Hongera Wakili Fatma Karume "make love" not war!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
unnamed.jpg


Nachukua fursa hii kumpongeza wakili stadi Fatma Karume kwa kuchaguliwa kuiongoza taasisi ya kitaalamu ya wanasheria nchini.

Nauangalia uchaguzi wa TLS kwa kumchagua Mama/binti huyu katika angle tatu muhimu ambazo ni chachu ya ushindi wake.

1-Fatma Karume ni mwanamke na hivyo inadhihirisha ukomavu wa wanawake kisiasa na kitaaluma nchini. Yaani hatuhitaji tena sera za upendeleo wa jinsia ya kike katika nafasi kubwa mbalimbali nchini. Tunahitaji kuwawezesha wanawake kupata elimu tu bila kuwabagua kama wao ni wanawake. They can compete in class and wherever ili wawe kama walivyo wanaume.

2-Fatma Karume ni mzanzibari ambaye amepractise sheria ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikimasnisha ndani ya Visiwa vya Zanzibar na bara la Tanganyika.
Uzanzibari wake haujaweza kuwa hoja ya yeye kukataliwa kuongoza taasisi yenye jina na mipaka ya Kitanganyika. Amechaguliwa kama mtanzania kuongoza taasisi ya Tanganyika yenye mandate inayoishia Tanzania Bara.
Hii ni maana kubwa sana kwa muungano wetu wenye sifa ya kipekee duniani.

3-Fatma Karume amemrithi Tundu Lissu ambaye ni kiongozi ndani ya upinzani nchini kutoka Chadema.
Fatma Karume ametokea kwenye familia namba moja nchini, yaani familia ya mmoja wa waasisi wa CCM. Ni mwanaCCM kwa kuzaliwa, kulelewa na pengine kwa kuwa na kadi ya CCM. Ingawa ni wakili aliyejitoa katika kukinzana na UCCM na hivyo kushabiihana na wapinzani wa CCM.

Sifa hizi tatu zinamfanya kuwa peculiar sana na msaada kwa jamii ya wanasheria.

Nimeongea na baadhi ya wanasheria waliopiga kura wenye mrengo wa upinzani na wakasema wamemchagua Binti Karume kwa kuwa wanajua Serikali haitaweza kumsumbua kutokana na profile yake yenye background ya watawala.

Nimeongea na wanasheria wapiga kura wenye mrengo wa ki-CCM wakasema tumemchagua kwa kuwa ni matunda ya CCM.

Ushauri: Bi Fatma Karume anatakiwa kutumia profile yake, kipaji chake na weledi wake kurudusha mahusiano 'neutral' ya TLS kwa Serikali, CCM, VYAMA VYA UPUNZANI na jamii kwa ujumla. Hii ndio task kubwa mbele yake.

Tanzania ina changamoto nyingi sana za kisheria
-Ongelea mikataba mibaya ya kitaifa na kimataifa.
-Tanzania ina changamoto za kesi kuhusu ubakaji,udhalilishaji na dhuluma dhidi ya watoto na wanawake.
-Tanzania ina matatizo ya haki katika umiliki wa ardhi.
-Tanzania ina matatizo ya ucheleweshaji wa kesi.
-Tanzania ina tatizo la ufisadi papa...n.k
Haya ni baadhi ya matatizo halisi ya watanzania ukiondoa the so politically claimed issues of democracy.
Work hard on true issues of wananchi !!

ALL in ALL naamini anaweza kuhandle taasisi hii ya wanasheria yenye mgawanyiko wa kisiasa.

Please over please "make love" not War!!!!!

Ni mimi Jingalao nikiwa katika viunga karibu kabisa na hoteli ya Mt Meru. Nipo Mt point pub !

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Nimesikitishwa sana na HUJUMA alizo fanyiwa FATMA KARUME leo.

ITV walicho fanya kwenye habari zao za saa mbili,ni uhuni na hujuma za wazi kabisa kwa huyu dada.

Hujuma walizo mfanyia ni:-
1.Ni habari yake kutopewa kipaumbele kabisa kwa kuwekwa ya mwisho kabisa.
2.Ni utangazaji wa matokeo yake,yamesomwa ilimradi tuu,lakin ni kama ITV wamedhamiria hiyo habari isipate umakini.
3.Ni sauti ya FATMA akirekodiwa,imekuwa totally distorted,kwanza sauti ilikuwa chini alaf mbovu,pili ilichanganywa na mtu mwengine,tatu picha ilionekana ya mtu mwingine na chafu.

Uhuni huu hauvumiliki,hata kama ni kujipendekeza mmezidi.
 
Nimesikitishwa sana na HUJUMA alizo fanyiwa FATMA KARUME leo.

ITV walicho fanya kwenye habari zao za saa mbili,ni uhuni na hujuma za wazi kabisa kwa huyu dada.

Hujuma walizo mfanyia ni:-
1.Ni habari yake kutopewa kipaumbele kabisa kwa kuwekwa ya mwisho kabisa.
2.Ni utangazaji wa matokeo yake,yamesomwa ilimradi tuu,lakin ni kama ITV wamedhamiria hiyo habari isipate umakini.
3.Ni sauti ya FATMA akirekodiwa,imekuwa totally distorted,kwanza sauti ilikuwa chini alaf mbovu,pili ilichanganywa na mtu mwengine,tatu picha ilionekana ya mtu mwingine na chafu.

Uhuni huu hauvumiliki,hata kama ni kujipendekeza mmezidi.
Hata mimi nilikuwa naangalia nilivyoona ujinga wao nikabadili channel
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom