesha kuwa CHADEMA ilipata hati yenye mashaka kutokana na kufanya manunuzi bila idhini ya bodi? Si mnasema CHADEMA inazingatia kanuni na taratibu, mbona kwenye manunuzi hizo taratibu hazizingatiwi? kuna tofauti gani sasa ya CHADEMA na CCM? hamka ndugu acha kutumika kama toilet paper.

Kwenye siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu, CHADEMA ilisema CUF ni CCM B na inafuata sera ya ushoga, mbona leo wako wote UKAWA? CUF imebadilika na kuacha kufuata sera za ushoga au CHADEMA ndio kigeugeu?

Dhambi ya usaliti haina rangi ya kuipaka ikapendeza..... Zitto ni zaidi ya msaliti usipoteze muda.

Hakuna mtu mnafiki na mwenye njaa kama Zitto, Ukitaka kujua lijamaa linapenda vyeo angalia alivyoanzisha mgogoro na mwenyekiti wake, kiasi cha kumpa mipaka ya kazi yake. Hapo ndipo tunapoamini Anna Mghwira ni Mwenyekiti wa chama, wakati Zitto ni mmiliki wa Chama, ndiyo maana ni yeye tu anaweza kufanya maamuzi yake toka mfukoni.

Hata hivyo Zitto hana ujanja zaidi ya kujikakamua na li ACT lao ili maccm wamwone bado ana move kuivuruga CHADEMA, baada ya kushindwa kuiua CHADEMA akiwa ndani ya CHADEMA. Sasa anajitahidi kujitutumua akiwa nje nyooooooooo!

Kelele za Zitto za kipuuzi zinaisaidia chadema kupanda na kuchukua Dola bila yeye na wapumbavu wenzio kujua!
 
Usijitoe ufahamu wa Kusahaulisha kwa ile pesa yenu mliompa yakuhujumu Chadema
Pesa ipi tena ndugu? Mimi hela yangu ya kula tu ninapambana mpaka kijasho kinanitoka halafu nimpatie mtu baki tu bila sababu ya msingi? Nyooooooooooo! Ndugu inabidi mjifunze kuelewa kuwa siyo kila anayehoji maandiko yenu kuhusu ACT au Zitto basi ni mfuasi au mfadhili wake. Kama umefuatilia vyema maandiko yangu ya nyuma utajua vyema ninachoongea.
 
Usaliti ndani ya CHADEMA hatovumilika kwa gharama yoyote .
 
Mbona kila siku mnaanzisha thread mpya kuhusu Zitto? Ukisikia obsession ndio hiyo.

Mkuu usiwe myopic in vision and thinking. Think Big, Think globally

ACT ni CCM na CCM ni ACT. Hapa M-saliti ZZK kafika bei na anatumika. TISS walimsoma vizuri wakajua anapenda sana madaraka na publicity, hapo hapo wakamchomekea na kumvuna Zitto.

Once again ACT ni CCM ipo makusudi kuvuruga upinzania ndio maana wenye akili zao wanawapiga kweli kweli hawa manyang'au hasa Le Great King Ayatoll-ah ZZK
 
CEO WA ACT kutokewa ilikuwa lazima maana MKUU WA USALAMA PALE DODOMA YULE MAMA ALIFIKIA ATUA YA KUOMBA WAWEKE UZIO ILI ZITTO ASIONEKANE KWENYE NYUMBA MPYA ILIYOKUNGULIWA.

That is exactly what the guy wanted and he finally achieved. To be a CEO of the Party. Teh teh teh...
 
Pesa ipi tena ndugu? Mimi hela yangu ya kula tu ninapambana mpaka kijasho kinanitoka halafu nimpatie mtu baki tu bila sababu ya msingi? Nyooooooooooo! Ndugu inabidi mjifunze kuelewa kuwa siyo kila anayehoji maandiko yenu kuhusu ACT au Zitto basi ni mfuasi au mfadhili wake. Kama umefuatilia vyema maandiko yangu ya nyuma utajua vyema ninachoongea.
Usaliti hautavumilika kwa namna yoyote ile usiku asubui na mchana
 
Back
Top Bottom