Kama ni msaliti kama mnavyoamini kwa nini msimuwache tuone jinsi atakavyoharibikiwa kama yuda iskariote.
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Utabiri kinzani na mchanganyiko:
NAVAA VIATU VYA "SHEIKH YAHYA" KWA MUDA.!
Apumzike kwa amani huko alipo mnajimu mkuu, ustaadh, mtaalamu wa nyota na anga za mbali, bingwa wa kusoma alama za nyakati, mtaalamu wa kuita na kufukuza majini marehemu Sheikh Yahya Hussein. Miaka kadhaa baada ya kifo chake leo naomba kurithi kazi yake japo kwa dadika chache.
Nimesoma interview ya leo ya ZZK na gazeti la JamboLeo ameeleza juu ya umakini wa usalama wa taifa. Amesema wanaopuuza usalama wa taifa ni watu ambao hawafikiri vizuri.
Kauli hii ya ZZK imenifanya nijaribu kuunganisha dots na hivyo kuweza kufanya utabiri wangu vzr.
Dot ya kwanza. Siku chache zilizopita maafisa wa juu wa Usalama wa taifa waliripotiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Ndg.Edward Lowassa na kuwa wanamuunga mkono kwny mbio zake za Urais. Usalama wanaodaiwa kumuunga mkono Lowassa ndio haohao ZZK anawasifia leo kuwa wako makini.
Dot ya pili. ZZK wakati anafukuzwa CHADEMA alisema ipo siku atakuwa kiongozi mkubwa nchini na eti chadema watamheshimu kwa hilo.
Dot ya tatu. Fedha nyingi na nguvu kubwa inayotumika kukitangaza chama cha ACT inatoka wapi?
UTABIRI.!
Mpango wa ZZK kuanzisha chama cha ACT wakati akiwa bado mwanachama wa CHADEMA ni mpango ulioratibiwa vizuri na usalama wa taifa wanaomuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa.
Lowassa is very strategic person. Anajua kuwa hawezi kupitishwa na CCM kugombea Urais. So ametafuta chama mbadala. Chama ambacho kitamfanya ashinde kirahisi.
Lowassa anajua kuwa akijiunga CHADEMA hatapokelewa na hata akipokelewa hawezi kupewa nafasi ya kugombea Urais. So ndoto yake itakuwa imekufa. Sasa afanyeje ili agombee nje ya CCM na kushinda?
Mbinu aliyotumia ni kuanzisha chama ambacho kitapata support CCM na upinzani. Na chama hicho ni ACT.
Alichofanya Lowassa ni kutafuta mtu mwenye ushawishi ndani ya CHADEMA ambaye akiondoka anaweza kuhama na wafuasi wengi. Na mtu huyo ni ZZK.
So ZZK kazi yake kubwa ni kuibomoa CHADEMA. Aondoke na wafuasi wengi wa CHADEMA kwa kadri iwezekanavyo. Ndio maana hadi sasa hatujasikia mtu kutoka TLP, UDP au PPT Maendeleo, kajiunga na ACT. Wengi tunaowasikia wametoka CHADEMA. Hiyo ndiyo kazi aliyopewa ZZK. Kuibomoa CHADEMA.!
Na wapo wabunge kadhaa wa CHADEMA watakaojiunga na ACT baada ya bunge kuvunjwa (baadhi majina tunayo). Wamehofia kujiunga sasa hivi kwa sababu watapoteza "kiinua mgongo" chao kama ilivyokua kwa Fredy Mpendazoe mwaka 2010. So baada ya bunge kuvunjwa mwezi July kuna utitiri wa wabunge wa CHADEMA watajiunga ACT.
Baada ya hapo Lowassa mwenyewe atajiunga ACT akifuatwa na mamia ya wabunge wa CCM na mawaziri lukuki. Wapo wafuasi na viongozi wa vyama vingine vya upinzani ambao nao watajuinga ACT. Kufikia hapo ACT kitakuwa chama tishio kwa CCM na upinzani maana kina wafuasi kutoka chama tawala na upinzani.
Wakati CCM na CHADEMA wakiwa kwenye taharuki ya mpasuko kwenye vyama vyao, ACT watatumia fursa hiyo kujinasibu na kujitafutia uhalali kwa wananchi. Ushawishi wa Lowassa na ZZK utawafanya watu wengi wajiunge na ACT kutokea CCM na Upinzani hasa CHADEMA.
Wakati wa uchaguzi ACT itapata kura nyingi kutoka kwa waliokua supporters wa CHADEMA na waliokua supporters wa CCM na vyama vingine vya upinzani. So ACT itapunguza kura za CCM na za CHADEMA kisha watachanganya pamoja na kudeclare ushindi.
Baada ya hapo Edward Lowassa atatangazwa Rais kupitia ACT na ndipo atamteua ZZK kuwa Waziri mkuu. Na hapo ndipo litakapotimia lile neno la ZZK kuwa "ipo siku nitakuwa kiongozi mkubwa nchini na CHADEMA wataniheshimu"
Mkakati huu unadaiwa kupangwa kwa ustadi mkubwa na Usalama wa taifa ndio maana ZZK amediriki kusema "wanaobeza usalama wa taifa hawajui kazi yake".
‪#‎MWISHO WA UTABIRI‬.
[21:52, 4/11/2015] Jackson Teshs SUA: Copy and paste...👆👆