Hongereni CCM: Nitaendelea kuwa Mpinzani mpaka mwisho wa uhai wangu

FAHAD KING

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
300
500
Habari Wanabodi

Kwanza ningependa kuwapongeza CCM kwa kutwaa viti vingi vya ubunge. Na Kile kiti kikubwa kabisa cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Visiwani Zanzibar.

Bila shaka hakuna dhambi yoyote ya kuwa mpinzani. Hata kikatiba sidhani kama kuna sheria unasema ukiwa pinzani basi ni kosa.Hapana.

Wala sio kwa ubaya. Lengo ni jema tu kwamba sio lazima ushabikie kila lisemwalo na Chama tawala.

Pongezi tena kwa CCM japo kuna ukakasi mkubwa sana ndani ya Uchaguzi huu. Sitegemei kuwepo kwa bunge bora la kujenga hoja miaka mitano hii (2020-2025). Nasubiria kila hoja kuungwa mkono hata kama ni dhaifu kiasi gani. Kati ya Wabunge 256, Tume imesema wabunge 251 wote ni CCM sasa hapo kuna kujenga hoja?

Anyway nasisitiza,nitaendelea kuwa mpinzani wala sio kwa lengo baya.

Lengo letu ni moja. Sote kuijenga Tanzania moja. Kuijenga Tanzania iliyo BORA kabisa.

Shukrani
 

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
998
1,000
Umesema vizuri na huko ndio kukomaa kisiasa. Hongera kwa wote walioshinda kwa kishindo. Sasa wakachape kazi kweli kweli ili kusudi tutoke hapa kwenye uchumi wa kati tuweze kukwea kwenye angalau mwanzoni mwanzoni mwa nafasi za juu juu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom